Karibu Fadhaget Sanitarium Clinic

Tunapenda kukukaribisha katika Kitengo cha Sayansi ya Tiba Asilia.

Kitengo Cha Sayansi Ya Tiba Asilia

Kwa Muda mrefu tumekuwa tukisaidia wengi katika matibabu na kutengeneza dawa bora kabisa kiafya.

Je Unapenda Kufahamu Jinsi Ya Kupata Mapacha?

Tunafundisha jinsi ya kupata jinsia unayotaka, jinsi ya kupata mtoto kama umekosa mtoto kwa muda mrefu. Pia hata jinsi ya kupata watoto mapacha tunaweza kukusaidia.

Tunapatikana Katika Mikoa Zaidi ya 10 Tanzania

Tunazidi kuongeza matawi yetu nchini Tanzania na Nje ya Nchi. Kwa sasa tunapatikana katika mikoa zaidi ya 10 na tunazidi kuongeza matawi yetu. Karibu sana.

Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Wednesday, December 17, 2014

TAMBUA VIMBE MBALIMBALI KWA MWANAMKE NA JINSI YA KUZIONDOA PASIPO UPASUAJI



Leo tutazungumzia vimbe mbalimbali ambazo hutokea katika mwili wa mwanamke kwani wengi hawajui kama kizazi cha mwanamke kinaweza kutokewa na vimbe tofautitofauti katika maeneo tofauti kwa sababu vimbe zina vyanzo mbalimbali.

Jambo la msingi la kuzingatia leo ni kwamba aina zote hizi za vimbe tuna uwezo wa kuziondoa pasipo kufanya upasuaji.

AINA ZA VIMBE
Zipo aina tofautitofauti za vimbe katika mwili wa mwanamke, nazo ni kama;

VIMBE KATIKA MJI WA MIMBA {Uterus}
Vimbe hizi wataalamu wanaziita FIBROIDS au MAYOMA, na uvimbe huu hupatikana katika mji wa mimba iwe kwa juu au upande wa kushoto au upande wa kulia wa mji wa mimba. Na wanawake wengi sana wanakutwa na uvimbe kama huu.

VIMBE KATIKA VIFUKO VYA MAYAI YA UZAZI {Ovaries}
Katika vifuko vya mayai kunakua na vimbe za aina mbili, nazo ni kama;
Ovarian Cysts hii ni ile hali ya mwanamke kutokewa na uvimbe mmoja kwenye kifuko cha mayai ya uzazi, na kinaweza tokea upande mmoja au pande zote mbili za vifuko vya mayai, lakini vimbe hiyo inakua ni moja.

Polycystic ovarian syndromes {PCOS} au Multiple cysts na hizi ni zile vimbe ndogondogo nyingi zinazoweza kutokea kwenye kifuko cha mayai cha mwanamke, lakini nazo pia huweza kutokea katika pande zote mbili za vifuko vya mayai kwa mwanamke. Na hizi ndiyo vimbe kuu zilizokua zikitambulika kwa watu wengi sana lakini zipo nyingine nyingi sana.

KUVIMBA KWA MIRIJA YA UZAZI {Fallopian tubes}
Wataalamu wanaita salpingitise yaani kuvimba kwa mirija ya uzazi katika mwili wa mwanamke, na hii inawezekana ikatokea kwenye upande mmoja wa mrija wa uzazi na baadaye unaweza ukaambukiza mrija mwingine na yote ikawa imevimba, na hii nayo ni aina nyingine ya vimbe katika mwili wa mwanamke.

KUVIMBA KWA KIFUKO
CHA MAYAI {Ovary}
Wataalamu wanaita Ovary ties yaani kuvimba kwa kifuko chote cha mayai na hii inakua ni tofauti kidogo na uvimbe katika kifuko cha mayai au vimbe nyinginyingi ndogo katika kifuko cha mayai.

Kwa maana hiyo basi sote tutakuwa tumetambua aina mbalimbali za vimbe katika mwili wa mwanamke, na pale unapoambiwa una uvimbe au mke wako ana uvimbe katika mji wake wa uzazi basi ni bora kabisa ukauliza kuwa uvimbe huo ni wa aina gani ili iwe rahisi kuuondoa au kuutibia kwa haraka.

Na kama umeshawahi kupima na ukaambiwa kwamba una uvimbe katika mji wako wa mimba na hupendi kufanya upasuaji basi ni bora ukawasiliana nasi kupitia namba zetu.Kwa ushauri, vipimo na tiba dokta wetu anapatikana kwenye vituo vyake vya Dar es Salaam, Tanga, Morogoro na Mwanza.

Itaendelea wiki ijayo.

