Karibu Fadhaget Sanitarium Clinic

Tunapenda kukukaribisha katika Kitengo cha Sayansi ya Tiba Asilia.

Kitengo Cha Sayansi Ya Tiba Asilia

Kwa Muda mrefu tumekuwa tukisaidia wengi katika matibabu na kutengeneza dawa bora kabisa kiafya.

Je Unapenda Kufahamu Jinsi Ya Kupata Mapacha?

Tunafundisha jinsi ya kupata jinsia unayotaka, jinsi ya kupata mtoto kama umekosa mtoto kwa muda mrefu. Pia hata jinsi ya kupata watoto mapacha tunaweza kukusaidia.

Tunapatikana Katika Mikoa Zaidi ya 10 Tanzania

Tunazidi kuongeza matawi yetu nchini Tanzania na Nje ya Nchi. Kwa sasa tunapatikana katika mikoa zaidi ya 10 na tunazidi kuongeza matawi yetu. Karibu sana.

Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Sunday, June 29, 2014

KWANINI MWANAMKE ASHIKI MIMBA?

MWANAMKE kutoshika mimba kumegawanyika katika makundi makubwa mawili. Kwanza ni hali iitwayo ‘primary Infertility’ ambapo mwanamke hana historia ya kupata ujauzito. Pili kuna hali iitwayo ‘Sekondari Infertility’, hapa mwanamke anayo historia kama alishawahi kupata ujauzito haijalishi kama alizaa au alitoa au iliharibika.

Matatizo ya kutoshika mimba kwa mwanamke kitaalamu tunaita ‘infertility’ au ugumba.
Kutoshika mimba kwa mwanamke husababishwa na mambo mengi ingawa tutakuja kuona vyanzo vikuu.
Maambukizi katika viungo vya uzazi, hali duni ya lishe na magonjwa sugu pia huathiri hali hii ya ugumba kwa mwanamke.

Chanzo cha matatizo ya ugumba kwa mwanamke
Vyanzo vya matatizo haya vinahusisha aina zote mbili za ugumba za ‘Primary’ na sekondari’. Kwanza kabisa ni chanzo kinachohusu upevushaji wa mayai ‘Ovulatory’. Tatizo hili huathiri wanawake kwa kiasi kikubwa ambapo mwanamke anapata siku zake kama kawaida lakini hapevushi mayai.
Hii husababishwa na matatizo katika mfumo wa homoni mwilini, tatizo linaweza kutokea lenyewe kutokana na mabadiliko ya mwilini au matumizi yanayohusiana na dawa za homoni kutumika kiholela au matumizi ya baadhi ya vyakula au vipodozi, tutakuja kuona.


Dr. Fadhili Emily

Dalili za upevushaji wa mayai zipo nyingi, tutakuja kuziona hapo baadaye lakini kubwa ni kwa mwanamke kupata ute wa uzazi ambapo upo wa aina tatu. Pia upevushaji tunaweza kuuona kwa kutumia vifaa maalumu ambavyo unatumia mwenyewe nyumbani kwa kupima mkojo siku unazohisi unaweza kupata mimba.
Tatizo lingine la chanzo cha ugumba ni kwenye mirija, mirija inaweza kuziba, kutanuka au kuweka usaha au maji. Maambukizi katika mirija au upasuaji wa mimba nje ya kizazi au kufunga kizazi.
Utoaji wa mimba, maambukizi ya mara kwa mara ukeni husababisha athari katika kizazi na mirija. Matatizo ya mirija husababisha ugumba kwa kiasi kikubwa ambacho ni kati ya asilimia 15 hadi 40 kwa wanawake ambacho ni kiwango kikubwa kuliko matatizo mengine.

Mwanamke pia anaweza kuwa na kasoro katika tabaka la ndani la kizazi ambapo linatoka kwa nje badala kuwa ndani. Hali hii kitaalam inaitwa ‘Endometriosis’. Siyo tatizo linalojitokeza kwa ukubwa sana lakini linaathiri baadhi ya wanawake.

Mwanamke mwenye tatizo hili hulalamika maumivu chini ya tumbo na huwa makali wakati wa hedhi na kusababisha damu ya hedhi kutoka kidogokidogo, mwanamke hupoteza uwezo wa kushika mimba.
Matatizo ya mwanaume kushindwa kufanya tendo la ndoa, anamaliza lakini manii hazitoki pia husababisha ugumba kwa mwanaume ambao humuathiri mwanamke. Mwanaume pia anaweza kufanya tendo la ndoa vizuri, anatoa manii lakini mbegu hakuna, hili pia ni tatizo kubwa.

