Karibu Fadhaget Sanitarium Clinic

Tunapenda kukukaribisha katika Kitengo cha Sayansi ya Tiba Asilia.

Kitengo Cha Sayansi Ya Tiba Asilia

Kwa Muda mrefu tumekuwa tukisaidia wengi katika matibabu na kutengeneza dawa bora kabisa kiafya.

Je Unapenda Kufahamu Jinsi Ya Kupata Mapacha?

Tunafundisha jinsi ya kupata jinsia unayotaka, jinsi ya kupata mtoto kama umekosa mtoto kwa muda mrefu. Pia hata jinsi ya kupata watoto mapacha tunaweza kukusaidia.

Tunapatikana Katika Mikoa Zaidi ya 10 Tanzania

Tunazidi kuongeza matawi yetu nchini Tanzania na Nje ya Nchi. Kwa sasa tunapatikana katika mikoa zaidi ya 10 na tunazidi kuongeza matawi yetu. Karibu sana.

Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Wednesday, March 18, 2015

MIMEA INAYOSAIDIA KUONDOA TATIZO LA HEDHI NDOGO KUPITA KIASI


Leo tutazungumzia ni mimea gani ambayo inaweza kumsaidia mwanamke hapohapo nyumbani kuweza kuondoa matatizo ya hedhi na kuondokana na adha za hapa na pale ambazo zinaweza kumsumbua kwa muda mrefu hata kumhangaisha sana katika harakati yake na mume wake kwenye kuijenga familia yake.

Hivyo basi tutaangalia tatizo hili la hedhi ndogo kupita kiasi likoje kitaalamu na baadaye tutaangalia ni jinsi gani tunaweza kuliondoa kwa kutumia mimea ya kawaida hapo nyumbani.

Kwa kawaida mwanamke anaingia hedhi kwa siku zisizozidi saba na hedhi yake ikawa ya kawaida na yenye mtiririko unaoeleweka, lakini hedhi ikitoka kidogo sana kwa mwanamke na ikawa inatoka leo, anakaa siku moja inatoka kidogo tena, na baadaye inakata ujue ni tatizo na kama mwanamke anatokewa na hali kama hii na anaona ni jambo la kawaida basi kuanzia sasa ajue kuwa hili ni tatizo na kama halitatibiwa kwa haraka linaweza kusababisha mwanamke akapatwa na Amenorrhea ambayo itamsababishia ugumba.

Japokuwa ni muhimu tufahamu kwamba ugumba siyo kilema kwani una vyanzo, dalili (kama kutokwa na uchafu mithili ya maziwa mtindi, kukosa hedhi, maumivu ya kiuno na mgongo na pia chini ya kitovu, maumivu wakati wa tendo, kurudi nje kwa mbegu za mwanaume, nk) na ni muhimu kuelewa kuwa ugumba unatibika.
Amenorrhea ni ile hali ya mwanamke kutokupata hedhi kwa muda mrefu na wakati huohuo mwanamke huyu yuko kwenye umri wa balehe na si mjamzito.

DALILI ZAKE NI ZIPI?
Dalili za ugonjwa huu (Oligomenorrhea) ni kama;
Kupata hedhi iliyo ndogo sana.
Kupata hedhi iliyo nyepesi sana.
Kuwa na mzunguko unaozidi siku 35.

VISABABISHI VYAKE NI VIPI?
Ugonjwa huu husababishwa na mambo yafuatayo;
Mwanamke kuwa na msongo mkubwa wa mawazo (stress).
(b) Kuvurugika kwa homoni.
(c) Mwanamke mwenye matatizo ya sukari (diabetes).
Kufanya mazoezi sana.
Matatizo mbalimbali kwenye mji wa mimba (uterus).
Kupungua sana kwa uzito kwa mwanamke.
Matatizo mbalimbali kwenye vifuko vya mayai (mfano, Polycystic Ovary Syndrome {PCOS})

HUDUMA YA KWANZA IKOJE?
Kwa mwanamke mwenye tatizo hili ni vizuri akachukua maji ya moto, aweke kwenye chupa na aweke chupa hiyo maeneo ya chini ya kitovu wakati wa hedhi.

