Karibu Fadhaget Sanitarium Clinic

Tunapenda kukukaribisha katika Kitengo cha Sayansi ya Tiba Asilia.

Kitengo Cha Sayansi Ya Tiba Asilia

Kwa Muda mrefu tumekuwa tukisaidia wengi katika matibabu na kutengeneza dawa bora kabisa kiafya.

Je Unapenda Kufahamu Jinsi Ya Kupata Mapacha?

Tunafundisha jinsi ya kupata jinsia unayotaka, jinsi ya kupata mtoto kama umekosa mtoto kwa muda mrefu. Pia hata jinsi ya kupata watoto mapacha tunaweza kukusaidia.

Tunapatikana Katika Mikoa Zaidi ya 10 Tanzania

Tunazidi kuongeza matawi yetu nchini Tanzania na Nje ya Nchi. Kwa sasa tunapatikana katika mikoa zaidi ya 10 na tunazidi kuongeza matawi yetu. Karibu sana.

Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Sunday, March 29, 2015

KANISA LA GOSHENI ENTERNATIONAL MINISTRY LA AZIMISHA KUTIMIZA MWAKA MMOJA WA HUDUMA

Leo katika kanisa la Gosheni Enternational Ministry lililoko Kimara Jijini Dar es Salaam wamesherekea mwaka mmoja wa huduma ya injri Tanzania Tangu kuanzishwa kwake.
kanisa hilo lilianza kwa huduma ya kinamama sita mpaka sasa lina zaidi ya Wahumini 50 wakiwemo wamama ,vijana ,wanaume na watoto likiwa na lengo la kusambaa Tanzania nzima na baadae kupanuka katika nchi nyingine Afrika na hata ughaibuni.

Akiongea na blog hii kanisani Mchungaji wa kanisa hilo Mch: Flora Kisui amesema kanisa hilo lina nia ya dhati ya kutangaza injiri ya kweli na kuinua vipaji vya huduma ya dini katika kuhubiri,kusambaza neno la Mungu na Uimbaji.

Tazama picha za matukio ya leo....Na Lonely Nzali

Dr.Kisui akifundisha neno la mungu


Mch: Frola Kisui Kiongozi wa kanisa la Gosheni akihubiri



Keki ilikatwa na Happy Birthday Gosheni Ikatimizwa


Mch Frola Na Dr.Kisui wakikata keki 

Upendo ulioneshwa kwa kila mtu


Kikundi cha vijana wajasiliamari cha UBORA

Kumbukumbu pia iliwekwa





Wednesday, March 25, 2015

MUME ALIVYOMFANYIA UKATILI MKEWE

Na Hamida Hassan
HUU ni ukatili uliopitiliza! Mwanamke mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Neema Mwita, anateseka katika Hospitali ya Mkoa wa Mara kufuatia jereha kubwa alilopata baada ya mumewe aliyemtaja kwa jina la Juma Mwita kummwagia uji wa moto kisa kikiwa ni kuchuma mahindi shambani bila ridhaa ya mumewe huyo.Akizungumza na Uwazi huku akimwaga machozi kila wakati, mwanamke huyo alisema siku ya tukio, yeye na mumewe walikuwa kazini na mwanaume huyo ambaye alipata tenda kubwa ya kufyatua matofali.


Neema Mwita akihojiwa.

MSIKIE MWENYEWE
“Nilikuwa nakusanya majani. Baada ya kukusanya kwa muda mrefu ambapo niliagizwa na mume wangu, niliamua kwenda shambani kuchuma mahindi kisha nikarudi nyumbani kupika chakula cha mchana ili akitoka kazini ale.

“Nikiwa jikoni nasubiri uji uchemke ili nisonge ugali, mume wangu alirudi ghafla na kuanza kunigombeza eti kwa nini nilichuma mahindi shambani na nilirudi nyumbani bila ridhaa yake?” alisema na kuanza kulia.

MUME ACHUKUA UJI WA UGALI
Mwanamke huyo aliendelea kusema: “Alinihoji ni kazi gani kubwa niliyoifanya kule kwenye matofali mpaka nikaamua kurudi nyumbani. Kabla sijajibu aliifuata sufuria yenye uji unaochemka jikoni na kunimwagia ambapo ulitua kifuani kwangu na kuniunguza vibaya, kama unavyoona. Sijajua mume wangu alikusudia nini kunifanya hivi!”

JIRANI AMWOKOA
Mwanamke huyo aliendelea kusema kuwa, baada ya kumwagiwa uji huo na kuungua, alianguka chini na kulia kwa maumivu, ndipo jirani yake mmoja alimwona akihangaika na kumchukua hadi ndani.

AKAA NYUMBANI SIKU SABA
“Ndani nilikaa kwa wiki nzima, maumivu yalikuwa makali sana. Ndipo wazazi wangu walipopata taarifa wakaja kunichukua. Hata hivyo, wazazi wangu nao hawakunipeleka hospitali, waliniweka nyumbani na kuniletea mganga wa kienyeji.”


Mwandishi akizidi kumuhoji Neema Mwita.

MUME AKIMBILIA KUSIKOJULIKANA
Neema alisema mumewe aliyeoana naye kwa upendo na kiapo cha kuishi katika shida na raha mpaka kufa, alikimbia baada ya tukio hilo na hajawahi kuonekana mpaka sasa ambapo polisi wanaendelea kumsaka usiku na mchana.

TAARIFA ZINAFIKA SERIKALINI
Mwanamke huyo ambaye kutokana na kuungua huko mishipa yake ya sehemu ya kidevuni imeshikana na ya shingo, alisema baada ya wiki moja, taarifa zilimfikia Mwenyekiti wa Kijiji cha Nyamisanga, Boke Chacha ambaye alimchukua mikononi mwa wazazi hao na kumpeleka hospitali kwa matibabu.

