Karibu Fadhaget Sanitarium Clinic

Tunapenda kukukaribisha katika Kitengo cha Sayansi ya Tiba Asilia.

Kitengo Cha Sayansi Ya Tiba Asilia

Kwa Muda mrefu tumekuwa tukisaidia wengi katika matibabu na kutengeneza dawa bora kabisa kiafya.

Je Unapenda Kufahamu Jinsi Ya Kupata Mapacha?

Tunafundisha jinsi ya kupata jinsia unayotaka, jinsi ya kupata mtoto kama umekosa mtoto kwa muda mrefu. Pia hata jinsi ya kupata watoto mapacha tunaweza kukusaidia.

Tunapatikana Katika Mikoa Zaidi ya 10 Tanzania

Tunazidi kuongeza matawi yetu nchini Tanzania na Nje ya Nchi. Kwa sasa tunapatikana katika mikoa zaidi ya 10 na tunazidi kuongeza matawi yetu. Karibu sana.

Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Wednesday, July 29, 2015

Shuhuda Aliyeteseka Miaka 10 Bila Kupata Mtoto, Hatimaye Atoa Ushuhuda Baada ya Kupata Mtoto.

Shuhuda ajulikanaye kwa jina moja tu la Bi. Sophia ametoa ushuhuda wa kupata mtoto baada ya kupata matibabu kutoka The Fadhaget Sanitarium Clinic.

Bi. Sophia akiwa na mwanae.
Bi.Sophia amesema kuwa kwa muda wa miaka 10 amekuwa akitafuta mtoto lakini hakubahatika kupata mtoto. Kupitia matibabu kutoka kwetu aliweza kupimwa, na baada ya kupimwa akapatiwa dawa na sasa analea mtoto. The Fadhaget Sanitarium Clinic wamekuwa ni mabingwa wa kutibu magonjwa hasa yale yaliyo sugu kwa kutumia mimea na matunda. Ni jambo la furaha kuona wateja wetu wanatoa shukrani na kuonyesha furaha zao baada ya kutimiza ndoto zao hasa pale walipokata tamaa kuona kuwa matatizo yao hayatibiki. 
Tunapenda kutoa shukrani za Dhati kwa Bi. Sophia na pia kwa wale wote ambao wameshukuru kwa huduma zetu. Karibuni sana.
Bi. Sophia akionyesha furaha na Mwanaye.


Sunday, July 19, 2015

MAGONJWA HATARI KWA WANAWAKE


KUNA magonjwa mengi ya hatari kwa wanawake ambayo huwakumba kwenye viungo vya uzazi na dalili za kuyatambua ni nyingi japokuwa wanaume pia huweza kupatwa na matatizo hayo.

DALILI KWA WANAWAKE
Kwa upande wa wanawake, wanaweza kutambua kwamba wana ugonjwa ambao utaathiri viungo vya uzazi kwa kutokwa na majimaji au ute kwenye uke.

Wanawake wanapaswa kutafuta msaada wa kimatibabu kwa daktari wakigundua lolote kati ya haya yafuatayo:-
Majimaji ya ukeni ambayo yana harufu isiyo ya kawaida na yenye rangi tofauti na wingi kuliko ilivyo kawaida au kuhisi maumivu au kusikia kama unaungua au muwasho wakati wa kwenda haja ndogo.

Dalili nyingine ya kupata maradhi haya au kitaalamu Sexually transmitted disease
ni kusikia maumivu na muwasho katika maeneo ya uke au maumivu ukeni wakati wa kufanya ngono.
Wanawake wengine watatambua kuwa wana magonjwa hatari kwa kutokwa na vidonda na malengelenge katika eneo la uke.

Kumbuka, baadhi ya maambukizi huenda yasiwe na dalili hivyo kama una wasiwasi au umetokewa na dalili hizi ni vyema kuchunguzwa na daktari haraka iwezekanavyo, ama nenda katika kliniki.

DALILI KWA WANAUME
Mwanaume anaweza kupata magonjwa yanayoweza kuathiri viungo vyake vya uzazi na dalili zake ni hizi zifuatazo:-
Majimaji kutoka uumeni ambayo yana harufu isiyo ya kawaida, au yakiwa mengi, kuhisi muwasho ndani ya uume, wakati na baada tu ya kwenda haja ndogo au kutokwa na vijidonda au malengelenge juu au katika sehemu za kiume.
Wengine wanatokwa na vipele au uvimbe katika sehemu za siri.

Kila mtu awe mwanaume au mwanamke ambaye ataona dalili zilizotajwa hapo juu ili kugundua ugonjwa ni lazima aende kuonana na daktari na kufanyiwa vipimo.

itaendelea wiki ijayo

KUTOKUPEVUKA KWA MFUMO WA UZAZI (HYPOGONADISM)



Hali hii hutokana na viungo vya uzalishaji wa vichocheo vya uimarishaji uzazi kwa mwanamke na mwanaume kutofanya kazi. Viungo au glandi hizi ni korodani kwa mwanaume na ovari kwa mwanamke.

CHANZO CHA TATIZO
Tatizo hili linaweza kuwa linatokea tangu kuzaliwa au linatokea katika mfumo mzima wa mwili. Kwa tatizo la kuzaliwa nalo, korodani au vifuko vya mayai huwa havifanyi kazi ya kuzalisha vichocheo au homoni zinazohitajika ambapo kwa korodani huzalisha homoni za kiume na ovari huzalisha homoni za kike.

Vyanzo vya matatizo ni kama vile:-
-Matatizo katika mfumo wa kinga mwilini,
-Matatizo katika mfumo wa vinasaba.
-Matatizo ya Ini na Figo.

-Mionzi iwe ya X-ray au viwandani.
-Upasuaji wa kuondoa korodani zote mbili au ovary zote mbili.
Matatizo ya vinasaba yanayotokea kwa wanawake huitwa ‘Turner syndrome’ na kwa wanaume huitwa ‘Klinifelter Syndrome’.

Katika matatizo mengine ya ‘hypogonadism’ mfumo wa ubongo unaohusisha pituitary na Hypothalamus ambazo hudhibiti utolewaji wa homoni mwilini huwa haufanyi kazi vizuri hivyo husababisha matatizo ya mfumo wa mwili na uzazi ambapo vyanzo vikuu vinaweza kuwa;-

-Endapo mama mjamzito wakati wa kujifungua akatokwa na damu nyingi sana na ikija kukata inakata moja kwa moja, yaani hapati tena siku zake na uwezo wa kuzaa unapotea.-Matumizi holela ya dawa zenye ‘steroids’, mfano krimu za kufanya ngozi hasa ya uso ing’ae, kubadilisha rangi ya ngozi au kutuliza miwasho ya ngozi pamoja na matumizi ya dawa za kulevya pia huathiri kwa kiasi kikubwa mfumo wa uzazi.