Mwanaume anaweza kupata tatizo la uzazi hata kama anayo historia ya kumpa mwanamke mimba au kuwa na watoto kwa hiyo ni vema naye akafanyiwa uchunguzi endapo wanatafuta mtoto au ujauzito kwa mwaka mmoja bila ya mafanikio.

Ugumba pia unaweza kutokea na baada ya uchunguzi wa kina inaonekana mume hana tatizo wala mke hana tatizo, hali hii inaitwa kitaalamu ‘Unexplained Inferlity. Kwa hiyo, ni vema uchunguzi wa kina ufanyike. Tatizo hili tutakuja kuliona katika makala zijazo.

Uchunguzi
Matatizo ya ugumba ni makubwa na huumiza vichwa vya watu wanaotafuta ujauzito. Tumeona sababu kuu za ugumba lakini mambo mengine yanayohusiana na lishe na magonjwa sugu yanayoathiri uzazi. Tutakuja kuzungumzia.

Uchunguzi hufanyika kwa madaktari wa magonjwa ya kinamama na matatizo ya uzazi katika hospitali za mikoa na wilaya. Vipimo mbalimbali hufanyika kama damu kuangalia viwango vya homoni, ultrasound na mirija uzazi.

THE FADHAGET SANITARIUM CLINIC INAKULETEA UKWELI KUHUSU UGONJWA WA SIKO SELI (SICKLE CELL)

Siko seli ni nini?
Siko seli ni ugonjwa wa kurithi unaosababisha mabadiliko yasiyo ya kawaida katika chembechembe nyekundu za damu.
• Kwa kawaida chembe nyekundu za damu zina umbo la mviringo ambalo huzirahisishia kupita kwenye mishipa midogo ya damuili kusafirisha hewa safi ya oxygen katika sehemu mbali mbali za mwili.

• Kwa mtu mwenye ugonjwa wa siko seli chembe hizi huwa tofauti, zinanata na zina umbo la mwezi mchanga (siko).

• Tanzania ni moja wapo kati ya nchi zenye wagonjwa wengi wa siko seli duniani ambapo inakadiriwa kuwa kati ya watoto 8,000 -10,000 huzaliwa na ugonjwa wa siko seli kila mwaka pia inakadiriwa kuwa 13% ya watu wote nchini wana vinasaba vya ugonjwa wa siko seli. (sickle cell traits).

Nini husababisha ugonjwa huu?
• siko seli ni ugonjwa wa kurithi, ugonjwa huu hurithiwa katika njia sawa sawa ambavyo mtu hurithi rangi yake ya mwili, au macho, urefu nk, hivyo basi mtu huzaliwa na ugonjwa huu.

• Vinasaba vya sikoseli hurithiwa sawa sawa kutoka kwa wazazi wote wawili yani baba na mama.

• Mtu hawezi kupata ugonjwa wa siko seli kwa kuambukizwa kwa njia yeyote ile.

HUWEZI KUPATA SIKO SELI KWA KULA, KUCHEZA AU KULALA NA MTU MWENYE SIKO SELI.
Dr. Fadhili Emily

Matibabu
Lengo la matibabu ni kupunguza madhara ama dalili zitokanazo na ugonjwa huu kama vile kutibu na kuzuia maumivu , kuzuiamaambukizi ya vimelea vya ugonjwa ,upungufu wa damu ,kiharusi nk.
• Hakuna tiba moja mahususi kwa wagonjwa wa siko seli hivyo matibabu hutofautiana kutokana na dalili za mgonjwa mfano; kuongezwa damu au maji mwilini na dawa za maumivu.

Je kuna tiba ya siko seli?
Hadi leo tiba pekee ya ugonjwa huu ni kupandikizwa kiini kwenye shina la mfupa kitaalam BONE MARROW TRANSPLANT.

• Tiba hii hufanywa kwa kuchukua urojo wa mifupa kutoka kwa mtu asiye na siko seli (donor) na kupandikiza kwenye mifupa ya mgonjwa hivyo husaidia mifupa yake kuzalisha chembe za damu zilizo nzima.

• Kwa upande mwengine tiba hii,pamoja na kutokupatikana katika nchi nyingi ikiwemo Tanzania, ni hatarishi na husababisha madhara makubwa kwa wagonjwa na mara nyingine hata kifo.

Dalili
Dalili za kuwa na maradhi haya ni homa, maumivu ya kifua, kupumua harakaharaka, uchovu, kuvimba kwa tumbo au sehemu za chini yake, kupoteza nguvu na macho kukosa nuru ya kuona vizuri.

