Karibu Fadhaget Sanitarium Clinic

Tunapenda kukukaribisha katika Kitengo cha Sayansi ya Tiba Asilia.

Kitengo Cha Sayansi Ya Tiba Asilia

Kwa Muda mrefu tumekuwa tukisaidia wengi katika matibabu na kutengeneza dawa bora kabisa kiafya.

Je Unapenda Kufahamu Jinsi Ya Kupata Mapacha?

Tunafundisha jinsi ya kupata jinsia unayotaka, jinsi ya kupata mtoto kama umekosa mtoto kwa muda mrefu. Pia hata jinsi ya kupata watoto mapacha tunaweza kukusaidia.

Tunapatikana Katika Mikoa Zaidi ya 10 Tanzania

Tunazidi kuongeza matawi yetu nchini Tanzania na Nje ya Nchi. Kwa sasa tunapatikana katika mikoa zaidi ya 10 na tunazidi kuongeza matawi yetu. Karibu sana.

Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Monday, July 28, 2014

THE FADHAGET SANITARIUM CLINIC LEO INAKUPA ELIMU KUHUSINA NA UGONJWA WA ZINAA WA CHLAMYDIA

Ni matumaini yangu kuwa, u-bukheiri wa afya mpenzi msikilizaji na uko tayari kutegea sikio sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Ijuwe Afya Yako. Leo katika sehemu hii ya pili ya muendelezo wa makala ya magonjwa ya zinaa nitazungumzia kuhusu ugonjwa wa Chlamydia ambao ni ugonjwa wa zinaa unaoongoza kwa maambukizi duniani. Ni matumaini yangu mtajumuika nami hadi mwisho wa kipindi, karibuni.



Kwanza kabisa tunachukua fursa hii kuelezeachlamydia ni nini? Chlamydia ni aina ya ugonjwa wa zinaa unaosababishwa na bakteria aina ya chlamydia Trachomatis, ambao wanaweza kuathiri viungo vya uzazi na pia kusababisha ugonjwa wa homa ya mapafu unaojulikana kama typical pneumonia. Kati ya magonjwa ya zinaa yanayosababishwa na bakteria, chlamydia ndio ugonjwa unaoongoza kwa maambukizi duniani ambapo nchini Marekani pekee inakisiwa watu milioni 4 huambukizwa ugonjwa huo kila mwaka.

Tumeamua kuzungumzia ugonjwa wa chlamydia baada ya ugonjwa wa kisonono, kwa sababu magonjwa haya mawili ya zinaa mara nyingi huambatana pamoja kama tulivyoashiria katika kipindi chetu kilichopita. Inawezekana jina la ugonjwa huo halijazoeleka katika masikio ya wengi na hii huenda ni kutokana na kutokuwepo kwa takwimu za kutosha kuhusiana na suala hilo katika nchi nyingi barani Afrika na hasa katika nchi zetu za Afrika Mashariki, hivyo ni vigumu kujua idadi kamili ya maambukizi. Lakini bila shaka chlamydia ndio ugonjwa wa zinaa unaotokana na bakteria unaoongoza kwa maambukizi mengi zaidi duniani ukifuatiwa na ugonjwa wa gono. Gonjwa hili ambalo huwaathiri wanawake na wanaume pia linaweza kuleta madhara makubwa ikiwa ni pamoja na kuharibu mfumo wa uzazi wa mwanamke. Nchini Marekani pekee mwaka 2011, kesi milioni 1 na nusu ziliripotiwa katika hospitali katika majimbo 50 ya nchi hiyo, katika hali ambayo kesi nyingi hazikuripotiwa kwa kuwa watu wengi wenye kuambukiza ugonjwa huo huwa hawaonyeshi dalili na hivyo huwakwenda hospitali. Kama yalivyo magonjwa mengi ya zinaa, chlamydia pia huwapata zaidi vijana na takwimu zinaonyesha kuwa kati ya wasichana walio na umri wa miaka 14 hadi 15 wenye kufanya ngono zembe mara kwa mara, mmoja wao huambukizwa chlamydia.

Ugonjwa wa chlamydia huweza kuambukizwa kupitia njia za kujamiana. Mtu yoyote mwenye kufanya ngono zembe na mtu aliye na ugonjwa huo anaweza kuambukizwa. Pia mama mjamzito huweza kumuambukiza mtoto wake wakati wa ujauzito. Vile vile ugonjwa huo wa zinaa unaweza kuambukizwa kupitia mbawa, vinyesi vya wanyama kama vile ndege walioambukizwa aina ya Chlamydia inayopatikana kwa wanyama kwa mfano kuku, bata, kasuku na kadhalika na kusababisha aina ya homa ya mapafu inayojulikana kama psittacosis ambayo huambatana na homa kali yenye nyuzi joto kati ya celsius 39.4 hadi 41.1. Chlamydia huathiri sehemu tofauti za mwili wa binadamu kama macho, mfumo mzima wa kupumua, sehemu za siri, viungo vya uzazi na tezi (lymph nodes). Lakini je, dalili na viashiria vya ugonjwa wa chlamydia ni vipi? Asilimia 75 ya wanawake na asilimia 50 ya wanaume wanaopata maambukizi ya ugonjwa huu huwa hawaonyeshi dalili zozote za ugonjwa huo.