MAAMBUKIZI YA FANGASI SEHEMU ZA SIRI -2




WIKI iliyopita tulieleza matatizo ya fangasi sehemu za siri na jinsi wanavyowasumbua waliokumbwa na maradhi haya, tunaeleza ni wanawake gani hupatwa na tatizo hili. Leo tunaendelea kuwaelimisha na tunaanza kufafanua wale wanaopatwa na ugonjwa huu, endelea:

Wengine wanaopatwa na fangasi hawa sehemu za siri ni wale wanaotumia sana dawa za kuua bakteria (antibiotics, steroids) ambazo zina tabia ya kushusha kinga ya mwili.Mabadiliko ya mfumo wa homoni mwilini kwa mwanamke husababisha mabadiliko katika sehemu za siri na hivyo kufanya kuwepo kwa ukuaji wa kasi wa fangasi hawa.

Ujauzito (kutokana na kubadilika kwa mfumo wa homoni mwilini na kupungua kwa kinga ya mwili) huweza kusababisha mtu kuwa na fangasi hawa. Hata hivyo, ieleweke hapa kuwa si kila mjamzito hupatwa na maambukizi haya.

Matumizi ya dawa za kupanga uzazi (vidonge vya majira) au mtu kuwa na upungufu wa kinga mwilini kutokana na magonjwa sugu kama kisukari, saratani aina yoyote ile, ugonjwa aina ya Mononucleosis na nk, husababisha mtu kupata maambukizi ya fangasi hawa.

Wengine wanaoweza kuambukizwa fangasi hawa ni wale wenye ugonjwa wa Ukimwi (HIV/AIDS), wanaopata matibabu ya homoni (hormonal replacement therapy) kutokana na sababu mbalimbali au wenye matibabu ya kusaidia kushika mimba kwa wale wenye matatizo ya uzazi (infertility treatment), wenye utapia mlo (malnutrition), wenye kuvaa nguo au mavazi yanayoleta joto sana sehemu za siri kwa muda mrefu kama nguo za kuogelea (swimwear), nguo za ndani (chupi) zilizotengenezwa kwa kitambaa aina ya nailoni, nguo za ndani zinazobana sana n.k.

Au wale wanaojamiiana kwa njia ya kawaida mara tu baada ya kujamiana kupitia njia ya haja kubwa (anal sex) au matumizi ya vilainishi vyenye glycerin wakati wa kujamiana pia yamehusishwa na maambukizi haya.
Wanawake wenye umri wa miaka kati ya ishirini na thelathini wapo kwenye hatari kubwa ya kupata maambukizi haya wakati wale ambao wameshaacha kupata hedhi au wale ambao hawajaanza kupata hedhi kabisa hawako kwenye hatari kubwa.

LUNGI ADAIWA KUTUPIWA JINI, APOOZA

Hamida Hassan
NYOTA wa filamu za Kibongo Lungi Maulanga hivi karibuni anadaiwa kutupiwa jini na wabaya wake wakiwemo wanafamilia yake kitendo kilichosababisha apooze upande mmoja wa mwili wake.


Nyota wa filamu za Kibongo Lungi Maulanga.

Chanzo makini kinasema hofu yao kubwa ni kuwa kitendo hicho kilifanywa na baadhi ya ndugu zake kufuatia tofauti zao za kifamilia zilizosababisha kufikishana mahakamani.

“Katika shauri hilo mahakamani, yeye alishinda, sasa baada ya siku mbili akaanguka na kupoteza fahamu, alipozinduka akajikuta amepooza upande wa kulia, watu wanaunganisha tukio hilo na kesi ya mahakamani,” kilisema chanzo.

Gazeti hili lilimkuta Lungi akiwa amelala nyumbani kwake na alikiri kuanguka na kupooza na kwamba hawezi kutembea vizuri lakini anamtumaini Mungu kuwa hali yake itakaa vizuri kwani hana imani na mambo ya kishirikina.

DOKTA: SHILOLE MGONJWA!

