Karibu Fadhaget Sanitarium Clinic

Tunapenda kukukaribisha katika Kitengo cha Sayansi ya Tiba Asilia.

Kitengo Cha Sayansi Ya Tiba Asilia

Kwa Muda mrefu tumekuwa tukisaidia wengi katika matibabu na kutengeneza dawa bora kabisa kiafya.

Je Unapenda Kufahamu Jinsi Ya Kupata Mapacha?

Tunafundisha jinsi ya kupata jinsia unayotaka, jinsi ya kupata mtoto kama umekosa mtoto kwa muda mrefu. Pia hata jinsi ya kupata watoto mapacha tunaweza kukusaidia.

Tunapatikana Katika Mikoa Zaidi ya 10 Tanzania

Tunazidi kuongeza matawi yetu nchini Tanzania na Nje ya Nchi. Kwa sasa tunapatikana katika mikoa zaidi ya 10 na tunazidi kuongeza matawi yetu. Karibu sana.

Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Friday, June 12, 2015

NISHA, SAJENTI WAWACHANA MASTAA KUCHAGUA MSIBA


Msanii wa Filamu za Kibongo, Salma Jabu ‘Nisha’.

Gabriel Ng’osha na Gladness Mallya
Wasanii wa Filamu za Kibongo, Salma Jabu ‘Nisha’ na Husna Idd ‘Sajenti’ hivi karibuni wamewachana wasanii wenzao kuwa ni watu wa kuchagua misiba.

Wasanii hao waliongea hayo walipokuwa kwenye msiba wa msanii aliyewahi kutamba na Tamthiliya ya Jumba la Dhahabu, Mzee Kankaa aliyefariki dunia siku ya Jumanne nyumbani kwake Tandale jijini Dar.


Husna Idd ‘Sajenti’.

Nisha alisema: “Wasanii tunapaswa kuwa na ushirikiano katika shida na raha, hasa kwenye misiba ya wenzetu, leo yeye kesho mimi, au wewe. Tuache kuchagua misiba siyo ubinadamu.’’

Sajenti naye alishadadia: “Haipendezi kuona wasanii tunapendana wakati wa uzima tu, mwenzetu anapofariki hatujitokezi kumsindikiza kwenye safari yake ya mwisho, tunaishia kuangalia aliyekufa ni nani ana mashabiki kiasi gani.”

P FUNK MAJANI, SARAHA MVUNGI NA AMBWENE KUMSAPOTI FLORA MBASHA JUMAPILI..USIKOSE




Tuesday, June 9, 2015

WATOTO WANUFAIKA NA DAWA MPYA ZA ARV

Dawa mpya za ARV kwa watoto ambazo azina ladha kama za zamani

Watoto walioathirika na Virusi vya Ukimwi watanufaika kutokana na uamuzi wa mamlaka ya Chakula na Dawa ya Marekani kuidhinisha dawa mpya ambazo zinaweza kuchanganywa kwenye Chakula ili kuwarahisishia matumizi watoto wanaoishi na virusi vya ukimwi.Shirika la Umoja wa Mataifa la kushughulikia Ugonjwa wa Ukimwi ,UNAIDS na Shirika linalohudumia watoto duniani, UNICEF yameeleza.
Mkurugenzi mtendaji wa UNAIDS, Michel Sidibe' amesema kuwa dawa hizi ni mbadala wa zile ambazo zilikuwa hazifurahiwi na watoto, zenye ladha mbaya.Dawa hizi zitawawezesha watoto kuzidi kupata tiba nzuri na kuwafanya watoto wawe na afya, amesema haikubaliki kuwa asilimia 24 pekee ya watoto walioathirika wapate dawa za kupunguza makali.
Dawa hizi zimetengenezwa nchini India, zina viambata vya Lopinavir na ritonavir ambazo zinaweza kuchanganywa kwenye chakula cha mtoto.Dawa hizi haziharibiwi na joto la chakula na zina ladha nzuri kuliko zinazopatikana sasa, vidonge hivi vinafaa kwa matibabu kwa watoto.
Hii ni hatua mpya katika mipango ya kuokoa maisha ya Watoto waishio na virusi vya ukimwi, Mkurugenzi wa Mradi wa Ukimwi wa UNICEF,Craig McClure amesema '' tunatarajia kuimarisha upatikanaji wa matibabu kwa ajili ya watoto wengi zaidi na kuunga mkono mpango wa kuwafikia watoto wasiopata huduma hii duniani kote''.
Na: Lonely Nzali                                                                               Chanzo: BBC SWAHILI                                                                           

Sunday, June 7, 2015

THE FADHAGET SANITARIUM CLINIC WADHAMINI TAMASHA LA FLORA MBASHA


MBUNGE EUGENE MWAPOSA AZIKWA UKONGA DAR



Sehemu ya waombolezaji waliofika nyumbani kwa marehemu Eugene Mwaiposa huko Ukonga Dar.