Dalili hutokea wiki 1 hadi 3 baada ya mtu kupata maambukizi.Wanawake wanaweza kuonyesha dalili zifuatano:
1) Kutokwa na majimaji ya rangi ya njano yanayotoka kwenye utupu, ambayo huwa na harufu kali.
2) Kuhisi maumivu wakati wa haja ndogo.
3) Kuhisi kama kuwaka moto wakati wa kukojoa.
4) Kutokwa na damu katikati ya kipindi cha hedhi yaani baada ya kumaliza mzunguko wa hedhi na kabla ya kuanza mzunguko mwengine.
5) Kuhisi maumivu sehemu ya chini ya tumbo.
6) Kuhisi maumivu wakati wa kujamiana.
7) Kutokwa na damu wakati wa kujamiana na pia kuvimba na kuhisi maumivu kwenye tezi zilizopo sehemu za siri.

Dalili kwa wanaume zinaweza kuwa ni:
1) Kuhisi maumivu wakati wa kukojoa.
2) Kuhisi kama kuwaka moto wakati wa kukojoa.
3) Kutokwa na majimaji kwenye uume ambayo yanaweza kuwa ya rangi nyeupe kama maziwa, kijivu au rangi ya njano.
4) Sehemu ya tundu kwenye uume kuwa nyekundu, kuvimba na kuwasha.
5) Kuhisi maumivu kwenye korodani na tezi zilizopo sehemu za siri ambazo huvimba na kuambatana na maumivu. Mara nyingi dalili hizi kwa wanaume hukuja na kupotea au zinaweza kuonekana tu wakati anapoenda kukojoa asubuhi baada ya kuamka kutoka usingizini.

Dalili za ugonjwa huu kama umeathiri puru (rectum) kwa wanawake na wanaume ni kama ifuatavyo: Kuwashwa na kutokwa na damu kwenye puru, maumivu wakati wa kujisaidia haja kubwa na kutokwa na uchafu kama kamasi kutoka kwenye puru. Iwapo vimelea vya chlamydia vitaathiri macho, wanawake na wanaume huwa na dalili zifuatazo: Uvimbe kwenye macho, macho kuwa mekundu, kuwasha na hata kutokwa na majimaji machoni. Chlamydia inayoambukiza kwenye macho (Chlamydia conjunctivitis or trachoma) ndiyo inayoongoza kwa kusababisha upofu duniani.

Tunasonga mbele na kipindi cha afya wapenzi wasikilizaji kinachowajia kupitia Idhaa ya Kiswahili Sauti ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Baada ya mtu kuhisi dalili hizo tulizozitaja, hupaswa kwenda hospitalini au katika kituo cha afya ili kupimwa na kuthinitishwa kwamba ana ugonjwa huo ili apatiwe matibabu. Vipimo vya uchunguzi vya ugonjwa wa Chamydia ni Urethral swab for culture. Katika kipimo hiki majimaji kutoka kwenye uume au uke huchukuliwa kwa kutumia kijiti chenye pamba au swab maalum ambayo hupelekwa maabara ili kuoteshwa na kuangalia aina ya uoto wa bakteria. Pia huchukuliwa vipimo vya mkojo na pia kipimo cha PCR au Polymerase Chain Reaction, ambacho ni cha kuangalia vinasaba vya bakteria au DNA na hufanywa katika maabara. Baada ya majibu kuonyesha kuwa mgonjwa ameambukizwa vimelea vya ugonjwa huo matibabu hufuata.Chlamydia ni kati ya magonjwa ya zinaa yanayotibika na ugonjwa huu hutibiwa kwa dawa aina ya antibiotiki zilizopo kwenye makundi ya macrolides, Quinolones na Polyketides ambazo hutolewa chini ya maelekezo ya daktari.

Lakini madhara ya ugonjwa huu ni yapi? Mpenzi msikilizaji madhara ya ugonjwa huu kwa wanaume, ni kuwa huathiri korodani na kusababisha mwanamume kukosa uwezo wa kuwa na watoto au kuwa tasa na pia husababisha maambukizi kwenye tezi dume (prostatitis). Kwa wanawake, husababisha maambukizi kwenye mirija ya uzazi, mfuko wa uzazi, na mayai ya uzazi, kwa hivyo kusababisha ugonjwa wa uvimbe katika fupanyomga au Pelvic inflammatory disease (PID). Pia huongeza uwezekano wa wanawake kupata mimba zinazotunga nje ya mfuko wa uzazi ambazo kitaalamu hiutwa Ectopic pregnancy. Mbali na hilo, mwanamke hupata maumivu sugu kwenye nyonga na ugonjwa wa mifupa arthritis aina ya Reiters syndrome. Vilevile, Chlamydia huweza kusababisha ugumba kwa mwanamke kama hatapata tiba. Si hayo tu, kwa wanawake wajawazito, chlamydia husababisha wajifungue kabla ya wakati wake. Pia mtoto anaweza kuzaliwa na maambukizi kwenye masikio, sehemu za siri, macho na kwenye mapafu yaani homa ya mapafu, na kama mtoto hatapatiwa tiba ya haraka ya macho baada ya kuzaliwa basi anaweza kuwa kipofu. Dalili za chlamydia kwa watoto wachanga hutokea katika kipindi cha wiki mbili kwenye macho, na iwapo ni homa ya mapafu dalili zake hujitokeza katika kipindi cha wiki 2 hadi miezi 3 baada ya kuzaliwa.

Wapenzi wasikilizaji tuhitimishe kipindi chetu cha leo kwa kuelezea jinsi ya kujikinga na ugonjwa wa zinaa wa chlamydia. Kwanza kabisa kama nilivyoeleza kwenye kipindi kilichopita, njia sahihi ya kujikinga na magonjwa ya zinaa ni kuacha au kuepuka kujamiiana au kufanya ngono zembe na sizizo salama. Kwa wanawake wajawazito, ni vizuri kuhudhuria kliniki mapema wakati wa ujauzito na kupimwa vipimo mbalimbali ambapo kimojawapo ni cha kuangalia iwapo mama mjamzito ameathirika na ugonjwa huu na kupatiwa matibabu mapema. Kwa wale wenye maambukizi wanashauriwa kuchukua tahadhari ya kutowaambukiza wapenzi wao kwa kufanya ngono salama, pia kuepuka kushika macho kwa kutumia mikono na hata ikiwezekana kuwaepuka wapenzi wao ili kuwalinda na maambukizi. Vilevile kwa wale ambao wapenzi wao wameambukizwa au wameonyesha dalili za ugonjwa huu, wanashauriwa na wao pia kupata tiba hata kama hawana dalili zozote.