-Matatizo haya pía yanaweza kuwa ya kurithi endapo kwenye ukoo wenu wapo watu wenye matatizo katika mfumo wa uzazi wa aina hii.-Maambukizi, hasa virusi wa aina yoyote yanaweza kuathiri mfumo wa uzazi.
-Lishe duni hasa kwa watoto wanaokaribia balehe huweza kuwadumaza na aidha kutobalehe au kuchelewa kubalehe na kuonekana bado wadogo pamoja na umri kwenda.

-Kuwa na madini mengi ya chuma mwilini, na hili linategemea na mazingira ya kuishi na vyakula au vinywaji hasa kwa mama mjamzito na watoto.-Mionzi ya X-ray ya mara kwa mara na mionzi ya viwandani.
-Kupungua uzito kwa kasi au kujipunguza uzito sana, kwa mwanamke anaweza kupoteza siku zake au asivunje ungo, hivyohivyo kwa mwanaume hudumaa viungo vyake vya uzazi.

-Upasuaji wa viungo vya uzazi kama tulivyozungumza hapo awali.
-Kuumia korodani utotoni au hata katika umri wa ujana.-Uwepo wa uvimbe kwenye korodani au vifuko vya mayai ambao ni saratani.

Matatizo haya husababisha mtu asikue aonekane bado mdogo hata kama umri unaenda. Mwanaume mwenye tatizo hili linaweza kwenda mbali zaidi na kupoteza uwezo wa kunusa harufu ya aina yoyote.

DALILI ZA TATIZO
Dalili hizi zinatusaidia kufahamu kama tuna matatizo haya au la, au watoto, wadogo zetu na ndugu zetu wanaweza kuwa na matatizo haya. Mara nyingi tumezoea kuona watu wenye matatizo haya na kuwaita wamedumaa au vijeba.

Dalili kwa mtoto wa kike ambaye hajavunja ungo, utamwona bado ni mtoto yaani habadiliki yupo vilevile tangu alipokuwa na umri wa miaka kumi hadi anafikisha ishirini, matiti hayakui, urefu haongezeki. Kama tatizo likitokea baada ya kuvunja ungo huhisi joto muda wote hata kama kuna baridi, nywele sehemu za siri na makwapani hupuputika zenyewe, hupoteza hamu ya tendo la ndoa kabisa na haendelei tena kupata siku zake na kufunga hata zaidi ya mwaka.

Friday, July 17, 2015

Utafiti wa Jinsi Mbu anavyoweza Kutafuta Chakula Chake.

Mbu

Utafiti mpya umebaini kwamba mbu hutafuta kitu cha kula kwa kutumia vigezo vitatu,
  1. Harufu, 
  2. Macho na 
  3. Joto.
Utafiti huo unasema kuwa mbu anaweza kufahamu aliko mwanadamu kupitia hewa ya kaboni ambayo watu hupumua nje. Inasemekana mbu hunusa hewa hii kiasi cha mita 50. Wanasayansi wamesema kwamba walimfuatilia mbu mwenye njaa, ndani ya mtaro uliofunikiwa. Kisha waligundua kwamba mbu hao walianza kunusa nusa hewa ya kaboni, na kutema mapovu yenye matone meusi yaliowekwa na watafiti hao sakafuni.

Imebainika kwamba wakati mbu yuko mita chache karibu na kile anacholenga, huvutiwa sana na joto. Hii imebainisha kwamba hata hufuata joto hilo na kisha kumshambulia mwanadamu. Huenda ukapata Malaria au ukaponea lakini utakua na vipele pale vya mbu anapokuuma.

Sehemu za Mbu

Wednesday, July 15, 2015

Technology and It's Hazardous on Health.

It's hard to imagine life without cellphones, BlackBerrys and WiFi. But some people believe the technology that makes modern life so convenient may be hazardous to our health.



Mobile communications devices, along with microwave ovens, power lines, cellphone towers and wireless base stations, generate electromagnetic fields, a form of low-frequency radiation. EMFs have been studied as a possible factor in conditions from cancer to cognitive damage, particularly in teenagers and children, who have thinner skulls and still-developing brains.

A 2003 report from Lund University in Sweden found that rats at the development level of human teenagers experienced brain damage after being exposed to normal cellphone radiation; several recent studies have linked cellphone use to male reproductive damage and sleep disturbances in humans.
"There are enough scientific data to indicate that one should limit direct exposures to cellphone radiation," says Henry Lai of the University of Washington in Seattle, a leading researcher on the subject. "Much less is known on biological effects of wireless Internet systems, and exposure of radiation from these devices are much lower than that from cellphones. If exposure to cellphone radiation does turn out to be a health hazard, as present evidence suggests, then wireless Internet would be like passive smoking."



The World Health Organization and the National Institute of Environmental Health Sciences have classified ultra-low-frequency waves from power lines as possible carcinogens. But the WHO's Web site also states: "Considering the very low exposure levels and research results collected to date, there is no convincing scientific evidence that the weak RF [radio frequency] signals from base stations and wireless networks cause adverse health effects."

World Health Organization headquarters (W.H.O) at Geneva, Switzerland.

Not every scientist is convinced there's a problem. Many studies have found no definitive connection between cellphone and wireless Internet EMFs and health problems, and proponents of the technology point out that humans have transmitted long-range radio broadcasts for decades with no apparent problems.

Some people aren't taking any chances. Ontario's Lakehead University banned WiFi on campus because of its suspected health risks. A parents' group in Oak Park, Ill., filed suit against the school district in 2003 to prevent wireless Internet from being installed in schools, although the suit was later withdrawn.

Should you be concerned? The jury's still out. Unfortunately, there isn't much you can do to escape EMFs, though you can limit your use of cellphones and wireless devices, use headsets when possible and avoid living near power lines and cellphone towers.

And stay tuned for updates. Because mobile-phone and wireless technology is fairly new, studies examining the long-term effects of the devices are still underway.

-- Eviana Hartman


Learn How to Protect Yourself from harmful Radiation
Emitted by your Cell Phone, Cell Towers, and Wireless
Radiation. Click here Now
www.emfnews.org

Research Center For Wireless Technology
355 Hukilike Street Suite 206
Kahului,HI 96732
USA
Unsubscribe | Change Subscriber Options

The Fadhaget Sanitarium Clinic Ni Namba Moja Nchini kwa Matibabu Kamili ya Uzazi na Magonjwa Sugu.


Sasa The Fadhaget Sanitarium Clinic tumefanikiwa kuingia katika Namba ya kwanza nchini Tanzania kwa Kuwasaidia kikamilifu wanawake wanaotafuta uzazi. Riport zilizotufikia Asilimia 90% ya waliofika wakisumbuliwa na 

  1. Uvimbe wa kizazi,
  2. Kuziba kwa Mirija ya Uzazi, na
  3. Ugumba au kutokushika Mimba.
Wamerudisha taarifa nzuri kuwa wamefanikiwa kupitia dawa Zetu zitokanazo na Sayansi ya mimea Asilia. 

