Karibu Fadhaget Sanitarium Clinic

Tunapenda kukukaribisha katika Kitengo cha Sayansi ya Tiba Asilia.

Kitengo Cha Sayansi Ya Tiba Asilia

Kwa Muda mrefu tumekuwa tukisaidia wengi katika matibabu na kutengeneza dawa bora kabisa kiafya.

Je Unapenda Kufahamu Jinsi Ya Kupata Mapacha?

Tunafundisha jinsi ya kupata jinsia unayotaka, jinsi ya kupata mtoto kama umekosa mtoto kwa muda mrefu. Pia hata jinsi ya kupata watoto mapacha tunaweza kukusaidia.

Tunapatikana Katika Mikoa Zaidi ya 10 Tanzania

Tunazidi kuongeza matawi yetu nchini Tanzania na Nje ya Nchi. Kwa sasa tunapatikana katika mikoa zaidi ya 10 na tunazidi kuongeza matawi yetu. Karibu sana.

Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Thursday, November 27, 2014

JE, VIDONDA VYA TUMBO VINATIBIKA?

watu wengi wanahangaika sana na tatizo la vidonda vya tumbo, pasipo kuwa na uhakika kama wanaweza kupona. Lakini leo tutaweza kujua maana ya vidonda vya tumbo (Ulcers), dalili zake, visababishi vyake na hata jinsi gani Watanzania waweze kujiepusha na maradhi hayo na tiba yake.


MAANA YA VIDONDA VYA TUMBO (ULCERS)

VIDONDA VYA TUMBO hotokea pale kuta za tumbo zinapotoa asidi iitwayo Hydrochrolic acid katika tumbo ambayo kazi yake ni kufanya mmeng’enyo wa chakula aina ya protein ndani ya tumbo, na ikumbukwe kwamba kuta za tumbo asili yake ni protein (protein in nature), na kwa maana hiyo basi kama kuta za tumbo zimeshatoa asidi hii katika tumbo kwa ajili ya mmeng’enyo wa chakula ndani ya tumbo na ikakuta ndani ya tumbo hakuna chakula cha kumeng’enywa basi mmeng’enyo huu huanza kufanyika katika kuta za tumbo na baadaye kuta zinakuwa zimelika hivyo kusababisha tatizo kubwa la vidonda hivyo.

Wataalamu wamegawanya vidonda vya tumbo katika makundi makubwa mawili, nayo ni;
Vidonda vya tumbo vinavyotokea tumboni (Gastric ulcers), hii ni ile hali ya kulika kwa kuta za tumbo, inapotokea hali hiyo huweza kuambatana na maumivu makali maeneo ya tumbo;

Vidonda vya tumbo vinavyotokea kwenye utumbo mwembamba (Duodenary ulcers), hii ni ile hali ya kulika kwa kuta za utumbo mwembamba ulio karibu na tumbo, na utumbo mwembamba unaweza kupata vidonda hadi inchi 11 kutoka sehemu inayopokelea chakula kutoka tumboni, na kwa maana hiyo maumivu huweza kusambaa hadi maeneo ya chini ya tumbo.

VISABABISHI
Kutokufuata ratiba nzuri ya chakula, kama mwanadamu anakua hapati chakula kwa wakati sahihi na anakaa muda mrefu bila kula, basi husababisha vidonda vya tumbo kwani kuta za tumbo zinapotengeneza asidi hii kwa ajili ya kumeng’enya chakula na wakati huo huo anakuwa hajapata chakula kwa muda mrefu basi mmeng’enyo huu huanza kufanyika kwenye kuta za tumbo na baadaye inaweza kusababisha vidonda hivyo.

Mawazo (stress), kwa mwanadamu anayekumbwa na msongo wa mawazo (stress) na wakati huo huo akawa hali vizuri, anaweza kukumbwa na maradhi hayo kwani husababisha kutengenezwa kwa Hydrochrolic acid ndani ya tumbo.

Kwa ushauri, vipimo na tiba dokta anapatikana kwenye vituo vyake vya Dar es Salaam, Tanga, Morogoro na Mwanza.Nawatakia afya iliyo njema kabisa.

Itaendelea wiki ijayo.

FATUMA RAMADHANI RASHID AKIMBIWA NA MUNGU KISA TUMBO KUJAA MAJI

Stori: Waandishi Wetu
MAMA wa watoto watano, Fatuma Ramadhani Rashid (37) amejikuta akitelekezewa watoto hao na mumewe Matola, kisa akidai ni yeye tumbo lake kujaa maji. Tukio hilo la kusikitisha lilitokea Juni 12, mwaka huu, Ukonga-Mongolandege, Dar ambapo mama huyo alikuwa akiishi na mume wake huyo lakini mara baada ya kuanza kwa dalili za ugonjwa huo mumewe alianza visa na kutoweka nyumbani.


Mama wa watoto watano, Fatuma Ramadhani Rashid aliyetelekezwa na mumewe kutokana na tumbo kujaa maji.

“Tulikuwa tukiishi vizuri lakini kutokana na maradhi yaliyonikumba mume wangu aliamua kunikimbia na kunitelekezea watoto hawa, sasa watoto wamekuwa ombaomba,’’alisema mwanamke huyo.
Hata hivyo, kufuatia na hali ya maisha yao kuendelea kuwa ngumu, nyumba hiyo waliyopanga walifukuzwa na kubaki wakitangatanga huku wakisaidiwa na majirani waliokuwa wakiwaonea huruma.
Nyaraka za hospitali za Fatuma Ramadhani Rashid.

Alielezea kuwa watoto wake wameamua kuishi mitaani baada ya kushindwa kwenda shule kwa kukosa ada ambapo mmoja wao alikuwa kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari Mbuyuni- Chanika wilayani Ilala, Dar.

Watoto watano aliotelekezewa Fatuma Ramadhani Rashid.

Mama huyo alisema kwa ugonjwa wake huo, alikwenda Hospitali ya Amana na kuambiwa tumboni kumejaa maji lakini anaweza kutibiwa pasipo kufanyiwa oparesheni ila anatakiwa kuwa na Sh. 500,000.
Mama huyo aliomba yeyote atakayeguswa na tatizo la familia yake na yeye mwenyewe anaweza kumchangia kwa simu; 0783 521 180 Fatuma Ramadhani.