Shani Ramadhani na Chande Abdallah
DAKTARI mmoja bingwa wa saikolojia, Erick Mutchumbh, amesema tabia zinazofanywa na nyota wa muziki, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ zinaashiria kuwa ni mgonjwa aliyeathirika kisaikolojia na matatizo ya unyanyaswaji wakati wa utoto wake.


Nyota wa muziki, Zuwena Mohamed ‘Shilole’.

Mutchumbh alitoa maelezo hayo baada ya kuombwa kuzungumzia tabia za Shilole za kugombana mara kwa mara na mpenzi wake, Nuh Mziwanda, kama zinaweza kuwa ni tatizo la kisaikolojia linalomsumbua mmoja wao au ni ugomvi wa kawaida wa kimapenzi.

“Mtu yeyote aliyepitia matatizo hasa unyanyasaji akiwa mtoto ‘child abuse’ iwe kunyanyaswa kwa kubakwa, kupigwa, kunyimwa chakula au mateso ya aina hiyo, akikua bila kupata tiba ya kisaikolojia huwa na tatizo kubwa kwa miaka mingi akiwa mtu mzima.

“Miongoni mwa matatizo hayo ni pamoja na kupenda kujitenga, hasira za karibu, tabia za ajabu na kubwa zaidi ni kumfanyia mtu mwingine hasa mtoto ukatili aliofanyiwa yeye kitaalamu wanaita ‘Propensity Victimization,’” alisema daktari huyo.


Nuhu Mziwanda.

Alisema katika nchi zilizoendelea, tatizo hilo hupewa kipaumbele katika matibabu kuliko ilivyo kwa nchi nyingi za kiafrika kwani madhara yake huwa ni pamoja na mwathirika kuamua kujinyonga au kuua.

Kwa maelezo hayo, mengi yanaonekana kufanana na matukio yaliyowahi kumkuta Shilole, kwani akiwa na umri wa miaka 14, aliwahi kubakwa, pia anatajwa kujihusisha kimapenzi na watu wenye umri mkubwa, ikiwa ni pamoja na kufanya kazi ngumu katika umri mdogo.

USIOMBE YAKUKUTE YALIYOMTOKEA MREMBO HUYU

 Issa Mnally
MAMBO mengine ni ya kuyasikia yakiwatokea wenzako na usiombe yakakukuta kama ilivyomtokea msichana huyu ambaye hakufahamika jina lake mara moja baada ya kuchukua kipigo ‘hevi’ ambacho nusura apoteze maisha yake, maeneo ya Sinza Afrikasana, juzi Jumatatu.

Dada huyo akilia baada ya kupokea kichapo kikali.

Mashuhuda wa tukio hilo wanasema, binti huyo akiwa na mwanaume mmoja, walionekana wakitoka katika baa iitwayo Kona, wakiongozana hadi kwenye baa nyingine iliyo maeneo ya Afrikasana ambako waliendelea na kinywaji.

“Yule msichana ni mmoja wa wanaojiuza pale Kona, nadhani walikuwa na makubaliano ambayo wamefikia, maana walikuwa wakinywa kwa raha zao, ghafla tukasikia wanaanza kuzozana, jamaa alikuwa anataka waondoke, bibie akawa analeta longolongo,” alisema dada mmoja aliyekuwa eneo la tukio.


Wasamalia wema wakimsaidia.

Inadaiwa kuwa dada huyo alianza kupiga yowe akitaka apewe kiasi cha shilingi 30,000, ndipo mwanaume huyo ambaye alitoweka haraka, alipoamua kumpa kipigo kikali kiasi cha kumpasua kichwani na kumsababishia maumivu makali.


Akiwa amelala.

Baada ya kupokea kipigo hicho, baadhi ya wahuni walifika eneo hilo na kuendelea kumfanyia vitendo vya kidhalilishaji hadi akina mama wa eneo hilo walipoamua kumhifadhi kwa kumfunika kanga, lakini katika hali ya kushangaza, msichana huyo alipitiwa na usingizi mzito.Kuona hivyo, majirani hao waliamua kumpeleka polisi ambako hata hivyo alifukuzwa kwa kile kilichodaiwa kuwa ni mlevi.