LICHA YA KUUNGUA, AMETELEKEZWA
Neema, anasikitisha sana kwani licha ya kupitia kipindi hicho kigumu, anadai ametelekezwa na wazazi wake na mtu anayemsaidia ni mwanaye wa kiume anayeitwa Wambura Juma aliyekuwa akisoma kidato cha tano.
“Mtoto wangu huyu kwa sasa hasomi kwa sababu ya kunisaidia mimi, alilazimika kuacha masomo toka tukio hili liliponitokea,” alisema Neema.

ANA MIEZI NANE HOSPITALINI
Neema anasema tangu alazwe hospitalini hapo, sasa ni mwezi wa nane lakini anamshukuru Mungu ameanza kujikongoja kutembea japo kwa taabu sana.

Muonekano wa jeraha alolipata Neema baada ya kuunguzwa na mumewe kwa uji wamoto.

MADHARA ALIYOYAPATA
Neema amepata madhara makubwa kufuatia tukio hilo kwani kwa sasa mkono wa kulia haukunjuki sawasawa kama zamani, hawezi kunyoosha shingo kutokana na nyama za shingo kuungana na kidevu, mdomo wake umepinda kidogo huku titi la upande wa kulia likiwa halipo tena!

APATIWA SIMU YA MKONONI
Joyce Kiria ni Mtangazaji wa Kipindi cha Wanawake Live kinachorushwa hewani na Runinga ya EATV, alimtembelea Neema hospitalini na kumpa msaada wa simu ya mkononi ili iwe rahisi kwa wale watakaojitokeza kutaka kumsaidia kwa ajili ya pesa za matibabu kutumia simu hiyo. ANAHITAJI MSAADA
Ndugu msomaji, Neema anahitaji msaada wako wa hali na mali. Kama utakuwa na chochote na umeguswa na maumivu yake, unaombwa kutumia mawasiliano yake 0656 151 072 au 0756 768 305

HAYA NDIYO MAAJABU YAKE MTOTO ALIYENUSURIKA KWA MKONO WA MUNGU




Na Haruni Sanchawa
MTOTO Jacqueline Lepenza, aliyenusurika katika ajali mbaya ya basi lililogongana na lori huko Mafinga mkoani Iringa wiki mbili zilizopita, ameripotiwa kuwa na maajabu baada ya baba yake mzazi kujitokeza na kusimulia, Uwazi linakutaarifu.


Jacqueline Lepenza, akiwa na baba'ke.

Willy Lupenza, baba mzazi wa mtoto huyo mwenye umri wa miaka mitatu na nusu, alisema marehemu mke wake, Anjela Osward (35) (pichani) alikuwa amekwenda nyumbani kwao Ilembula mkoani Njombe kwa ajili ya ubatizo wa binti yao huyo.

Alisema katika hali ya kushangaza, siku ya ubatizo huo, Jacqueline alibatizwa peke yake pasipo watoto wenzake kupewa baraka hizo kwa sababu ambazo hazikueleweka.“Ndugu mwandishi, hili ni tukio ambalo sitalisahau katika maisha yangu, kwa sababu haiwezekani mtoto abatizwe peke yake halafu kwenye ajali, idadi kubwa ya watu wapoteze maisha lakini yeye anusurike.”

Alisema baada ya ajali, mtoto wake huyo alikutwa na watu waliojitokeza kuwasaidia majeruhi akiwa amelala juu ya bati la kuzuia matope kwenye tairi ya lori lililokuwa limebeba kontena huku akilia na matairi yakiendelea kuzunguka.

Alisema haelewi mtoto huyo alitokaje ndani ya basi hadi kwenye bati hilo la lori, kwani licha ya kukutwa mzima, lakini eneo hilo pia lilikuwa hatarishi kwa mwanaye ambaye alimpoteza mama yake aliyekuwa mmoja kati ya watu zaidi ya 50 waliofariki dunia.


...Akiwa na bibi yake.

Willy alisema Machi 11, mwaka huu alipata taarifa kwa njia ya simu kutoka kwa shemeji yake ambaye yuko mkoani Iringa kwa shughuli zake za kibiashara juu ya tukio hilo, baada ya yeye naye kuarifiwa na Jeshi la Polisi Iringa baada ya kuokotwa kwa simu ya mkewe.

Alisema baada ya kupigiwa na polisi waliofika katika eneo la tukio mapema, shemeji yake huyo alimpigia na kumjulisha juu ya mkewe kupata matatizo Mafinga.“Nilianza safari mara moja kuelekea huko, lakini nilipofika Morogoro nilipata taarifa za uhakika zilizoniaminisha kuwa mke wangu alikuwa amefariki dunia,” alisema.

Aliongeza kuwa aliendelea kufanya mawasiliano na ndugu kujua alipo mtoto, hadi alipoambiwa kuwa kulikuwa na mtoto mmoja aliyekuwa wodini (Hospitali ya Wilaya Mafinga), hivyo akaambiwa kama anaweza kuwatumia picha yake kwa njia ya mtandao ili waweze kumfananisha.

“Niliwatumia picha kwa Mtandao wa WhatsApp, kumbe siku ya ajali mwanangu alikuwa amevaa gauni ambalo aliwahi kulivaa siku za nyuma, na ndiyo picha niliyowatumia, walimtambua kirahisi na alipofanyiwa uchunguzi wa kidaktari ikagundulika kuwa hakuwa na matatizo yoyote kiafya,” alisema baba huyo.


Mama wa Jacqueline, Anjela Osward enzi za uhai wake.