JINSI YA KUGUNDUA MAAMBUKIZI KWENYE UZAZI (DIAGNOSIS OF PID)


Baadhi ya wagonjwa watahitajika kulazwa hospitali ambapo watapewa dawa za saa na kuwa chini ya uangalizi wa haraka wa manesi na madaktari.Wagonjwa wanaohitaji kulazwa ni kama wale wanaodhaniwa kuwa wana uvimbe au jipu kwenye mfuko wa mayai yaani tube ovarian abscess au wale wenye kutapika sana na wenye homa kali pia wenye maumivu makali ya tumbo yanayofanana na kidole tumbo.

Wagonjwa ambao hawakupata nafuu baada ya matumizi ya dawa ya awali baada ya saa 48 ya kumaliza dawa na wale walioshindwa kumeza dawa pia wagonjwa wenye rirusi vya ukimwi watahitajika kulazwa.

Dawa zinazotumika kwa wale waliolazwa ni kama vile cefoxitin na clindamycine ikichanganywa na gentamycine.Nafuu ya mgonjwa itajulikana baada ya mgonjwa kujisikia vizuri na homa itashuka, pia maumivu ya tumbo yatapoa na vipimo vya maabara vitaonyesha kuwa vijidudu vimeisha.

Baadhi ya wagonjwa watahitaji upasuaji kama kutakuwa na madhara makubwa (complications) kama vile vijidudu kuingia kwenye utumbo, jipu kwenye viungo vya uzazi (pelvic abscess) usaha kwenye mfuko wa mayai (turbo ovarian abscess).

JINSI YA KUJIKINGA (PREVENTION)
Kwanza, matabibu wana wajibu wa kuelimisha jamii juu ya maambukizi yanavyotokea na kujiepusha nayo.

Pili, jamii iepushwe mwanamke kuwa na uhusiano wa kingono na wanaume wengi (multiple sexual partiners) na watu wajue matumizi sahihi ya kondom.

Mwanamke lazima amlete mwenza wake ili aweze kufanyiwa vipimo vya uhakika na akithibitika hana maambukizi ya kisonono basi ataweza kupewa dawa za kuua vijidudu vya clamydia maana ni vigumu kuweza kugundua vijidudu vya clamydia. Mwenza wake yaani atumie dawa kwa muda wa siku saba.

Ufuatiliaji wa mgonjwa kwa kumpima ufanyike baada ya wiki moja baada ya wote kutibiwa.
Kwa mwanamke apimwe kila anapomaliza hedhi na majibu yaonyeshe kuwa hana ugonjwa, upimaji ufanyike mara tatu mfululizo na majibu yaonyeshe kuwa hana ugonjwa. Mtu yeyote atakayejihisi ana tatizo hili asitumie dawa hizo bila kuonana na daktari ambaye atampima.

FAHAMU UGONJWA WA SARATANI YA TEZI DUME (PROSTATE CANCER)-4

Baada ya vipimo hivyo kama vitaashiria saratani ya tezi dume basi daktari anaweza kuamuru vipimo vingine ili kuthibitisha uwepo wa ugonjwa huo kama vile Transrectal Ultrasound au Prostatic Needle Biopsy. Tukumbuke kuwa kuwahi kugundua saratani mapema kabla ya dalili, kuna faida kubwa kwa muathirika kwani saratani ikigundulika mapema ni rahisi kutibika.

TIBA YAKE

Kuna njia kadhaa za matibabu ya saratani ya tezi dume. Hata hivyo uamuzi wa njia gani itumike unategemea ushauri na maoni ya daktari kulingana na hatua ya ugonjwa ulipofikia na umri wa mgonjwa husika.

Katika hatua za awali za ugonjwa, daktari anaweza kushauri mgonjwa atibiwe kwa kufanyiwa upasuaji na tiba ya mionzi. Hii ni katika hali ambayo kwa wagonjwa wazee, daktari anaweza kushauri mgonjwa kuwa chini ya uangalizi tu bila kufanyiwa upasuaji au bila kupatiwa tiba ya mionzi.

Iwapo saratani imesambaa na kuathiri sehemu nyingine za mwili, matibabu yake yanaweza kujumuisha upasuaji wa kuondoa korodani, matumizi ya dawa za kupunguza kiwango cha homoni ya testosterone katika damu au hormonal therapy, au matumizi ya kemikali za kuua seli za saratani (chemotherapy).

Saratani ya tezi dume ni ugonjwa wa kawaida kama yalivyo magonjwa mengine na uchunguzi na matibabu ya mapema huweza kuokoa maisha ya waathirika wengi wa ugonjwa huo.

USHAURI

Wanaume wanashauriwa kufanyiwa uchunguzi wa saratani ya kibofu cha mkojo au prostate cancer kwa kuwa imegundulika kuwa wanaume wengi wakiziona na kuzihisi dalili hizo huona soni kwenda kumwona daktari na kufanyiwa uchunguzi.

