Karibu Fadhaget Sanitarium Clinic

Tunapenda kukukaribisha katika Kitengo cha Sayansi ya Tiba Asilia.

Kitengo Cha Sayansi Ya Tiba Asilia

Kwa Muda mrefu tumekuwa tukisaidia wengi katika matibabu na kutengeneza dawa bora kabisa kiafya.

Je Unapenda Kufahamu Jinsi Ya Kupata Mapacha?

Tunafundisha jinsi ya kupata jinsia unayotaka, jinsi ya kupata mtoto kama umekosa mtoto kwa muda mrefu. Pia hata jinsi ya kupata watoto mapacha tunaweza kukusaidia.

Tunapatikana Katika Mikoa Zaidi ya 10 Tanzania

Tunazidi kuongeza matawi yetu nchini Tanzania na Nje ya Nchi. Kwa sasa tunapatikana katika mikoa zaidi ya 10 na tunazidi kuongeza matawi yetu. Karibu sana.

Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Tuesday, June 2, 2015

VIFO VYA WATOTO WENGINE WAWILI VYATIKISA DAR!

Stori: Haruni Sanchawa
NImajonzi tena! Simanzi kubwa ilitawala kwa wakazi wa Jiji la Dar hususan Ukonga Mazizini kufuatia familia ya Emanuel Chadaha kufiwa na watoto wao wawili, Boniface (6) na Kelvin (4) katika tukio moja la kuzama kisimani.


Majeneza yaliyobeba miili ya watoto hao yakiandaliwa kwa ajili ya mazishi.

Vifo hivyo ambavyo vimeacha historia ya kusikitisha, vilitokea Mei 23, mwaka huu tena kwa mateso makubwa kwa vile wakati wanazama mmoja mmoja ndani ya kisima hicho hawakupata msaada wowote.Kwa mujibu wa waombolezaji kwenye msiba huo, watoto hao ambao walikuwa wakipendana sana, siku ya tukio walikuwa wakicheza nje ya nyumba yao huku baba yao mzazi, Emanuel akiwa ndani akizungumza na mgeni.

“Baba yao kwa vile aliona hali ya hewa nje si nzuri, mvuamvua ilikuwa ikinyesha, aliwaonya watoto wake wasichezee nje.
“Baba yao aliwazuia mara tatu lakini si unajua watoto tena, waliendelea kucheza nje.

“Nyumba wanayoishi, kwa pembeni kuna kisima ambacho hakijafunikwa juu na mbaya zaidi kilijaa maji, sasa kwa uelewa wa watoto hao waliamini kisima hicho hakijajaa,” alisema mwombolezaji mmoja.Simulizi hii ya watoto, iliendelea kusema kuwa, baba wa watoto haoa alianza kuhisi utulivu uliopo nje si wa kawaida hivyo kudhani kwamba watoto wake walikwenda kucheza mbali.


Waombolezaji wakiwa kwenye foleni kwaajili ya kuaga miili ya watoto hao.

Alitoka nje kuwaangalia hakuwaona, akaenda kwa majirani ambako pia hawakuwepo. Alipokuwa akipita usawa wa kisima, alishtuka kuona kandambili moja ya Kelvin ikielea.“Kama mzazi mwenye uchungu tayari alishahisi mauti imemfika mtoto wake, akachukua uamuzi ya kuingia ndani ya kisima ambapo aliwakutana watoto wake wote wameishakunywa maji, alipoibuka akapiga kelele.

“Majirani tulijitokeza baada ya kuomba msaada, tukawatoa na kuwakimbiza Hospitali ya FFU Ukonga (Dar) lakini madaktari walisema walishafariki dunia hivyo miili ikapelekwa Hospitali ya Amana kwa ajili ya kuhifadhiwa.
“Inavyoonekana, aliyeanza kuzama ni mkubwa, mdogo wake alipoona kaka yake amezama na yeye akajitosa ili kumwokoa, kumbe naye anaitwa na mauti,” alisema jirani mmoja.

Waombolezaji wakiwa na nyuso za huzuni.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, watoto hao walikuwa wawili waliozaliwa tumbo moja, hivyo wazazi hao wamebaki watupu. Inauma sana!Mama mzazi wa watoto hao, Vailet Muhaha aliposikia watoto wake wamefariki dunia alipoteza fahamu na kukimbizwa hospitali kiasi cha kumfanya ashindwe kuaga miili ya watoto hao.

Watoto hao waliagwa Mei 27, mwaka huu katika Kanisa la Angalikana, Ukonga na kusafirishwa kwenda mkoani Dodoma kwa mazishi yaliyofanyika siku iliyofuata.
Mungu azilaze pema peponi, roho za watoto hao. Amina.

AKATWA MAPANGA KWA MADAI YA KUGONGANISHA MABWANA

 Na Gregory Nyankaira, Butiama
MCHEPUKO usitajwe kwako! Mrembo aliyejulikana kwa jina la Bahati Nyamkira (20) (pichani), mkazi wa Kijiji cha Singu, Kata ya Kukirango, Butiama, Mara, amenusurika kifo baada ya kucharangwa mapanga sehemu mbalimbali za mwili na mwanaume anayedaiwa kuwa hawara yake kisa kikisemekana ni kumkuta akiwa na hawara mwingine, (kuwagonganisha).
Bahati Nyamkira amenusurika kifo baada ya kucharangwa mapanga sehemu mbalimbali za mwili.