Naam wapenzi wasikilizaji, kwa hakika kama wasemavyo wahenga kinga ni bora kuliko tiba, basi tujilinde na kujiepusha na magonjwa yote yakiwemo ya zinaa yanayoweza kuepukika, na daima tuzilinde afya zetu!

Thursday, July 24, 2014

VYAKULA VYA KUEPUKA KUVILA KWA MAMA MWENYE UJAUZITO

Ili mtoto azaliwe akiwa na afya njema pamoja na akili timamu, akiwa tumboni lazima alishwe lishe bora na mlo sahihi. Mwenye jukumu la kutoa lishe bora na sahihi kwa kiumbe kilichomo tumboni ni mama. Anatakiwa kujua aina ya vyakula anavyopaswa kula. Vivyo hivyo, anatakiwa kujua aina ya vyakula vya kuviepuka.



Katika makala ya leo, tunaangalia orodha ya vyakula vilivyokatazwa. Mama mja mzito haruhusiwi kuvila vyakula vifuatavyo kwa faida ya kiumbe kilichomo tumboni na kwa faida yake mwenyewe:

NYAMA MBICHI
Epuka kula samaki au nyama mbichi au iliyopikwa lakini haikuiva vizuri. Utajiepusha na uwezekano wa kula bakteria na vijidudu vingine hatari kwa afya ya mtoto tumboni. Mjamzito anapokula nyama, anatakiwa kuhakikisha imeiva sawasawa.

‘SOSEJI’ NA ‘SANDWICHI’
Mjamzito haruhusiwi kula ‘soseji’, ‘sandwichi’ za nyama na vyakula vingine vilivyotengenezwa kwa nyama. Inaaminika kuwa nyama zinazoandaliwa kwa ajili ya kutengenezea vyakula kama hivyo, huwa vimewekewa vihifadhi vyakula (preservatives) ambavyo vinaweza visiwe vizuri kwa afya ya mtoto.

SAMAKI WENYE ZEBAKI (MERCURY)
Wajawazito wamekatazwa kula samaki wenye kiasi kingi cha madini ya zebaki. Ulaji wa zebaji kwa wajawazito umehusishwa na uzaaji wa watoto taahira. Mfano wa samaki hao ni pamoja na Papa, Chuchunge na dagaa wakubwa.

MAYAI MABICHI
Ulaji wa mayai mabichi au vyakula vilivyochanganywa na mayai mabichi, mjamzito haruhusiwi kuvila. Kuna baadhi ya ‘Ice Cream’ na ‘mayonaizi’ hutengenezwa kwa kuchanganywa na mayai mabichi. Mjamzito amekatazwa kuvila vyakula hivyo.

MAINI
Maini yana kiwango kikubwa cha madini aina ya chuma. Hata hivyo, yana kiasi kikubwa cha Vitamin A ambacho huweza kuwa na madhara kwa mtoto kikizidi.

MAZIWA MABICHI
Maziwa mabichi huweza kuwa na bakteria ajulikanae kama ‘Listeria’, ambaye huweza kusababisha kuharibika kwa mimba. Unapokunywa maziwa, hakikisha yamechemshwa au kama ni ya paketi hakikisha ni yale yaliyoandikwa ‘Pasteurized’ na siyo ‘Unpasteurized’.

KAFEINI (CAFFEINE)
Ingawa baadhi ya utafiti unaonesha kuwa unywaji wa kiasi kidogo cha kafeini hauna madhara, lakini kuna utafiti mwingine unaonesha kuwa unywaji wa kafeini una uhusiano na kuharibika kwa mimba. Kafeini ni aina ya kirutubisho kinachopatikana ndani ya kahawa.

Iwapo mjamzito atakunywa kahawa, basi anywe kiasi kidogo sana kisichozidi kikombe kimoja kwa siku. Kwa kawaida kahawa hukausha maji mwilini, hivyo unywaji wake husaidia kukauka maji mwilini ambayo ni muhimu sana kwa mjamzito.

Utafiti mwingine unaonesha kuwa kafeini inahusishwa pia na uharibikaji wa mimba, uzaaji wa watoto ‘njiti’ na watoto wenye uzito mdogo. Ni vizuri kunywa maji ya kutosha, maziwa na juisi na kuepuka kunywa vinywaji vyenye kahawa.

POMBE
Hakuna ushahidi unaothibitisha kuwa unywaji wa pombe kiasi kidogo wakati wa ujauzito hauna madhara, kwa maana hiyo matumizi ya pombe hayaruhusiwi kabisa wakati wa ujauzito, hata kama ni kidogo.
Unywaji wa pombe wakati wa ujauzito huweza kuathiri ukuaji mzuri wa mtoto. Kutegemeana na kiasi atakachokunywa mjamzito, pombe inaweza kumsababishia mtoto ugonjwa hatari utokanao na pombe (Fetal Alcohol Syndrome).