Kufuatia kufika Mafinga na kuutambua mwili wa mke wake, aliomba mwili huo kutopelekwa sehemu yoyote ili urudishwe nyumbani kwao Ilembula kwa mazishi yaliyofanyika katika Kijiji cha Mwambaga.Kuhusu hali ya mtoto kwa sasa, Willy alisema anaendelea vizuri na anamshukuru Mungu pamoja na madaktari na polisi walioshiriki katika tukio hilo ambalo mwanaye huyo alipona kimaajabu.

Ajali hiyo ilihusisha lori aina ya Scania namba T 689 APJ mali ya Cipex Company lililokuwa likiendeshwa na Maka Sebastian (26) na basi aina ya Scania namba T 438 CED mali ya Majinja lililokuwa likiendeshwa na Baraka Gabriel (38).

MAAMBUKIZI YA FANGASI SEHEMU ZA SIRI -3

WIKI iliyopita tulieleza madhara ya fangasi zehemu ya siri na jinsi ugonjwa huo unavyosumbua wanawake.
Leo tunaendelea kuelezea fangasi sehemu za siri wanavyosumbua na tuliahidi kwamba tutaeleza tiba yake.
Baada ya kueleza mengi kuhusiana na ugonjwa huu leo tutaeleza matibabu yake ambayo huusisha dawa za kutibu fangasi (antifungal drugs) kama vile dawa za kupaka za Topical Clotrimazole, Topical Nystatin, Fluconazole au Topical Ketoconazole.

Wagonjwa wenye maambukizi yasiyo makali yaani Uncomplicated Vaginal Candidiasis wanaweza kutumia dawa za kupaka (cream) za fangasi kama vile Butoconozale, Miconazole, Clotricomazole nk. Dawa hizi hutumika kwa muda wa siku 3-7 kulingana na aina ya dawa. Mgonjwa anashauriwa kupaka dawa ndani ya uke pamoja na maeneo yote yanayozunguka sehemu hiyo.

Lakini pia mgonjwa anaweza kupewa dawa za kutumbukiza ukeni ambayo atatumia kwa muda wa siku 3-14 kulingana na aina ya dawa. Dawa hizo ni pamoja na Miconazole, Tiaconazole, Terconazole, Nystatin nk.
Kwa wale wenye maambukizi makali yaani Complicated Vaginal Candidiasis, kabla ya kupewa tiba, ni muhimu kwanza kufanyiwa kipimo cha kuotesha sehemu ya uchafu unaotoka ukeni ili kuwa na uhakika kama kweli fangasi wanaosababisha maambukizi haya ni Candida Albicans ama la.

Fangasi wengine aina ya Candida Glabrata pia wanaweza kusababisha aina ya maambukizi haya na huwa siyo rahisi kutibika kwa kutumia matibabu ya kawaida na pia si rahisi kuonekana kwa kutumia hadubini (microscope).

Matibabu ya wagonjwa wenye aina hii ya fangasi hujumuisha matumizi ya dawa za kupaka (cream) au vidonge vya kuweka ukeni kwa muda mrefu, yaani kwa muda wa siku saba hadi kumi na nne.
Wengine hutibiwa kwa dawa aina ya Fluconazole ambayo hutumika kila baada ya siku tatu (yaani siku ya 1, siku ya 4 na siku ya 7). Mara baada ya kumaliza tiba hii, mgonjwa hutakiwa kuendelea nayo mara moja kwa wiki kwa muda wa miezi sita.

Ikiwa matibabu haya hayatasaidia basi mgonjwa anaweza kushauriwa kutumia mchanganyiko wa Fluconazole pamoja na dawa ya kupaka ya Clotrimazole mara mbili au moja kwa wiki kulingana na dozi ya dawa, au Fluconazole na dawa nyingine za kupaka kwa wakati mmoja.

Matibabu ya wagonjwa wenye maambukizi hatari sana yaani severe vaginal candidiasis ambayo kwa kawaida huambatana na dalili za uke kuwa mwekundu, kuvimba, michubuko ya ngozi ya ukeni (excoriation) na kutokea kwa mifereji kama vidonda (fissure formation) huwa ni dawa zozote za kupaka zilizotajwa hapo juu kwa muda wa siku 7 mpaka 14.

Pia anaweza kupewa dawa ya fluconazole ambayo hutolewa mara mbili, ambapo dozi ya pili hutolewa siku ya tatu baada ya kutolewa kwa dozi ya awali.Matibabu ya maambukizi ya fangasi ambayo hayasababishwi na Candida albicans ni dawa za kupaka jamii ya nonfluconazole azole groups kama vile Posaconazole, Voriconazole nk.

Zitolewazo kwa muda wa siku 7 mpaka 14 pamoja na kidonge cha boric acid kwa muda wa siku 14. Mtu mwenye maambukizi haya pia anashauriwa kuonana na daktari bingwa wa magonjwa ya akina mama.

WANAWAKE WAJAWAZITO
Kwa vile maambukizi ya fangasi hutokea sana kwa wanawake wajawazito, hivyo basi wanashauriwa kutibiwa kwa kutumia dawa za kupaka tu kwa muda wa siku 7.Nisisitize hapa kuwa dawa aina ya Itraconazole haipaswi kutumiwa na mwanamke mjamzito au anayekusudia kushika mimba kutokana na sababu za kitabibu.

Dawa ya Ketoconazole haipaswi kutolewa bila ushauri wa daktari kwani ina madhara ya kusababisha ugonjwa hatari wa ini. Maambukizi ya fangasi pia huonekana sana kwa wagonjwa wenye Ukimwi. Tiba ya maambukizi haya ni sawa na tiba ya watu ambao hawana ugonjwa wa Ukimwi.