Baadhi ya watu huzihusisha na magonjwa ya zinaa au na dhana potofu za kishirikina. Wapo wanaokwenda mbali zaidi hata kuuita ugonjwa huo kuwa ni wa walawiti huku wengine wakiurahisisha kwa kuuita kuwa ni ugonjwa wa utu uzima kana kwamba saratani ya tezi dume ni jambo la kawaida kwa watu wazee.

Kwa ajili hiyo tunatoa wito kwa wanaume kutoona soni na kuwa na tabia ya kufanyiwa uchunguzi wa afya kwa jumla, hasa tezi dume angalau mara moja kwa mwaka.

Thursday, December 11, 2014

JE, VIDONDA VYA TUMBO VINATIBIKA?-3


Wiki iliyopita tulizungumzia sana madhara yanayoweza kumkuta mtu mwenye vidonda vya tumbo. Lakini leo sanasana tutaweza kuangalia dalili kubwa za tatizo hili ni zipi na mtu anapoziona katika mazingira yake ya kawaida basi aweze kufika katika vituo vya afya kwa ajili ya kuweza kuliondoa tatizo hili kwa urahisi kabisa.

DALILI ZA VIDONDA VYA TUMBO
Dalili za tatizo hili la vidonda vya tumbo hutegemeana sana na tatizo linakuwa limefikia katika kiwango gani hasa, lakini tutazizungumzia kwa jumla lakini pia kwa kuzingatia tatizo kwa kila mtu. Dalili hizo ni kama zifuatazo;

Dalili kubwa ni maumivu kama ya kuungua maeneo ya kifua, mara nyingi mtu mwenye vidonda vya tumbo anaweza akawa anasikia maumivu makali sana maeneo ya kifuani kwa mwanaume au mwanamke na wakati mwingine mtu huyu akawa anakisikia au anakihisi chakula kikiwa kinashuka hasa wakati wa kula na wakati mwingine inakuwa ni kama moto unatembea kifuani kuja tumboni na hiyo ndiyo inakuwa dalili kubwa kabisa ya tatizo hili la vidonda vya tumbo.

Lakini kuna dalili nyingine pia mfano kusikia maumivu katika tumbo, mara nyingi maumivu haya katika tumbo huwa ni kama hali ya kuungua tumboni na hii ni kwa sababu kubwa ya kwamba mtu huyu kuta zake za tumbo zinakuwa zimeathirika sana na hasa maumivu haya huwa makali zaidi wakati tumbo likiwa halina kitu au pale mtu huyu akiwa anapata chakula.

Kupungua kwa uzito wa mtu na kukonda zaidi, na hii ni kwa sababu mtu huyu mwenye vidonda vya tumbo anakuwa anapata maumivu wakati anapopata chakula na pia anakuwa akila kidogo anahisi tumbo kujaa lakini kihalisia anakuwa na chakula kichache sana ndani ya tumbo basi matokeo yake ni kudhoofu mwili wa mwanadamu huyu na hivyo kukonda sana. Kama kuna mtu unamjua anakuwa anakumbwa na dalili kama hiyo basi ni vema kufika kwenye vituo vya afya bado mapema kwa ajili ya matibabu zaidi au tupigie simu kwa msaada zaidi.

Wednesday, December 10, 2014

FAHAMU UGONJWA WA SARATANI YA TEZI DUME (PROSTATE CANCER)-3


TUMEELEZA kuhusu kansa ya tezi dume, leo tutafafanua vihatarishi vinavyochangia mwanamume kupata saratani ya tezi dume. Vifuatavyo ni baadhi yake: Kwanza kabisa ni umri. Nafasi ya kupata saratani ya tezi dume huongezeka sana hasa ukifikia umri wa karibu miaka 50 na kuendelea.

Nasaba ni kihatarishi kingine ambapo wanaume wenye historia ya tatizo hili kwenye familia zao, yaani wale ambao mmoja wa ndugu zao wamewahi kuugua ugonjwa huu huwa katika hatari ya kupata kansa hiyo kutokana na kurithi ‘gene’ za ugonjwa huo.

Suala lingine ni lishe ambapo wanaume wanaopenda kula nyama nyekundu (red meat) na walaji wa chakula chenye kiasi kikubwa cha mafuta hasa ya wanyama huwa katika hatari kubwa ya kupata saratani ya tezi dume.

Vilevile wanaume wasiopenda kufanya mazoezi, wanene na wenye upungufu wa virutubisho vya Vitamin E pia wako kwenye hatari zaidi ya kupata saratani ya kibofu cha mkojo. Wanaume wengine walio katika hatari kubwa ya kupata saratani ya tezi dume ni pamoja na wale wakulima wanaotumia aina fulani ya mbolea za kemikali, wanaofanya kazi katika viwanda vya kutengeneza matairi na wachimbaji madini, hususan aina ya cadmium.

