Karibu Fadhaget Sanitarium Clinic

Tunapenda kukukaribisha katika Kitengo cha Sayansi ya Tiba Asilia.

Kitengo Cha Sayansi Ya Tiba Asilia

Kwa Muda mrefu tumekuwa tukisaidia wengi katika matibabu na kutengeneza dawa bora kabisa kiafya.

Je Unapenda Kufahamu Jinsi Ya Kupata Mapacha?

Tunafundisha jinsi ya kupata jinsia unayotaka, jinsi ya kupata mtoto kama umekosa mtoto kwa muda mrefu. Pia hata jinsi ya kupata watoto mapacha tunaweza kukusaidia.

Tunapatikana Katika Mikoa Zaidi ya 10 Tanzania

Tunazidi kuongeza matawi yetu nchini Tanzania na Nje ya Nchi. Kwa sasa tunapatikana katika mikoa zaidi ya 10 na tunazidi kuongeza matawi yetu. Karibu sana.

Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Tuesday, May 19, 2015

DOGO AWAHENYESHA TRAFIKI JIJINI MWANZA, WANANCHI WAINGILIA KATI KUWASAIDIA



Dogo akiwakomalia trafiki mpaka wananchi wakalazimika kuingilia kati.




Trafiki kwa msaada wa wananchi wakimtia pingu dogo huyo aliyekuwa akimpa kichapo mwenzake.


...Ilibidi itumike nguvu ya ziada kumtia pingu dogo huyo.




Mbali na kupigwa pingu bado dogo huyo aliendelea kuwakomalia trafiki.


...Dogo akitaka kuzipiga na afande mbali na kutiwa pingu.

Na Idd Mumba / GPL, Mwanza

KIJANA mmoja ambaye hakufahamika jina lake jioni hii amewahenyesha Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani jijini Mwanza walioingilia ugomvi uliokua ukimuhusisha kijana huyo na mwenzake katika eneo la Posta ya Zamani.

Tukio hilo limetokea majira ya saa 10:15 jioni wakati vijana wawili walipozichapa hivyo maofisa hao wa usalama barabarani kuamua kuingilia ugomvi ili kumuokoa kijana mmoja aliyoonekana kuzidiwa na mwenzake.

Tofauti na walivyofikiria, maafande hao walitolewa kijasho na dogo huyo aliyekuwa amemzidi ubavu mwenzake huku wakipata tabu wakati wakijaribu kumtia pingu ili wampeleke kituo cha polisi.

Mbali na kuwakomalia wanausalama hao, dogo huyo pia alikuwa akiwaporomoshea matusi wakati wakijaribu kumtia nguvuni hali iliyopelekea wananchi kuingilia kati kuwasaidia polisi kumtia pingu dogo huyo.

Baada ya ushirikiano wa wananchi, polisi walifanikiwa kumpiga pingu dogo huyo na kumpeleka Kituo cha Polisi Kati huku akila kichapo cha hapa na pale.

MANISPAA YA KINONDONI YAENDELEA KUTEKELEZA AGIZO LA RAIS LA KUONDOA MAJI KWENYE MAKAZI YA WATU



Mkuu wa mkoa wa Dar es slaam,Saidi Meck Sadiki(katikati) akiangalia athari ya maji yaliyotokana na mvua kubwa zilizonyesha hivi karibuni jijini Dar es slaam akiwa ameambatana na wakazi wa eneo hilo la Kunduchi Ununio.Manispaa ya Kinondoni kwa kushirikiana na DAWASA inaendelea na zoezi la kuyaondoa maji hayo pamoja na ujenzi wa mfereji mkubwa kuelekea baharini utakaokusanya maji kutoka Bunju na Kunduchi na kuyapeleka bahari ya Hindi.

Kazi ya ujenzi wa mfereji huo mkubwa wenye urefu wa kilometa 2.1 ikiendelea katika eneo la Kunduchi Ununio.

Maji yaliyotuama yakiwa bado yamezingira nyumba na makazi ya watu eneo la Boko jijini Dar es salaam ambayo harakati za kuyaoondoa zinaendelea kufanywa na manispaa ya Kinondoni.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akizungumza na baadhi ya viongozi wa Maniapaa ya Kinondoni leo jijini Dar es salaam wakati alipotembelea kata ya Bunju na Kunduchi kujionea utekelezaji wa agizo la Rais la kujenga mfereji wa maji kuelekea baharini.