Tuesday, March 17, 2015

YEMI ATANGAZA SIKU YA KUZIKWA BABA YAKE



Baba yake Yemi Alade aliyekuwa Kamishna Mstaafu wa Polisi, J.A. Alade enzi za uhai wake.

MWANAMUZIKI wa kike wa Nigeria, Yemi Alade, na familia yake watafanya maziko ya marehemu baba yake tarehe 7 na 8 Mei mwaka huu.

Baba yake Alade aliuyekuwa Kamishna Mstaafu wa Polisi, J.A. Alade, alifariki Januari 16 mwaka huu na binti yake huyo ambaye ni mtunzi wa wimbo maarufu wa ‘Johnny’, hajasema mengi kuhusiana na kifo hicho tangu kitokee.
Mwanamziki wa kike wa Nigeria anayetamba kwa wimbo wa Jonny, Yemi Aladeakiwa katika pozi.

Ni katika mahojiano ya gazeti la Tribune yaliyofanyika Machi 13, mwaka huu (siku ya kuzaliwa kwake) ndipo aliposema maziko ya baba yake yatafanyika Mei 7 na 8.

Yemi Alade ni mtoto wa mwisho kwa baba yake huyo kutoka kabila la Wayoruba na mama kutoka kabila la Waigbo.

MADAI: AK47 ALIPIGWA KABLA YA KIFO CHAKE



Mwili wa AK47 ukitolewa katika mochwari ya Hospitali ya Nsambya.

WAKATI wapenzi wa muziki nchini Uganda wakiwa bado wamegubikwa na simanzi kwa kuondokewa na mwanamuziki wa miondoko ya dancehall, Emmanuel Mayanja maarufu kwa jina la AK47, taarifa mpya zimeibuka kuwa kuna uwezekano kuwa alipigwa kabla ya kifo chake.


Jose Chameleon (katikati) akiwa na simanzi baada ya kuondokewa na mdogo wake.

AK47 amefariki dunia usiku wa kuamkia leo akiwa hospitali baada ya kuanguka akiwa bafuni.

Taarifa hizo zinadai kuwa atakuwa alipigwa katika baa aliyokuwemo iitwayo Dejavu, iliyopo eneo la Kabalagala kabla ya kupelekwa Hospitali ya Nsambya, Kampala ambapo mauti yalimkuta.

Baa hiyo inamilikiwa na Jeff Kiwanuka, aliyekuwa meneja wa wasanii wawili Radio na Weasel.


Pallaso (mwenye tisheti ya bluu) ambaye naye ni kaka wa marehemu akifarijiwa na mwanamuziki Bebe Cool.

Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Kabalagala, Nusulah Kemigisha ameeleza kuwa anahisi kuna mchezo mchafu umechezwa baada ya kukuta mwili wa marehemu ukiwa na majeraha sehemu za kifua na kuamua kufunga baa hiyo ili kuruhusu uchunguzi ambao bado unaendelea mpaka sasa.


Marehemu AK47 enzi za uhai wake.

Imeelezwa kuwa AK47, ambaye ni mdogo wa mwanamuziki nguli wa Uganda, Jose Chameleon (Joseph Mayanja), alipigwa na kuamua kwenda bafuni kunawa kabla ya kudaiwa kuteleza na kuanguka.

MAJONZI, VILIO NA SIMANZI VYATAWALA MAZISHI YA SYLVESTRE MARSH JIJINI MWANZA


MAJONZI, vilio na simanzi vimetawala wakati kocha wa zamani wa timu ya Taifa 'Taifa Stars', Sylvestre Marsh alipokuwa akiagwa leo na kisha kuzikwa katika makaburi ya Igoma, Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza.

Kocha Marsh alifariki dunia Jumamosi iliyopita katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa amelazwa akitokea Mwanza baada ya hali yake kuwa mbaya.

Mamia ya watu wakiwemo viongozi wa kiserikali, wadau wa soka, wanasoka na mashabiki wamehudhuria mazishi hayo yaliyoanzia katika Uwanja wa Shule ya Msingi Milongo ambapo marehemu Marsh na vijana wake walikuwa wakifanyia mazoezi.

Zoezi la kuaga mwili wa marehemu lilianza asubuhi katika uwanja huo baada ya mwili kuwasili kutoka katika Hospitali ya Seketule ulipokuwa umehifadhiwa.