Wednesday, November 26, 2014

JK APOKEA SALAMU ZA KHERI TOKA KWA RAIS BARACK OBAMA WA MAREKANI


Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mh.Liberata Mulamula akiwasilisha kwa Rais Dkt.Jakaya M rishoKikwete salamu za kumtakia kheri na afya njema kutoka kwa Rais wa Marekani Barack Obama jijini Baltimore, Maryland, Marekani.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea kwa furaha na ujumbe kutoka Ubalozi wa Tanzania ulioko jijini Washington DC uliomtembelea kumjulia hali na kwasilisha salamu za Rais Barack Obama.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Balozi Liberata Mulamula na ujumbe wake wa maafisa waandamizi wa ubalozi wa Tanzania nchini Marekani baada ya kupokea salamu maalumu za kumtakia kheri na afya njema kutoka kwa Rais Barack Obama wa Marekani jijini Baltimore, Maryland, Marekani.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na maafisa waandamizi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani uliopo Washington D.C. wakati walipomtembelea mjini Baltimore Maryland ambapo balozi Liberata Mulamula aliwasilisha kwa Rais Kikwete Salamu maalum za kumtakia kheri na afya njema kutoka kwa Rais Barack Obama jijini Baltimore, Maryland, Marekani. Picha na Freddy Maro

STEVEN JOHN ANATESEKA NA SARATANI YA TUMBO..TUMSAIDIE

Stori: Makongoro oging’
“Maishi yangu yako hatarini, nachungulia kaburi, nimeteseka kwa muda mrefu bila kupona wala msaada, nimetoka katika ukoo maskini unaotegemea kwa asilimia kubwa kilimo cha jembe la mkono, nitapata wapi shilingi milioni moja na laki tano na arobaini na tano elfu ili nikatibiwe?”
Hii ni sehemu ya kilio cha Steven John anayesumbuliwa na ugonjwa wa saratani ya tumbo.


Steven John anayesumbuliwa na ugonjwa wa saratani ya tumbo.

AMETOKA WAPI?
John ni mkazi wa Kijiji cha Sokoni One, mkoani Arusha, amekua akisumbuliwa na ugonjwa huo kwa kipindi cha miaka miwili bila kupata nafuu na hali yake inazidi kubadilika kila mara ingawa ametakiwa na madaktari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kufanyiwa upasuaji wa pili baada kufanyiwa hivyo huko nyuma.
Mgonjwa huyu anazunguka huku na kule kutafuta fedha bila mafanikio na kwa sasa anawaomba watu wenye huruma wamchangie ili akamilishe tiba yake.

FAMILIA INAISHIJE?
“Nina familia ya mke na watoto nane, walikuwa wakiishi kwa kunitegemea lakini kwa kipindi cha miaka miwili sasa wamekosa msaada wangu, kwani nimekuwa nikizunguka hospitali kadhaa huku nikiwa na mke wangu kutafuta matibabu lakini tunakumbana na vikwazo vingi kikiwemo cha ukosefu wa fedha.

“Jambo hilo linanifanya niwe na mawazo mengi sana ya kumtaka Mola aichukue roho yangu, kwani nimeanza kuchungulia kaburi kuliko kuisumbua familia yangu inayoteseka kwa kukosa matunzo nami kuteseka kwa maumivu makali, nimekuwa ombaomba hapa mjini ili nipate fedha lakini hakuna mafanikio.


Muonekano wa sehemu za kutolea haja kubwa na ndogo.

UGONJWA ULIANZAJE?
“Nakumbuka ugonjwa huu ulinianza Oktoba mwaka juzi, ulianza kwa tumbo kuunguruma pia nilipoteza hamu ya kula hali iliyonifanya niende katika zahanati ya kijijini kwetu, wao walinieleza kwamba nina vidonda vya tumbo walinipa dawa nikapata nafuu kidogo lakini baada ya muda hali ilibadilika na kuwa mbaya.

“Ikatokea kwa siku kumi na saba sikwenda haja kubwa, tumbo lilivimba kiasi cha kutaka kupasuka, nikaenda Hospitali ya Mount Meru, Arusha, nilifanyiwa vipimo kikiwemo cha x-ray, wakagundua kuwa sehemu ya haja kubwa kumeziba ikabidi wanifanyie upasuaji, pia walitoboa tumbo nikawa najisaidia kwa kutumia mpira.

“Baada ya siku mbili tangu nifanyiwe upasuaji huo, kibofu cha mkojo kikawa kinauma baada ya mrija kuziba, nilifanyiwa upasuaji nikawa najisaidia kwa kutumia mpira baada ya tumbo kutobolewa tena, huu mfuko wa kulia ni wa haja ndogo na wa kushoto ni wa haja kubwa.

AKATWA KIPANDE CHA NYAMA
“Nikiwa bado nipo Mount Meru madaktari walikata kipande cha nyama pajani na kukipeleka Hospitali ya Nairobi nchini Kenya kwa vipimo na majibu yalipokuja iligundulika kuwa nina saratani ya utumbo mpana.
“Walinieleza nije hapa Dar, Hospitali ya Ocean Road ambapo niliendelea na matibabu, ilipofika Septemba 16, mwaka huu nilishauriwa niende Muhimbili nikafanyiwe vipimo kama saratani imeisha.

“Lengo lilikuwa kama ugonjwa hakuna, niweze kurejeshewa mfumo wa haja kubwa na ndogo katika hali ya kawaida. Hata hivyo, nilipofika Muhimbili nilifanyiwa kipimo kimoja cha City Scan na vingine bado, ndiyo maana nahangaika kutafuta fedha ili nikakamilishiwe vipimo hivyo kisha nifanyiwe upasuaji mwingine.

“Kwa kuwa sina fedha, nawaomba wasamaria wema wanisaidie ili nifanyiwe vipimo na upasuaji mwingine, sina raha hapa nilipo. Napatikana kwa simu namba 0712 820440 au 0752 225061,” alisema John kwa huzuni.

BABY MADAHA ADAIWA KUAMBUKIZWA GONJWA BAYA

Na Mwandishi Wetu
MSANII wa Bongo Fleva, Baby Madaha anadaiwa kuambukizwa gonjwa hatari la zinaa ambalo halikutajwa jina lakini likielezwa kuwa linampa wakati mgumu kisaikolojia. Chanzo kimoja kimeiambia show bize kuwa, nyota huyo amekuwa akitumia dawa za kusafisha haja ndogo kwa muda mrefu lakini bila mafanikio.


Msanii wa Bongo Fleva, Baby Madaha.

Show bize ilimsaka Baby Madaha mwenyewe ambapo aling’aka kwa ukali.
“Hizo habari nani kakupa wewe? Hayo si moja ya maisha ya wanadamu kwani kipi kibaya hapo? Oke, sawa naumwa na hao wanaume wanaotaka nikatibiwe wanajua mimi naumwa nini? Magonjwa ya zinaa si yana dawa?” alihoji.