Dalili za saratani ya tezi dume hazitofautiani na zile za kuvimba kwa tezi dume au BPH. Dalili hizo ni pamoja na, kupata shida wakati wa kuanza kukojoa, kutiririka kwa mkojo baada ya kumaliza kukojoa, kukojoa mkojo wenye mtiririko dhaifu, kukojoa mara kwa mara hasa nyakati za usiku, kujikakamua wakati wa kukojoa na kushindwa kumaliza mkojo wote na kutoa mkojo uliochanganyika na damu.

Pamoja na kueleza dalili hizo wapenzi wasomaji mnapaswa kutambua kuwa, mwanaume anapoanza kuona na kuhisi baadhi ya dalili hizo, anapaswa kujua kuwa, seli za saratani katika tezi dume lake huwa zina umri wa takribani miaka saba na kuendelea.

Iwapo saratani imesambaa mwilini kiasi cha kuhusisha sehemu nyigine za mwili, mgonjwa anaweza kuwa na maumivu makali ya mifupa katika maeneo ya nyonga, mapajani na kiunoni. Aidha mgonjwa huwa na dalili nyingine zinazoweza kumpata mgonjwa mwingine yeyote wa saratani kama vile kupungua uzito, kuhisi kichefuchefu, uchovu, kizunguzungu na kadhalika.

UCHUNGUZI

Kuna vipimo viwili ambavyo daktari anaweza kumpima mwanaume ikiwa ni hatua ya kwanza ya kugundua ugonjwa huo. Vipimo hivyo vya kwanza ni “Digital Rectal Exam (DRE)” na cha pili ni “Prostate Specific Antigen (PSA)”. DRE pamoja na PSA huonesha uwepo wa tatizo kwenye tezi dume, lakini vipimo hivi havina uwezo wa kutofautisha iwapo tatizo hilo linamaanisha saratani au uvimbe katika tezi dume. Hivyo basi, ili kuweza kutofautisha kati ya magonjwa hayo mawili, kipimo kiitwacho Prostate biopsy hufanywa.

Itaendelea wiki ijayo.

Tuesday, December 9, 2014

UTAGUNDUAJE MAABUKIZI KWENYE UZAZI (DIAGNOSIS OF PID)


Kama tulivyokwisha kusoma wiki iliyopita katika safu hii dalili za maambukizi kwenye viungo vya uzazi kwa mwanamke kama vile kutokwa uchafu sehemu za siri, homa, maumivu chini ya kitovu, kutokwa na hedhi bila mpangilio, maumivu wakati wa tendo la ndoa na maumivu wakati wa kutoka hedhi na nyinginezo, hivyo basi ili kugundua ugonjwa wa PID ni lazima kuchukua historia vizuri ya mgonjwa.

Daktari atampima tumbo mama ili kugundua maumivu ya tumbo kama yapo sehemu gani na pia kufanyia vipimo kama vile kupima uchafu kutoka ukeni na vipimo vingine kama Ultrasound.

Magonjwa mengine yanayofanana na PID: Hayo ni kama kidole tumbo (appenditis), mimba kutunga nje ya mji wa mimba hasa ikitungwa kwenye mirija na kupasuka (ruptured actopic pregnance), kupasuka uvimbe kwenye mfuko wa mayai (reptured ovarian mass) au maambukizi ya vidudu kwenye mkojo (urinary tract infection).

MADHARA YA PID
Madhara ya haraka (immediate complication) ni magonjwa yanayoweza kusababishwa na maambukizi kwenye mji wa mimba, vijidudu huweza kusambaa na kuingia kwenye utumbo (peritonitis) au wadudu kuingia kwenye mfuko wa damu (septichemia) ambapo huweza kuathiri viungo kama magoti na mgonjwa kupata ugonjwa wa arthritis na moyo (myocarditis).

Madhara ya muda mrefu ni kama maumivu wakati wa tendo la ndoa (Dyspareunia), kukosa kupata mimba (infertity), maambukizi kuwa sugu (chronic imflammatory diseases) na uwezekano wa mimba kutunga nje ya mji wa mimba yaani ectopic pregnance.

MATIBABU
Mgonjwa atapatiwa tiba kwa muda usiopungua siku 14 dawa zinazotumika ni kama levoflaxacin ikichanganywa na metronidozole.

Pia dawa zingine kama cefriaxone, dnycyline hutumika kwa kipindi cha siku 14. Matibabu haya hutumika kwa wagonjwa wa nje (out patient), wagonjwa watahitaji kuonwa na daktari baada ya siku 2 baada ya kumaliza dawa. Itaendelea wiki ijayo.