Monday, July 21, 2014

THE FADHAGET SANITARIUM CLINIC INAPENDA UFAHAMU UGONJWA WA FIGO

Watu wengi wanateseka sana na ugonjwa huu wa figo, wamesumbuka sana bila hata ya kupata tiba, na watu wengine wamethbutu hata kukataa tammaa wakisubiria kifo. Dr. Fadhili Emily wa The Sanitarium Clinic anayepatikana Mbezi Afrikana Dar es Salaam anapenda kukutaarifu kuwa ipo dawa ambayo inatibu ugonjwa huu wa figo. Unachotakiwa ni kufika katika kituo chake naye atakutibu. Sasa anapenda kukupa baadhi ya vitu muhimu kwaajili yako kufahamu ugonjwa huu sugu wa figo



Mwili wa binadamu kuna viungo muhimu katika utendaji, miongoni mwa viungo hivyo ni FIGO.FIGO ni miongoni mwa viungo muhimu katika mfumo wa utendaji kazi wa mwili wa binadamu.Mwili wa binadamu una figo mbili zenye maumbo yanayofanana, yakiwa yamejificha nje ya utando unaozunguka tumbo chini ya mbavu.

Kazi kuu za figo ni kuchuja vitu mbalimbali pamoja na sumu katika damu, kusaidia kuhifadhi, kudhibiti kiwango cha maji na madini (electrolytes) mwilini.

Figo huchuja vitu hivyo pamoja na maji yaliyo mwilini na kutengeneza mkojo, huchuja pia maji yasiyohitajika mwilini huku yakinyonya madini na kemikali muhimu kuzirudisha katika mzunguko wa damu na kutoa nje uchafu usiohitajika.

Kazi nyingine za figo ni pamoja na kusaidia kutengeneza kiasili cha erythropoletin ambacho ni muhimu katika utengenezaji wa chembechembe nyekundu za damu, hupokea asilimia 25 ya damu na kila figo ina chembechembe hai ndogo milioni moja, pia kusaidia kudhibiti na kurekebisha shinikizo la damu mwilini (blood pressure).

Zipo sababu kadhaa zinazosababisha maradhi katika figo kwa binadamu ikiwamo matumizi mabaya ya dawa hasa za maumivu, baadhi ya dawa za Kichina, uvutaji wa sigara na unywaji wa pombe kupita kiasi.

Aina za ugonjwa wa figo
Kuna aina mbili kuu za ugonjwa huu, kwanza ni ile ya figo kushindwa kufanya kazi kwa ghafla na muda mfupi; pili ni ile ya figo kushindwa kufanya kazi polepole na kwa muda mrefu.
Figo kushindwa kufanya kazi polepole na kwa muda mrefu huharibiwa taratibu na kuendelea kupunguza uwezo wake wa kufanya kazi kadiri siku zinavyokwenda.

Dalili za aina hii ya ugonjwa huchelewa kujitokeza na wakati mwingine mwenye tatizo hajisikii dalili yoyote, hadi pale inapotokea akaugua ugonjwa mwingine na daktari kuhisi tatizo, ndipo hugundulika kuwa na ugonjwa huo baada ya vipimo.

Sababu kubwa ya figo kushindwa kufanya kazi ghafla ni kupungua kwa mzunguko wa damu kwenye figo, kemikali za mwilini au kushambuliwa na sumu.
Kushuka kiwango cha mzunguko wa damu humpata mtu anayetapika sana na hanywi maji ya kutosha, anayeharisha sana na hanywi maji ya kutosha na wale ambao hupoteza damu nyingi kama vile kwenye ajali.

Sababu nyingine ni mgonjwa kuwa na ugonjwa wa moyo, moyo kushindwa kusukuma damu kwa ghafla, au waliougua maradhi ya moyo kwa muda mrefu.

Mtu kuwa na kemikali zinazotokana na kutumia dawa iliyo na mzio kwa mtumiaji, dawa zinazosababisha mkojo utoke kwa wingi, na baadhi ya dawa za malaria.
Tatizo la figo kushindwa kufanya kazi kwa ghafla pia humpata mtu ambaye ana bakteria kwenye mzunguko wa damu, ambao wanaweza kusababisha homa ‘Septicemia’ na kuugua malaria.
Sababu zinazofanya figo ishindwe kufanya kazi taratibu na kwa muda mrefu na hatimaye kushindwa kabisa kuwa ni presha kuwa juu, kisukari, magonjwa yanayosababishwa na bakteria, HIV, saratani na sumu mbalimbali zinazoingia mwilini.

DALILI
Dalili ya kwanza ni kupungua kwa kiasi cha mkojo, maji kujaa mwilini, madini ya mwili kuwa juu hasa ya ‘potasiamu’, asidi nyingi, matatizo katika moyo, ubongo, kukosa hamu ya kula na kudhoofika mwili.

Nyingine ni kwa wagonjwa ambao hawagunduliki mapema ni kuvimba macho wakati wa asubuhi na uvimbe kupungua baadaye, kupungukiwa damu mwilini kama dalili za kwanza (figo ikishindwa kufanya kazi ya kusaidia kutengeneza damu). TIBA YAKE
Tiba ya maradhi haya utasoma wiki ijayo. usikose nakala ya gazeti hili.

Friday, July 11, 2014

SALAMU KUTOKA KWA DR. FADHILI EMILY WA THE FADHAGET SANITARIUM CLINIC


Leo napenda kuwasalimu wateja wangu, ninawapa pole na mihangaiko ya kutafuta riziki. Pia ninawapa pole wagonjwa wote wanaopata taabu kutoka na magonjwa sugu. Ninachotaka kusema kwako ni kufika katika kituo chetu Mbezi Beach Afrikana nasi tutakutibu. Mungu akulinde.