Hata hivyo, mrembo huyo alisema yeye ana tatizo la haja ndogo kuwa chafu lakini si ugonjwa wa zinaa.

MTOTO CAREEN MPONDO (4) ANATESEKA NA UGONJWA WA FIGO ANAHITAJI MSAADA WAKO

Stori: Imelda Mtema
Mtoto Careen Mpombo (4) (pichani), mkazi wa Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam, yuko katika mateso makali kufuatia kusumbuliwa na figo moja ambayo haifanyi kazi.


Mtoto Careen anayesumbuliwa na figo moja ambayo haifanyi kazi.

Licha ya kuugua figo, mtoto huyo pia ana ugonjwa wa mafindofindo (Tonsillitis) unaomfanya akose raha kutokana kuwa na maumivu makali yanayosababisha ashindwe kula.
Akizungumza na gazeti hili, mama mzazi wa mtoto huyo ambaye pia huitwa Careen, alisema mwanaye alianza kuumwa kwa kuvimba mashavu akadhani ana mafindofindo hivyo aliamua kumpeleka katika Hospitali ya Kisarawe iliyopo mkoani Pwani.

“Hospitalini walimpa dawa ya PEN V na kumchoma sindano wakijua ni mafindofindo lakini kadiri siku sinavyozidi kusonga mbele ndivyo anavyozidi kuumwa.“Imefikia sasa anashindwa kulala kabisa, tulimrudisha hospitali baada ya kuona tumbo limeanza kuvimba, tukashauriwa kumpeleka Hospitali ya Taifa Muhimbili.


Mtoto Careen akiwa na maumivu makali kutokana na ugonjwa wa figo.

“Madaktari waliniambia nimpeleke Hospitali ya Regency kwa vipimo zaidi ambapo waligundua kuwa figo yake moja haifanyi kazi na ana mafindofindo, wakaniambia anatakiwa kupima kipimo ambacho atakatwa nyama gharama yake ni Shilingi 140,000,” alisema mama huyo.

Aliongeza kuwa, baada ya kuambiwa hivyo aliumia sana kwa kuwa alijua mtoto wake atazidi kuteseka kwa kuwa hana uwezo ya kupata kiasi hicho cha fedha kwa sababu mume wake alipata ajali ya gari na bado ni mgonjwa na yeye hana kazi na isitoshe anaumwa.

“Nilivyoambiwa nahitaji kutoa shilingi laki moja na elfu arobaini niliumia na kutoka machozi kwa kuwa nilijua wazi mtoto wangu atazidi kuteseka kwa kuwa sina fedha hizo, sasa nashinda nikilia, naomba Watanzania wanisaidie,” alisema mama huyo.

Kama umeguswa na habari ya mtoto Careen na unapenda kumsaidia, wasiliana na mama yake kwa namba 0657 628 889, KUTOA NI MOYO SIYO UTAJIRI.

MWIGIZAJI WA FILAMU TANZANIA DK CHENI ALISHWA SUMU TENA!

Stori: Imelda Mtema
Staa wa kiume wa sinema za Kibongo, Mahsein Awadh ‘Dk Cheni’, kwa mara nyingine alilazwa katika Hospitali ya TMJ iliyopo Mikocheni jijini Dar baada ya kudaiwa kula chakula kinachosadikika kuwa na sumu (poisonous food).

Mahsein Awadh ‘Dk Cheni’ akiwa hoi hospitalini.

Akizungumza na mwandishi wetu wikiendi iliyopita Dk Cheni alisema kuwa alikuwa mshehereshaji (MC) kwenye harusi moja iliyofanyika maeneo ya Sinza jijini Dar ndipo akala chakula hicho ambapo muda mfupi baadaye alianza kujisikia vibaya ‘kichina’.

Staa huyo alisema kuwa baada ya hatua chache kutoka ukumbini, tumbo lilianza kumuuma kisha akaishiwa nguvu ndipo akaweka gari pembeni na kupiga simu kwa ndugu kuomba msaada.
Dk Cheni aliendelea kueleza kuwa baada ya kupata msaada moja kwa moja alipelekwa kwenye Hospitali ya Burhani jijini Dar.

‘Dk Cheni’,

Alisema kuwa baadaye alihamishiwa kwenye Hospitali ya TMJ ambapo madaktari walipompima waligundua alikuwa amekula chakula chenye sumu ndipo wakampatia matibabu na kulazwa.
Alisema siku ya pili yake aliruhusiwa huku akisema kitendo hicho kimemsikitisha mno.

Siyo mara ya kwanza kwa Dk Cheni kulishwa chakula chenye sumu kwani safari hii ni mara ya pili ambapo mwaka jana alilazwa tena kwa ishu kama hiyo, jambo ambalo haelewi kwa nini inakuwa hivyo

FAHAMU UGONJWA WA SARATANI YA TEZI DUME (PROSTATE CANCER)



Wiki hii wasomaji wengi wamependa nijadili kuhusu kansa ya tezi dume au Prostate Cancer kwa kitaalamu zaidi.Ugonjwa huu huweza kusababisha vifo. Ili kuujua vyema ugonjwa huo tafadhali fuatilia makala haya.

Saratani ya tezi dume upo katika nafasi ya tatu kwa kusababisha vifo vinavyotokana na kansa kwa wanaume duniani. Pia ni chanzo kikuu cha vifo vinavyosababishwa na saratani kwa wanaume wenye umri wa miaka 50 na kuendelea. Hata hivyo, satarani ya tezi dume kwa sasa inawapata sana wanaume kuanzia miaka 25.

Lakini kabla ya kuendelea mbele hebu kwanza tujue tezi dume ni zipi. Kama tulivyosema, neno saratani ni jina la ugonjwa ambalo hutokea wakati chembechembe za uhai au seli katika sehemu fulani ya mwili zinapoanza kukua bila kufuata utaratibu wa mfumo wa mwili na kutengeneza vijiuvimbe vidogovidogo.

Kwa kawaida seli huwa zinajigawa, kupevuka na baadaye kufa kwa kufuata taratibu za mfumo wa mwili. Lakini seli za saratani hazifuati mfumo huo. Badala ya kufa, zenyewe huishi muda mrefu kuliko chembechembe za kawaida na wakati huohuo huendelea kutengeneza seli nyingine na kuwa uvimbe wa saratani au tumour.

Tezi dume linapatikana katika mwili wa mamalia dume tu na pale seli katika kiungo hicho zinapoanza kukua bila kufuata utaratibu wa mfumo wa mwili hapo ndipo mtu hupata saratani ya tezi dume.
Saratani ya tezi dume huwapata wanaume tu na hasa wenye umri wa takribani miaka 50 na kuendelea. Saratani hii imethibitika kushika nafasi ya pili, ukiachia mbali saratani ya mapafu kwa kusababisha vifo vya wanaume wenye umri wa takribani miaka 50 na kuendelea.