Baadhi ya wafanyakazi wa DAWASCO Kinondoni wakiendelea na zoezi la uondoaji wa maji yaliyozingira makazi ya wananchi eneo la Basihayo Tegeta leo.

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Said Meck Sadiki ( katikati ) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa manispaa ya Kinondoni Musa Nati wakati akikagua utekelezaji wa zoezi la kuondoa maji katika makazi ya watu eneo la Basihayo Tegeta.

Sehemu ya mfereji huo ikiwa katika hatua za awali eneo la Kunduchi.

Na Aron Msigwa

Maelezo, Dar es Salaam.
Manispaa ya Kinondoni inaendelelea kujenga mfereji wa kudumu wenye urefu wa Kilometa 2.1 ili kuondoa maji yaliyojaa kwenye makazi ya watu, eneo la Basihayo -Tegeta,Bunju na Kunduchi na kuyapeleka bahari ya Hindi ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais alilolitoa hivi karibuni mara baada ya kuwatembelea wananchi katika maeneo hayo walioathiriwa na mafuriko.

Akitembelea maeneo yaliyoathiriwa na mvua hizo kujionea utekelezaji wa agizo hilo leo, Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecki Sadiki amesema kazi ya ujenzi wa mfereji huo utakaogharimu kiasi cha shilingi milioni 900 inafanyika kwa kasi inayoridhisha licha ya ugumu uliopo wa kutafuta uelekeo wa maji hayo kutoakana na uwepo wa makazi ya watu.

Amesema ujenzi wa mfereji huo mkubwa unakwenda sambamba na kazi ya uondoaji wa maji ya mvua yaliyojaa katika makazi ya watu katika eneo la Basihaya inayofanywa na Shirika la maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam huku Manispaa ya Kinondoni chini ya usimamizi wa Muhandisi wake Baraka Mkuya ikiendelea na uchimbaji wa mfereji wa juu na ule utakaopita chini ardhi kuelekea baharini.

Amesema kuwa katika kuhakikisha kazi hiyo inafanyika kwa ufanisi mkubwa bila kuathiri makazi ya watu na kulazimika kulipa fidia kwa wananchi Manispaa hiyo inaendelea kuzungumza na baadhi ya wananchi ambao maeneo yao yatatumika kupitisha mfereji huo waruhusu kazi hiyo iendelee huku taratibu nyingine zikiendelea kufanyika.

Aidha amesema kwa baadhi ya wananchi waliojenga kuta na nyumba kwenye mkondo wa maji hususani eneo la Kunduchi Ununio na kuzuia maji kuelekea baharini maeneo yao yatabomolewa na baadhi ya hati za viwanja kufutwa.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Mussa Nati akizungumza mara baada ya kutembelea eneo hilo kushuhudia zoezi la uondoaji wa maji na ujenzi wa mfereji huo amesema kuwa fedha zinazotumika katika kazi hiyo zinatolewa na manispaa ya Kinondoni, na kazi hiyo itafanywa na wataalam wa Manispaa hiyo na kufafanua kuwa kukamilika kwake kutaondoa adha ya muda mrefu ya mafuriko waliyokuwa wanaipata wakazi hao kipindi cha mvua.

"Manispaa ya Kinondoni tumetenga kiasi cha shilingi 900 kwa ajili ya kufungua maji na kujenga mifereji ya kudumu inayoelekea baharini katika ili wananchi waweze kuishi bila usumbufu wowote,na kazi hii tutaimaliza ndani ya mwezi mmoja" Amesisitiza.

Naye Muhandisi wa Manispaa hiyo Baraka Mkuya amesema kuwa kazi ya uondoaji wa maji na ujenzi wa mifereji ya wazi na ile inayopita chini ya ardhi kutokea eneo la Basihayo Tegeta na kukatisha barabara ya Bagamoyo kuelekea bahari ya Hindi urefu wa kilometa 2.1 itakamilika ndani ya mwezi mmoja.

Kwa upande wao madiwani wa eneo hilo Bw.Majisafi Sharifu,Diwani wa Kata ya Bunju (CHADEMA) na Bi.Janet Lite kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) wamesema kazi ya utekelezaji wa agizo la Rais la ujenzi wa mfereji huo inakwenda na kueleza kuwa itakuwa faraja kwa wakazi wa kata hizo kutokana na adha kubwa ya mafuriko ya maji waliyokua wanaipata wakati wa msimu wa mvua.