Katikati ni mume wa marehemu, Ally Mwaiposa, mtoto wao Salimila Mwaiposa (kushoto) na Mektrida Mwaiposa (kulia).


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda, akisalimia waombolezaji wakati alipofika nyumbani wa marehemu Eugene jana.


...Akimfariji mume wa marehemu, Ally Mwaiposa.


Spika wa bunge la Tanzania Anna Makinda akisaini katika kitabu cha maombolezo jana.


Askofu Msaidizi wa Kanisa la la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Chediel Lwiza (kushoto) akitoa ibada fupi ya kumwombea marehemu.


Baadhi ya watu waliosoma na marehemu nje ya Tanzania wakisoma risala ya maombolezo.


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick (kushoto), Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal (katikati) na Anne Makinda wakiwa katika maombolezo.


Baadhi ya waombolezaji waliofika mazishini.


Viongozi mbalimbali wa serikali wakiwa msibani.

MAKAMU wa Rais, Dk. Gharib Bilal, jana aliongoza mazishi ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Eugene Mwaiposa, huko Ukonga Kipunguni ‘A’ Matembele jijini Dar es Salaam ambako simanzi na vilio vilitawala miongoni mwa umati uliohudhuria huko akiwemo Waziri wa Serikali za Mitaa, Hawa Ghasia; Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Makongoro Mahanga na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda,.

PICHA STORI: DENIS MTIMA NA HARUN SANCHAWA/GPL

Saturday, June 6, 2015

THE FADHAGET SANITARIUM CLINIC NI MOJA YA KAMPUNI KUBWA ILIWEZA KUDHAMINI TAMASHA LA FLORA MBASHA

Eneo: Ubungo Plaza - Dar es Salaam Tanzania
KARIBU SANA

WASTARA: ‘ALIYENIONJA’ AJITOKEZE

Brighton masalu
VUNJA ukimya! Baada ya kuhusishwa kwa muda mrefu na fununu za kutembea na wanaume kadhaa tangu kufariki kwa aliyekuwa mumewe, Juma Kilowoko ‘Sajuki’, msanii wa filamu Bongo, Wastara Juma hatimaye amefunguka na kujiapiza kwa kulamba kidole, kuchovya mchanga na kukipitisha shingoni akidai tangu kuondoka kwa Sajuki hajawahi ‘kuchangia shuka’ na mwanaume yeyote na kama yupo, ajitokeze hadharani!


Msanii wa filamu Bongo, Wastara Juma.

‘Akibadilishana sentensi’ na ‘kiruka’ njia wetu kwa njia ya simu hivi karibuni, Wastara ambaye bado anafanya vyema kwenye sanaa, alishutumu na kuonekana kuchukizwa vikali na tetesi juu yake akihusishwa na wanaume kadhaa akiwemo msanii mwenzake, Bond Bin Suleiman.

“Nashangazwa sana na wanaoeneza uvumi wa mimi kutembea na wanaume wengi baada ya kifo cha mume wangu, kwani mimi sina haki kama mwanamke jamani? Kama kuna mwanaume mwenye uthibitisho wa kutembea na mimi si ajitokeze!” alisema Wastara huku akiashiria jazba.

RED CARPET KATIKA TAMASHA LA FLORA MBASHA UBUNGO PLAZA


MSAFARA WA MAKONGORO NYERERE WAPATA AJALI KASULU - KIGOMA


Gari lilivyopata ajali.

Wananchi wa Kasulu na Jeshi la Polisi wakiwa katika eneo la tukio.

MSAFARA wa Makongoro Nyerere ambaye ni miongoni mwa wagombea urais, umepata ajali ya kupinduka kwa gari wilayani Kasulu mkoani Kigoma leo.

Ajali hiyo imetokea wakati Makongoro na msafara wake walipokuwa wakitoka mkoani Geita kuelekea Kigoma ikiwa ni katika harakati za kusaka wadhamini wake watakaomuwezesha kujaza fomu kuwania urais.

Taarifa zinasema kuwa, majeruhi wa ajali hiyo wamepelekwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kasulu kwa ajili ya matibabu.

Akizungumza na Mtandao huu kwa njia ya simu, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Jafary Mohamed amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema Jeshi la Polisi Mkoani humo litatoa taarifa kamili baadaye, baada ya uchunguzi wa awali kukamilika.

MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI TANZANIA GLORY MAINAH ADHAMINI TAMASHA LA FLORA MBASHA