Tafiti za Chama cha Saratani cha Marekani (ACS) na cha Afrika Kusini (CANSA) zimebaini kuwa, mwanaume mmoja kati ya sita hupata saratani ya tezi dume katika uhai wake. Kutokana na takwimu za mwaka 2010 za dunia nzima, malaria iliua watu laki tano, kifua kikuu watu milioni 2.1, Ukimwi watu milioni 1.8 na saratani watu milioni 9.9.

Kwa mujibu wa takwimu hizo, idadi ya watu waliofariki dunia kutokana na ugonjwa wa saratani ni kubwa ikilinganishwa na ya magonjwa mengine. Itaendelea wiki ijayo.

Monday, November 24, 2014

TARATIBU ZA TIBA ZA RAIS WA TANZANIA DKT. J.K KIKWETE ZAKAMILIKA




Taratibu za matibabu ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete (Pichani), zimekamilika leo, Jumatatu, Novemba 24, 2014.

Taratibu hizo za matibabu za Mheshimiwa Rais Kikwete zimekamilika kiasi cha saa 12 asubuhi ya leo wakati madaktari bingwa katika Hospitali ya Johns Hopkins iliyoko mjini Baltimore, Jimbo la Maryland, Marekani, walipomfanyia hatua ya mwisho ya tiba.

Hata hivyo, Rais Kikwete ataendelea kupumzika na kuangaliwa kwenye Hoteli Maalum inayohusiana na Hospitali ya Johns Hopkins kwa siku mbili hadi tatu kabla ya kuanza safari ya kurejea nyumbani.
-----------------------------------------------------
Taratibu za matibabu ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete (Pichani), zimekamilika leo, Jumatatu, Novemba 24, 2014.

Taratibu hizo za matibabu za Mheshimiwa Rais Kikwete zimekamilika kiasi cha saa 12 asubuhi ya leo wakati madaktari bingwa katika Hospitali ya Johns Hopkins iliyoko mjini Baltimore, Jimbo la Maryland, Marekani, walipomfanyia hatua ya mwisho ya tiba.

Hata hivyo, Rais Kikwete ataendelea kupumzika na kuangaliwa kwenye Hoteli Maalum inayohusiana na Hospitali ya Johns Hopkins kwa siku mbili hadi tatu kabla ya kuanza safari ya kurejea nyumbani.

Kama kila kitu kitakwenda kama ilivyopangwa na madaktari, Rais Kikwete anatarajiwa kurejea nyumbani Jumamosi, Novemba 29, 2014.

Rais Kikwete aliondoka nchini Alhamisi ya Novemba 6, 2014, kwenda kufanyiwa uchunguzi wa afya yake lakini madaktari katika Hospitali ya Johns Hopkins waliamua kumfanyia upasuaji wa tezi dume Jumamosi ya Novemba 8, 2014.

Rais Kikwete anaendelea kuwashukuru Watanzania kwa sala na maombi yao ya kumtakia heri ya kupona haraka na kurejesha afya njema katika kipindi chote cha ugonjwa wake.

Imetolewa na:



Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
24 Novemba,2014

JINSI YA KUTUNZA NGOZI YENYE MAFUTA


Ngozi yenye mafuta kwa kawaida huwa inang'ara, nene na yenye rangi iliyotitia. Mara nyingi ngozi yenye mafuta mengi sana huwa na chunusi nyingi na vipelepele na mara nyingine huwa na chunusi zenye vichwa vyeusi. Katika aina hizi za ngozi mafuta hutokana na tezi za sebaceous na kuzalisha mafuta zaidi ya kiwango kinachotakiwa. Mafuta hayo husambaa katika ngozi na kuifanya iwe na mafuta mafuta.
Sababu zinazosababisha ngozi kuwa na mafuta:
• Kuridhi.
• Lishe.
• Kiwango cha homoni mbalimbali mwilini.
• Ujauzito.
• Vidonge vya kuzuia mimba.
• Baadhi ya vipodozi .
• Hali ya unyevu (humidity) na hali ya hewa ya joto.

Namna ya kutunza ngozi zenye mafuta
Faida kubwa ya kuwa na ngozi yenye mafuta ni kuwa haizeeki kwa haraka ikilinganishwa na aina nyinginezo za ngozi. Miongoni mwa mambo yanayosaidia ili kuitunza ngozi yenye mafuta na kuiepusha na chunusi na hali isiyopendeza ni:-

1. Ngozi yenye mafuta inahitajia kusafishwa vyema kwa maji ya moto na sabuni ili kuzuia vinyweleo visizibwe na mafuta.

2. Epusha vifaa vigumu visikwaruze uso wako na kupelekea ngozi kubanduka, kwani suala hilo husababisha tezi za mafuta kufanya kazi zaidi ili kujaza sehemu iliyopotea ya mafuta.

3. Epuka kutumia vipodozi ambavyo huifanya ngozi yako ipotze maji au kukauka. Kwani husababisha sehemu ya juu ya ngozi inyauke, na hivyo kusababisha mafuta kuziba vinyweleo na kupelekea kutokea vichwa vyeusi.

4. Jitahidi kuitunza vyema ngozi yako na kuisafisha vizuri. Jaribu kuosha uso mara mbili au tatu kwa siku. Usioshe mara nyingi kwani kufanya hivyo huufanya uso kutoa mafuta zaidi.

5. Chagua kile unachosafishia kwa makini, jiepushe kutumia cream nzito nzito au vifaa vugumu wakati wa kuosha uso wako. Ni bora utumie sabuni za kawaida zisizokuwa na madawa. Unaweza kutumia lotion ya kuua bacteria au sabuni zisizo na dawa nyingi (lightly medicated), au sabuni zenye madini mbalimbali. Ni bora usioshe au kutumia lotion au michanganyiko yenye alkoholi.

6. Tumia maji ya moto au ya vuguvugu wakati unaosha uso wako.

7. Wakati unapoosha uso wako, ukande kwa kutumia ncha za vidole, jiepushe kupaka sabuni moja kwa moja usoni, inaweza kuganda na kuzuia vinyweleo kuziba.

8. Kutumia mask za udongo (clay) na tope (mud) husaidia katika ngozi za aina hii. Ni bora utumie mask mara moja au mbili kwa wiki.