Tukio hilo la kushangaza lilitokea saa 4 usiku wa Mei 23, mwaka huu nyumbani kwa mwanamke huyo katika kijiji hicho.
Kwa mujibu wa mashuhuda, siku ya tukio, saa 2 usiku, kijana mmoja aitwaye Nyamkinda James (23), mkazi wa Kijiji cha Buturu ambaye anadaiwa aliwahi kuishi na mwanamke huyo na kuzaa naye mtoto mmoja, alikwenda nyumbani kwa mwanamke huyo kwa lengo la kumchukua ili aende kulala naye kwao lakini mwanamke aligoma na kumfanya mwanaume huyo kutia shaka kwamba, huenda ana mwanaume mwingine.

Ilizidi kudaiwa kuwa, mara baada ya mwanamke huyo kugoma, kijana huyo aliondoka kimyakimya hadi nyumbani kwao na kuchukua panga kisha akarudi kwa kunyatia na kujificha sehemu.“Yule kijana akiwa amejificha huku macho yakiwa kwenye nyumba ya mwanamke huyo, ghafla alimwona mwanaume mwingine akifika nyumbani hapo na kugonga mlango.
“Mwanamke alifungua mlango na kuondoka na mwanaume huyo. Ndipo Nyamkinda alitoka pale alipokuwa amebana na panga lake na kumvamia kisha kuanza kumcharanga hovyo mwanamke huyo na kumsababishia majeraha makubwa,” alisema shuhuda mmoja.

“Sisi tulisikia kelele kutoka nyumbani kwa Bahati, tulipofika tulimkuta anagaragara chini huku akitokwa na damu nyingi mwilini na akilia kwa uchungu.“Tulipomuuliza kulikoni alisema amecharangwa mapanga na hawara yake wa zamani baada ya kumwona akiondoka na mwanaume mwingine, hivyo tukampa msaada wa kumpeleka Hospitali ya Wilaya ya Butiama ambako amelazwa,” aliongeza shuhuda huyo.

Afisa mmoja wa polisi mjini Butiama ambaye ameomba jina lake lisitajwe kwa kuwa siyo msemaji, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba, mtuhumiwa huyo anasakwa baada ya kutokomea kusikojulikana.

MBUNGE WA UKONGA, EUGENE MWAIPOSA AFARIKI DUNIA






Eugene Mwaiposa enzi za uhai wake.

MBUNGE wa Jimbo la Ukonga, Eugene Mwaiposa (CCM) amefariki dunia akiwa nyumbani kwake mkoani Dodoma leo baada ya kusumbuliwa na shinikizo la damu kwa muda mrefu.

Taarifa iliyotolewa na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kwamba marehemu alikuwa na tatizo la shinikizo la damu kwa muda mrefu na amefariki akiwa nyumbani kwake Dodoma.

Ameongeza kuwa nyumbani kwa marehemu ni eneo la Chaduru jirani na jengo jipya la Hoteli ya Shabiby barabara ya Dar es Salaam.
Mwili wa marehemu umepelekwa hospitali ya Mkoa wa Dodoma kwa uchunguzi zaidi.

Shughuli ya kuaga mwili itafanyika kesho. Naibu Spika ametumia kanuni ya 152 kuahirisha bunge hadi keshokutwa Alhamisi kutokana na msiba huo.

KAMPENI YA KUTOKOMEZA MARADHI YA FISTULA YAENDELEA WILAYANI UVINZA-KIGOMA


Wakazi wa Wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma wakimsikiliza kwa makini Meneja Biashara Idara ya Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Grace Lyon (wapili kutoka kushoto ) alipokuwa akiwafafanulia jambo wakina baba hao kuhusiana na kampeni inayoendelea katika mikoa mitatu nchini ya kuelimisha wakina baba na wananchi kwa ujumla kuwaruhusu wakina mama wajitokeze ili wakatibiwe maradhi fistula kwani yanatibika, Inakadiriwa ni wastani ya wanawake 3,000 hupatwa na maradhi hayo wanapojifungua.Kampeni hiyo inaendeshwa na CCBRT na Vodacom Foundation.


Meneja Mawasiliano wa Hospitali ya CCBRT Abdul Kajumul , akiwaelezea wakazi wa kata ya Nguruka Wilaya ya Uvinza Kigoma waliofika kwenye mkutano na kupatiwa elimu kuhusiana na kampeni inayoendelea katika mikoa mitatu nchini ya kuelimisha wakina baba na wanchi kwa ujumla kuwaruhusu wakina mama wajitokeze ili wakatibiwe maradhi ya fistula bure katika hospitali ya CCBRT kwani yanatibika, Inakadiriwa ni wastani ya wanawake 3,000 hupatwa na maradhi hayo wanapojifungua.Kampeni hiyo inaendeshwa na CCBRT na Vodacom Foundation.