USHAURI
Hata hivyo, kwa wale wagonjwa wa Ukimwi ambao wanapata maambukizi ya fangasi mara kwa mara wanashauriwa kunywa dawa aina ya fluconzole mara moja kwa wiki kama kinga dhidi ya maambukizi haya au kama njia ya kupunguza fangasi hawa.

NDEGE YA UJERUMANI YAANGUKA IKIWA NA WATU 150

Ndege ya shirika la ndege la Germanwing inayofanana na ile iliyoanguka.

NDEGE ya abiria inayomilikiwa na shirika la ndege la Germanwing Airbus A320 imeanguka katika milima ya Alps nchini Ufaransa.

Mchoro ukionyesha eneo ambalo ndege hiyo ilipoteza mawasiliano na rada.

Ndege hiyo ilikuwa imebeba abiria 142 na wahudumu sita ikitokea jijini Barcelona nchini Uhispania kuelekea Duesseldorf, Ujerumani.


Ubao wa kuonyesha ndege zilizowasili kwenye uwanja wa ndege wa Duesseldorf, Ujerumani.

Ndege hiyo inayomilikiwa na shirika la ndege la Ujerumani Lufthansa chini ya nembo Germanwings imeripotiwa kuanguka katikati ya Barcelonnette na Digne.

Rais wa Ufaransa amesema: "Mazingira ya ajali hiyo ambayo bado hayajawekwa bayana, yanawapa wasiwasi kufikiri kama kuna mtu yeyote aliyenusurika"

KIFUA KIKUU: UGONJWA UNAOUA ZAIDI YA WATU MILIONI 1 DUNIANI KILA MWAKA


Mgonjwa wa kifua kikuu akipatiwa matibabu.


KWA Tanzania, watu 120,191 hukisiwa kuwa na ugonjwa wa kifua kikuu kila mwaka, hii ni kutokana na taarifa ya Shirika la USAID ya mwaka 2007 na vifo vinavyotokana na ugonjwa wa kifua kikuu ni 32,000 kila mwaka hapa nchini Tanzania.


Muonekano wa mapafu ya binadamu yaliyoathirika kwa TB.


Takwimu za Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) zinaonyesha kuwa Tanzania ni ya 15 kati ya nchi 22 ambazo zimeathiriwa sana na ugonjwa huu na kwa mujibu wa takwimu za shirika hilo, kwa dunia nzima mwaka 2012 watu milioni 8.6 waliambukizwa ugonjwa wa kifua kikuu, na watu milioni 1.3 walifariki kwa ugonjwa huo wengi kutoka katika nchi
zinazoendelea.

Ugonjwa huu huathiri asilimia 98 ya watu katika nchi zinazoendelea ikiwamo Tanzania.

SIKU YA KIFUA KIKUU DUNIANI

Kwa nyakati tofauti, walimwengu wakiwamo wanasayansi walikaa na kukubaliana hivyo kuanzisha Siku ya Kifua Kikuu duniani, Machi 24.
Siku hiyo ni mahsusi kwa ajili ya kufanya mapitio kuhusu hali halisi ya mapambano dhidi ya ugonjwa huo.



KIFUA KIKUU NI NINI

Kitaalamu, unaelezwa kuwa ni ugonjwa wa kuambukiza kutoka mtu mmoja kwenda kwa mwingine kwa njia ya hewa.
Inaelezwa kuwa mtu menye vijidudu vya ugonjwa huo akihoa, kupiga chafya au kwa namna yoyote nyingine kurusha vitone vya makohozi yake kutoka katika mfumo wake wa hewa na kuvieneza hewani na mtu mwingine kumpata akivuta hewa ndani na hivyo kuingia katika mfumo wa hewa.

Ugonjwa wa kifua kikuu ni kati ya magonjwa matatu yanayotokea kwa kiasi kikubwa na kuwapata watu masikini zaidi.

CHANZO AU SABABU ZA KIFUA KIKUU

Ugonjwa huu husababishwa na bakteria waitwao, Mycobacteria tuberculosis.
Kuna aina nyingi za jamii hii ya Mycobacterium kama Mycobacteria tuberculosis (ambao husababisha kifua kikuu), Mycobacteria leprae (wao husababisha ugonjwa wa ukoma), Mycobacteria bovis (huathiri ng’ombe na binadamu), Mycobacteria afrikanum na wengineo.


Mycobacteria tuberculosis (ambao husababisha kifua kikuu).

Ugonjwa wa Kifua Kikuu unaweza kuathiri mapafu, mishipa ya fahamu, mifupa, mfumo wa mzunguko wa damu, ngozi, viunganishi vya mifupa (joints) na mfumo wa tumba zakuchuja vimelea vya maradhi(lymphatic system.

Mycobacteria bovis ambao huathiri ng’ombe, ni jami inayoweza kuambukiza pia binadamu kama atakula nyama au bidhaa zinazotokana na maziwa ya ng’ombe ambayo yameathirika na bakteria hawa.

Mazao mengine ya mifugo kama vile siagi, mtindi, maziwa yenyewe, cheese, ice cream na kadhalika, yanaweza kumdhuru mwanadamu endapo yalikuwa na virusi hao.

Aina hii ya bakteria huathiri mapafu, tezi (lymph nodes), tumbo na sehemu nyingine za mwili.
Wataalam wanaeleza kuwa asilimia 10 tu ya watu walio na bakteria hao jamii ya Mycobacteria tuberculosis hawapati ugonjwa huu wa Kifua Kikuu.