9. Jitahidi kutumia vipodozi vya uso ambavyo vimetengenezwa kwa ajili ya ngozi yenye mafuta.

JINSI YA KUONDOA MADOA YA CHUNUSI

JUISI YA LIMAO NA MAJI YA ROSE
Chukua maji ya rose kiasi kama ni kijiko kimoja na maji ya limao nayo yawe kijiko kimoja paka eneo liloathiriwa na madoa, kaa kwa muda wa nusu saa mpaka saa moja kisha osha uso wako, fanya hivyo kwa muda wa wiki tatu utapona madoa doa yote usoni.

Juisi ya limao na liwa
Chukua juisi ya limao kiasi changanya na liwa kisha paka eneo lililoathirika, kaa kwa muda wa dakika tano utaona matokeo.
Juisi ya limao na unga wa mdalasini pia ni tiba nzuri ya kusafisha uso kuondokana na madoa yote.


Asali na mdalasini
Chukua vijiko vitatu vya asali na kimoja cha mdalasini changanya kisha paka usoni pia ni tiba nzuri inasaidia kwa kiasi kikubwa.

Apple na asali
Chukua apple liponde changanya na asali kiasi, kisha paka usoni mbali na kutibu madoa pia inatibu chunusi.

Maji ya kitunguu swaumu
chukua maji ya kitunguu swaumu paka kwenye madoa yote utaona matokeo.
Nyanya
chukua kipande cha nyanya paka usoni kisha kaa kwa muda wa saa moja nayo ni tiba nzuri.

Tango
Tango pia ni tiba, chukua kipande sugua uso wako kila siku asubuhi utaona matokeo.


Papai

Chukua papai liponde kisha paka usoni litakusaidia kuondoa tatizo la madoa yote usoni.

Saturday, November 22, 2014

MAADHIMISHO YA SIKU YA UKIMWI DUNIANI KUFANYIKA KITAIFA MKOANI NJOMBE


Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Taifa ya kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) , Dkt. Fatma Mrisho akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu Kauli Mbiu ya Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani isemayo, Tanzania Bila Maambukizi Mapya ya VVU, Vifo vitokanavyo na Ukimwi na Ubaguzi na Unyanyapaa inawezekana inayolenga kupunguza maambukizi Mapya ya Ukimwi, kupunguza vifo vitokanavyo na Ukimwi na kukomesha vitendo vya unyanyapaa kwa asilimia Sifuri.

Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Taifa ya kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) , Dkt. Fatma Mrisho akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya Siku ya Ukimwi duniani yatakayofanyika kitaifa mkoani Njombe kuanzia Novemba 24, 2014 na kufikia kilele chake Desemba 1, 2014.

Mkurugenzi wa ufuatiliaji wa Tathmini wa Ofisi ya Taifa ya kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) Dkt. Jerome Kamwela akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu utoaji wa huduma na upatikanaji wa dawa za kufubaza makali ya Virusi vya Ukimwi kwa watu wanaoishi na VVU katika maeneo mbalimbali nchini.

Mkurugenzi wa ufuatiliaji wa Tathmini wa Ofisi ya Taifa ya kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) Dkt. Jerome Kamwela akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu utoaji wa huduma na upatikanaji wa dawa za kufubaza makali ya Virusi vya Ukimwi kwa watu wanaoishi na VVU katika maeneo mbalimbali nchini.

Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa TACAIDS akiwaonesha waandishi wa habari (hawapo pichani) mbinu na elimu inayotolewa na TACAIDS katika maeneo mbalimbali ikiwemo matumizi ya mipira ya kike kwa wanawake ili kuzuia maambukizi mapya ya VVU.

RAIS KIKWETE ATOLEWA NYUZI KATIKA MSHONO, AFYA YAKE YAZIDI KUIMARIKA


Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoka katika hospitali ya Johns Hopkins iliyopo Baltimore Maryland baada ya kutolewa nyuzi katika mshono baada ya kufanyiwa upasuaji wiki iliyopita. Rais Kikwete anatarajiwa kurudi tena hospitalini hapo Jumatatu kwa ukaguzi wa maendeleo ya kidonda na ushauri. Kulia kwake ni Daktari wa Rais Profesa Mohamed Janabi.…



Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoka katika hospitali ya Johns Hopkins iliyopo Baltimore Maryland baada ya kutolewa nyuzi katika mshono baada ya kufanyiwa upasuaji wiki iliyopita. Rais Kikwete anatarajiwa kurudi tena hospitalini hapo Jumatatu kwa ukaguzi wa maendeleo ya kidonda na ushauri. Kulia kwake ni Daktari wa Rais Profesa Mohamed Janabi.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa amepumzika kwenye hoteli maalumu baada ya kutoka katika hospitali ya Johns Hopkins iliyopo Baltimore Maryland alikotolewa nyuzi katika mshono baada ya kufanyiwa upasuaji wa Tezi Dume wiki iliyopita. Rais Kikwete anatarajiwa kurudi tena hospitalini hapo Jumatatu kwa ukaguzi wa maendeleo ya kidonda na ushauri.

(Picha na Freddy Maro)

Thursday, November 20, 2014

HOSPITALI YA AGA KHAN YATOA VIPIMO VYA BURE KWA WABUNGE DODOMA‏

Mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi John Komba akipimwa urefu kwenye viwanja vya Bunge na jopo la madaktari kutoka hospitali ya Aga Khan. Zaidi ya wabunge 200 pamoja na wafanyakazi wa bunge walipata semina ya afya pamoja kupima afya zao bure mwishoni mwa wiki kwenye zoezi ambalo liliongozwa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Mh. Seif Rashid.


Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mh. Margaret Sitta akichukuliwa damu kwa ajili ya vipimo na mshauri wa afya kutoka hospitali ya Aga Khan kwenye jengo la Bunge. Zaidi ya wabunge 200 pamoja na wafanyakazi wa bunge walipata semina ya afya pamoja kupima afya zao bure mwishoni mwa wiki kwenye zoezi ambalo liliongozwa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Mh.Seif Rashid.

Waziri wa Ofisi ya Rais, Prof. Mark Mwandosya akijiandaa kupimwa urefu na mshauri wa afya kutoka hospitali ya Aga Khan kwenye jengo la Bunge. Zaidi ya wabunge 200 pamoja na wafanyakazi wa bunge walipata semina ya afya pamoja kupima afya zao bure mwishoni mwa wiki kwenye zoezi ambalo liliongozwa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Mh.Seif Rashid.

NABO PHILIPO ASUSIWA WATOTO NA MKE WAKE MARIANA SILAYO ETI WANA KIFAFA


MAMA AWAKIMBIA WANAYE WENYE KIFAFA



Bw. Nabo Philipo aliyekimbiwa na mkewe.

HILI nalo ni tukio! Mwanaume mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Nabo Philipo ameibuka na kudai kuwa, mkewe Mariana Thomas Silayo (pichani) amekimbia nyumbani na kumwachia watoto wawili wenye ugonjwa wa kifafa.