Msanii wa nyimbo za kiasili na Balozi wa maradhi ya Fistula Mrisho Mpoto akitoa elimu kwa wakazi wa Kata ya Nguruka wilaya ya Uvinza Kigoma, Kuhusiana na kampeni inayoendelea katika mikoa mitatu nchini ya kuelimisha wakina baba na wanchi kwa ujumla kuwaruhusu wakina mama wajitokeze ili wakatibiwe maradhi ya fistula bure katika hospitali ya CCBRT kwani yanatibika,Inakadiriwa ni wastani ya wanawake 3,000 hupatwa na maradhi hayo wanapojifungua.Kampeni hiyo inaendeshwa na CCBRT na Vodacom Foundation.
Umati wa wakazi wa kata ya Nguruka Wilaya ya Uvinza Kigoma wakiwa kwenye mkutano wa kampeni ya kutoa elimu kuhusiana na maradhi ya Fistula yanayowakabili wanawake hapa nchini,Kampeni hiyo inayoendeshwa na Hospitali ya CCBRT kwa kushirikiana na Vodacom Tanzania kupitia taasisi yake ya Vodacom Foundation inaendelea kufanyika katika mikoa mitatu kuwasisitiza wakina baba kuwaruhusu wakina mama wajitokeze ili wakatibiwe maradhi hayo kwani yanatibika. Inakadiriwa ni wastani ya wanawake 3,000 hupatwa na maradhi hayo wanapojifungua.

MELI ILIYOKUWA NA WATU ZAIDI YA 450 YAZAMA NCHINI CHINA


China
Meli ya Dongfangzhixing ikiwa imebeba zaidi ya watu 450 imepinduka na kuzama jana usiku baada ya kukumbwa na dhoruba la upepo mkali katika mto Yangtze kusini mwa China.

Taarifa zimeeleza kuwa, meli hiyo ilikuwa ikisafiri kutoka Mashariki mwa Mji wa Nanjing kwenda Chongqing Kusini Magharibi mwa China ndipo ilipozama katika kaunti ya Jianli katika jimbo la Hubei.

Meli hiyo ya Dongfangzhixing au Nyota ya Mashariki ilikuwa imewabeba abiria wa Kichina 405, wafanyakazi watano wa Shirika la Usafiri na wafanyakazi 47 wa meli hiyo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Serikali ya China, Xinhua ni kwamba, kifaa maalum cha kurekodia video (CCTV Camera) kimeonesha watu watano wakiwa mamefariki dunia kutokana na ajali hiyo na18 wakiwa wameokolewa mpaka sasa. Kikosi cha Uokoaji kinaendelea na juhudi za uokoaji kwa abiria wengine ambao hawajapatikana mpaka sasa. Japo kazi ya uokoaji inakwamishwa na upepo mkali na mvua kubwa zinazonyesha.

Waziri Mkuu wa China, Li Keqiang amedfika eneo la tukio na kujionea maafa hayo.

Kwa upande wao Nahodha na Mhandisi Mkuu, ambao ni miongoni mwa waliookolewa wamekaririwa wakisema kuwa, meli ilikumbwa na kimbunga kikali ikapinduka na kuzama wakati huohuo.

Kwa mujibu wa shirika la utangazaji la serikali ya China, meli hiyo inamilikiwa na Shirika la Meli la Chongqing Eastern ambalo linaendesha shughuli za utalii katika maeneo matatu ya vivutio katika mto Yangtze.

Inasemekana kuwa, waliokuwa katika meli hiyo wengi wao walikuwa watalii wenye umri kati ya miaka 50 na 80 wakiwa katika safari ya kitalii iliyokuwa imeandaliwa na Kampuni ya Shanghai.

Ikumbukwe kuwa, mwezi Januari watu 22 walifariki dunia kwenye mto huo wakati boti iliyokuwa kwenye majaribio kuzama karibu na Zhangjiagang, katika jimbo la Jiangsu.

NA BBC

Mwanamke aliyekuwa amezama akiokolewa.


Kikosi cha waokoaji katika mto Yangtze wakiendelea na shughuli ya uokoaji.


Kikosi cha uokoaji kikijiandaa kwenya kuwatafuta waliozama kwa ajali hiyo.


Meli ya Dongfangzhixing iliyozama.

Shughuli za uokoaji zikifanyika.


Kikosi cha Uokoaji kikiwa kazini.


Juhudi za uokoaji zikiendelea.
Boti maalum za uokoaji.


Waandishi wa habari wakichukua tukio hilo.


Meli iliyozama.
Mmoja wa wahanga wa ajali hiyo akifungwa kamba ili aokolewe kutoka majini.

...akiokolewa.
Kikosi cha uokoaji cha dharula wakiendelea na oparesheni katika mto Yangtze.


Wanakiji wawili wa China wakitazama tukio hilo.

Majeruhi katika ajali hiyo akipelekwa kwenye huduma.


Ndugu wa baadhi ya watu waliokuwa kwenye meli hiyo wakiwa na simanzi.
Simanzi na majonzi.

Waziri Mkuu wa China Li Keqiang (aliyeketi) akiwa kwenye Mkutano huko Beijing wakipanga mkakati na namna ambavyo uokoaji utafanyika.