HAKUNA LISILOWEZEKANA KWA DR. FADHILI EMILY


Monday, May 18, 2015

BABA ALIYEMBAKA BINTI YAKE WA KAMBO AKAMATWA PARAGUAY



Bw. Gilberto Benitez Zarate anayedaiwa kumbaka binti yake wa kambo na kumsababishia ujauzito.
...Akihojiwa na waandishi wa habari.
...Akipelekwa kituo cha Polisi.

Asuncion, Paraguay
GILBERTO Benitez Zarate wa Paraguay amekamatwa akishitakiwa kwa kumbaka na kumpa ujauzito binti yake wa kambo mwenye umri wa miaka 10.

Zarate aliyekamatwa baada ya kutoroka na kujificha kwa zaidi ya wiki mbili na kusababisha mgogoro mkubwa wa kitaifa kwa vile mama yake anataka ujauzito huo utolewe, alikamatwa Mei 9 mwaka huu.

Mtuhumiwa huyo mwenye umri wa miaka 42 anayekabiliwa na kifungo cha miaka 15 jela, amekana kosa hilo na kusema anasingiziwa na rafiki yake wa kike, ambaye ni mama wa binti huyo, kwa vile alimtishia kumwacha.

“Niko tayari kufanya kipimo chochote kuonyesha si mimi niliyefanya hivyo. NImetembea na wanawake kibao lakini kamwe hakuna niliyempa mimba,” alisema Zarate katika mahojiano, ambapo tukio hilo limezua mjadala mkali katika mabunge mawili ya nchi hiyo.

Utoaji mimba kwa mila za Kanisa Katoliki ni kitendo cha jinai, labda tu pale ambapo maisha ya mwanamke husika yakiwa hatarini.

Ujauzito wa msichana huo uligundulika Aprili 21 wakati mama yake alipompeleka hospitalia kiamini alikuwa na uvimbe tumboni. Mama huyo amekamatwa akiaminika alisababisha kudhalilishwa kwa binti yake huyo.

CHANZO: MTANDAO WA PULSE

DIAMOND AANZA MAANDALIZI KWA AJILI YA MTOTO WAKE WA KIKE




STAA wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' ameonyesha kuanza maandalizi kwa kijacho wake ambaye imeelezwa ni mtoto wa kike.
Diamond na mpenzi wake Zarinah Hassan 'The Boss Lady' wanatarajia mtoto wa kike mwaka huu. Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Diamond ametupia picha akiwa na kitanda cha magurudumu kwa ajili ya mtoto mchanga.

USILE ETI UNATATIZO SUGU LA KIAFYA..TUPIGIE SIMU TUTAKUSAIDIA - DR. FADHILI EMILY


MSANII BONGO MUVI ALIVYONUSA KIFO!

Mayasa Mariwata
Pole! Msanii wa sinema za Kibongo, Ummy Mohammed amenusa kifo baada ya kunusurika kwenye ajali ya Basi la Al-Saeed alilopanda akitokea mkoani Morogoro kwenda Dar ambapo ameumia mkono wa kushoto.


Msanii wa sinema za Kibongo, Ummy Mohammed akionekana na jeraha lake baada ya kunusurika katika ajali.

Akilisimulia Ijumaa Wikienda mkasa mzima, Ummy ambaye ni mwigizaji mkongwe aliyeibuka staa kwenye Sinema ya Mke Mchafu, alisema kuwa basi hilo liligongana na lori maeneo ya Mikese Morogoro na kupondeka.

Jeraha alilapata msanii wa sinema za kibongo baada ya kunusurika kwenye ajali likionekana kwa karibu.

Ummy alisema kilichosababisha ajali hiyo ni kutokana na mwendo kasi wa basi hilo ambapo abiria wengi walipata majeraha akiwemo yeye.

Basi ambalo alipata nalo ajali msanii wa sinema za kibongo Ummy Mohammed.

“Kwa jinsi ile ajali ilivyokuwa sikutegemea kabisa kama ningenusurika kifo, nilikuwa nasali sala ya mwisho, namshukuru Mungu nimeambulia jeraha la mkono japokuwa ninapata maumivu makali ya mwili,” alisema Ummy.