AINA ZA KIFUA KIKUU

Kuna aina kuu tatu za ugonjwa wa Kifua Kikuu;

-Kifua kikuu kinachosababisha madhara (active tuberculosis) – Huu hutokea pale ambapo bakteria waliopo mwilini wapo hai na kinga ya mwili imeshindwa kuwadhibiti hawa

bakteria wasisababishe madhara. Watu hawa wanaweza kumuambukiza mtu yoyote kifua kikuu kwa njia ya kuvuta pumzi kama watakohoa, kutema mate, kupiga chafya, kupiga kelele iwapo watafanya vitendo hivi karibu na watu wasio na ugonjwa huu.

-Ugonjwa usiosababisha madhara (inactive tuberculosis) – Kwa kitaalamu huu pia huitwa Latent TB. Hapa inaamaanisha kuwa kinga ya mwili imeweza kuwadhibiti bakteria na kuwafanya kushindwa kusababisha madhara.
Mtu mwenye Latent TB, hana dalili za ugonjwa huu, hajisikii mgonjwa na hawezi kuambukiza mtu mwingine ugonjwa wa kifua kikuu.

Aina hii inaweza kujirudia baadaye na kuathri sehemu ya juu ya mapafu na hivyo kusababisha kikohozi cha kawaida ambacho baadaye huongezeka na kusababisha kikohozi cha damu au makohozi, homa, kupungua hamu ya kula, kupungua uzito bila sababu ya msingi na kutokwa jasho kwa wingi kuliko kawaida wakati wa usiku.

-Ugonjwa uliosambaa mwilini (milliary tuberculosis) – Hii hutokea pale ambapo kinga ya mwili imepungua na kusababisha ugonjwa wa kifua kikuu kuenea kupitia damu hadi sehemu nyingine za mwili kama mifupa, mishipa ya fahamu, ngozi, figo, kibofu cha mkojo, ngozi ya moyo (pericadium), mfumo wa uzazi, viunganishi vya mifupa (joints) na lymphatic system. Husababisha homa, kupungua hamu ya kula, kuchoka na kupungua uzito.

VIHATARISHI VYA UGONJWA HUU NI;

-Uzee
-Unywaji pombe kupindukia
-Kuishi sehemu zilizo na mrundikano wa watu kama mabweni, kambi za jeshi, hospitali, mabasi ya abiria.
-Magonjwa yanayoathiri kinga ya mwili kama Kisukari.
-Wafanyakazi wa huduma ya afya
-Ugonjwa wa Ukimwi
-Utapiamlo
-Umaskini au hali duni ya kipato
-Kuishi kwenye nyumba za jamii, mfano nyumba za wazee
-Wale wasio na makazi
-Baadhi ya dawa – Dawa za ugonjwa wa maumivu ya mifupa (athritis)
-Wasafiri au watalii kutoka nchi zilizo na idadi kubwa ya ugonjwa wa kifua kikuu.



DALILI NA VIASHIRIA VYA UGONJWA WA KIFUA KIKUU
-Kukohoa zaidi ya wiki 2-3 na kuongezeka kutoa makohozi
-Kukohoa damu
-Homa za mara kwa mara
-Kupungua au kukosa hamu ya kula
-Kupungua uzito kwa asilimia 10.
-Kutokwa na jasho kwa wingi hasa wakati wa usiku
-Uchovu
-Maumivu makali ya kichwa
-Maumivu ya kifua
-Kupumua kwa shida



VIPIMO VYA KIFUA KIKUU NA MATIBABU
-Kipimo cha makohozi (Sputum for AFB) – Makohozi huchukuliwa kwa siku tatu mfululizo muda wa asubuhi na kupelekwa maabara kufanyiwa uchunguzi ili kuweza kugundua kama mtu ana TB.
-Kwa wale wagonjwa wasioweza kutoa makohozi au wale wenye TB ya tumbo, basi hufanyiwa kipimo cha gastric lavage.
-Matibabu ya kifua kikuu ni bure katika hospitali zote za serikali na binafsi. Unapoona mtu ana dalili mojawapo za kifua kikuu au wewe mwenyewe mshauri awahi kituo cha huduma za afya kwa uchunguzi na tiba kwani mtu mmoja huweza kuwaambukiza watu kati ya 10 hadi 15 kwa mwaka kama hajapata matibabu.
-Ikitokea umegundulika kuwa una kifua kikuu usihofu kwani kinatibika na mamilioni ya watu duniani kote wameugua na kupona. Unachotakiwa kufanya ni kufuatisha masharti utakayopewa na daktari kama; kunywa dawa kila siku kwa muda uliopangiwa ili kupona kabisa.
-Matibabu yake huchukua kati ya miezi sita hadi minane.

JINSI YA KUKABILIANA NA KIFUA KIKUU
-Jambo la msingi na muhimu ni kuwahi kufika katika huduma za afya mapema mara unapohisi dalili za kifua kikuu.
-Zingatia matibabu pale unapoanza kutumia dawa za kifua kikuu na hakikisha unatumia dawa kama ulivyoelekezwa na wataalamu wa afya, kumbuka usugu wa dawa na kushindwa kwa dawa hizi ni hatari zaidi katika kupambana na ugonjwa huu.
-Usiache kutumia dawa za kifua kikuu ili kuepuka kupata TB sugu na ile isiyotibika kwa dawa mchanganyiko.
-Hakikisha pale unapoona unakohoa zaidi ya wiki mbili unafika katika huduma za afya kwa ajili ya uchunguzi na matibabu.
-Funika mdomo na pua kwa kitambaa pale unapokohoa au kupiga chafya hii inasaidia kuzuia kuenea maambukizi.
-Kuepuka mikusanyiko au mrundikano wa watu kama vile kwenye mabweni, kambi za jeshi, baa na kadhalika.
-Kuishi kwenye nyumba ambayo ina mfumo mzuri wa kuingiza na kutoa hewa yaani iwe na madirisha makubwa na ya kutosha.
-Pia, kuishi katika mienendo bora inayozingatia afya, kula mlo kamili, kunywa maji mengi angalau lita 1.5 kwa siku na mazoezi mepesi kama kutembea kwa dakika 15 kwa siku yanachangia kuujenga mwili na kuwa wenye afya njema.
-Pata mapumziko ya kutosha angalau lala masaa sita kwa siku, epuka matumizi ya ulevi wa pombe.