GOMBO TOURS WADHAMINI TAMASHA LA FLORA MBASHA


HUDUMA YA GOOD NEWS FOR ALL MINISTRY YAOMBA KUWEPO MJADALA WA WAZI KUJADILI TATIZO LA ULEVI NCHINI‏

Taarifa kwa Umma
KUONGEZEKA KWA JOTO DUNIANI NA ATHARI ZAKE KWA NCHI ZETU NA HIVI KARIBUNI NCHI YA INDIA.
Ndugu waandishi wa habari, nawasalimu katika jina la Yesu. Kwanza nawashukuru kwa kufika kwenu kuja kunisikiliza. Jina langu ni Askofu Charles Gadi wa huduma ya Good News for All Ministry.
Ndugu waandishi wa habari napenda kuchukua nafasi hii kuzungumzia hali ya joto la la dunia. Tunashukuru Mungu kwa nchi yetu kupata mvua nyingi mwaka huu, ingawa baadhi yetu zilituathiri kwa njia moja ama nyingine kutokana na mafuriko. Lakini tunapaswa kujua kuwa hali ya joto la dunia kwa ujumla siyo nzuri hasa ukichukulia taarifa za mara kwa mara za kupungua kwa barafu ya mlima Kilimanjaro na kuyeyuka kwa mabonge ya barafu katika mabara ya barafu ya Actic na Antarctica. Taarifa hizo za kisayansi zinaonyesha kuwa ongezeko hilo la joto linatokana na uharibifu wa mazingira na kuongezeka kwa hewa ya ukaa (CO2 CARBON DAIOKSIDE).

Upungufu wa misitu ambayo husaidia kunyonya hewa ya ukaa inayotumiwa na miti kutengeneza chakula yaani phososynthesis na utumiaji wa madawa mbali mbali yanayoharibu mazingira pia huchangia ongezeko hilo la Joto. Sote ni mashuhuda wa jinsi misitu yetu inavyoendelea kuangamia kutokana na shughuli za kibinadamu.

Ndugu waandishi wa Habari, Hivi karibuni imeripotiwa kuwa wimbi kubwa la upepo wa Joto (heat wave) limeikumba limeikumba nchi ya India na kuua zaidi ya watu 2000 na bado wengine wanaendelea kupoteza maisha yao. Hiyo si habari njema kwetu sisi tunaokaa duniani kwani jambo kama hilo linaweza kutufika sisi wakati wowote maana hatuna kinga yoyote inayotuzuia na ongezeko hilo la joto Duniani. Cha kusikitisha ni kuwa waliokufa wengi ni wazee, maskini na watoto ambao hawana uwezo wa kujikinga na wimbi hilo la joto kwani unahitaji uwe na viyoyozi (air conditioning) au maji baridi ya kujinyunyuzia wakati wimbi hilo la joto likipita.

Kwa sababu hiyo tumesukumwa na Mungu kuandaa mkutano wa maombi huko India ili Mungu atukinge na madhila hayo ya mawimbi ya hewa ya joto. Katika safari hiyo ya India tutaambatana na wachungaji zaidi ya 10 pamoja na waandishi wa Habari kadhaa ili kufanya maombi hayo, yatakayoambatana na kutoa misaada kwa waathirika wa upepo joto huo. Ni muhimu kwetu kutoa misaada kwa sababu wale walioathirika ni maskini na wahitaji wa nchi ile na Biblia inasema kuwa unapomsaidia Maskini unamkopesha Bwana. Ina maana Mungu anaweza kutumia sadaka hiyo kutuepusha na sisi kupata tatizo linalofanana na hilo katika nchi yetu.

Ili kufanikisha safari hiyo, tunawaomba wananchi wote wenye moyo kutuchangia nauli na msaada wa kuwapelekea waathirika hao. Tunaiomba jamii ya kiasia katika nchi yetu kusaidia katika hilo, na hata taasisi mbali mbali za fedha na mashirika yasiyo ya kiserikali. Safari hiyo ni ya uhamasisho na itahusisha pia kushauri au kuelimisha dhana nzima ya utunzaji wa mazingira hasa misitu na kupunguza hewa ya ukaa inayochochea ongezeko hilo la joto duniani.

TATIZO LA ULEVI KWA TAIFA
Ndugu waandishi wa habari, Kuna habari kwenye vyombo mbali mbali vya habari na mitandao ya kijamii, na hata Bungeni jambo hilo limetajwa kwamba vijana wetu na wanandoa wengi wameathirika sana kwa ulevi wa kupindukia utokanao na matumizi ya pombe za kienyeji zenye vilevi vikali. Eneo la Rombo limetajwa kwa taarifa iliyotolewa na mkuu wa Wilaya hiyo na kushuhudiwa pamoja na baadhi ya akina mama waliohojiwa na vyombo vya habari kuwa limeathirika sana. Lakini napenda kuwaambia kuwa wilaya hiyo ni mfano tu, hilo nitatizo la kitaifa kwani tunaona mara nyingi katika vijiji, miji na mikoa watu walivyoathirika na ulevi, hadi kushindwa kutimiza majukumu yao ya kulijenga taifa hilli. Pamoja na kuwepo kwa habari ya aibu kuwa baadhi ya wanawake wanakodisha wanaume toka nchi jirani ya Kenya, lakini kinachotakiwa kuangaliwa hapa ni hali halisi ya kuathirika kwa wananchi wetu.