Vijana waliokuwa wakifundishwa na Marsh katika Kituo cha soka cha Marsh Academy ndiyo waliopewa jukumu la kubeba jeneza la mwalimu wao.

Wanasoka wa zamani akiwemo Edibily Jonas Lunyamila na Fumo Felician ambao waliwahi kucheza soka na marehemu kabla ya kuwa kocha walimwaga machozi wakati wa zoezi la kumuaga mwenzao.

Wasanii wakiwemo Steve Nyerere na H-Baba nao wameungana na waombolezaji kumuaga mwalimu Marsh.

Sylvestre Marsh aliyezaliwa miaka 55 iliyopita, licha ya kuwa kocha msaidizi wa Taifa Stars tangu enzi za Marcio Maximo hadi Kim Poulsen, pia aliwahi kuwa kocha wa timu kadhaa zikiwemo Azam FC na Kagera Sugar.
Jeneza lenye mwili wa marehemu Sylvestre Marsh likiingizwa kaburini kwenye makaburi ya Igoma, mkoani Mwanza.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo akiaga mwili wa marehemu Marsh.

Vijana walio katika Kituo cha soka cha Marsh Academy kilichokuwa kikiongozwa na marehemu wakishusha jeneza la mwalimu wao kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Milongo tayari kwa kuaga.


Mke wa marehemu (wa pili kushoto) akilia kwa simanzi. Wa kwanza kushoto ni binti wa marehemu aitwaye Anna Marsh na kijana wake Wyne Marsh (wa tatu kushoto).

Wadau mbalimbali wa soka wakiwemo viongozi wa serikali wakishiriki kumuaga marehemu Marsh.

Mmoja wa wadhamini wa kituo cha marehemu kutoka nchini Ujerumani akitoa salamu za rambirambi.

Nahodha wa timu ya vijana ya U-16 katika kituo cha marehemu akisoma historia ya Academy yao.

...Nahodha huyo akikakabidhi historia hiyo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo.

Sehemu ya waombolezaji waliohudhuria zoezi hilo.

(PICHA ZOTE NA JOHNSON JAMES / GPL, MWANZA)

MWANAFUNZI ATEKWA, AUAWA

Na Waandishi Wetu
DUNIA imekwisha jamani! Mwanafunzi wa kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari ya Mabibo, Dar, Irene Said (15) ametekwa, amebakwa na kuuawa kikatili kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali sehemu mbalimbali za mwili huku ikidaiwa kuwa, kijana mmoja asiyejulikana alifika nyumbani kwao, Kigogo Luhanga na kutaka kiroba na mtu mmoja waongozane akabebe ndizi.

Polisi wakiwa wamebeba mwili wa marehemu.

Akizungumzia tukio hilo la kusikitisha sana, mama mdogo wa marehemu, Doto Lucas alisema:
“Siku ya tukio ambayo ni Alhamisi iliyopita (Machi 12), kijana mmoja ambaye hakuna aliyemfahamu alikuja hapa nyumbani na kumtaka mtu mmoja na kiroba ili akachukue ndizi ambazo kuna mtu aliagiza ziletwe.

“Marehemu ndiye aliyekuwa karibu akijisomea baada ya kutoka shuleni. Mtu mkubwa aliyekuwa nyumbani muda huo ni bibi wa marehemu ambaye ni mtu mzima hivyo alimwambia Irene aongozane na mtu huyo akachukue mzigo akijua uko jirani kwa mujibu wa mtu huyo.

“Baada ya muda, yule kijana alirudi akiwa peke yake na kusema anataka chombo kingine cha kubebea kwa kuwa kile kiroba kilikuwa hakitoshi.“Bibi mtu alimuonesha ndoo kwa vile hakukuwa na kiroba kingine, alipoitwaa na kuondoka nayo ndiyo hakurudi yeye wala Irene.Wanafunzi wenzake wakiwa na majonzi msibani.

“Baada ya kuona muda unayoyoma bibi wa marehemu alianza kupata wasiwasi. Ndipo akatutaarifu kilichotokea nyumbani na sisi tukaanza kumsaka Irene na kijana yule.”