Monday, July 7, 2014

TAHADHARI KWA WANAOTUMIA SIMU NA KUWEKA VYAKULA KATIKA MIFUKO AU VYOMBO VYA PLASTIC


Dr. Brian Berry wa Marekani amegundua  kansa mpya kwa binadamu inayosababishwa na Silver Nitro Oxide. Unaponunua kadi ya simu usichune kwa kucha kwani imo hiyo Silver Nitro Oxide na inaweza kusababisha  kansa ya ngozi. Watumie ujumbe huu wale unaowafahamu:
http://i.telegraph.co.uk/multimedia/archive/02414/mobilePhone_2414866b.jpg
NUKUU MUHIMU ZA AFYA
1.       Sikiliza simu kwa sikio la kushoto
2.       Usimeze dawa na maji baridi
3.       Usile chakula kizito baada ya saa kumi na moja jioni
4.       Kunywa maji mengi asubuhi na kidogo usiku
5.       Wakati mzuri wa kulala ni kuanzia saa nne  hadi kumi usiku
6.       Usilale mara baada ya kula dawa au chakula
7.       Ikiwa chaji imebaki kijino cha mwisho usipokee simu kwani mionzi inakuwa na nguvu kwa mara 1000 zaidi
Unaweza kuwatumia haya wale unaowajua? Mie nimeshafanya. Huruma haigharimu kitu lakini elimu ni nuru.

UMUHIMU
Jumauiya ya uchunguzi ya Marekani imetoamajibu mapya
1.       Usinywe chai kwa kikombe cha plastic
2.       Usile chochote kwenye mifuko ya plastic.
Pastic ikikutana na joto inatoa vitu vinavyosababisha aina 52 za kensa. Kwahiyo ujumbe huu ni borakuliko mijumbe 100 isiyo na maana. Tafadhali wapelekee unaowajua. Nimefanya kwa sehemu yangu kwa wale ninaowajali

Wako mpendwa
Dr. Fadhili Emily
THE FADHAGET SANITARIUM CLINIC


Sunday, July 6, 2014

THE FADHAGET SANITARIUM CLINIC LEO INAKUPA SOMO LA KUKABILIANA NA KANZA YA MATITI


CONCHITA hakuwa na dalili zozote za kansa.Alikuwa na umri wa miaka 40, mwenye afya nzuri, na hakuna mtu yeyote katika familia yao aliyewahi kuugua ugonjwa huo. Eksirei ya matiti ambayo alipigwa kwa ukawaida haikuonyesha tatizo lolote. Lakini siku moja alipokuwa akijichunguza mwenyewe akiwa bafuni, alihisi uvimbe fulani. Uvimbe huo uligunduliwa kuwa kansa. Conchita na mume wake waliketi wakiwa wamechanganyikiwa huku daktari akiwaeleza kuhusu matibabu mbalimbali wanayoweza kuchagua.

Zamani, daktari angemwambia mwanamke aliye na kansa ya matiti kwamba matibabu pekee ni kukatwa titi kabisa, upasuaji ambao uliacha kovu kubwa sana kwa kuwa ulihusisha kukata titi, tezi za limfu kwenye kifua na kwapa, na misuli ya kifua. Mara nyingi kutibiwa kwa kutumia kemikali au miale kulifanya hali iwe mbaya hata zaidi. Kwa sababu hiyo, watu wengi waliogopa matibabu ya ugonjwa huo kuliko ugonjwa wenyewe.

Jitihada nyingi zimefanywa ili kutibu kansa hiyo hatari ya matiti bila kumwacha mgonjwa na kovu kubwa na athari za matibabu. Kama ilivyokuwa katika kisa cha Conchita, leo wagonjwa walio na kansa ya matiti wanaweza kuchagua matibabu mbalimbali.* Na utafiti wa kitiba unaoendelea kufanywa pamoja na ripoti za kitiba kwenye vyombo vya habari zinawapa watu tumaini kwamba matibabu mapya, mbinu mpya za kuchunguza ikiwa mtu yuko katika hatari ya kupatwa na ugonjwa huo, na kula vyakula vinavyoimarisha mfumo wa kinga hatimaye zitamaliza ugonjwa huo.


Hata hivyo, licha ya maendeleo ya kitiba, bado kansa ya matiti ndiyo kansa inayosababisha vifo vingi zaidi vya wanawake.* Nchi zilizoendelea za Amerika Kaskazini na Ulaya Magharibi ndizo zenye idadi kubwa zaidi ya watu walio na kansa, lakini idadi ya wanawake walio na kansa ya matiti inaongezeka katika bara la Asia na Afrika ambako kwa kawaida kumekuwa na idadi ndogo. Kwa kweli, idadi ya wanaokufa kati ya wale wanaogunduliwa kuwa na ugonjwa huo huko Asia na Afrika ni ya juu. Kwa nini? Daktari mmoja barani Afrika anasema: “Kansa hiyo haigunduliwi mapema. Wagonjwa wengi huja ikiwa tayari imeenea sana.”

Hatari ya kupatwa na kansa hiyo huongezeka kadiri umri unavyosonga. Asilimia 80 hivi ya wanawake wenye kansa ya matiti wana umri unaozidi miaka 50. Lakini jambo linalofariji ni kwamba kansa ya matiti ni mojawapo ya kansa zinazoweza kutibiwa kwa urahisi. Kwa kweli, asilimia 97 ya wanawake nchini Marekani waliotibiwa kabla ya kansa hiyo kuenea wangali hai miaka mitano baada ya kansa hiyo kugunduliwa. Kufikia sasa, miaka mitano imepita tangu kansa ya Conchita ilipogunduliwa.