Sisi tunatoa ushauri kuwa uwepo mjadala wa wazi juu ya tatizo hilo la ulevi badala ya kutumia nguvu nyingi kumkemea Mkuu wa wilaya aliyejaribu kutumia nguvu zake kukomesha unywaji huo mbaya wa pombe. Inasemekana kuwa ndani ya wilaya hiyo kuna aina za pombe za kienyeji zaidi ya 50 na nyingi huwekwa kweye chupa maalum kama zile za kiwandani huku zikiwa hazina viwango vya TBS. Baadhi yake zina kilevi (Alkohol) zaidi ya asilimia 58% jambo ambalo ni hatari kubwa kwa maini na figo za wanywaji. Uwezekano wa kupuguza nguvu za kiume upo kwani wengi huamka asubuhi na mapema kunywa vilevi hivyo na hivyo kushindia bila kula jambo ambalo linawathoofisha kimaumbile.

Hivi karibuni dada mmoja mwanasheria alitufuata na kutaka tuombe sana kwa ajili ya tatizo la ulevi katika taifa kwa wanaume kwani amefanya utafiti katika kazi yake na kugundua kuwa kwenye ndoa nyingi wanaume hawana nguvu za kiume baada ya kuzoelea ulevi na wamama wengi wanalalamika. Hii inaonyesha kwamba hili si tatizo la wilaya moja tu, bali ni la kitaifa, na tunashauri lichukuliwe kwa uzito na kuwekewa mjadala mpana zaidi wa kitaifa ili ufumbuzi upatikane. Tunamwomba waziri mkuu aliundie tume ili hatua za haraka na za kimakusudi ziweze kuchukuliwa ikiwa ni pamoja na za kiroho, kwa kushirikisha wadau mbali mbali ikiwa ni pamoja na serikali, vyombo vya sheria, vyombo vya kiroho (viongozi wa dini) kutafuta usuluhishi.

Sisi tunaona kuwa ni tatizo la kiroho kwani upo msemo kuwa ulevi unachangia uzinzi, lakini kinyume chake sasa inaharibu nguvu za kiume. Ukisoma Kumbukumbu la Torati 28:30 katika Biblia inasema, “Utaoa mke na mume mwingine atalala naye . . . .” Andiko hilo linamaanisha mtu aliyelaaniwa. Kama mtu akishindwa kulala na mkewe amelaaniwa.

Maana ikiwa kwa sababu ya pombe wanawake wa Rombo wanaazima wanaume Kenya, basi na wa Mtwara wataazima Msumbiji na wa Kagera na Kigoma wataazima Burundi Rwanda na uganda. Sasa ikiwa ulevi huo uko nchi nzima, wale walio mikoa ya kati wataazima wapi? Napenda muone kuwa tatizo hili litafika pabaya kama halijachukuliwa hatua stahiki.

Kutokana na hali hiyo tunashauri itafutwe namna ya kuwashauri wananchi na vijana kwa ujumla nchi nzima namna ya kuepukana na ulevi huo, na pia sisi kama viongozi wa dini kushirikiana kuwaelimisha kwa kanuni za kiroho na kimwili, kwani bahati nzuri madhehebu mengi ya dini hukemea utumiaji wa pombe. Pia watengenezaji wa vilevi hivyo washauriwe kutafuta miradi mingine ya kuwaingizia kipato badala kutegemea pombe hizo zinazoumiza vijana wetu.

Sasa tatizo la pombe hizo za viroba na kienyeji ni tatizo kubwa kwa vijana wa primary, secondary, waendesha bodaboda, madereva wa noa, bajaji nk hata kupunguza kiwango cha elimu, ajali za mara kwa mara, na nguvu kazi ya nchi kwa ujumla. Hili tatizo ni kubwa mno na linalenga kuharibu (generation) au kizazi hiki cha vijana na kutengeneza jamii ambayo haitafundishika au kutawalika kwa urahisi.
Tunawashukuru sana kwa kutusikiliza.

Wako Charles Gadi Mwenyekiti: GOOD NEWS FOR ALL MINISTRY.
Stori na mtandao wa habari za jamii


Askofu Charles Gadi wa Huduma ya Good News for All Ministry

Askofu Charles Gadi wa Huduma ya Good News for All Ministry (kulia), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kuhusu kuongezeka kwa joto duniani na athari zake pamoja na tatizo la ulevi nchini ambapo kanisa hilo limeshauri kuwepo na mjadala wa wazi kujadili jambo hilo. Kutoka kushoto ni Mchungaji, Martin Ndaki na Katibu wa huduma hiyo, Palemo Massawe.

Mchungaji Fabian Msimbe akizungumza katika mkutano huo. Kulia ni Mchungaji Leons Kajuna.

Mchungaji Martin Ndaki (kushoto), akizungumza katika mkutano huo.

Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.

Askofu Charles Gadi wa Huduma ya Good News for All Ministry (katikati), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kuhusu kuongezeka kwa joto duniani na athari zake pamoja na tatizo la ulevi nchini ambapo kanisa hilo limeshauri kuwepo na mjadala wa wazi kujadili jambo hilo. Kutoka kushoto ni Mchungaji Martin Ndaki, Katibu wa huduma hiyo, Palemo Massawe, Mchungaji Fabian Msimbe, Mchungaji Leons Kajuna, Mchungaji Denis Kumbiiho na Mchungaji James Manyama.

Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
.........................................................................................

MJANE: UKIPATA AJALI UKATOKA SALAMA MSHUKURU MUNGU!


Na Mwandishi Wetu
“SIKUAMINI kama kungekuwa na siku ndoto ya maisha yangu ingebadilika na kufikia hatua hii ya mateso yasiyo na ukomo, kwa sasa shughuli zangu zote zimesimama nimekuwa mtu wa kuishi kwa kuombaomba ndani ya miaka minne”

Luna Hassan Mwampyati aliyekatika mkono baada ya kupata ajali.
Hivyo ndivyo mkazi huyu wa Tandika Azimio, jijini Dar es Salaam, Luna Hassan Mwampyati (34) alivyoanza kuelezea mkasa wa ajali aliyopata na kupoteza kiganja cha mkono wake wa kushoto.
Ajali iliyosababisha mama huyo kupatwa na masaibu hayo, ilihusisha Basi la New Force iliyotokea Januari 28,2012 maeneo ya Nyororo, Mafinga mkoani Iringa.
Akisumulia zaidi, mama huyo anasema:
NILIJIKUTA NIMELOA DAMU
“Nakumbuka siku hiyo ya tukio nilikua nikisafiri kutoka Dar kwenda mkoani Mbeya, nikisafirisha biashara yangu ya vitenge, nilikua nimesinzia, wakati huo ilikuwa saa tisa alasiri. Nikiwa nimekaa kiti namba 28, nilisikia kishindo kikubwa na nilipozinduka ndani ya basi kulikuwa na vumbi basi lilikuwa limepinduka, niligundua mkono umebanwa.
“Katika hali isiyokuwa ya kawaida, kila mmoja alikuwa akilia huku akiomba msaada, mwili wangu ulikuwa umeloa damu yangu na abiria waliokuwa wamejeruhiwa waliokuwa wakilia, hakuna aliyeweza kumuokoa mwenzake, kila moja alitafuta jinsi ya kujinasua.
“Nilijaribu kuvuta mkono wangu lakini ilishindikana, nikawa napata maumivu kupita kiasi, niliomba msaada kwa watu bila mafanikio.Wasamaria wema walipojitokeza, walianza kuchana gari kwa kutumia shoka na mapanga.
MKONO WASAGIKA
“Mkono wangu ulipotolewa ulikua umesagika na vipande vikawa vinaning’inia.
Miili kadhaa ya watu waliopoteza maisha walikuwa wamenilalia, hivyo ikawa vigumu kujinasua.
“Nikiwa katika hali hiyo, mtoto wa miaka kama mitatu hivi aliyekuwa na mama yake, alinikumbatia alifikiri nilikuwa mama yake.
Alipokuwa hospitali baada ya kupata ajali.
“Alikuwa akilia kwa uchungu huku akitoa sauti ‘mama,mama,mama nakufaaa’, alinikumbatia muda wote hadi pale wasamaria wema walipokuja kumbandua kwangu.
MKONO WAKATWA
“Tuliondolewa na kulazwa pembeni mwa barabara, watu walikuwa wakisema kulikuwa na watu watano waliojeruhiwa vibaya, nilisikia kwamba basi letu lilikuwa likijaribu kulipita basi lingine ndipo liligongana na lori uso kwa uso.
“Tulichukuliwa hadi Hospitali ya Makambako kwa bahati mbaya kipindi hicho kulikua na mgomo wa madaktari hapo tukahamishiwa Hospitali ya Misheni ya Ilembula.
“Polisi walikuwa bega kwa bega kuhakikisha tunapata huduma, kesho yake ndugu zangu walifika wakitokea Mbeya baada ya kupata taarifa, walikuta kiganja changu kimeshakatwa.“Niliendelea kupata matibabu, nikapata nafuu lakini mizigo yangu ya vitenge vya biashara yenye thamani ya shilingi milioni moja ilipotea, mtaji ukawa umekatika, sikuwa na jinsi ya kuinuka tena katika maisha, mume wangu alishafariki miaka 15 iliyopita nikawa mama na baba wa watoto wangu watatu.
Ajali iliyomsababishia kupoteza mkono wake.
“Mmoja alikuwa anasoma sekondari aliacha kusoma, nilikosa fedha za kumsomeshea, hali hiyo iliwakuta hata hawa wadogo, nimeshindwa maisha kwa ujumla.“Nyumba niliyopanga kodi ikawa imeisha ilibidi tutimuliwe kutokana na kutokuwa na fedha ya kulipia, nilifikiria mengi sana kwani hata njaa ilitukabili.
“Nilihama pale baada ya chumba kimoja na bibi mmoja, chumba hicho kilitumika kufugia nguruwe awali, nilikisafisha, tukawa tunaishi kwa dhiki kubwa licha ya kusaidiwa na wasamaria wema wachache waliojua historia yetu.
“Hata hivyo, baada ya muda mfupi tukafukuzwa kwa madai kwamba anataka kuifanyia ukarabati kisha aiuze.
“Hapo ndipo nilipatwa na majonzi huku nikifikiria pa kwenda, sikuweza kupata majibu kwa urahisi, baadaye nikahamia Tandika kwa mdogo wangu anayeendesha maisha yake kwa kuuza mbogamboga, akikosa tunalala njaa.
“Kwa sasa bado sijapona vizuri kwani wakati wa baridi napata maumivu makali. Sina biashara yoyote, kazi yangu ilikuwa ni biashara ya vitenge na saluni, nimepata pigo kubwa sana na familia yangu nayo imeathirika.
Akiwa na familia yake kabla ya kupata ajali.
“Nawaombeni Watanzania wenzangu mnisaidie nipate mtaji ili niweze kufanya biashara ambayo naamini itaniwezesha kuendesha maisha na kuacha kuombaomba jambo ambalo silipendi isipokuwa nalazimika kufanya hivyo kwa sababu ya shida,” alisema mama huyo.Kwa yeyote atakayeguswa na kilio chake awasiliane naye kwa namba 0763 224986 au 0656 238087- Mhariri