Tiba na ushauri
Ukiona dalili kama hizi zinakutokea mara kwa mara muone daktari mara moja ambaye atakupima damu yako kubainisha iwapo una huo ugonjwa na atakupa matibabu.
Daktari wako atakupa ushauri, atakupatia dawa pia atakupa ushauri wa vyakula ambavo utakuwa ukitumia hasa mboga za majani kwa wingi,samaki,dagaa maziwa na matunda ambayo yatakusaidia kwa kiasi ili tatizo hilo lisikudhuru kwa kiasi kikubwa.
Wapo watu wanaishi muda mrefu bila kusumbuliwa na tatizo la kupungukiwa na damu kwa sababu wanazingatia masharti.
Ugonjwa wa upungufu wa damu mwilini ni hatari sana hivyo inapaswa wanaosumbuliwa na maradhi hayo kuzingatia masharti ikiwa ni pamoja na kula vyakula vinavyoongeza damu hasa mboga za majani.
Aidha, watumie dawa za kuongeza damu watakazoshauriwa na madaktari wao.

Friday, June 27, 2014

THE FADHAGET SANITARIUM CLINIC INAKUPA ELIMU YA KUTOKWA NA MAJIMAJI KWENYE MATITI (GALACTORRHEA)

Tatizo hili husimama lenyewe kama ugonjwa ingawa pia inaweza kuwa ni dalili kama mwanamke ni mjamzito, ananyonyesha au ametoa mimba au ameharibikiwa na mimba.Kusimama kwake kama ugonjwa ni pale yanapotoka wakati mwanamke hana historia ya dalili hizo hapo juu.

Tatizo hili huwapata wanawake wengi na kwa mujibu wa takwimu huathiri asilimia tano hadi 32 ya wanawake walio katika umri wa kuzaa.Pamoja na kuwapata zaidi wanawake, hali ya kutokwa na majimaji katika matiti pia huweza kuwatokea wanaume watu wazima, vijana walio katika umri wa balehe, wa kike na wa kiume, watoto wachanga wa kike na wa kiume.

Chanzo cha tatizo
Matiti yanaweza kutoa majimaji endapo chuchu zitachezewa au kunyonywa mara kwa mara na kusababisha kuvuruga baadhi ya homoni mwilini.

Homoni zinazohusika zaidi na tatizo hili ni homoni ya ‘prolactine’.
Vilevile katika hali hii ya kutokwa na majimaji asilimia 50 ya matatizo chanzo chake bado hakijulikani.
Mama anayenyonyesha homoni zinazochangizwa na kusababisha matiti yatoe maziwa ni ‘Prolactin’, Estrogen’ na Progesterone.

Dawa nyingine zinazoweza kumfanya mtu atokwe na majimaji katika matiti ni dawa kama Methyldopa, madawa ya kulevya na dawa za magonjwa ya akili.

Pamoja na matatizo katika mfumo wa homoni, hali ya kusuguasugua kifua mara kwa mara, hali ya kuwa na hofu na wasiwasi au shauku f’lani, mfano ya kuhitaji kupata ujauzito husababisha kuamsha homoni za uzalishaji wa maziwa au hayo majimaji.

Vyanzo vingine ni matatizo kichwani kwenye tezi ya ‘pituitary au pituitary adenoma’.
Dawa nyingine zinazoamsha tatizo hili ni kama vile ‘Cimetidine’ ambazo hutibu vidonda vya tumbo.
Pia zipo dawa nyingine za asili ambazo hazijafanyiwa utafiti wa kutosha zinazoweza kusababisha tatizo hili.

Dalili za tatizo
Mwanamke mwenye tatizo hili la kutokwa na maziwa kwenye matiti wakati si mjamzito na wala hana historia ya kuwa na mimba, huwa hapati ujauzito.
Mwanaume mwenye tatizo hili hupungukiwa na nguvu za kiume, uzalishaji wa mbegu za kiume huwa mdogo.

Kwa ujumla tatizo hili husababisha ugumba.
Kwa vijana na watoto wa kiume au wa kike ni vema uchunguzi wa kina ufanyike.
Maziwa yanaweza kutoka tu yenyewe au kwa kuminyaminya matiti au chuchu.

Uchunguzi
Hufanyika hospitalini kwa madaktari wa masuala ya uzazi. Vipimo vya damu kuangalia homoni, matatizo katika matiti, na ikibidi CT-Scan vitafanyika kuangalia matatizo katika tezi ya Pituitary.