Mambo ya Msingi Kuhusu Kansa ya Matiti

Kama katika kisa cha Conchita, mara nyingi kansa ya matiti huanza kama uvimbe usio wa kawaida. Jambo lenye kufariji ni kwamba asilimia 80 hivi ya uvimbe huo si hatari bali ni vifuko vyenye umajimaji.

Kansa ya matiti huanza wakati ambapo chembe moja inajigawanya haraka sana isivyo kawaida na bila utaratibu, na hatua kwa hatua inafanyiza uvimbe. Uvimbe unakuwa kansa wakati chembe zake zinapovamia tishu nyingine. Uvimbe fulani unaweza kukua kwa haraka; mwingine unaweza kuchukua miaka kumi hivi kabla ya kugunduliwa.

Ili kuchunguza ikiwa uvimbe wa Conchita ulikuwa na kansa, daktari wake alitumia sindano nyembamba kutoa tishu kutoka kwenye uvimbe huo. Uvimbe huo ulikuwa na kansa. Hivyo, alifanyiwa upasuaji ili kuondoa uvimbe huo na tishu zilizozunguka titi. Upasuaji huo ulisaidia pia kuonyesha uvimbe huo ulikuwa umefikia hatua gani (ukubwa, aina, na kuenea kwake) na kuchunguza ulikuwa ukikua upesi kwa kadiri gani.

Baada ya upasuaji, wagonjwa wengi hupata matibabu mengine ambayo yatazuia kansa isirudi au kuenea. Chembe zenye kansa zinaweza kutoka kwenye uvimbe na kusafiri kupitia mfumo wa damu au mfumo wa limfu, na kuanza kukua tena mahali pengine mwilini. Kuenea kwa kansa hadi kwenye viungo na tishu muhimu kama vile ubongo, ini, uboho wa mfupa, au mapafu ndio hufanya ugonjwa huo uwe hatari.

Conchita alitibiwa kwa miale na kemikali ili kuharibu chembe za kansa kwenye titi na pia katika sehemu nyingine za mwili. Kwa kuwa uvimbe wenye kansa aliokuwa nao ulichochewa hasa na homoni ya estrojeni, alipewa matibabu ya kuzuia kutokezwa kwa homoni hiyo ili kuzuia uvimbe mpya wenye kansa usitokee.

Kwa sababu ya maendeleo katika matibabu ya kansa ya matiti, kumekuwa na matibabu mbalimbali ikitegemea umri, afya, historia ya kansa katika familia, na aina ya kansa. Kwa mfano, katika kisa cha mwanamke anayeitwa Arlette, uchunguzi ulifanya kansa yake igunduliwe kabla haijaenea nje ya vijia vya kupitishia maziwa. Kwa hiyo, alifanyiwa upasuaji wa kuondoa uvimbe huo, na titi lake halikukatwa. Kabla ya kufanyiwa upasuaji, Alice alitibiwa kwa kemikali ili kupunguza ukubwa wa uvimbe. Daktari wa Janice aliondoa tu uvimbe na tezi za limfu zilizokuwa karibu, ambazo huwa za kwanza kuingia umajimaji kutoka kwenye uvimbe. Kwa kuwa tezi nyingine hazikuwa na chembe zenye kansa, hakuziondoa. Hilo lilifanya mkono wa Janice usivimbe kwa sababu ya kufungika kwa mishipa ya limfu, jambo ambalo hutokea wakati tezi nyingi za limfu zinapoondolewa.

Utafiti mwingi umefanywa kuhusu ukuzi wa kansa ya matiti, lakini swali la msingi ni, Ni nini husababisha kansa ya matiti, nayo huanza jinsi gani?

Visababishi Ni Nini?

Visababishi vya kansa ya matiti bado ni fumbo. Wachambuzi wanasema kwamba utafiti mwingi unafanywa kuhusu tiba na kuchunguza ikiwa mtu ana kansa hiyo—jambo ambalo linaleta faida kubwa—badala ya kutafuta visababishi vyake na jinsi ya kuizuia. Hata hivyo, wanasayansi wamegundua mambo kadhaa muhimu. Wengine wanaamini kwamba kansa ya matiti hutokana na hatua nyingi tata ambazo huanza wakati ambapo chembe fulani ya urithi yenye kasoro inapofanya chembe zitende kwa njia isiyo ya kawaida, yaani, zigawanyike kwa kasi sana, zishambulie tishu nyingine, na kuepuka kuharibiwa na mfumo wa kinga, kisha pole kwa pole chembe hizo zinashambulia na kuharibu viungo muhimu vya mwili.

Chembe hizo za urithi zenye kasoro hutoka wapi? Asilimia 5 hadi 10 ya visa vya kansa hiyo huonyesha kwamba wanawake huzaliwa na chembe za urithi ambazo zinaweza kusababisha kansa ya matiti. Lakini inaonekana kwamba katika visa vingi, chembe za urithi zenye afya huharibiwa na vitu vingine vilivyo nje ya mwili kama vile, miale na kemikali. Huenda utafiti wa wakati ujao ukathibitisha jambo hilo.

Jambo lingine linalohusianishwa na kansa ya matiti ni homoni ya estrojeni ambayo huenda inachochea aina fulani za kansa hiyo. Kwa hiyo, mwanamke anaweza kupatwa na kansa hiyo ikiwa alianza kupata hedhi mapema maishani au ikiwa aliacha kupata hedhi akiwa amechelewa isivyo kawaida, ikiwa alipata mimba ya kwanza umri wake ukiwa umesonga au ikiwa hakuwahi kupata mimba, au ikiwa alipata matibabu ya kurudisha homoni fulani mwilini. Kwa kuwa chembe za mafuta hutokeza estrojeni, huenda wanawake walionenepa kupita kiasi waliofika umri wa kuacha kupata hedhi na hivyo ovari zao hazitokezi tena homoni, wakawa katika hatari ya kupatwa na kansa hiyo. Pia watu walio na viwango vya juu vya insulini na watu walio na viwango vya chini vya homoni ya usingizi inayoitwa melatonin, kama vile watu wanaofanya kazi usiku, wako pia katika hatari ya kupatwa na kansa hiyo.