UVIMBE KATIKA VIFUKO VYA MAYAI (OVARIAN CYST) - 3





MATATIZO KATIKA KORODANI ZA MWANAUME (TESTICULAR FAILURE)

Kazi ya korodani ni kuzalisha mbegu za kiume na homoni za kiume (Testosterone). Kwa hiyo korodani kushindwa kufanya kazi maana yake ni kushindwa kuzalisha mbegu na homoni za kiume.
Chanzo cha tatizo

Tatizo hili huwapata baadhi ya wanaume na chanzo chake ni kama vile matumizi ya baadhi ya dawa kwa muda mrefu mfano dawa kama Ketoconazole, Glucocorticoids na dawa za usingizi hasa zile za kutuliza maumivu makali.
Pia yapo magonjwa yanayoshambulia korodani, mfano ugonjwa wa Mump ambao huambatana na kuvimba nyuma ya sikio na mashavu, maambukizi na maumivu ya korodani, kansa ya korodani na ugonjwa uitwao kitaalamu Hemochromatosis unaoambatana na mfumo wa damu.

Kuumia korodani na kuzungukwa na mishipa ya damu pia ni mojawapo ya chanzo cha korodani kutozalisha mbegu za uzazi. Mambo ya hatari yanayoweza kuharibu korodani ni shughuli zetu za kila siku na hizi husababisha kila siku korodani iumie taratibu.

Mfano kuendesha pikipiki kwa muda mrefu. Vilevile uvutaji bangi na sigara unachangia tatizo hili. Dalili za korodani kushindwa kufanya kazi Mojawapo ya dalili hizi ni kutokuongezeka kwa ukubwa au urefu wa viungo vya uzazi, yaani uume na korodani zenyewe.

Mwanaume kuwa na matiti makubwa, kukaa na mwanamke muda mrefu zaidi ya mwaka bila ya kumpa mimba, mwili kutoendelea vizuri hata ukila vizuri na kufanya mazoezi unaona mwili haujengeki. Pia kutokuwa na hamu ya tendo la ndoa au kupungukiwa na nguvu za kiume kwa kiasi kikubwa, kutoota nywele kwapani au sehemu za siri au kuota kwa kiasi kidogo sana.

Mabadiliko ya balehe kuendelea taratibu sana utakuwa umri unakua mkubwa lakini bado unakuwa kama mtoto, yaani baadhi ya viungo haviendelei mfano kuota ndevu, mabadiliko ya sauti na sehemu za siri.

Uchunguzi kwa watoto wachanga wenye matatizo haya viungo vyao vya uzazi huwa havieleweki kama ni vya kiume au vya kike, kadiri anavyoendelea kukua viungo vya uzazi huwa vidogo na wakati mwingine korodani zake huvimba yaani moja huwa kubwa kuliko nyingine.
Itaendelea toleo lijalo

DUNIA IMEKWISHA! WANAFUNZI DAR WAFANYA MAPENZI NA MBWA

RICHARD BUKOS
NI kweli kabisa dunia imekwisha! Kanisa la Maombezi la Ebenezer Deliverance la Mbezi ya Salasala jijini Dar lililo chini ya Mchungaji Benson Shirima limegeuzwa danguro la kufanyia ‘usodoma’ kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Benaco waliotoroka majumbani mwao na kukacha masomo.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Benaco waliotoroka majumbani mwao na kukacha masomo wakiwa ndani ya Kanisa la Maombezi la Ebenezer Deliverance la Mbezi ya Salasala jijini Dar.

WAZAZI, WASAMARIA WEMA
Kufuatia kushamiri kwa vitendo hivyo kwenye kanisa hilo, wazazi wa wanafunzi hao na wasamaria wema walikwenda kutoa taarifa kwenye Ofisi ya Serikali ya Mtaa Kilimahewa, Kata ya Wazo, Mbezi Salasala na kuweka bayana kila kitu.
Wanafunzi hao wakiwa katika katika pozi baada ya kunaswa na Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’.
KISA CHA KUTOA TAARIFA
Awali ilidaiwa kuwa, baadhi ya wanafunzi kwenye eneo hilo walikuwa wakisakwa na wazazi wao kwani waliondoka majumbani wiki kadhaa kwenda shuleni lakini hawakurudi na shuleni hawakuwepo.
“Hata walimu walisema wanafunzi hao hawafiki shuleni na majumbani hawapo. Ndiyo tuliposikia kuna kanisa limefanywa geto tukaamua kwenda serikalini kutoa taarifa ili uongozi wa serikali ujipange tukavamie,” alisema mtu mmoja akiomba hifadhi ya jina lake.
Godoro ambalo watoto hao walikua wakilitumia.