Ushauri
Wahi hospitali kwani athari ya tatizo hili ni kupoteza uwezo wa kuzaa.
Epuka kuchezea chuchu ziwe zako mwenyewe au za mpenzi wako au za mtoto kwani unaamsha homoni ambazo katika wakati huo hazitakiwi.

Wednesday, June 18, 2014

THE FADHAGET SANITARIUM CLINIC INAPENDA KUKUFAHAMISHA AINA ZA KIHARUSI (STROKE) SEHEMU YA PILI




WIKI iliyopita tulielezea ugonjwa wa kiharusi na aina zake na tukafafanua kwa nini unawapata watu. Endelea kuelimika.

Iwapo mgonjwa ataathirika sehemu ya ubongo kwenye shingo kuelekea kwenye uti wa mgongo (brainstem), mgonjwa anaweza kuwa na dalili za kuhisi mabadiliko ya harufu, ladha, kusikia na kuona, kulegea kwa misuli ya macho (ptosis), kupungua kwa ufahamu na kulegea kwa misuli ya uso, ulegevu wa ulimi (kushindwa kutoa nje au kusogeza upande upande).

Pia atakuwa na upungufu wa uwezo wa kumeza, ulegevu wa misuli ya shingo na kushindwa kugeuza shingo upande mmoja, kushindwa kusimama sawasawa na kuona vitu kwa hali ya utofauti, mabadiliko ya upumuaji na kiwango cha moyo kudunda.

Iwapo sehemu mojawapo ya mfumo mkuu wa neva kitaalamu huitwa central nervous system imeathirika, mgonjwa atakuwa na dalili za kupoteza ufahamu kwa upande mmoja wa mwili na kulegea kwa misuli ya uso, kuhisi ganzi mwilini na kupungua kwa ufahamu wa hisia na kutetemeka mwili.
Mgonjwa anaweza kukumbwa na matatizo ya kupoteza fahamu, maumivu makali ya kichwa na kutapika hasa kwa wale wenye kiharusi cha kuvuja damu (hemorrhagic stroke) ambacho husababisha ongezeko la shinikizo na mgandamizo wa ubongo ndani ya fuvu kutokana na kuvuja kwa damu.

TIBA
Mgonjwa kabla ya kutibiwa ni lazima afanyiwe vipimo kama vile cha ECG, ECHOCARDIOGRAM ambacho huwezesha kutambua hitilafu katika mapigo ya moyo ( na kama kuna damu iliyoganda kwenye moyo ambayo inaweza kufika kwenye ubongo.
Holter monitor husaidia kutambua hitilafu katika mapigo ya moyo (arrhythmia) zinazotokea kwa vipindi na Angiogram huwezesha kugundua matatizo kwenye mishipa ya damu, na ni mishipa ipi ya damu iliyoziba.

Vipimo vya damu huwezesha kutambua uwepo wa lijamu mwilini (hypercholesterolemia) na mabadiliko mengine katika damu.

Mgonjwa hutibiwa kwa kutumia dawa za kuyeyusha damu iliyoganda (thrombolytics) au kwa kuondoa damu iliyoganda kwa njia mbalimbali (thrombectomy). Dawa nyingine kama vile junior Aspirin na Clopidogrel hutolewa kwa ajili ya kuzuia chembe sahani kukusanyika na kuganda.

Matibabu ya kiharusi kinachotokana na damu kuvujia kwenye ubongo (Hemorrhagic stroke) huhitaji tathmini ya upasuaji wa neva ili kuchunguza na kutibu sababu ya damu kuvuja. Haishauriwi kabisa kumpa mgonjwa wa aina hii ya kiharusi dawa za kuyeyusha damu iliyoganda au za kuzuia kuganda maana huhatarisha maisha ya mgonjwa badala ya kumsaidia. Kwahiyo ni vizuri kwa wataalamu kufanya uchunguzi wa kutosha ili kuwa na uhakika na tatizo.

Mgonjwa wa kiharusi inafaa kumuelimisha ili arudishe ujuzi wake wa maisha ya kila siku. Inashauriwa wataalamu wa viungo wanahitajika ili kumpa mazoezi mgonjwa.
Hatari ya ugonjwa huu ni kwamba asilimia 75 ya wanaonusurika kifo huwa walemavu wa akili au kimwili na kusababisha kuathirika kwa ufanyaji kazi wao .

Ulemavu wa kimwili ni pamoja na ulegevu wa misuli, kujihisi ganzi sehemu mbalimbali za mwili hususan zilizoathirika, kutoona vizuri, vichomi na kadhalika.