The Fadhaget Sanitarium Clinic Ni Kitengo cha Sayansi Ya Tiba Asilia Ambapo kwa Hakika tunahusika na Kutibu Maradhi Karibia Yote Hasa yale yaliyo Sugu kama vile 

  • Vidonda vya tumbo
  • Maumivu ya Chembe ya moyo
  • Kiungulia
  • Kutopata choo
  • Kutapika au kupata choo yenye Damu.
  • Matatizo ya Uzazi kwa Akina mama
  • Uvimbe wa Kizazi
  • Muambukizo katika via vya Uzazi kama vile Kuwashwa ukeni
  • Kutokwa na uchafu Mweupe wa harufu mithili ya Maziwa ya Mgando ukeni
  • Kutopata hamu ya Tendo la ndoa
  • Kuziba kwa Mirija ya Uzazi
  • Maelekezo kuzaa Mtoto jinsia unayoitaka.
  • Kupata maumivu makali chini ya kitovu au kiuno kuuma wakati wa Hedhi
  • Upungufu wa nguvu za kiume
  • Malaria Sugu
  • Kisukari
  • Figo na Uchafu wa mkojo kwa Ujumla
  • U.T.I Sugu
  • Magonjwa ya watoto (Watoto chini ya Miaka 5 hutibiwa bure)
  • Matatizo ya Arthima yaani Pumu
  • Miguu kufa Ganzi Miguu kuwaka Moto Miguu kuvimba na Kuuma Na Dalili nyingine nyingi Za Hatari kiafya. 

Kumbuka The Fadhaget sanitarium Clinic ni watu wa Jamii utakapo wafikia Utaweza kumuona Dr. Bure Ushauri ni Bure Vipimo Vyote ni Bure isipokuwa Kipimo cha Computer ndicho Utachangia Shilingi elfu 25 tu Karibu The Fadhaget Sanitarium Clinic Kwa Vipimo na Tiba

Tupigie kwa Ushauri 0757931376 au 0712705158 au 0787705158 au 0757505158 Utakutana na Dr.Fadhili Emily Mtaalam wa Tiba Asilia nchini Tanzania.

Dr Fadhili Emily

Monday, July 13, 2015

FAHAMU KINACHOSABABISHA KUTOSHIKA MIMBA-2



NiLiaNza wiki iliyopita kueleza kinachosababisha kutoshika mimba. Leo naendelea kufafanua. Kuna njia au aina mbili za wanawake kushindwa kushika mimba au kwa maneno rahisi, ugumba kitaalamu Infertility,  ambao unatambuliwa kitabibu.
Aina moja huitwa kitaalamu Secondary infertility na aina nyingine huitwa Primary infertility.
Ugumba unaotokea baadaye maishani hujulikana kitaalamu kama Secondary infertility
Ugumba huu hugundulika pale ambapo wote wawili, mwanamke na mwanaume wameshawahi kupeana mimba mara moja maishani mwao na baada ya hapo hawajafanikiwa kupata au kutungisha mimba tena.
Utafiti umegundua kuwa asilimia kati ya 30 na 40 ya tatizo la ugumba huu huwakumba wanaume ambapo wanawake ni kati ya asilimia 40 na 50.
Asilimia kati ya 10 na 30 zilizobakia ya tatizo hili husababishwa kwa pamoja na matatizo kati ya  wanaume na wanawake, japokuwa sababu halisi hazijulikani.
Kwa upande wa wanawake hufikia kilele cha kupata ujauzito (peak fertility) wakiwa kwenye umri wa  miaka 20 na 25 ambapo aliye na umri wa kati ya miaka 35 na 40  ana uwezekano wa kupata ujauzito kwa asilimia 10 tu.

Ugumba wa asili Primary infertility.
Ugumba huu hujulikana pale ambapo mwanaume na mwanamke hawajawahi kutungisha mimba kabisa maishani mwao licha ya kujamiiana kwa muda wa mwaka mmoja tena bila kutumia kinga yoyote ile ya kuzuia kupata mimba.

Jinsi mimba inavyotungwa
Mimba hutungwa baada ya mwanamke kutoa yai kutoka sehemu maalum ya kutengenezea mayai ya kike iitwayo kitaalamu Ovaries, kitendo hiki hujulikana kama Ovulation.
Baada ya hapo husafiri hadi kwenye mfuko wa uzazi ujulikanao kama Uterus (womb) kupitia kwenye mirija ya uzazi iitwayo kitaalamu  Fallopian.
Mbegu moja (sperm) ya kiume ni lazima itungishe au iungane (fertilize) na yai au mayai ya kike (ovum au ova) wakati yai likielekea kwenye Uterus. Baada ya mbegu ya kiume na yai la kike kuungana, muunganiko uliotengenezwa yaani Embryo hushuka mpaka kwenye mfuko wa uzazi na kujiwekeza hapo.

Sunday, July 12, 2015

A New Study Shows That Use of Mobile Phones Could Cause Cancer.

Weizmann Institute of Science in Rehovot
A new study published by New Scientists states that the use of mobile phones for a long duration could eventually cause cancer.


The study which was conducted by Weizmann Institute of Science in Rehovot, Israel revealed that using the mobile phone for a meager five minutes could generate cell growth or division through particular pathways that are often used by cancer only.

Prof Rony Seger
Prof Rony Seger from the Weizmann Institute along with his colleagues exposed rat and human cells to electromagnetic radiation of 875 megahertz, which is similar to that emitted by cell phones, but at only about one tenth of the power.



Just within five minutes of exposure to the radiation ended up in the generation of extra-cellular signal-regulated kinases (ERK1/2) - natural chemicals that stimulate cell division and growth.

Since the power is low, thereby not being able to produce considerable amount of heat to affect the cells or tissue, the effect was believed to come from the radiation itself, as per the researchers.

Prof Seger stated, "The real significance of our findings is that cells are not inert to non-thermal mobile phone radiation. We used radiation power levels that were around one tenth of those produced by a normal mobile. The changes we observed were clearly not caused by heating."

The pathways involving extracellular signal-regulated kinases ERK1/2 even though they exist naturally are often used by cancer. ERK1/2 is a naturally occurring chemical that stimulates cell division and growth. Even though activation of these pathways does not always lead to the development of cancer, the effect of the cell phone radiation may perhaps in the long run increase the risk.

In that case one wonders how are there yet so many people on the face of this earth. If such less mobile phone talking can lead to so much damage, then perhaps the earth should be a much emptier place.

Learn How to Protect Yourself from harmful Radiation
Emitted by your Cell Phone, Cell Towers, and Wireless
Radiation.

www.emfnews.org

Research Center For Wireless Technology
355 Hukilike Street Suite 206
Kahului,HI 96732
USA

Kuzuia na Kudhibiti Kupanda Kwa Shinikizo La Damu.