Akizungumza kwa uchungu na gazeti hili hivi karibuni, Nabo alisema alifunga ndoa na Mariana mwaka 2002 na kujaliwa kupata watoto wawili, Madelin na Joyce Nabo na ndani ya miaka 13 ya ndoa waliishi kwa amani.


Mke wa Bw. Nabo Philipo, Mariana Thomas Silayo.

“Visa vilianza hivi karibuni baada ya mimi kupata hundi ya shilingi milioni 50 kupitia kazi zangu za ufundi wa kusuka mashine za magari, za kusaga na kukoboa na za matofari.“Nilimuonesha mke wangu hundi ili tupange tuzifanyie nini fedha hizo, lakini baada ya siku mbili hundi ikiwa benki kusubiri iwe tayari kutumika, nilianza kuumwa vitu visivyoeleweka na kuishiwa nguvu.


Mmoja wa watoto wa Bw. Nabo Philipo na mkewe, Mariana Thomas Silayo.

“Nilikimbizwa Hospitali ya Aga Khan (Dar) na kugundulika kuwa nilipewa sumu kwenye chakula.
“Nilimuuliza mke wangu ni nani atakuwa ameniwekea sumu akasema sijui. Siku nyingine nilimkuta ana dawa za ajabuajabu, nikamkalisha chini na kumsema aachane na habari za dawadawa.
“Nilishangaa sana kwani mambo mengi mke wangu alianza kuyafanya kuanzia hapo. Niligundua pia kwamba alikuwa akichukua nguo zake kidogokidogo na kuhamishia sehemu nyingine, ndipo siku moja akatoroka nyumbani moja kwa moja.


Mmoja wa watoto wa Bw. Nabo Philipo na mkewe, Mariana Thomas Silayo.

“Kinachoniuma ni kitendo cha kuniachia watoto wagonjwa, hasa huyu mdogo (Joyce) ambaye hushikwa na kifafa mara kwa mara, wakati mwingine humwangusha asubuhi na kumwachia jioni.
“Nilijaribu kumsihi mke wangu arudi kwa ajili ya watoto lakini kwake imekuwa ngumu. Nimeeleza haya ili jamii imfahamu ni mwanamke wa aina gani kwani hana huruma, maana nilishangaa hata alipoondoka watoto walifurahi,” alisema Nabo.

Mariana alipotafutwa ili kusikia kauli yake kufuatia madai hayo ya mumewe hakupatikana, waandishi wetu wanaendelea kumsaka.

Tuesday, November 11, 2014

MAAMBUKIZI KATIKA MFUMO WA KIZAZI (PELVIC INFLAMMATORY DISEASE)



Mambukizi katika mfuko wa kizazi au kitaalamu pelvic inflammatory disease ni maambukizi ya vijidudu yanayoshambulia sehemu ya ndani ya viungo vya uzazi kama vile mji wa mimba, mirija ya uzazi (follopian tubes), mifuko ya uzazi (ovaries), na viungo vingine vya uzazi vilivyopo kwenye nyonga ya mwanamke ambapo vijidudu hivyo huweza kuleta madhara makubwa kama kutengeneza jipu kati ya mirija ya uzazi na mifuko ya mayai (tubo-ovarian abscess).

SABABU ZA MAAMBUKIZI HAYO (aetiology)
Vijidudu vinavyopanda kwenda kwenye mji wa mimba kutoka katika uke (ascending infection), magonjwa ya zinaa (Sexual transmitted diseases-STDS), vifaa vya hospitali vinavyotumika katika vipimo au kutolea tiba (instrumentation) pia vijidudu huweza kusafiri kupita katika mishipa ya damu (haematogenous and hymphatic spread).

Wadudu wanaoambukiza kwa wingi ambao ni wa magonjwa ya zinaa kama wadudu wa kisonono (neisela gonococca na chylamydia trachomitis). Hawa ni wadudu hatari sana wanaotesa akina mama na kuwasababishia maumivu makali ya tumbo la chini ya kitovu.
Pia kuna vijidudu vingine ambavyo havitegemei oxygen na ambavyo vinategemea oxygen (aerobic organism and anaerobic organism).

Licha ya vijidudu, kuna vihatarishi vinavyoweza kusababisha maambukizi kwenye mji wa mimba, hivyo ni kama kuwa na wapenzi wengi yaani multiple sexual partners, matumizi ya kitanzi kwa ajili ya kuzuia mimba (IUCD), kusafisha kizazi, kuugua magonjwa ya zinaa mara kwa mara, mwanamke kunawa na sabuni zenye kemikali nyingi sehemu za siri.

Pia kuna vitu ambavyo husaidia mwili kujikinga na maambukizi ya vijidudu katika mfumo wa uzazi, kama msichana kuwa hajavunja ungo (intact hymen), pia kuna vinyweleo kwenye njia ya mimba ambavyo vinazuia vijidudu kupanda na ute unaotoka kwenye shingo ya kizazi yaani cervicl mucosa barrier.

MAMA: AWALI NILIJUA NINA UJAUZITO KUMBE SIYO

Stori: Na Makogoro Oging’
Mama mmoja mkazi wa Kijiji cha Kipanga, Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa, Flora Samweli Luvinga (24) hali yake ipo hatari baada ya kuvimba tumbo na kumsababishia maumivi makali.“Awali nilidhani ni mimba baadaye nikajua kuwa kumbe siyo bali ni ugonjwa ambao unanipa mateso kwa muda mrefu, sasa sijui hatima ya maisha yangu hapa duniani,” alisema Flora.


Flora Samweli Luvinga (24) anyesumbuliwa na uvimbe mkubwa tumboni.

Mgonjwa huyo ambaye kuumwa kwake kumechukua muda mrefu bila mabadiliko ya kupata nafuu, afya yake imezidi kudhoofu jambo lililomfanya mama yake mzazi kupatwa na presha siku za hivi karibuni na kufariki dunia baada ya kushindwa kupata fedha kwa ajili ya kumtibia.

Katika mahojiano na mwandishi wa habari hii wiki iliyopita saa chache baada ya kurejea jijini Dar akitokea Iringa, Flora aliyekutwa amekaa chini maeneo ya Mwenge akipumzika kutokana na maumivu makali, alikuwa na haya ya kusema:

“Siamini kama ipo siku nitapona na kurejea hali yangu ya kawaida, hapa nilipofikia nimekata tamaa, kwani nimehangaika kwa muda mrefu katika matibabu bila kupata nafuu.
“Ugonjwa wangu ulisababisha mama yangu kukatisha maisha. Nimekuwa nikiwapa shida ndugu zangu, wanashindwa kufanya shughuli zao kwa ajili yangu.”