Je, kuna tumaini lolote la kugunduliwa kwa tiba bora ya kansa ya matiti isiyotokeza madhara? Watafiti wanachunguza matibabu ambayo yatahusisha kutumia mfumo wa kinga wa mwili na dawa ambazo zitalenga hasa utendaji wa chembe za urithi na protini ambazo huchochea ukuzi wa kansa. Kwa sasa, teknolojia iliyoboreshwa ya kupiga picha za eksirei inapaswa kuwasaidia madaktari kutibu kwa njia hususa kwa kutumia miale.

Wanasayansi pia wanajifunza mambo mengine kuhusu kansa kutia ndani: kuelewa ni kwa nini kansa huenea, kudhibiti chembe za kansa ambazo haziharibiwi kupitia matibabu ya kemikali, kuzuia kugawanyika kwa chembe, na kutibu kila uvimbe kwa njia hususa.

Hata hivyo, katika ulimwengu wa leo, magonjwa hayawezi kuondolewa kabisa na wanadamu wataendelea kufa. (Waroma 5:12) Ni Muumba wetu tu anayeweza kubadili hali hiyo yenye kusikitisha. Je, atafanya hivyo? Biblia inajibu, ndiyo! Inasema kwamba kutakuwa na wakati ambapo “hakuna mkaaji atakayesema: ‘Mimi ni mgonjwa.’”* (Isaya 33:24) Hicho kitakuwa kitulizo kwelikweli!

Baadhi ya majina yamebadilishwa. Amkeni! halipendekezi matibabu yoyote hususa. Idadi ya wanaume wanaopatwa na kansa ya matiti ni ndogo sana ikilinganishwa na ya wanawake.

Ahadi hiyo inazungumziwa kwa urefu katika kitabu Biblia Inafundisha Nini Hasa? kilichochapishwa na Mashahidi wa Yehova.

DALILI UNAZOPASWA KUANGALIA

Ugunduzi wa mapema ni muhimu, lakini utafiti fulani unaonya kwamba huenda uchunguzi wa matiti na eksirei ya matiti kwa wanawake wachanga isitoe habari sahihi na hivyo kufanya wapate matibabu wasiyohitaji na kuwa na wasiwasi. Hata hivyo, wataalamu wanawahimiza wanawake waangalie mabadiliko yoyote katika matiti yao na mfumo wao wa limfu. Zifuatazo ni baadhi ya dalili unazopaswa kuangalia:

● Uvimbe wowote au kuongezeka kwa unene wa ngozi kwenye makwapa au titi

● Umajimaji wowote unaotoka kwenye chuchu ambao si maziwa

● Mabadiliko yoyote ya rangi au ngozi ya titi

● Chuchu iliyodidimia kwa njia isiyo ya kawaida au inayowasha

UNAPOGUNDULIWA UNA KANSA YA MATITI

● Tazamia kwamba itakuchukua zaidi ya mwaka mmoja kutibiwa na kupata nafuu.

● Ikiwezekana, chagua madaktari wenye ujuzi ambao wataheshimu mahitaji na imani yako.

● Mkiwa familia, amueni ni nani mtakayemwambia kuhusu ugonjwa wako, na mtafanya hivyo wakati gani. Hilo litawawezesha marafiki wenu waonyeshe upendo na kusali nanyi na kwa niaba yenu.—1 Yohana 3:18.

● Kabiliana na mkazo wa kihisia kwa kusoma Biblia, kusali, na kutafakari mambo yanayofaa.—Waroma 15:4; Wafilipi 4:6, 7.

● Zungumza na wale ambao wamewahi kuugua kansa ya matiti na watakaokutia moyo.—2 Wakorintho 1:7.

● Jaribu kukazia fikira mahangaiko ya leo tu, na si ya kesho. Yesu alisema: “Msihangaike kamwe juu ya kesho, kwa maana kesho itakuwa na mahangaiko yake yenyewe.”—Mathayo 6:34.

● Tumia vizuri nguvu zako. Unahitaji kupumzika vya kutosha.

KUZUNGUMZA NA DAKTARI WAKO

● Jifunze maneno machache ya kitiba kuhusu kansa ya matiti.

● Kabla ya kwenda kumwona daktari, andika orodha ya maswali, na umwombe mwenzi wako au rafiki aandamane nawe ili akusaidie kuandika mambo machache.

● Daktari wako akisema jambo ambalo huelewi, mwombe akufafanulie zaidi.

● Mwulize daktari wako ametibu watu wangapi wenye kansa kama yako.

● Ikiwezekana, tafuta maoni ya daktari mwingine.

● Ikiwa madaktari wako wanatofautiana, chunguza ujuzi wa kila mmoja wao wa kutibu kansa hiyo. Waombe wajadiliane kuhusu hali yako. Unaweza pia kutafuta maoni ya daktari mwingine.

KUKABILIANA NA ATHARI ZA MATIBABU

Huenda matibabu fulani yakatokeza athari kama vile kichefuchefu, nywele kung’oka, kujihisi mchovu sana, maumivu, kufa ganzi au kuwashwa kwenye mikono na miguu, na matatizo ya ngozi. Hatua zifuatazo zinaweza kupunguza athari hizo:

● Kula chakula kizuri ili mfumo wako wa kinga uwe na nguvu.