Shinikizo la damu ni msukumo wa damu kwenye kuta za mishipa. Shinikizo la damu laweza kupimwa kwa ukanda wa mpira unaoweza kujazwa hewa. Ukanda huo hufungwa kwenye sehemu ya juu ya mkono na kuunganishwa na kifaa cha kurekodi shinikizo. Kifaa hicho hurekodi vipimo viwili. Kwa mfano, chaweza kurekodi kipimo cha 120/80. Nambari ya kwanza huonyesha kipimo cha shinikizo la damu wakati moyo unapopiga (systole). Nambari ya pili huonyesha kipimo cha shinikizo la damu katikati ya mapigo ya moyo (diastole). Shinikizo la damu hupimwa kulingana na milimeta za zebaki. Madaktari husema kwamba shinikizo la damu ya mgonjwa limepanda wakati kipimo kinapozidi 140/90.
Nini hupandisha shinikizo la damu? Hebu wazia unamwagilia shamba lako maji. Unapofungua mfereji au unapopunguza ukubwa wa shimo la mfereji, unaongeza shinikizo la maji. Ndivyo ilivyo pia na shinikizo la damu. Shinikizo la damu hupanda wakati damu nyingi inapopita mshipani au wakati mshipa unapokuwa mwembamba. Mtu hupataje ugonjwa huo? Mambo mengi yanahusika.

Mambo Usiyoweza Kuepuka
Watafiti wamegundua kwamba iwapo mtu ana watu wa familia wenye tatizo la kupanda kwa shinikizo la damu, basi anakabili uwezekano mkubwa zaidi wa kupata ugonjwa huo. Takwimu zinaonyesha kwamba mapacha wanaofanana hupata ugonjwa huo zaidi ya mapacha wasiofanana. Uchunguzi mmoja ulizungumza juu ya “kuchunguza habari zinazopatikana katika chembe za urithi ambazo husababisha tatizo la kupanda kwa shinikizo la damu.” Hiyo inathibitisha kwamba kuna chembe za urithi zinazosababisha tatizo la kupanda kwa shinikizo la damu. Inasemekana kwamba uwezekano wa kupata tatizo hilo huongezeka mtu anapozidi kuzeeka, na kwamba wanaume weusi wanakabili uwezekano mkubwa zaidi wa kupata ugonjwa huo.

Mambo Unayoweza Kuepuka
Tilia maanani lishe bora! Shinikizo la damu ya watu fulani linaweza kupanda wanapokula chumvi (sodiamu). Hiyo inahusu hasa wagonjwa wa kisukari, watu ambao shinikizo la damu yao hupanda sana, wazee, na watu fulani weusi. Mafuta mengi katika damu yanaweza kufanyiza utando wa kolesteroli kwenye kuta za ndani za mishipa. Hivyo, mishipa huwa myembamba na shinikizo la damu huongezeka. Watu ambao ni wazito kupita kiasi kwa asilimia 30 wanaweza kupata tatizo la kupanda kwa shinikizo la damu. Uchunguzi mbalimbali unaonyesha kwamba kula vyakula vingi vyenye potasiamu na kalisi kwaweza kupunguza shinikizo la damu.

Uvutaji wa sigara unaweza kusababisha utando mgumu wa mafuta kwenye kuta za mishipa, ugonjwa wa kisukari, mshtuko wa moyo, na kiharusi. Kwa hiyo, mvutaji wa sigara aliye na tatizo la kupanda kwa shinikizo la damu anaweza kupata magonjwa ya moyo. Ijapokuwa uthibitisho unapingana, mfadhaiko na kafeini—inayopatikana katika kahawa, chai, na vinywaji vya kola—yaweza kusababisha tatizo la kupanda kwa shinikizo la damu. Kwa kuongezea, wanasayansi wanajua kwamba kunywa kileo mara nyingi na kupita kiasi na kutofanya mazoezi kwaweza kuongeza shinikizo la damu.

Kutunza Afya
Si jambo la busara kungoja hadi upate tatizo la kupanda kwa shinikizo la damu ndipo uanze kuchukua hatua zinazofaa. Mtu anapaswa kutunza afya toka anapokuwa kijana. Kutunza afya sasa kutafanya maisha yako yawe mazuri wakati ujao.

Mwafikiano wa Tatu wa Brazili Kuhusu Kupanda kwa Shinikizo la Damu ulionyesha mabadiliko fulani maishani ambayo yanaweza kupunguza tatizo hilo. Madokezo hayo yatawasaidia watu wasio na ugonjwa huo na wale wanaougua ugonjwa huo.

Watafiti walipendekeza kwamba watu walionenepa kupita kiasi wanapaswa kula lishe kamili isiyo na kalori nyingi, kufanya mazoezi ya kiasi kwa ukawaida, na kuepuka mbinu za kupunguza uzito haraka. Walipendekeza kwamba watu watumie gramu sita tu za chumvi au kijiko kidogo tu cha chumvi kila siku.* Hiyo inamaanisha kutumia kiasi kidogo tu cha chumvi wakati wa kutayarisha mlo, na pia kutokula sana vyakula vinavyouzwa makoponi, nyama baridi zilizopikwa (salami, hemu, soseji, na kadhalika), na vyakula vilivyokaushwa kwa moshi. Mtu anaweza kupunguza matumizi yake ya chumvi kwa kuepuka kuongeza chumvi anapokula na kwa kuchunguza vibandiko vilivyowekwa kwenye makopo ya vyakula vilivyotengenezwa viwandani ili kuona kiasi cha chumvi ambacho kimetumiwa.

Vilevile, Mwafikiano wa Brazili ulidokeza kula vyakula vingi vyenye potasiamu kwa kuwa vinaweza “kuzuia kupanda kwa shinikizo la damu.” Kwa hiyo, lishe bora yapaswa kuhusisha “vyakula vilivyo na chumvi kidogo na potasiamu nyingi,” kama vile maharagwe, mboga za kijani iliyokoza, ndizi, matikiti, karoti, viazi-sukari, nyanya, na machungwa. Ni muhimu pia kutokunywa kileo kupita kiasi. Watafiti fulani wanasema kwamba wanaume walio na ugonjwa wa kupanda kwa shinikizo la damu hawapaswi kunywa zaidi ya mililita 30 za kileo kila siku; wanawake na vilevile watu ambao si wazito sana hawapaswi kunywa zaidi ya mililita 15 za kileo.*

Mwafikiano wa Brazili ulikata shauri kwamba kufanya mazoezi ya mwili kwa ukawaida hupunguza shinikizo la damu na hupunguza uwezekano wa kupata ugonjwa wa kupanda kwa shinikizo la damu. Kuna faida kufanya mazoezi kwa kiasi kama vile, kutembea, kuendesha baiskeli, na kuogelea, kwa siku tatu hadi tano kila juma kwa muda wa dakika 30 hadi 45.* Mambo mengine yanayochangia afya bora yanatia ndani kuacha kuvuta sigara, kudhibiti ugonjwa wa kisukari na kiasi cha mafuta katika damu (kolesteroli na triglyceride), kula vyakula vyenye kalisi na magnesi ya kutosha, na kuepuka uchovu na kufadhaika kupita kiasi. Dawa fulani zaweza kuongeza shinikizo la damu, kama vile dawa za kuzibua pua, dawa za kutuliza kiungulia zilizo na sodiamu nyingi, dawa za kudhibiti hamu ya kula, na dawa za kumaliza maumivu ya kichwa na kichefuchefu zilizo na kafeini.