KWA NINI WALIMWAMINI KIJANA HUYO?
“Sisi tuna makaka zetu wakubwa ambao wana kawaida ya kutuagizia mizigo mbalimbali kwenye magari, kwa hiyo tuliamini ni wao. Lakini tulipowapigia simu na kuwaeleza tukio hilo wote walikanusha kuwa si wao na kushangaa.

“Kauli hiyo ilianza kututia shaka zaidi hivyo tulianza kuwasiliana na ndugu na jamaa ambao wote waliishia kushangaa. Tukaenda kutoa taarifa Kituo cha Polisi, Kigogo na kuanza msako wa kumsaka binti yetu pamoja na mtuhumiwa.”
Gari la polisi likiwa eneo la tukio.

IRENE APATIKANA AKIWA AMEUAWA
Mwanamke huyo anaendelea kusimulia: “Kesho yake asubuhi (Ijumaa) tukasikia kuna binti amekutwa ameuawa kinyama kwenye Bonde la Mto Msimbazi, eneo la Sukita. Tulipatwa na mshituko, tukaenda na kuukuta mwili, tulipoukagua tuligundua ni Irene.

“Alikuwa ameharibiwa vibaya. Sehemu za mwii alikuwa na damu, alichomwa na kitu chenye ncha kali. Kwa vyovyote yule kijana alikuwa na wenzake, walimteka huko mbele ya safari na kumbaka kabla ya kumuua. Inauma sana jamani.”

Marehemu Irene ambaye katika mazishi yake wanafunzi wenzake walikuwa wakilia sana, alizikwa Jumamosi iliyopita katika Makaburi ya Mburahati, Dar.


Wanafunzi wenzake wakiaga mwili wa mpendwa wao.

Katika ibada hiyo, Katekista aliyesaidiana na paroko kuendesha ibada hiyo aliyetajwa kwa jina moja la Henjewele aliwalaani vikali walioshiriki kufanya unyama huo na kuwataka wafanye toba haraka iwezekanavyo na kumrudia Mungu wao vinginevyo laana na moto wa milele utawaangukia.
Mungu ailaze roho ya marehemu Irene mahali pema peponi- Amina.

Imeandikwa na Richard Bukos, Makongoro Oging’ na Haruni Sanchawa.

MTOTO ALIYENUSURIKA KWA MKONO WA MUNGU! AJALI YA KONTENA MAFINGA

Na Mwandishi Wetu, Iringa
BADO Mji wa Mafinga wilayani Mufindi mkoani hapa haujakaa sawa kufuatia vifo vya watu 50 waliopoteza maisha kwa ajali ya kontena kudondokea Basi la Majinja lenye namba za usajili T 438 CED iliyotokea Machi 11, 2015, Uwazi limechimba.

Mtoto aliyenusurika kwenye ajali.

Ajali hiyo ilitokea maeneo ya Changarawe mjini Mafinga ambapo kontena hilo lilikuwa kwenye lori la mizigo la Scania lenye namba za usajili T 689 APJ mali ya Kampuni ya Cipex lililokuwa likitokea Dar kwenda Mbeya huku basi hilo likitokea Mbeya kuelekea Dar.

KILICHOTOKEA BAADA YA AJALI
Kilichotokea baada ya ajali hiyo ni kuonekana kwa Mkono wa Mungu ambapo mtoto anayekadiriwa kuwa na umri wa mwaka mmoja mpaka miwili kunusurika katika ajali hiyo huku watu 50 wakipoteza maisha.
“Mimi naweza kusema ni Mkono wa Mungu kwa sababu, yule mtoto alikutwa hajaumia popote lakini wazazi wake wakiwa wamepoteza maisha. Huoni kama ni uwezo wa Mungu mwenyewe?” alisema askari polisi mmoja aliyekuwa miongoni mwa waliokuwa wakisimamia zoezi la uokoaji.

WAZAZI WA MTOTO
Akisimulia ilivyokuwa kwa wazazi wa mtoto huyo ambaye jina lake halijajulikana, mmoja wa abiria walionusurika, Aidan alisema kuwa, kabla ya kuanza safari jijini Mbeya, mtoto huyo alibebwa na mama yake akiwa ameongozana na abiria wengine.