Friday, December 5, 2014

MTOTO ALIYEZALIWA AKIWA NA UZITO WA KILO 13 NA UREFU WA INCHI 22

Tumezoea kusikia watoto wakizaliwa na uzito wa kilo mbili na nusu hadi tano lakini hii inaweza kuwa sehemu ya maajabu kwani si rahisi mama kujifungua mtoto mmoja na si mapacha mwenye uzito mkubwa kama huyu aliyezaliwa huko Marekani.
Mwanamke huyo mw enye makazi yake nchini Marekani ameushangaza umma baada ya kujifungua mwanaye wa kike mwenye uzito wa kilo 13 kwa mara ya kwanza ikiwa ni uzao wake wa tano.

Mtoto huyo aliyepewa jina la Mia Yasmin amezaliwa akiwa na urefu wa inchi 22 baada ya mama yake kukaa chumba cha kujifungua kwa muda wa siku tatu.
Mama yake Alisha Hernandez alitarajia kujifungua mtoto mwenye uzito wa kilo saba lakini alijifungua mtoto huyo siku ya jumatatu.
Binamu yeka Alisha alisema baada ya kuzaliwa kwa mtoto huyo,aliamua kwenda kwenye hospitali ya watoto kwa ajili ya kumfanyia uchunguzi wa kisayansi na kubaini hana tatizo lolote na kwa sasa yuko katika hali nzuri.

Baba wa mtoto huyo Fransisco Garcia amefurahia ujio wa mtoto wake huyo na kusema ameshukuru kupata mtoto wa tano wa kike ndani ya familia yake baada ya kutangulia wengine wanne wa kike ambao ni Britney, Ximena, Yulissa na Yuliana Hernandez.

HUYU NDIYE DAKTARI ANAYETUMIA PAMPU YA BAISKELI KUFANYA UPASUAJI.



Daktari anayetumia pampu ya baiskeli kulifurisha tumbo la mwanamke anayetaka kukatwa kizazi nchini India.

Jimbo moja nchini India limesitisha shughuli ya kufungwa kizazi wanawake baada ya daktari mmoja kupatikana akitumia pampu ya kuweka pumzi kwenye baiskeli kuweka hewa kwenye matumbo ya wanawake waliokuwa wanafanyiwa operesheni hizo.

Daktari Chandra Rout, aliyetumia pampu hiyo kwa wanawake 56, Ijumaa wiki jana, aliambia BBC kuwa pampu hizo hutumiwa sana katika jimbo hilo la Orissa.
Maafisa wa serikali walisema gesi ya kaboni, ndio inapaswa kutumiwa kwa operseheni hizo wala sio pampu za kuweka hewa baiskeli.

Maafisa hao wamesema kuwa watu wanaweza kutumia hewa ya kaboni lakini utumizi wa pampu hiyo ni hatari kwa maisha ya binaadamu.

Mwezi Uliopita ,kashfa nyingine ilizuka kuhusu ukataji wa kizazi baada ya wanawake 15 kufariki walipofanyiwa upasuaji katika jimbo jengine.
Madawa ya kulevya yalitumika wakati wa upasuaji huo katika jimbo la Chhattisgarh.

Kambi za ukataji kizazi hufanyika mara kwa mara ili kuwakata kizazi kwa pamoja wanawake nchini India kama mojawapo ya mipango ya kudhibiti ongezeko la idadi ya watu nchini humo.Ripoti kwamba daktari Rout alitumia pampu ya baiskeli ili kuyafurisha matumbo ya wanawake kwa lengo la kupata nafasi ya vifaa vya upasuaji kuingia ndani, imezua pingamizi nchini India tangu habari hizo zitangazwe.

Maafisa wa serikali wamesema kuwa utumizi wa hewa ya kawaida badala ya ile ya kaboni unaweza kusababisha magonjwa kadhaa.
Mkuu wa afya katika jimbo la Orrisa Arati Ahuja amesema kuwa ukataji wa kizazi katika jimbo hilo sasa utafanyika katika hospitali zenye vifaa vyote .

''Madaktari watalazimika kuambatana na maagizo ya kimataifa ili kukinga maambukizi yoyote '',bi Ahuja alsema.Ukataji wa kizazi hufanyika kupitia kuzifunga tubu zinazobeba mayai ya mwanamke.

Hii hufanyika kupitia kufunga na kamba na baadaye kukata tubu hizo,swala linalozuia mayai na mbegu za kiume kukutana ili kutengeza mimba.

Lakini daktari Rout amesema kuwa amekuwa akitumia pampu kwa zaidi ya mara 100 lakini hakujawahi kutokea tatizo lolote.
Anasema kuwa waliamua kutumia pampu hiyo wakati kifaa kinachojulikana kama Insafleta kilipokosekana kwa upasuaji.