Kwa wazi, iwapo shinikizo la damu yako hupanda, daktari wako anaweza kukushauri kuhusu lishe na mazoea yako kulingana na mahitaji yako binafsi. Hata hivyo, kutunza afya tangu ujanani ni jambo lenye manufaa kwa watu walio na tatizo la kupanda kwa shinikizo la damu na kwa washiriki wote wa familia. Marian, aliyetajwa mwanzoni mwa makala hii, alilazimika kufanya mabadiliko maishani mwake. Ijapokuwa yeye ni mgonjwa, sasa anatumia dawa na anafurahia maisha. Vipi wewe? Endelea kudhibiti shinikizo la damu yako huku ukisubiri wakati ambapo watu wote watakuwa na afya bora na “hapana mwenyeji atakayesema, Mimi mgonjwa.”—Isaya 33:24.

KUPAMBANA NA UGONJWA WA KUPANDA KWA SHINIKIZO LA DAMU

1. Mambo Yanayoweza Kusaidia Kudhibiti Kupanda kwa Shinikizo la Damu

• Punguza uzito wa mwili
• Punguza kiasi cha chumvi unachotumia
• Kula vyakula vingi vyenye potasiamu
• Usinywe sana vileo
• Fanya mazoezi kwa ukawaida

2. Mambo Mengine Yanayoweza Kusaidia Kudhibiti Shinikizo la Damu
• Tumia vidonge vyenye kalisi na magnesi
• Kula vyakula vyenye makapi mengi tu
• Dhibiti mfadhaiko

3. Madokezo ya Ziada
• Acha kuvuta sigara
• Dhibiti kiwango cha kolesteroli mwilini
• Dhibiti ugonjwa wa kisukari
• Usitumie dawa zinazoweza kuongeza shinikizo la damu

Wednesday, July 8, 2015

Mtanzania mwenzangu, Tambua Matunda na Faida Zake.

The Fadhaget Sanitarium Clinic ikiongizwa na Dk. Fadhili Emily inapenda kukujuza kidogo faida za matunda mwili mwako. Karibu


Dk. Fadhili Emily

AFRIKA imejaaliwa mimea, madini, rutuba na hali ya hewa safi, ikiwa ni urithi tangu enzi na enzi. Pamoja na bara hili kujaa vyakula vyote vinavyohitajika na wanadamu, bado uhai wa watu wake wengi ni mfupi.

Katika orodha ya wastani wa maisha iliyowahi kutolewa na Shirika la Ujasusi Marekani (CIA) na Umoja wa Mataifa (UN) mwaka 2011, nchi zinazoongoza kwa maisha marefu ni Japan. Wajapani wanaishi hadi miaka 90 na kuendelea, Ulaya, Marekani na China kati ya 75 hadi 90, nchi za bara Asia mathalan India wanaishi miaka 65 na Tanzania ikiwekwa katika wastani wa miaka 50 hadi 53.
Wajapani wanasifika kwa kula vyema, hawali vyakula vyenye mapishi ya mambo mengi, ulaji wao ni mdogo mdogo, wa mara kwa mara, hawajazi sana matumbo na siri yao kubwa ni ulaji wa vyakula ambavyo husaidia kukarabati na kuhifadhi mwili, ikiwemo mimea ya baharini. Mmea mkubwa ambao Wajapani uhutumia unaitwa Kombu ambao unachemshwa na kutumia maji yake kwa kupikia mchuzi, chai na uji.

Moja ya faida ya Kombu ni kukinga na kuuponyesha mwili kutokana na maradhi, kuongeza nguvu za nywele, ngozi na maisha na ndiyo sababu hasa wataalamu wanaeleza kuwa ni nadra kumwona Mjapani asiyekuwa na nywele nyingi.

Vitu vinavyosaidia mwili
Mbegu mbichi za maboga zina faida sana mwilini; kwa kutoa mafuta asilia yasiyodhuru moyo, kutoa kinga ya maradhi, ujenzi na kukarabati ngozi, mifupa, kucha, nywele, kuupa mwili nguvu za rijali. Kiafya kila mtu anatakiwa ale matunda ya aina tano kwa siku ili kupata faida zote mwilini. Matunda humeng’enywa kwa vimeng’enyo tofauti na vyakula mama kama wanga na protini. Faida kuu za matunda ni kuzuia maradhi, kurutubisha, kinga ya mwili, sukari, nguvu na mafuta asilia. Faida nyingine ni madini na vitamini mbalimbali yanayosaidia kujenga, kukarabati na hata kuzuia bakteria na maadui wakubwa wakubwa wa miili.

Cherry
Tunda la ‘Cherry’ hupendwa sana na ndege na lina faida nyingi ambazo husaidia kupambana na maradhi yanayosakama damu au mzungunguko wa maji mwilini kama Jongo. Jongo ni ugonjwa unatokana na kurithi, kunywa sana pombe, ulaji wa nyama nyekundu, mayai, kutofanya mazoezi. Ni muhimu kuzingatia kwamba matunda yanatakiwa kuliwa yakiwa katika kitengo kimoja yaani chachu, asidi au alkali.

Matunda yenye chachu ni embe, nanasi, chungwa, zabibu na kiwi na kwa upande wa matunda yenye alkali ni tikiti maji, ndizi mbivu, tufaha, pera na strawberry. Faida za matunda haya ni kinga ya magonjwa. Husaidia kukinga na kupambana na takataka zinazotolewa na mwili au zinazotoka katika mazingira machafu. Vitamin C ni muhimu sana mwilini kwani ukosefu wake husababisha uchovu, kukosa usingizi, uvivu, kutokuwa na hamu ya kula.

Ukila matunda yenye vitamin C unapata kinga ya majeraha mwilini, vidonda hupona haraka, huboresha wajihi, haiba na nafsi ya ngozi, mifupa, meno na mzunguko mzima wa damu mwilini, hivyo kusaidia usingizi na kwa watoto kusaidia kukua vizuri. Lakini kwa tunda kama papai linasaidia kuukinga mwili na kulainisha tumbo ndiyo maana kama mtu amevimbiwa au haendi haja kubwa sawasawa, akila papai humsaidia.

Tuesday, July 7, 2015

Njia Rahisi 10 za Kupunguza Unene, Zingatia Haya.

 

UTANGULIZI.
Ugali kwa samaki; mboga ya majani ya matango kwa nyanya. Usiweke chumvi kwenye hiyo mboga mbichi ya majani.


Ni makala muhimu sana. Wastani wa maisha ya Mtanzania ( na Waafrika wengi) hata wale waliosoma au wanaojiweza kiuchumi ni miaka 40-50. Kati ya sababu kuu zinazopunguza uhai wetu ni afya, unene na kutojua kujiangalia vyema afya zetu.