Flora Samweli Luvinga akiuguzwa na Ndugu yake, Selina Samweli.

HISTORIA YA UGONJWA
Flora alielezea historia ya kuumwa kwake alisema: “Mwishoni mwa Desemba, mwaka 2012 nilianza kusikia maumivu makali tumboni, nikafikiri ni vidonda vya tumbo, nilipata mimba nikajifungua kichanga cha miezi saba katika Hospitali ya Mwananyamala lakini kwa bahati mbaya mtoto akafariki.
“Baada ya muda tumbo likawa linakua, nilifikiri nimepata mimba nyingine lakini cha ajabu nilisikia maumivu kifuani, yalishuka hadi tumboni,wakati huo tulikuwa tukiishi na mume wangu Tandale hapa Dar.

“Ingawa tumbo liliendelea kukua lakini nilipata maumivu makali sana, nilihisi mtoto ambaye ningemzaa angekuwa na matatizo.

TIBA MUHIMBILI, MUME AKIMBIA
“Ilibidi mume wangu anipeleke Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, ili kujua tatizo ni nini na kupata tiba, wakati huo tayari nilikua na watoto wawili. Nikawa sipati unafuu, mume wangu akanikimbia, nikawa sina fedha kwa ajili ya matibabu na kuwanunulia chakula wanangu. “Maisha yalizidi kuwa magumu hali iliyomfanya mama kuuza mazao yake yote na kuja hapa Dar kuniuguza, hata hivyo, aliishiwa fedha.
Flora Samweli Luvinga akisaidiwa na Ndugu na majirani zake.

“Maisha yetu yalizidi kuwa magumu hata chakula kikawa kupata ni shida, tuliishi kwa kusaidiwa na majirani, mama aliamua kwenda Iringa. “Dada yangu aitwaye Selina Samweli alitoka Makambako alikoolewa na kuja kunichukua baada ya mama kumpa taarifa kuhusu jinsi ninavyoumwa.

KODI YA NYUMBA IKAISHA
“Nilimwambia dada sina fedha ya matibabu wala ya kununulia chakula huku kodi ya nyumba nayo ikiwa imeisha.

“Akanihamisha Dar, nikawa naishi naye huko Makambako, nilikua nikipata matibabu katika zahanati ya hapo bila mafanikio, daktari alishauri nipelekwe Hospitali ya Rufaa ya Mbeya. Nilienda.
Tulikaa huko kwa siku 18, tumbo liliongezeka, hakukua na unafuu.

JINSI MAMA ALIVYOAGA DUNIA
Dada naye akawa amechoka alinichukua na kunirudisha kwa mama, tulipofika, mama alitokwa machozi, aliona hali yangu si ya kupona. “Mama hakuchukua muda mrefu, alipatwa na presha, akafariki dunia, nililia sana kwa sababu alinipenda sana, nilibaki nyumbani kwetu peke yangu, nilichukuliwa na dada Selina tukawa tunaishi naye kwake Makambako.

“Aliishiwa fedha akawa anaelekea kukata tamaa, shemeji yangu alishauri niletwe huku Muhimbili, aliomba msaada kwa watu, tukapata nauli ya kuja hapa Dar.
“Hapa unaniona nimekaa, nimetoka Makambako, napumzika, hali yangu imezidi kuwa mbaya, nikipata nafuu nitapelekwa Muhimbili,” alisema Flora.

SINA UWEZO WA DAWA ZA SHILINGI LAKI MBILI
Mwishoni mwa wiki iliyopita mwandishi wa habari hii aliwasiliana naye kwa njia ya simu akiwa Muhimbili kumjulia hali ambapo alisema kwamba tayari amepata baadhi ya vipimo na kimojawapo majibu yamepatikana.

“Natakiwa kununua dawa za shilingi laki mbili. Nimeambiwa hospitali haina dawa hizo, bado nasubiri majibu mengine wiki hii.“Hapa Muhimbili nimetolewa maji tumboni lita sita lakini bado sijaambiwa kinachonisumbua, natarajia kupata majibu wiki ijayo (wiki hii).

“Nawaomba Watanzania wenye moyo wa huruma wanisaidie fedha ya matibabu na chakula kupitia namba hii 0756 613148 au 0657 908261,” alisema mgonjwa huyu akitokwa na machozi.

SADICK SULEIMAN ANAHITAJI MSAADA WAKE ASIKATWE TENA MGUU

Stori: Hamida Hassan na Imelda Mtema

Kijana mmoja Sadick Suleiman (24) (pichani), mkazi wa Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam amesema kuwa madaktari wanataka kuukata mguu wake kwa mara ya tatu baada ya oparesheni mbili kufanyika pasipo mafanikio.


Sadick Suleiman akionyesha sehemu ya mguu wake uliokatwa.

Akizungumza na gazeti hili mwishoni mwa wiki iliyopita akiwa Hospitali ya Ocean Road, Sadick alisema mguu wake ulikatwa kwa mara ya kwanza baada ya kuungua moto mwili mzima alipokuwa amekwenda kuvuna korosho.

“Nakumbuka nikiwa darasa la nne, nikiwa na watoto wenzangu tulikwenda kuokota korosho shambani Mtwara vijijini nilikokuwa nikiishi na wazazi wangu, huko kuna kawaida ya watu kuandaa mashamba yao kwa kuyachoma moto.

“Sasa mimi na mwenzangu ambao tulikuwa wakubwa tukiwa hatujui nini kinachoendelea tulipanda juu ya mti kwa ajili ya kuangua korosho huku wenzetu wakiwa chini wanasubiri kuokota, tukiwa juu tukaona moto unawaka unakuja tulipokuwa lakini kabla hatujashuka chini, ukatuzingira,” alisema Sadick.

Aliongeza kuwa wenzao waliokuwa chini walifanikiwa kukimbia wao wakiwa juu ya mti, uliwakuta na kila walipojaribu kushuka ndivyo ulivyozidi wakapanda zaidi juu ya mti lakini mwisho walizidiwa na kuamua kujitosa kwenye moto ambapo yeye aliungua sehemu kubwa ya mwili na mwenzake aliungua mwili mzima ikiwa ni pamoja na kichwani.

Alisema kuwa alifanikiwa kukimbia huku nguo zake zikiwaka moto, alipofika nyumbani kwao alikuwa tayari ameungua mwili mzima, akakimbizwa Hospitali ya Ndanda, Masasi.Sadick aliongeza kuwa, huko alitibiwa akapona majeraha isipokuwa sehemu ya mguuni kwani mfupa ulikuwa ukionekana ndipo walipokata nyama eneo la paja lake na kuziba ile sehemu.