FAHAMU UGONJWA WA SARATANI YA TEZI DUME (PROSTATE CANCER)-2


Wiki iliyopita nilianza kuelezea ugonjwa wa saratani ya tezi dume, leo nitafafanua dalili za ugonjwa huu kama ifuatavyo:

Daktari mmoja ambaye ni miongoni mwa waathirika wa saratani hiyo na mwanzilishi wa kampeni ya kuangamiza saratani ya tezi dume nchini Tanzania ya ‘50 Plus Campaign’ anasema kuwa, ugonjwa huu ukitambuliwa mapema huweza kutibika kwa urahisi.

Kuna vihatarishi vingi vinavyochangia mwanamume kupata saratani ya tezi dume. Vifuatavyo ni baadhi yake; kwanza kabisa ni umri. Nafasi ya kupata saratani ya tezi dume huongezeka sana hasa ukifikia umri wa karibu miaka 50 na kuendelea.

Nasaba ni kihatarishi kingine ambapo wanaume wenye historia ya tatizo hili kwenye familia zao, yaani wale ambao mmoja wa ndugu zao wamewahi kuugua ugonjwa huu huwa katika hatari ya kupata kansa hiyo kutokana na kurithi ‘gene’ za ugonjwa huo. Suala lingine ni lishe ambapo wanaume wanaopenda kula nyama au (red meat) na walaji wa chakula chenye kiasi kikubwa cha mafuta hasa ya wanyama huwa katika hatari kubwa ya kupata saratani ya tezi dume.

Wanaume wasiopenda kufanya mazoezi, wanene na wenye upungufu wa virutubisho vya Vitamin E pia wako kwenye hatari zaidi ya kupata saratani ya kibofu cha mkojo. Wanaume wengine walio katika hatari kubwa ya kupata saratani ya tezi dume ni pamoja na wale wenye asili ya Afrika (weusi) ikilinganishwa na wazungu, wakulima wanaotumia aina fulani ya mbolea za kemikali, wanaofanya kazi katika viwanda vya kutengeneza matairi na wachimbaji madini, hususan aina ya cadmium.

DALILI
Katika hatua zake za awali, dalili za saratani ya tezi dume hazitofautiani na zile za kuvimba kwa tezi dume au BPH. Dalili hizo ni pamoja na, kupata shida wakati wa kuanza kukojoa, kutiririka kwa mkojo baada ya kumaliza kukojoa, kukojoa mkojo wenye mtiririko dhaifu, kukojoa mara kwa mara hasa nyakati za usiku, kujikakamua wakati wa kukojoa na kushindwa kumaliza mkojo wote na kutoa mkojo uliochanganyika na damu.

Pamoja na kueleza dalili hizo wasomaji wanapaswa kutambua kuwa, mwanaume anapoanza kuona na kuhisi baadhi ya dalili hizo, anapaswa kujua kuwa, seli za saratani katika tezi dume lake huwa zina umri wa takribani miaka saba na kuendelea.

Iwapo saratani imesambaa mwilini kiasi cha kuhusisha sehemu nyingine za mwili, mgonjwa anaweza kuwa na maumivu makali ya mifupa katika maeneo ya nyonga, mapajani na kiunoni. Aidha mgonjwa huwa na dalili nyingine zinazoweza kumpata mgonjwa mwingine yeyote wa saratani kama vile kupungua uzito, kuhisi kichefuchefu, uchovu, kizunguzungu na kadhalika.

JE, VIDONDA VYA TUMBO VINATIBIKA?-2



Kama tulivogusia wiki iliyopita kuhusiana na visababishi vinavyoweza sababisha tatizo hili la vidonda vya tumbo, navyo ni kama;•Kutofuata ratiba nzuri ya chakula.
•Mawazo (Stress).

•Kula chakula kingi kupita kiasi, hii imekuwa kama hali ya kawaida hasa kwa wanaume wengi na hata wengine kudiriki kusema kwamba “Sifa ya mwanaume ni kula sana”

wakati hii siyo sahihi na kama mwanadamu anakuwa na tabia hii ya kula sana basi kunauwezakano mkubwa wa kupata tatizo hili la vidonda vya tumbo hasa kwenye utumbo mwembamba ndiyo maana wanaume wanapatwa na tatizo hili mara mbili zaidi ya wanawake na hasa kwa wanaume wenye umri kuanzia miaka 40 – 55, lakini hii haimaanishi kwamba kwa watu wenye umri chini au juu zaidi ya hapo hawawezi kupatwa na tatizo hili.

Inaaminika kwamba asilimia 15 ya Watanzania wote wana tatizo hili la vidonda vya tumbo na nusu tu ya watu wenye tatizo hilo wanakuwa wamefanyiwa vipimo na wako tayari kwa matibabu.