1-ULAJI
Ipo mifumo miwili ya kula. Chakula unachokula na namna unavyokila.

Unavyokula.
-Kuna kula vyakula vidogo vidogo vyenye madini, vitamini, mafuta nk mara nyingi kwa siku; au kula milo michache (mmoja au miwili) mikubwa ili kujaza tumbo. Ulaji mdogo mdogo husaidia afya na kuingia mwilini vyema kuliko ulaji mkubwa wa mara chache.

Tumbo lina musuli zinazofanya kazi kama mashine au mnyama. Gari likijaa sana hupata taabu kwenda. Punda hivyo hivyo. Ulaji mdogo mdogo unaosambazwa mara kadhaa kwa siku ni bora maana mwili unachambua kila kitu kwa wepesi na haraka. Unapokula milo michache mikubwa unapalilia zaidi mafuta mwili.

PENDEKEZO la kwanza.
Asubuhi, kunywa maji kwanza, matunda, kisha ndiyo chai na vitu vingine kama mkate au maandazi). Wapo wanaodai kwamba wanakula matunda na mboga.
Tatizo ni kwamba mipangilio yao huwa ya makosa. Mathalan wengi hula matunda baada ya chakula.

Vimeng’enya chakula (enzymes) tumboni hufanya kazi namna tofauti. Mathalan vile vinavyonyambua matunda ni tofauti na vinavyomeng’enya vitu vigumu zaidi kama nyama au wanga. Matunda hunyambuliwa haraka zaidi kuliko vyakula vingine.

Hivyo ni bora kula matunda dakika10-20 kabla ya chakula. Ukila baadaye matunda hugeuzwa aina fulani ya pombe (fermented food) inayoelea tu juu ya chakula na kubakia kitu kingine badala ya kuingizwa haraka ndani ya damu kupitia utumbo mdogo, uwengu, moyo, ini, nk.

Tatizo jingine ni kupika sana mboga hadi zikapoteza nguvu.
-Mseto wa vyakula pia ni muhimu. Kwa mfano vyakula vyenye uchachu (“acid”) na vile vinavyomumunyuka haraka (“alkaline”) havitakiwi viliwe pamoja. Mfano ni matunda. 

Matunda chachu kama machungwa, mananasi na maembe yatakiwa yawe pamoja; na yale laini zaidi: ndizi mbivu, matikiti maji, mapapai, matufaha, nk yaende kivyake, maana yana mfumo tofauti, wa kumeng’enywa.

Hali hiyo pia iko katika nyama. Nyama nyeupe (ndege na samaki) tofauti na nyama nyekundu (ng’ombe, kondoo, nk) ziliwe tofauti.

Chakula unachokula Watanzania/Waafrika hatuna tabia ya kula mboga mboga mbichi. Tunafuata ladha na mazoea kuliko thamani.

Bara letu lina mboga na vyakula bora kuliko bara lolote duniani lakini sisi tunakufa mapema na kwa utapia mlo kuliko wale wanaotoka nchi kame. Ulaya nzima imejazana mboga mboga zinazoagizwa toka Afrika.

Kenya na Tanzania zinauza mboga za maharagwe mabichi (green beans), matunda toka Afrika Kusini na Ivory Coast; nk. Waafrika tunapenda kujaza matumbo. Unene umekithiri hata wale walio matajiri waliosoma bado wanakufa kwa kisukari shauri ya kutokula mboga mbichi.

Ulaji wa mboga mbichi ni upi ?.
Ni mathalani ulaji wa salad. Tanzania tunaita kachumbari. Lakini si lazima iwe kachumbari ya nyanya, vitunguu na chumvi tu. Waweza kuchanganya matango, nyanya kwa maparachichi; au vitunguu saumu, giligilani na karote.

Huu mseto wa mboga mbichi ni mzuri ukienda na chakula chenye nyama za minofu na wanga (ugali, wali, ndizi za kupika nk). Ulaji wa wanga asubuhi, mchana na jioni kila siku huchangia sana katika unene. 


PENDEKEZO LA 2.
Ugali kwa samaki; mboga ya majani ya matango kwa nyanya. Usiweke chumvi kwenye hiyo mboga mbichi ya majani.)

2-UNYWAJI MAJI
Waafrika hatunywi maji, hasa wanawake. Wanaokunywa maji zaidi ni wacheza michezo. Wengi wetu hunywa zaidi soda (vinywaji baridi kama Cocacola, Pepsi, Mirinda ,Tangawizi na gesi za kisasa kama Red Bull) zilizojaa gesi inayoleta vidonda tumboni; na chai. Kuliko maji.

Na maji haya hutakiwa dakika 10-20 kabla ya chakula au nusu saa kuendelea baada ya chakula. Ukila chakula huku unasakatia maji huimanisha mtu una kiu. Ulaji chakula na unywaji maji ni vitu viwili tofauti.


Ila utawaona watu wanakula huku wakibugia maji. Unapokula chakula huku unabugia maji unapunguza nguvu za chakula, unajaza tumbo maji na kuchelewesha mmeng’enyo wa chakula (digestion). Chakula kisipomeng’enywa vizuri kinaketi tu tumboni.

Matokeo wengi wetu tuna matumbo makubwa. Kama hufanyi mazoezi lile tumbo linakwenda pembeni (chini ya mbavu) hasa kwa watu wa makamo linaleta maradhi kama kisukari, kiungulia, kuvimbiwa, uyabisi wa tumbo, nk. Kizungu huitwa “love handles.”.

3-SUALA LA UMENG’ENYAJI
Chakula huanza kumeng’enywa au kusagwa (kwa lugha iliyozoeleka) mdomoni. Mate yako mdomoni ni chanzo cha uchambuaji chakula. Unapobugia chakula bila kutafuna sawasawa unasababisha mambo mawili. Moja chakula kutochambuliwa vizuri, pili chakula kwenda kukaa tu tumboni, au kama kikipita hakisaidii lolote mwilini.


Utafunaji wa taratibu husaidia umeng’enyaji. Chakula kinapofika tumboni hukaa pale dakika ishirini. Hapo huchanganywa na asidi (ya manjano iitwayo Hydrochloric) inayokibadilisha tayari kupelekwa utumbo mkubwa, kupitia kongosho.

Kule uchafu utapelekwa chini na rutuba kusafirishwa na utumbo mdogo kuelekea katika uwengu, moyo. Moyo utadunda chakula kilichoshageuzwa damu kuelekea mwilini kufanya kazi na akiba hubakishwa katika ini.

Sasa kama usipotafuna vizuri, ukila huku unakunywa sana maji au vinywaji vingine chakula hakimeng’enywi vizuri. Ndiyo maana unawaona watu wengine wanakula sana lakini hawana afya. Wanaugua ovyo ovyo, wanatoka jasho ovyo, wanajamba ovyo, wana matumbo makubwa, wanavimbiwa, wanakaa siku nyingi bila kwenda choo (inatakiwa mtu kwenda haja kubwa mara moja au mbili kwa siku) nk.