Muonekano wa kontena lililosababisha ajali hiyo.

“Wazazi wa mtoto waliingia na kukaa siti ya tatu tu kutoka kwa dereva. Hakuna aliyehisi kwamba mbele ya safari kuna janga kubwa kama hili.“Basi lilianza safari, kila abiria alikuwa akizungumza na mwenzake, wengine walikuwa wakiongea na simu. Wapo waliokuwa wakichati, nadhani ni wale wanaotumia WhatsApp. Kumbe bwana shetani alikuwa anatembea na sisi,” alisema abiria huyo akiwa kwenye Hospitali ya Wilaya ya Mufindi.

KABLA YA AJALI
Kwa mujibu wa majeruhi mwingine wa ajali hiyo, baada ya kufika eneo la Changarawe, kwa mbele lilionekana lori hilo likiwa katika mwendo wa kawaida na hakuna aliyewaza kwamba litaangukia basi lao.

“Mbele tuliliona lile lori likija, lakini mimi nimekuwa nikisafiri mara kwa mara kwa kutumia barabara hiyo. Najua eneo hilo lina shimo lakini sikuwa na wazo kwamba shimo lile litakuwa mtoa roho wa abiria wa basi letu.
“Wakati tunapishana sasa, lori linapita kulia kwetu, mimi nilikaa siti ya nyuma upande wa abiria. Ghafla nilishtuka kuona kama giza linatanda upande wa dereva, mara nikasikia watu wakianza kulia.

“Kabla sijajua ni nini, nikasikia kishindo kikuu. Puuu! Abiria wengine walisikika wakisema wanakufa, wengine wakiwa kimya! Ndipo nikajua tumeangukiwa na kontena lakini sikuweza kufuatilia ilikuaje kwani akili zikawa kama zimeniruka,” alisema abiria huyo bila kutaja jina lake.


Mabaki ya basi la Majinja baada ya ajali.

KILICHOMTOKEA MTOTO HUYO
Baadhi ya waokoaji waliofika mapema mara baada ya ajali hiyo waliliambia Uwazi kwamba, wakati wanahangaika kuitoa miili ya majeruhi na marehemu, walishangaa kumkuta mtoto huyo akiwa chini ya siti ya nyuma kabisa maarufu kwa jina la ‘kwa balozi’, akiwa hana michubuko.

“Baadhi ya abiria walionusurika wakatuambia huyu mtoto alikaa na wazazi wake kwenye siti ya tatu kutoka kwa dereva. Sasa amefikaje kule nyuma kwa balozi? Nadhani anayejua ni Mungu.“Unajua watoto wadogo wana mkono unaowalinda. Mara nyingi katika ajali wao wanasalimika kwa njia ya ajabu sana,” alisema askari mmoja wakati wa uokoaji.

Picha ya mtoto huyo ilipigwa na mpiga picha Francis Godwin kwenye Wadi Namba 3 kwa kusaidiwa maelekezo na polisi wa kike na muuguzi mmoja aliyekuwa na orodha ya watu walionusurika. Watu wengine wawili kitandani hapo walikuwa ni wasamaria wema waliokuwa wakimsaidia mtoto huyo ambapo wazazi wake wanasadikiwa walipoteza maisha.

Polisi wakiwa eneo la tukio.

MGANGA MKUU NA MKUU WA MKOA
Juzi, Uwazi lilizungumza na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Salimin Mahimbo kuhusu ajali hiyo ambapo alisema mpaka sasa, majeruhi waliolazwa ni saba baada ya mmoja kufariki dunia na majeruhi mwingine kupelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kutokana na hali yake kuzidi kuwa mbaya.

“Mpaka sasa tuna majeruhi saba tu, mmoja alifariki dunia. Mmoja amekimbizwa Muhimbili kwa matibabu zaidi, hali yake si nzuri, hawa saba wanaendelea vizuri,” alisema Mahimbo.Naye Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza alisema mpaka juzi, marehemu wote walishatambuliwa na ndugu zao na waliolazwa wametambuliwa pia.