Kwa uhakika ugonjwa huu wa ngozi ulinitesa sana zaidi ya mika 7. Nilipelekwa hospitali nyingi bila ya mafanikio na wakajaribu kunipima na ugonjwa haukuweza kuonekana. Baada ya kuona siponi nilienda kwa waganga wa kienyeji au wa jadi bila mafanikio, ilifika hatua nikakata tamaa.
Niliteseka sana ilifika kipindi wadogo zangu na ndugu zangu wakawa wananinyanyua na kuniweka juani na kunigeuza geuza, maana ilifika hatua siwezi kusimama wala kujigeuza kutoka na vidonda vilivyotapakaa katika mwili wangu. Ilifika kipindi inzi wakawa kelo kwangu kwani walikuwa wakinifuata kutokana na harufu mbaya niliyokuwa nayo.
Matumaini ya kupona yakaanza kupotea. Kwahiyo nikwa ni mtu wa kutolewa nje na kulazwa kwenye sponji kasha natandikiwa neti ya mbu (chandarua) mchana kwaajili ya inzi wasiguse mwili wangu. Niliumia sana na hata nikikaa kwenye kiti nje nikawa natundikiwa chandarua.
Baada ya muda baba yangu akasikia Dk. Fadhili Emily wa The Fadhaget sanitarium Clinic katika kipindi radio ya Praise Power akieleza matibabu ya magonjwa mbalimbali. Baba aliamua kunipeleka katika kituo cha The Fadhaget sanitarium Clinic Mbezi Beach hapa jijini Dar es Salaam kutibiwa. Baada ya kupata matibabu ni mwezi mmoja tu kilio change kiliweza kunyamazwa na huduma ya Dk. Fadhili Emily, niliweza kupona na sina maumivu yeyote yale.
Kupitia dawa za The Fadhaget sanitarium Clinic nimepona, na nimashukuru sana Baba yangu na Dk. Fadhili Emily kwa huduma yao juu ya maisha yangu. Uzalendo ulinishinda kwa kuwa sasa niliweza kumtembelea Dk. Fadhili Emily nyumbani kwake kwa kumshukuru kwa huduma yake, kwani amenitoa mbali
Unaweza kuangali picha zangu hapo chini.
KABLA YA KUPONA
Dada akisumbuliwa na ugonjwa wa ngozi
BAADA YA KUPONA
Dada aliyekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa ngozi akiwa huru na mateso hayo ya ngozi aliyokuwa nayo kwa muda wa zaidi ya miaka 7
Mungu ni mwema
0 comments:
Post a Comment