4-ULAJI WA VYAKULA VYA MAFUTA
Mafuta ni suala muhimu sana mwilini. Ila ulaji wake shurti uwe wa mpangilio. Yaani unaowiana.

Lazima mtu uwe na wastani mzuri wa vyakula vya nguvu, yaani “wanga” (ugali, ndizi, wali, viazi mbalimbali, mikate, mahindi, nk), ujenzi yaani “protini” (mboga na nyama), “madini” (mbegu mbegu mbichi si za kukaanga sana na chumvi) na “vitamini” (matunda, maziwa, mayai, nk).


Waafrika tunapenda nyama. Nyama ni muhimu sana maana ina madini aina ya chuma (nyama nyekundu) protini,nguvu na mafuta. Ila mafuta yaliyoko katika nyama mara nyingi si mazuri shauri hayatoki, huganda.

Chukua nyama ya kuku na samaki ambayo huwa na ngozi. Wengi wetu hupenda sana kula ile ngozi ya wanyama hawa kwa kuwa tamu. Lakini haya ni mafuta mabaya.
Mafuta ya samaki lakini ni mazuri. Samaki anayo mafuta ya Omega-3 ambayo husaidia mwili na kinga maradhi mwilini.
Tunapokula nyama choma au ya kukaanga, lazima tule pia mboga za majani (mbichi) na si vizuri kula nyama kila siku. Kama huwezi kukaa bila nyama kila siku, fanya mazoezi ya mwili.

PENDEKEZO LA 3.
Kula mbegu mbegu za korosho, karanga (ziwe mbichi badala ya kukaanga na chumvi) kati kati ya siku. Haya ni mafuta yenye rutuba mwilini kuliko nyama za mafuta.

5-MAZOEZI YA MWILI NA VIUNGO.
Mazoezi ni mfalme wa kupunguza unene.
Ukiwauliza wengi watakuambia wanafanya kazi ngumu za sulubu (wanachuruzikwa jasho) kwa hiyo hayo ni mazoezi. Ila kazi na mazoezi ni vitu viwili tofauti. Ingekuwa kufanya kazi ni mazoezi basi kusingekuwa na wastani mfupi wa maisha kwa maskini hasa sisi Waafrika.

Wengine watadai kwamba walipokuwa wadogo shuleni walifanya mazoezi sasa wamekuwa watu wazima (miaka 40 kuendelea) kwamba eti mazoezi ni suala la ujana; kumbe kadri unavyokuwa ki umri ndivyo kadri unavyotakiwa kufanya mazoezi na kujitazama zaidi kiafya.


Watazame Wachina na Wajapani wanavyoishi maisha marefu.
Mazoezi ni shughuli inayokufanya kwanza uheme (mapafu na moyo kwenda kasi), viungo na mifupa kujinyoosha (stretching), kutoka jasho na usafishaji wa damu.

Mazoezi yanayosaidia haya ni pamoja na kutembea kasi, kukimbia, kuogelea, michezo mbalimbali ya riadha (kama mpira wa miguu, nyavu, kikapu, mikono, nk); michezo ya kupigana na kujilinda yaani masho ati(karate, kung fu, judo, capoeira, krav maga, jiu jitsu, systema, kickboxing, thai boxing, kempo, kalari payatu, aikido, nk.

Ni muhimu mwanadamu ufanye mazoezi makali ya viungo mara mbili tatu kwa juma. Si vizuri kufanya kila siku kwani musuli na mishipa inahitaji kupumzika na kukua.
Kama unapenda kuinua vyuma lazima uwe na mwalimu wa kukuelekeza; na si vizuri kufanya kila siku. Wastani wa mara mbili tatu kwa juma inatosha kabisa.

6-UPO UFANYAJI MAZOEZI WA AINA MBILI
Mazoezi ya nguvu ya kuhema niliyotaja hapo juu (cardio-vascular) na yale laini ya kujinyoosha yaani ambayo hutumia zaidi nguvu za ndani na pumzi. Haya ya pili ni kama Yoga (India), Tai Chi Chuan (China) na aina mpya mazoezi iliyoanza Majuu miaka ya karibuni yaani Pilates (hutamkwa hivyo hivyo ilivyoandikwa Pilates). Haya laini yanawafaa zaidi watu wazima na nchini China na Japan mathalan utawakuta wazee wa miaka 80 hadi 90 bado wanayafanya. Husaidia moyo, damu na akili.


Michezo na mazoezi ya mwili ni njia kuu ya kupunguza unene, kurefusha maisha, kuchangamsha ubongo, kupunguza ulevi, uvutaji sigara, dawa za kulevya, tabia mbaya za uvivu, ugomvi, nk. Mataifa yenye watu wanaofanya mazoezi kama Japan, Brazili, India, China nk huwa na wachapa kazi wengi na wananchi wanaoipenda jamii yao.

7-KULA SANA CHUMVI SI VIZURI
Ulaji chumvi mwingi hutokana na suala la ladha. Kisayansi vyakula vyote vina chumvi asilia sema tu tumezoea kuongezea madini hii iitwayo Sodium. Sodium inachangia sana kufupisha maisha.

Huifanya mishipa ya damu ichoke; ni kama bomba lolote la maji ukilitazama baadaye hugeuka rangi kutokana na yale maji kupita pale kila siku.


Kwa wale tunaoishi nchi za joto na kutoka sana jasho kula chumvi ni muhimu. Ila tatizo letu ni kwamba hatunywi maji ya kutosha. Mtu ukiwa na kiu unakunywa soda au kinywaji cha sukari; inakuwa kama unaendelea kuutesa mwili.

Kwa vipi? Mishipa inayopitisha damu mwilini badala ya kusaidiwa kwa maji inawekewa kazi zaidi ya kusafisha sukari na chumvi. Ndiyo maana vifo vingi vinatokea mapema; wastani wetu wa maisha haupiti miaka 50.

Utafiti uliofanywa chuo kikuu cha California, Marekani mwanzoni mwa 2010, umethitibisha kwamba vifo vingi duniani husababishwa na maradhi ya moyo na saratani ambavyo hutokana na uvutaji sigara, unene, ulevi na ulaji sana wa chumvi na sukari. Tukipunguza ulaji wa chumvi tunasaidia pia kupunguza maradhi ya moyo, utafiti unasema.

8-TAFITI ZA VYUO KADHAA ULIMWNGUNI KUHUSIANA NA AFYA.

-Jarida la Kimarekani la sayansi lilieleza mwaka jana kwamba utapunguza ugonjwa wa moyo (ambao husababishwa na unene , wasiwasi na purukshani) kwa asilia mia 42 kama utakula matunda na mboga za majani peke yake kila siku, juu ya msosi wa kawaida.