ANGELINA JOLIE AFANYIWA UPASUAJI, ATOLEWA OVARI, MIRIJA YA UZAZI


Angelina Jolie.

MWIGIZAJI wa filamu nchini Marekani, Angelina Jolie amelazimika kutoa ovari zake pamoja na mirija ya uzazi baada ya uchunguzi kuonesha kuwa alikuwa katika hatari ya kuathirika na saratani ya nyumba ya uzazi.

Angelina Jolie, mumewe Brad Pitt wakiwa na watoto wao.

Staa huyo maarufu wa Hollywood amelidokezea jarida la New York Times, kuwa alilazimika kutoa viungo hivyo wiki iliyopita katika upasuaji wa dharura.

"Upasuaji huo ulitokana na ripoti ya uchunguzi wa daktari uliobaini kuwa nilikuwa na asilimia 50 ya chembechembe zenye hatari ya kuambukizwa saratani" alisema Jolie

Habari hizi zimewashtua mashabiki wa mrembo huyo ambaye miaka miwili iliyopita alilazimika kukatwa titi kwa sababu ya tishio hilo hilo la Saratani.

Angelina Jolie akiwa na mumewe Brad Pitt.

Mama mzazi wa staa huyo aliaga dunia kufuatia hitilafu iliyotokana na matibabu ya saratani.
"Siyo jambo rahisi sana kukabiliana na swala hili gumu linalohusu afya yangu" aliongeza Jolie.
Jolie ambaye ni mke wa mwigizaji nyota wa Holywood, Brad Pitt, anasema kuwa vipimo vilionesha chembechembe za maradhi hayo na ikamlazimu kuchukua hatua hiyo mara moja.
Mastaa hao wana watoto sita ambapo kati yao wengine ni wakuhasili.

Sunday, March 22, 2015

WASAFIRI RAIA WA CAMEROON WATEKWA NYARA




Wasafiri kadhaa raia wa Cameroon wameripotiwa kutekwa nyara na watu wasiojulikana karibu na mpaka wa Jamhuri ya Afrika ya Kati. Duru za kuaminika zimeripoti kuwa, watu hao 15 wametekwa nyara na watu wenye silaha wa kundi linaloongozwa na mtu mmoja anayetambulika kwa jina la Abdoulaye Miskine, huko kaskazini mashariki mwa Cameroon karibu na mpaka wa pamoja na Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Chanzo kimoja cha usalama nchini Cameroon kimeeleza kuwa, wasafiri hao 15 walitekwa nyara usiku wa Alkhamis iliyopita katika kijiji cha Gbabio kilichoko umbali wa kilometa 10 kutoka mji wa Garoua-Boulaï, mashariki mwa Cameroon.

Chanzo hicho ambacho hakikutaka kutaja jina lake kimesema kuwa, bila shaka yoyote raia hao wa Cameroon walitekwa nyara na wanachama wa kundi la Abdoulaye Miskine ambalo ni maarufu kwa vitendo vya ukatili na machafuko mashariki mwa taifa hilo.

Kwa mujibu wa jeshi la polisi la Cameroon, wasafiri hao walitekwa nyara majira ya saa 11 za usiku kutoka katika mji wa Bertoua, makao makuu ya mkoa wa mashariki mwa nchi hiyo. Itakumbukwa kuwa mwaka uliopita, Abdoulaye Miskine alitiwa mbaroni karibu na mpaka wa Cameroon na Jamhuri ya Afrika ya Kati na kufungwa jela miezi kadhaa.

CHANZO: BBC SWAHILI

IS YAKIRI KUSHAMBULIA MISIKITI YEMEN

Majeruhi wakiokolewa baada ya shambulizi lililotekelezwa na Kundi la wapiganaji wa IS katika misikiti ya Yemen.

Kundi la Islamic State linasema kuwa wapiganaji wake waliendesha mashambulizi ya kujitoa mhanga kwenye misikiti miwili nchini Yemen ambapo zaidi ya watu 130 waliuawa.

Washambuliaji wanne wa kujitoa mhanga walilenga waumini kwenye mji mkuu Sanaa wakati wa maombi ya Ijumaa.

Maeneo hayo mawili hutumiwa na waumini wanaowaunga mkono waasi wa Shia wanaofahamika kama Houthi ambao walichukua udhibiti wa mji wa Sanaa mwaka uliopita.

Zaidi ya watu 200 walijeruhiwa wakati wa mashabulizi hayo ambapo wito wa kuwaomba watu kutoa damu umekuwa ukitolewa.

CHANZO: BBC SWAHILI

WATU WAPATAO 70 WANAOSADIKIWA KUUAWA NA BOKO HARAM WAGUNDULIKA DAMASAK, NIGERIA



Askari wa Chad na Niger wakiwa Damasak.

Makumi ya miili ya watu wanaosadikiwa kuuawa na wanachama wa kundi la kigaidi na kitakfiri wa Boko Haram, imegunduliwa katika Mji wa Damasak uliopo Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.