MADHARA YA TATIZO HILI (CONSTIPATION)
Basi leo tutayaona madhara makubwa yanayowakuta watu wanaopatwa na tatizo kama hili na wanakuwa hawachukui hatua za haraka kulitibu moja kwa moja. Na madhara hayo ni kama;
•Kupatwa na hali ya tumbo kujaa gesi na miungurumo ya hapa na pale.

MAGONJWA YA KIKE NA JINSI YA KUKABILIANA NAYO (GYNO PROBLEMS)-2


Uvimbe katika viungo vya uzazi vya mwanamke ‘Pelvic Mass’
Uvimbe katika viungo vya uzazi vya mwanamke ni tatizo sugu linalosumbua wanawake wengi walio katika umri wa kuzaa.

\Hakuna chanzo halisi cha uvimbe ingawa baadhi husababishwa na matatizo katika mfumo wa homoni.
Uvimbe katika viungo vya uzazi vipo nje na ndani. Uvimbe unaweza kuwa mkubwa kama mimba au mdogomdogo na mwingi.

Uvimbe pia unaweza kuwa katika vifuko vya mayai ‘Ovarian Cyst’ ambapo hizi zipo aina mbili. Kuna Lutel Cyst ambayo hupona yenyewe na nyingine huwa ndogo tu katika vifuko vya mayai na hupona kwa dawa.

Kuna Cyst nyingine huwa kubwa kiasi kwamba humsababishia mwanamke apate maumivu makali upande mmoja wa tumbo kwa chini. Uvimbe ukifikia hali hii tiba yake ni upasuaji.Kuna aina nyingine ya uvimbe unakuwa nje ya kizazi, nje ya mrija na nje ya kifuko cha mayai ‘Tubal Ovarian Mass’ au kwa kifupi huitwa ‘TOM’. Aina hii ya uvimbe husababisha maumivu.

Uvimbe huu wa Cyst na TOM daima huwa na maji tu na wakati mwingine damu. Ukiwa na damu ndipo huwa na maumivu makali chini ya tumbo aidha kulia au kushoto. Uvimbe wa damu tiba yake ni upasuaji.

Kuna tatizo lingine ambalo ni vivimbe katika vifuko vya mayai. Tatizo hili hutokea katika vifuko vyote viwili vya mayai na husambaa na mwanamke hufunga kupata hedhi bila ya kuwa na mimba. Tatizo hili pia husababisha mabadiliko kwa mwanamke mikononi, miguuni na wengine huota ndevu na hata sauti hubadilika na kuwa nzito.

Athari za kuwepo na uvimbe katika viungo vya uzazi ni kutoshika mimba, mimba kuharibika, maumivu yasiyoisha chini ya kitovu, maumivu wakati wa tendo la ndoa, damu kutoka ukeni bila ya mpangilio.
Uchunguzi na tiba ya tatizo hili hufanyika katika hospitali za mikoa kwenye kliniki za magonjwa ya kike na matatizo ya uzazi. Endapo uvimbe utakuwa mkubwa sana kwa kuchelewa kutibiwa, athari zake ni kuondolewa kizazi.

Maumivu wakati wa hedhi
Maumivu wakati wa hedhi ni tatizo li nalowasumbua wanawake.
Zipo aina mbili za maumivu, kwanza ni ‘Primary Amenorrhoea’ ambapo ni maumivu yanayowasumbua sana wasichana hasa baada ya kuvunja ungo.

Maumivu haya husababishwa na matatizo katika mfuko wa homoni kutokana na kizazi cha usichana kuwa hakijatanuka vizuri na bado kinaendelea kukua.Tatizo hili huisha kwa tiba baada ya uchunguzi wa kina katika mfumo wa homoni, vilevile likiendelea kwa muda mrefu huwa linaisha baada ya kujifungua.

Msichana pia anaweza kupatwa na tatizo la kutokwa na damu kidogokidogo au nyingi kwa muda mrefu hata zaidi ya mwezi. Hii inatokana na tatizo katika mfumo wa homoni.

Aina nyingine ya maumivu haya ni Secondary Dysmenorrhoea. Hii huwapata wanawake ambao awali hawakuwa na maumivu wakati wa usichana na wanafikia utu uzima wanaanza kupata maumivu. Maumivu haya ya hedhi katika umri wa zaidi ya miaka ishirini huweza kusababishwa na maambukizi sugu katika mfumo wa uzazi.

Matatizo ya maumivu wakati wa hedhi huchunguzwa na kutibiwa kwenye hospitali ya mkoa katika kliniki za magonjwa ya kike na uzazi. Tiba inaweza kuwa ni dawa au upasuaji kutegemea na ukubwa wa tatizo.