PENDEKEZO LA KULA- Na 4.
Kula mlo wako. Baada ya saa mbili au tatu, sakatia tunda au matunda; baada ya mlo mwingine, kula sahani ya mseto wa mboga mbichi kama karote na matango. Utaona tofauti ya afya, ngozi, wajihi, kinyesi, usingizi, nk. Kidesturi tumezoea kunywa chai au soda za sukari sukari na gesi kati kati nya milo badala ya matunda na mboga mbichi za majani).

-Utafiti uliofanywa na wanasayansi chuo kikuu cha South Carolina mwanzo wa mwaka 2010 kuhusu faida za kuogelea.

Zoezi la kuogelea lina faida zaidi ya kukimbia au kutembea kwa vile huchanganya mazoezi makali na pumzi, kusaidia mapafu na moyo. Utafiti ulithibitisha kuogelea hupunguza hatari za kifo kwa asili mia hamsini.

-Utafiti wa jarida la chuo cha uganga Ulaya umeeleza (desemba 2009) kwamba kulala nusu saa kila mchana (“nap”) husaidia kupunguza ugonjwa wa moyo kwa asilimia 37.

-Uchunguzi wa chuo cha michezo cha Hispania mwanzoni mwa 2010 umethibitisha kwamba ukikimbia mara tatu kwa juma (jogging) unaongeza nyege mwilini kwa asili mia 75. Hasa kwa watu wa makamo mnaoanza kupoteza nguvu za urijali.

-Uchunguzi chuo kikuu cha Leeds, Uingereza mwanzoni mwa 2010 umeonyesha unapotembea kwa miguu, ukikwepa barabara kubwa zisisokuwa na mioshi ya magari (pollution) unapunguza matatizo ya maradhi ya hewa chafu kama pumu, mapafu na appendix.
-Uchunguzi wa chuo kikuu cha Texas mwaka 2010 umegundua kwamba kula tunda la divai nyekundu mara kwa mara husaidia kupunguza kupata ugonjwa wa kisukari.

-Hapo hapo tunaelezwa kwamba watu weusi na bara la Asia wanakumbwa zaidi na ugonjwa wa kisukari kutokana na vinywaji vya sukari sukari na gesi (fizzy drinks). Ukinywa kiasi cha miligramu 300 za vinywaji hivi (Cocacola, Red Bull, Fanta, nk) kwa siku unajitahadharisha kupata kisukari.

9-KUFUNGA
Neno kufunga linatambuliwa rasmi kuhusiana na Waislamu (mwezi Ramadhani) au Wakristo (Lenti nk). Ufungaji huo una masharti mengine ya kidini tofauti na haya ya kiafya.

Mathalani wafungaji hawa hula chakula kingi usiku; ukihesabu wanafunga wastani wa saa 12 tu. Kawaida ukitaka virusi na takataka nyingine mwilini zitoweke, au viungo vipumzike wahitaji saa 20 kuendelea.

Ufungaji ninaouongelea ni ufungaji wa kutokula kabisa kwa saa 24, 36 hadi 48 kuendele


Ufungaji ni nini?

Kama mashine yeyote mwili wa mwanadamu unahitaji kupumzika na kujisafisha. Hata tukiwa tumelala bado viungo mbalimbali mwilini vinafanya kazi. Kwa hiyo faida ya kwanza kabisa ya kufunga ni kuupumzisha mwili kama mfanyakazi yeyote anapokwenda likizo.

Faida ya pili ya kufunga ni kusafisha mwili kutokana na uchafu ambao haukutoka (kinyesi hakitoi mabaki yote toka utumbo mkubwa), dawa na takataka za mazingira tunayoyavutia hewa, virusi au kuyanywa katika maji na vyakula mbalimbali na pia uchafu wa hisia, yaani hasira, huzuni, nk.
Kuna ufungaji wa aina mbalimbali.

1-Kufunga kwa kunywa maji tu, saa 24 kuendelea…
2-Kufunga kwa kutokunywa maji au kula chochote, saa 24 kuendelea.
3-Kufunga kwa kula tu matunda au mboga zilizopondwa kama karote, matango nk, saa 24 kuendelea.

Ufungaji huu unatakiwa ufanywe kwa mpangilio. Kitu muhimu si tu kufunga bali NAMNA unavyofungua. Ukianza kula tena, unaanza taratibu. Kawaida ni vizuri kuanza na maji, kikombe au bilauri ya kwanza taratibu. Subiri tena nusu saa, bilauri nyingine, halafu hadi ya tatu, halafu ndiyo matunda yasiyo ya chachu, na kadhalika. Kuanza kufungua kwa kunywa chai ya maziwa, uji au vyakula vingine vya wanga hakusadii sana mfungo huu.
Maana lengo lake ni kusafisha mwili.

PENDEKEZO LA 5.
Kwa wenye imani za kidini. Unaweza pia kufunga hivi ukawa pia unasali au kuvaa mavazi yanayokufanya mtu wa amani. Ukifanya hivi unajitakasa kimwili na kiroho. Si lazima ungojee ile miezi ya kufunga na wengine.

10-USINGAJI
Usingaji au masaji ni njia nzuri sana ya kupunguza unene. Ikiwa unaangalia namna unavyokula, unafanya mazoezi na kusingwa mara moja au mbili kwa mwezi unaupalilia mwili vizuri. Nini faida ya usingaji? Kusinga husaidia ngozi, mishipa ya damu na sura nzima ya mwili na taswira yako mwanadamu.

Wengi wetu tunaposikia neno kusinga tunafikiria usingaji wa mapenzi. Hivi ni vitu viwili tofauti kwani usingaji wa mapenzi unaimanisha mahusiano ya kihisia.


Kifupi mwanadamu unatakiwa uwe unautunza na kuungalia mwili wako kama nyumba au hekalu lako. Wengi wetu tunaoga, tunajipaka marashi, tunasuka, tunanyoa nywele au ndevu; lakini miili yetu kiundani inaoza taratibu.

Kama alivyosema mpiganaji, msanii, mwanafalsafa, mwigizaji, mwandishi mashuhuri marehemu Bruce Lee katika shairi lake Mazingira Yako Kimya (toka kitabu “Msanii wa Maisha”, Turtle Publishing, 2001):

Thursday, July 2, 2015

The Fadhaget Sanitarium Clinic Inapatikana Zaidi ya Mikoa 10 Nchini Tanzania.

 

 The Fadhaget Sanitarium Clinic katika kuhakikisha inatoa huduma zake kwa kila mmoja, na kuweza kukufikia karibu na kutoa huduma ya matibabu inahakikisha inasambaa mikoa yote na kuwa karibu na watu wote kwa pamoja. Katika mikoa zaidi ya 10 kwa Tanzania, The Fadhaget Sanitarium Clinic imeweza kuweka vituo vyake vikuu na kuhakikisha inakupa huduma bora kabisa. 

Kwa watu kutoka mikoa mbalimba mnaweza KUBONYEZA HAPA KUTAZAMA VITUO VYETU VILIVYO KARIBU NA WEWE.