Taarifa zinaeleza kuwa, miili hiyo ya watu 70 ambayo mingi kati yake imekutwa ikiwa imekatwa vichwa, imegunduliwa na askari wa Chad na Niger katika mji huo wa Damasak nchini humo. Tayari uchunguzi umeanzishwa kwa lengo la kuwatambua wahusika wa ukatili huo, ingawa kidole cha lawama tayari kimeelekezwa kwa wanachama wa kundi la kitakfiri la Boko Haram, ambalo limekuwa likitekeleza mauaji kama hayo.

Hadi siku ya Jumamosi iliyopita, ambapo askari hao wa Chad na Niger waliuvamia mji huo na kuukomboa kutoka kwa wanachama wa kundi la Boko Haram, ulikuwa umetelekezwa kabisa na serikali ya Nigeria.

Tangu mwezi Novemba mwaka jana ambapo mji huo ulidhibitiwa na kundi hilo, wakazi wake walikuwa wakijaribu kutoroka ingawa hata hivyo walikuwa wakizuiliwa na magaidi hao wanaotekeleza jinai kwa jina la Uislamu.

Inaelezwa kwamba, baada ya mji huo kudhibitiwa na kundi hilo, wanachama wake walivamia maduka na makazi ya watu na kupora kila walichokitaka, huku wakiwabaka na kuwanajisi wanawake na wasichana wa mji huo.

CHANZO: BBC NEWZ

MISS TANZANIA AFUNGUA MFUKO MAALUM KUWASADIA WATOTO WANAOZALIWA KABLA YA SIKU ZAO


Dorice Molle (katikati) akiwa na Waziri wa Afya wa Zanzibar, Thabit Kombo.

Hapa wakizindua rasmi mfuko wa kusaidia watoto ambao ni njiti (Premature).

Mkurugenzi wa Shindano la Miss Tanzania, Hashimu Lundenga akiteta jambo na Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu.

Mama mzazi wa mrembo huyo na kaka yake ambao nao walihudhuria hafla hiyo.

Kada wa chama CCM, Chrisant Mzindakaya naye alikuwepo.

Dorice akizungumza jambo na kutoa shukrani.

Baadhi ya wageni waalikwa katika hafla hiyo.

Mh. Thabiti Kombo, akizungumza jambo.

Kamati ya Miss Tanzania ikiwa na baadhi ya warembo waliopita kama Hoyce Temu, Rashida Wanjara na Basila Mwanukuzi.

Hoyce Temu ,Christina John na Rachel Temu baada ya kumalizika kwa hafla.

Mrembo anayeshikilia nafasi ya tatu katika Miss Tanzania, Dorice Mollel, leo amezindua rasmi mfuko wake wa kusaidia watoto ambao wanazaliwa kabla ya siku zao kutimia “ Premature” unaoitwa Dorice Mollel Foundation (DMF) katika hafla fupi iliyofanyika katika Hotel ya Hyatt Kempski, Jijini Dar.

Katika uzinduzi huo mgen rasmi alikuwa Waziri wa Afya wa Zanzibar, Mhe Mhmuud Thabith Kombo.

Uzinduzi huo ulihudhuriwa na mabalozi na warembo waliowahi kushiriki mashindano ya urembo nchini. Dorice ni mrembo ambaye ameweza kufanya vizuri sana kwa kujitolea kwa jamii ikiwemo kutoa vifaa mbalimbali mashuleni.

(PICHA NA IMELDA MTEMA/GPL)

Wednesday, March 18, 2015

MWANAO WA KUMZAA UNAWEZA KUMTESA HIVI?

HARUNI SANCHAWA
MWANAMKE mmoja mkazi wa Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam, Violet Manyondo (40) anadaiwa kumtesa na kumfanyia vitendo vya kikatili mtoto wake wa kumzaa, anayejulikana kwa jina la David (14).David ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tano katika shule moja ya msingi iliyopo Mzambarauni, Dar kwa sasa haendi shule kutokana na majereha aliyonayo kiasi cha kuwaliza majirani.


Mtoto David akiwa na majeraha mwilini aliyosababishiwa na mama yake mzazi.

Akizungumza na Amani, mmoja wa majirani aliyeomba hifadhi ya jina lake, alisema ni mara yake ya kwanza kushuhudia mama akimtesa mtoto wake wa kumzaa kama anavyofanya mama huyo.“Tunaomba vyombo vya haki za binadamu hata Jeshi la Polisi kushughulikia tukio hili haraka iwezekanavyo vinginevyo mtoto huyo ataathirika kisaikolojia, halafu cha kushangaza, ana watoto watatu, lakini ni huyu tu ndiye anayekutana na kipigo,” alisema jirani huyo.

Alisema katika kumsaidia kijana huyo, wamewahi kwenda kituo cha polisi Gongo la Mboto, lakini polisi jamii walipokwenda nyumbani hapo, waliambulia matusi.Mtoto David aliliambia gazeti hili kuwa ni kweli mama yake anamtesa kwa muda mrefu na kwamba hivi karibuni alikwenda kumshtaki katika kanisa lao liitwalo Universal Ufalme wa Mungu, Mzambarauni, Ilala, Dar na alipotakiwa kumwita mama yake alikataa kwenda.


David akiwa nyumbani kwao.

“Baada ya mama kupata wito ule hata kanisani ameacha kwenda kwa kuhofia kikao na ushauri wa viongozi wa kanisa. Sina cha kufanya wala pa kwenda, namuomba Mungu anisaidie nimalize shule,” alisema kijana huyo.
Kuhusu sababu za kuteswa, alisema hafahamu chochote, ingawa alihisi huenda ni kwa sababu ya baba yake kutopeleka hela ya matumizi nyumbani, kitu ambacho hata hivyo haifahamu kwani hamfahamu mzazi wake, zaidi ya kusikia kuwa ni dereva wa daladala.