Matatizo katika mfumo wa uzazi wa watoto
Matatizo haya yapo mengi ambayo huwasumbua watoto wadogo wa kike na wa kiume kabla ya balehe na kuvunja ungo.Watoto kama ilivyo watu wazima hupatwa na matatizo katika mfumo wa uzazi na athari kubwa hutokea baadaye ukubwani. Tunazungumzia mfumo wa uzazi wa watoto na jinsi ya kuyagundua katika makala zijazo.

Monday, December 1, 2014

SIKU YA UKIMWI DUNIANI; MKOA WA NJOMBE BADO UNAONGOZA KWA MAAMBUKIZI




Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Dkt. Fatma Mrisho akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu Kauli Mbiu ya Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani isemayo, Tanzania Bila Maambukizi Mapya ya VVU, Vifo Vitokanavyo na Ukimwi na Ubaguzi na Unyanyapaa inawezekana inayolenga kupunguza maambukizi Mapya ya Ukimwi, kupunguza vifo vitokanavyo na Ukimwi na kukomesha vitendo vya unyanyapaa kwa asilimia Sifuri.

LEO ni Siku ya Ukimwi Dunia ambapo Kitaifa maadhimisho hayo yanafanyika mkoani Njombe. Kwa takwimu zilizotolewa na Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (Tacaids) 2011/12, Mkoa wa Njombe, Mbeya na Iringa ni vinara wanaoongoza kwa maambukizi ya Virusi vya Ukimwi nchini huku Pemba na Unguja zikiwa chini kwa maambukizi hayo.



Mkoa wa Njombe unaongoza kwa maambukizi ukiwa na asilimia 14.8, ukifuatiwa na Iringa yenye maambukizi asilimia 9.1 na Mkoa wa Mbeya unashika nafasi ya tatu kwa asilimia 9.

Mikoa mingine na asilimia za maambukizi katika mabano ni Shinyanga (7.4), Ruvuma (7.0), Dar es Salaam (6.9) Rukwa (6.2), Katavi (5.9), Pwani (5.9),Tabora (5.1), Kagera (4.8) na Geita (4.7).

Mikoa mingine aliyoitaja ni Mara (4.5), Mwanza (4.2), Mtwara (4.1), Kilimanjaro (3.8), Morogoro (3.8), Simiyu (3.6), Kigoma (3.4), Singida (3.3), Arusha (3.2), Dodoma (2.9), Lindi (2.9), Tanga (2.4), Manyara (1.5), Unguja (1.2) na Pemba (0.3).

Nchi nzima, asilimia 5.1 ya wanawake na wanaume wenye miaka 15-49 wana maambukizi ya VVU. Wanawake wana kiwango kikubwa cha maambukizi kuliko wanaume mijini na vijijini. Asilimia 7.2 ya wakazi wa mijini wana maambukizi ya VVU ukilinganisha na asilimia 4.3 ya wakazi wa vijijini.

Katika takwimu hizo, Watanzania walioonesha kuwa na ufahamu sahihi wa elimu kuhusu Virusi vya Ukimwi (VVU) na Ukimwi wanafikia asilimia 60 jambo linalosababisha kuwepo mwamko mdogo wa kubadili tabia.

Kuhusu tohara kwa wanaume, takwimu zilionyesha inapunguza maambukizi ya Ukimwi kwa asilimia 60 na kusisitiza kuwa ipo haja ya kutoa elimu zaidi juu ya uelewa wa ugonjwa huo.

Visababishi vya Ukimwi:
Miongoni mwa vipengele muhimu ni pamoja na vifuatavyo:
-Uasherati
-Matumizi madogo na yasiyo endelevu ya kondomu
-Ngono za marika yanayotofautiana sana
-Kuwa na wapenzi wengi.
-Ukosefu wa elimu ya maambukizo ya UKIMWI
-Kuwepo kwa maradhi mengi ya ngono kama vile tutuko, homa,
-Jando kwa wanaume
-Sababu za mahali husika, za kushamiri kwa janga nchini ni:
-Umaskini na biashara ya ngono pamoja na ongezeko la wafanyabiashara wa ngono
-Tabia mbaya za ngono za wanaume kutokana na kuruhusiwa kimila kuwa na nguvu
-Kukosekana usawa wa kijamii, kiuchumi, kisiasa na kijinsia pamoja na unyanyaswaji wa wanawake na wasichana walio ndani na nje ya mahusiano.
-Matumizi ya pombe na dawa za kulevya.
-Tabia za kimila (kama vile utakasaji wajane na jando na unyago)
-Safari za aina zote zinazosababisha kuwa mbali kwa wanandoa na ongezeko la mahawara
-Kutokutahiriwa