UAMUZI WA SERIKALI YA MTAA
Maelezo ni kwamba, baada ya taarifa hiyo kufikishwa ofisini hapo, wajumbe wa ofisi hiyo na vijana wa ulinzi shirikishi wakiongozwa na mwenyekiti wa ofisi hiyo, Kulthum Juma walikwenda kulivamia geto hilo kwa lengo la kulisambaratisha.
Wanafunzi wakiwa na mbwa hao.
OFM WAPASHWA
Wakati safari hiyo ikiandaliwa, mmoja wa wanyetishaji wetu alipiga simu kwenye Ofisi za Global Publishers,  kitengo cha Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’, Bamaga- Mwenge, Dar na kuweka bayana kila kitu ambapo bila kuchelewa mmoja wa makachero wa OFM alitumia usafiri wa pikipiki iendayo kasi na baada ya dakika chache alikuwa ameshafika Salasala.
Wazazi na ulinzi shirikishi wakiwa katika geto baada ya kuwanasa wanafunzi wanaodaiwa kufanya ngono na mbwa.
Wasamaria wema wakikagua eneo hilo ambalo watoto hao walilkuwa wanalitumia kwa ajili yavitendo viovu.
KILICHOKUTWA GETO
Kama wewe ni mzazi lazima ushtuke! OFM, wazazi na ulinzi shirikishi walilivamia geto na kuwanasa wanafunzi wakifanya ngono na mbwa lakini baadhi yao walifanikiwa kuchoropoka kupitia juu ya paa huku wengine watano walikamatwa.
WALIOKAMATWA!
Miongoni mwa wanafunzi waliokamatwa ni; (kwa jina moja kwa sababu maalum,) David, Goodluck, Joseph, Mrisho na aliyetajwa kuwa kiongozi wao, Juma aliyefaulu darasa la saba na kuteuliwa kwenda katika Shule ya Sekondari ya Twiga, Dar lakini akakataa kuendelea na masomo! Inauma sana!
MAAJABU YA MBWA
Katika hali isiyotarajiwa katika akili za kibinadamu, wakiwemo wazazi wa watoto hao, mbwa waliokutwa kwenye danguro hilo, kwa kuzoea kuingiliwa na binadamu, hata msafara huo ulipovamia wao (mbwa) waliendelea kuwasogelea kimahaba wanafunzi hao.
Mbwa hao walionesha hisia zao hadharani jambo lililomfanya, Edresi ambaye ni mama mzazi wa mwanafunzi David kuangua kilio kama mzazi mwenye uchungu.
WAELEZA WALIVYOKUWA WAKIISHI
Baada ya kibano kizito, wanafunzi hao walianza kueleza jinsi walivyokuwa wakiwaingilia kimaumbile mbwa hao na jinsi walivyokuwa wakipata chakula kwa kuiba kuku, mahindi, pesa na vitu vingine mitaani.
WAMTAJA  DADA ANAYEWAPIKIA
Wanafunzi hao, walimtaja msichana mmoja aliyefahamika kwa jina la Salome ambaye ndiye mpishi wao kwenye danguro hilo.
MSAFARA KWA MPISHI
Baada ya kumtaja msichana huyo, msafara huo ulitia timu nyumbani kwa Salome ambaye baada ya kubanwa alisema alishawahi kuwapikia mara moja.
MCHUNGAJI WA KANISA HILO ANENA
Kwa kutumia namba za simu zilizokutwa kwenye vipeperushi vya matangazo ya mikutano ya hadhara ya Neno la Mungu ya kansia hilo na kwenye bango la utambulisho wa jina la kanisa, kando ya barabara, paparazi wetu alifanikiwa kuzungumza na Mchungaji Benson ambaye alikiri kulimiliki kanisa hilo.
“Ndugu mwandishi ni kweli mimi ndiye mchungaji wa kanisa hilo lakini kwa sasa niko mbali na huko lakini nimeshapigiwa simu hivyo nitakuja kuweka mambo sawa.
“Kama hao wanafunzi wanaishi humo watakuwa wamevunja na kuingia wenyewe. Vipi, kitanda na vile vyuma vya jukwaa na vitu vingine umevikuta?” mchungaji alimuuliza paparazi wetu.
“Vipo baba mchungaji, nimeviona,” alijibu paparazi wa OFM.
 MWENYEKITI WA MTAA
Akizungumzia tukio hilo, mwenyekiti wa mtaa huo aliyeongoza msafara huo aliwaomba wazazi wenye watoto hao kupima afya zao kwani ilidaiwa kuwa walikuwa wakiingiliana hata wenyewe kwa wenyewe na kuna uwezekano mkubwa wa kupata maradhi ya ngono ambayo hupatikana zaidi kwa mbwa na binadamu.