Mguu wake uliobakia ambao nao unatakiwa kukatwa

“Nilipata nafuu nikaendelea kusoma mpaka kidato cha tatu ambapo tulihamia Mafia na ndugu zangu, nilikuwa naumwa mara kwa mara lakini nilifanikiwa kumaliza kidato cha nne kwa tabu ndipo nikaanza kupata vipele ambavyo vilivimba na kuwa vidonda na kunisababishia maumivu makali,” alisema.

Aliongeza kuwa alipozidiwa alipimwa na kuonekana ana kansa hivyo alilazimika kukatwa mguu kwa mara ya kwanza, ilipofika mwezi wa saba alianza tena kuumwa kwa kasi ya ajabu akakatwa kwa mara ya pili sehemu ya mguu iliyobaki.

Baada ya kuendelea kuumwa madaktari wakampa rufaa ya kwenda Hospitali ya Muhimbili ambao nao walimpeleka Hospitali ya Ocean Road anakoendelea kutibiwa.“Baada ya kufika Hospitali ya Ocean Road nilianza tiba ya kuchomwa mionzi lakini bado siwezi kulala wala kukaa naumwa mpaka naona dunia chungu,” alisema kijana huyo.

Kijana huyo amewaomba Watanzania wenye moyo wa huruma wamsaidie gharama za matibabu kwani zinahitajika shilingi 1, 470,000. “Fedha hizo ni kwa ajili ya matibabu katika Hospitali ya For Life iliyopo jijini Dar es Salaam ambao wamesema wanaweza kunitibu na kupona tatizo langu,” alisema Sadick.

Yeyote aliyeguswa na tatizo la kijana huyu awasaliane naye kwa simu namba, 0654 003 611 au 0785745261.

MWANAFUNZI OMARY MAYUNGA ATESWA NA MACHO MIAKA 10

Stori: Joseph Ngilisho, Arusha

MTOTO Omar Mayunga (10) (pichani) ambaye ni mwanafunzi wa darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Sombetini jijini hapa, ameshindwa kuendelea na masomo kutokana na ugonjwa wa kuvimba macho na anahitaji msaada wa kufanyiwa upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya Kilimanjaro, Christian Medical Centre ‘KCMC’.


Mtoto Omar Mayunga akiwa na mama yake.

Mayunga anayeishi Sombetini na mama yake, alizaliwa na ulemavu wa mdomo na macho bila kujulikana chanzo ambapo katikati ya mwaka huu alijitokeza mfadhili aliyemsaidia kufanyiwa upasuaji wa mdomo uliokuwa umechanika pande mbili kwa kujazwa nyama kisha kushonwa.

Akizungumzia ulemevu huo, mama mzazi wa mtoto huyo, Jafara Hussein ambaye ndiye anayezunguka naye mitaani kuomba msaada, alisema mwanaye alizaliwa akiwa na ulemavu huo na kwamba hadi kufikia umri huo ameshindwa kumtibu kutokana na kukosa fedha na muda wote macho huonekana kuvimba na kutiririka machozi.

Aliongeza kuwa, adha hiyo imesababisha kukimbiwa na mumewe, Mayunga Kondo ambaye ni baba mzazi wa mtoto huyo hali iliyomlazimu yeye kuacha shughuli zake za kuuza mbogamboga na kushinda akizunguka mtaani kuomba fedha kwa wasamaria wema waweze kumsaidia kupatikana kwa shilingi milioni 4 za matibabu ya upasuaji wa kuondoa uvimbeuliopo kwenye macho ya kijana wake.

“Hadi sasa sifahamu baba yake huyu mtoto alipo ila nasikia yupo Shinyanga. Alinikimbia na kunitelekeza mimi na wanangu wanne,’’ alisema mama huyo.

Alisema hadi sasa hajafanikiwa kupata kiasi hicho cha fedha kwani baadhi ya wasamaria wema wanaojitokeza wamekuwa wakitoa kiasi kidogo ambacho hujikuta akikitumia kwa ajili ya kuendesha familia yake kutokana na yeye kusimamisha biashara zake.

“Nalazimika kutembea na mgonjwa wangu kama unavyoniona ili jamii ishawishike kumchangia, muda mwingi nautumia kuomba kwenye mabaa na madukani kwa watu,” alisema mama Mayunga.
Mwanamke huyo aliomba kupitia habari hii, yeyote atakayeguswa na tatizo la mtoto wake anaweza kumchangia pesa kutumia namba 0766 350 664 ambayo ni yake.

TAASISI YA STARKEY HEARING FOUNDATION YA MAREKANI YAENDESHA KLINIKI YA MASIKIO MKOANI ARUSHA



DAKTARI,Assay Shibanda (kushoto) na John Yuccas wakimwekea mwanafunzi wa Shule ya Msingi Elbol,Levina Innocent mashine ya kuongeza kiwango cha usikivu kwenye Kliniki inayoendeshwa kwa pamoja kati ya Montage Limited na taasisi kutoka Marekani ya Starkey Hearing Foundation ya kuwawekea vifaa vya kuongeza usikivu inayofanyika kwenye viwanja vya Hoteli ya Kibo Palace jijini Arusha jana
Mtaalamu wa matatizo ya usikivu kutoka Taasisi ya Starkey Hearing Foundation ya nchini Marekani, Derek Johson akimfanyia uchunguzi wa awali wa masikio mmoja wa watu wenye usikivu hafifu waliokuja kuhudhuria Kliniki inayofanyika kwenye viwanja vya Hoteli ya Kibo Palace jijini Arusha jana

Mratibu wa Taasisi ya Starkey Hearing Foundation kutoka Marekani, Derek Johnson akitoa maelezo ya awali kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mount Meru na chuo cha Biashara cha Arusha, (IAA) waliokuja kujitolea kutoa huduma mbalimbali ya matibabu na uwekaji vifaa vya kuongeza kiwango cha usikivu masikioni kwenye Kliniki inayofanyika kwenye viwanja vya Hoteli ya Kibo Palace jana. Kushoto ni Msimamizi Mkuu wa zoezi hilo, Teddy Mapunda.

MMOJA wa wataalamu wa kuchunguza matatizo ya masikio,Stuart Specer kutoka Taasisi ya Starkey Hearing Foundation ya nchini Marekani inayoendesha kliniki ya masikio akitaniana na mkazi wa Arusha,Ally Abdulrahman aliyewahi kuishi nchini humo ambaye kwa sasa ana matatizo ya kusikia kwenye kliniki inayofanyika kwenye viwanja vya Hoteli ya Kibo PalaceJijini Arusha jana