Katika hali ya kushangaza, mama huyo alipotafutwa na gazeti hili, alijibu kijeuri;
“Yule ni mwanangu, naweza kumfanya lolote lile. Mimi ni mzazi wake, natakiwa kumrekebisha kwa njia yoyote.” Uongozi wa Serikali ya Mtaa wa Gongo la Mboto umesema unashukuru kwa kupata taarifa hizo, kwani watahakikisha wanafuatilia jambo hilo na kulipatia ufumbuzi.

Kamanda Msangi: “Ni kweli tukio hilo limetokea na inadaiwa kuwa chanzo cha kifo cha mtu huyo ni kipigo kilichotokana na imani za kishirikina.”

DENTI MWENZAKE LULU ACHOMWA KISU, AFARIKI

WAANDISHI WETU, DAR
CHAMIWA Adamu (23), kijana ambaye ni mkazi wa Kilimahewa- Manzese jijini Dar, ameuawa kwa kuchomwa kisu cha shingo na mtu aliyetambulika kwa jina moja la Mpelu kisa kikidaiwa ni shilingi mia mbili tu!

Marehemu Chamiwa Adamu enzi za uhai wake.

Marehemu Chamiwa (pichani)alikuwa mwanafunzi mwenzake na staa wa filamu za Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ kwenye Chuo cha Magogoni, Dar.

Tukio la Chamiwa kuchomwa kisu lilijiri saa 11 jioni ya Machi 12, mwaka huu katika eneo lililofahamika kwa jina la Tishio, Manzese Midizini, Dar.

SIKU YA TUKIO
Akisimulia mkasa huo mwanzo mwisho, mmoja wa wanafamilia ambaye hakupenda kutaja jina alisema, siku ya tukio, Chamiwa alikuwa na wenzake (hakuwataja majina), kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Mpelu alitokea na kumwomba shilingi mia mbili.

“Marehemu alimwambia ana hela kubwa, kwa hiyo hana chenji, hivyo akamtaka amwache aende kutafuta chenji ili ampatie hiyo 200.“Ile anaondoka tu, Mpelu alimshika begani kwa nyuma, marehemu alipogeuka kumtazama, Mpelu akamchoma kisu sehemu ya shingoni. Palepale damu zikaanza kuchuruzika na marehemu akaanguka.
“Watu, akiwemo aliyemchoma kisu walimnyanyua marehemu na kumpakia kwenye gari iliyokuwepo pembeni ili kumpeleka Kituo cha Polisi Magomeni,” alisema mwanafamilia huyo.

KISU KILIVYOZAMA
Kwa mujibu wa mashuhuda, inadaiwa kuwa kisu alichochomwa Chamiwa, kilizama ndani ya mwili wake kwa umbali wa zaidi ya nchi mbili.


Simu ya marehemu.

MTUHUMIWA ATAKA KUTOROKA
Habari zinadai kwamba, wakiwa njiani kumpeleka marehemu kituo cha polisi, mtuhumiwa huyo alibaini Chamiwa alishafariki dunia, akaomba afunguliwe mlango wa gari ili ashuke (kwa maana ya kukimbia) lakini wasamaria wema hao walimkatalia kwa vile walishtukia kwamba kesi ingekuwa yao, hivyo wakaongeza ulinzi kwa mtuhumiwa mpaka kituo cha polisi.

WALIVYOSEMA MAJIRANI
Amani lilifanikiwa kufika nyumbani kwa marehemu na kuzungumza na baadhi ya majirani ambapo walisema Chamiwa alikuwa kijana mpole, mwenye kujituma na alikuwa hana shida kwa wenzake.“Tumeumia sana kusikia ameuawa kwa kuchomwa kisu. Tukimfikiria kijana wa watu alivyokuwa bado mdogo, maskini Chami! Amepoteza ndoto zake. Yeye ndiye aliyekuwa akishika nafasi ya baba mwenye nyumba kama mzee Adamu hayupo. Inauma! Ila tumuachie Mungu atamlipia,’’ alisema jirani mmoja.

SIMU YA MAREHEMU YAKUTWA NA DAMU
Amani lilifanikiwa kuiona simu aliyokuwa akiitumia marehemu enzi za uhai wake ikiwa imezimwa na kuchafukwa kwa damu iliyoganda.Mpaka juzi, mtuhumiwa huyo alikuwa bado anashikiliwa katika Kituo cha Polisi Magomeni huku uchunguzi ukiendelea.


Staa wa filamu za Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’.

CHUONI KWA MAREHEMU
Amani lilifika kwenye chuo alichokuwa akisoma marehemu Chamiwa ambapo liliambiwa alikuwa mwaka wa kwanza akichukua masomo ya Information of Technology (IT).Mkuu wa wanafunzi (Dean of Students) aliliambia Amani kwamba, taarifa za mwanafunzi huyo kuuawa kwa kisu zimewafikia na wanachosubiri ni ratiba ya mazishi ili washiriki pamoja na familia.

“Kusema kweli tumepokea taarifa hizo lakini tunachosubiri ni ratiba ya mazishi ili na sisi tuweze kushiriki,” alisema mkuu huyo bila kutaja jina lake.

Wakati Amani linaondoka chuoni hapo liliwapa pole wanafunzi wenzake marehemu hasa wale wa mchepuo sanjari na wake, lakini pia lilimtafuta Lulu kwa lengo la kumpa pole lakini ilidaiwa kwamba, alishaondoka kurudi nyumbani.

Marehemu Chamiwa alizikwa Machi 13, mwaka huu mkoani Morogoro.
Mungu ailaze pema peponi roho yake. Amina.