● Weka rekodi inayoonyesha jinsi nishati yako inavyobadilika na jinsi unavyoathiriwa na vyakula mbalimbali.

● Jaribu kupunguza kichefuchefu na maumivu kwa kutumia dawa, tiba ya kuchoma kwa sindano ili kuamsha mishipa ya fahamu, au kukandwa mwili.

● Fanya mazoezi ya kiasi ili uwe na nguvu, udhibiti uzito wako, na kuboresha utendaji wa mfumo wako wa kinga.*

● Pumzika mara nyingi, lakini zingatia kwamba kulala kwa muda mrefu huongeza uchovu.

● Usiache ngozi yako ikauke. Vaa nguo ambazo hazikubani. Oga kwa maji yenye joto.

Watu wanaougua kansa wanapaswa kumwona mtaalamu wa kitiba kabla ya kuanza kufanya mazoezi yoyote.

IKIWA MTU UNAYEMPENDA ANA KANSA

Unaweza kumtegemeza jinsi gani mpendwa aliye na kansa? Fuata kanuni hii ya Biblia: “Shangilieni pamoja na watu wanaoshangilia; lieni pamoja na watu wanaolia.” (Waroma 12:15) Mwonyeshe kwamba unampenda na kumjali kupitia simu, barua, kadi, barua pepe, na kumtembelea kwa muda mfupi. Salini pamoja, na kusoma maandiko yenye kufariji kutoka kwenye Biblia. Beryl, ambaye mume wake ni mwangalizi anayesafiri wa Mashahidi wa Yehova, anahimiza hivi: “Usiwataje watu waliokufa kutokana na kansa, lakini taja wale ambao bado wako hai.” Janice, ambaye wakati mmoja aliugua kansa anasema hivi: “Nenda tu na umkumbatie rafiki yako. Akitaka kuzungumza kuhusu hali yake, atafanya hivyo.” Waume hasa wanahitaji kuwahakikishia wake zao kwamba wanawapenda.

“Mara kwa mara, tulikuwa na siku ambayo hatukuzungumza kuhusu kansa,” anasema Geoff. “Mke wangu alikuwa ameazimia kwamba hatutakazia fikira afya yake tu. Kwa hiyo tuliamua kwamba mara kwa mara, kwa siku nzima, hatutazungumza kuhusu kansa. Badala yake, tulikazia fikira mambo mengine mazuri katika maisha yetu. Ni kana kwamba tulichukua likizo kutokana na ugonjwa huo.”

Tuesday, July 1, 2014

THE FADHAGET SANITARIUM CLINIC INAKUPA BAADHI YA SABABU ZA MENO KUOZA KWA WATOTO

Meno mbali na kuwa ni msaada katika kukatakata chakula mdomoni pia ni urembo kwa mwanadamu. Mtu anapokosa meno anaonekana wa ajabu kidogo. Kuna umuhimu wa kutunza sana meno yetu kwa njia mbalimbali tunazofundishwa madarasani na hata kwa marafiki zetu mitaani. Mzazi unapokosa kumtunza mwanao na kuhakikisha meno yake ni imara na bora, siku hayo meno yatakapooza na kung'ooka, mtoto huyo akikua na kupata ufahamu atakulaamu.
http://static.guim.co.uk/sys-images/Observer/Columnist/Columnists/2011/1/29/1296296490076/Young-boy-brushing-his-te-007.jpg
Meno na uzuri au ubora wake huanzia kwa watoto. Tangu mtoto anapoota meno, anapofikisha miaka mitano na kuanza kung’oa, ni kipindi mujarabu kwa mwonekano wake wa kinywa siku za usoni.

Meno na uzuri au ubora wake huanzia kwa watoto. Tangu mtoto anapoota meno, anapofikisha miaka mitano na kuanza kung’oa, ni kipindi mujarabu kwa mwonekano wake wa kinywa siku za usoni.

Lakini watu wengi huoza meno na watoto pia hukumbwa na hali hii.

Kuoza kwa meno ambayo hushambulia zaidi meno ya utotoni (milk teeth or primary dentition), japo wakati mwingine hata huweza kushambulia hata ukubwani. Ugonjwa huu unajidhihirisha kwa kuanza kushambulia meno na vyanzo vyake.

Meno hushambuliwa kwa mpigo hasa kuanzia meno ya juu mbele, ingawa meno ya chini mbele ni mara chache kushambuliwa kwa vile yanakingwa na visababisha vya kuoza na ulimi.

Ugonjwa huu hushambulia hata maeneo ya meno ambayo kwa hali ya kawaida si rahisi kuoza, kama sehemu ya kukatia kwa meno ya mbele (incisal edges) na sehemu ya mbele kati na nyuma kati (facial and lingual surfaces).
http://cdn.inquisitr.com/wp-content/uploads/2013/05/cavities.jpg

Sababu ya kuoza kwa meno utotoni
Nadharia nyingi zinaonyesha kuna uhusiano mkubwa kati ya ugonjwa huu na tabia ya ulaji ya mtoto (feeding habits).

Vinywaji vyenye sukari: Mfano kisababishi kikubwa ni watoto kunywa vinywaji vyenye sukari kwa muda mrefu na mara nyingi kwa kutumia chupa za kunyonyea (nursing bottles) ndiyo maana ugonjwa huu wakati mwingine huitwa nursing bottle caries.

Hii hujitokeza hasa kwa watoto wanaochwa na yaya zao, ambao huwapa vinywaji hivyo kila wanapohitaji au wakilia.

Pamoja na kwamba ugonjwa huu hutokana zaidi na chupa za kunyonyea lakini pia yawezekana kutokana na mama kumnyonyesha mtoto mara kwa mara au tuseme kila anapo hitaji.