USHAURI
Wagonjwa wanashauriwa kutibu au kuzuia tatizo la shinikizo la damu, kisukari na wanapewa ushauri wa kufanya mazoezi kila siku, kuacha kuvuta au kunywa pombe kupita kiasi, kula chakula kisichokuwa na mafuta mengi na kisicho na chumvi nyingi.

Tumia dawa za kupunguza mafuta mwilini (statins) kwa mfano Simvastatin.
Watu waepuke unene kupita kiasi (obesity) na wajichunge wasipate cholesterol nyingi kwenye damu ambayo huchangia kuziba kwa mishipa ya damu mwilini.

Friday, June 13, 2014

THE FADHAGET INAPENDA KUKUPA DALILI ZA SARATANI YA KIZAZI SIKU YA LEO


Saratani ya kansa huwa na dalili zake za awali ambazo tutakuja kuziona. Tunapozungumzia saratani ya kizazi tunalenga zaidi saratani ya shingo ya uzazi ‘Carcionoma of Cerix’ na saratani ya mfumo wa uzazi au ‘Endometrial Carcinoma.

Saratani ya mfuko wa kizazi hushambulia zaidi tabaka la ndani la kizazi ‘Endometrium’ na kusababisha maumivu ya tumbo kwa muda mrefu na hata tumbo kuvimba.

Saratani hii siyo kubwa sana hivyo hatutaelezea kwa undani ila endapo utakuwa na maumivu chini ya tumbo na yanasambaa kulia na kushoto na upande wa juu, tumbo likiwa linaongezeka ukubwa na siku za hedhi zinavurugika, basi muone daktari wa kinamama kwa uchunguzi wa kina.

Saratani ya shingo ya uzazi huwapata wanawake walio katika umri wa kuzaa wenye wapenzi zaidi ya mmoja au ambao mara leo kaolewa na huyu,…


Saratani ya kansa huwa na dalili zake za awali ambazo tutakuja kuziona. Tunapozungumzia saratani ya kizazi tunalenga zaidi saratani ya shingo ya uzazi ‘Carcionoma of Cerix’ na saratani ya mfumo wa uzazi au ‘Endometrial Carcinoma.

Saratani ya mfuko wa kizazi hushambulia zaidi tabaka la ndani la kizazi ‘Endometrium’ na kusababisha maumivu ya tumbo kwa muda mrefu na hata tumbo kuvimba.

Saratani hii siyo kubwa sana hivyo hatutaelezea kwa undani ila endapo utakuwa na maumivu chini ya tumbo na yanasambaa kulia na kushoto na upande wa juu, tumbo likiwa linaongezeka ukubwa na siku za hedhi zinavurugika, basi muone daktari wa kinamama kwa uchunguzi wa kina.

Saratani ya shingo ya uzazi huwapata wanawake walio katika umri wa kuzaa wenye wapenzi zaidi ya mmoja au ambao mara leo kaolewa na huyu, anaachana naye anaishi na mwingine, yaani mara kwa mara hana msimamo, anabadilibadili wanaume, wanawake wanaofanya ngono na wanaume wasiofanyiwa tohara pia hupatwa na tatizo hili la saratani ya shingo ya uzazi.

Saratani ya shingo ya uzazi pamoja na kuchangiwa na mambo yote hayo hapo juu, husababishwa hasa na kirusi kiitwacho ‘Human Papilloma virus’ au kwa kifupi ‘HPV’. Kirusi hiki huenezwa kwa njia ya ngono, mwanaume huwa hakimuathiri bali yeye hukibeba na kukisambaza kwa wanawake kwa hiyo mwanamke anayechanganya wanaume hajui wapi atakipata.

Ukubwa wa tatizo
Saratani ya shingo ya kizazi ina tabia ya kusambaa endapo haitagundulika na tiba haitafanyika mapema. Saratani husambaa katika kizazi, nyonga hadi katika mapafu. Ikishambulia nyonga, mwanamke hulalamika maumivu chini ya tumbo.

Saratani hii ina tabia ya kusambaa kwa kasi na endapo hatua za haraka hazitachukuliwa husababisha kifo kwa mwanamke. Saratani huwa haiambukizi.

Dalili za awali za saratani ya shingo ya uzazi
Mwanamke mwenye tatizo hili hulalamika maumivu ya tumbo chini ya kitovu, kutokwa na majimaji yenye harufu ukeni na muwasho mara kwa mara. Tatizo hili hutibiwa na kujirudia tena mara kwa mara.

Mwanamke hulalamika kwamba ametibiwa sana kwa dawa za kumeza na kuingia ukeni lakini hapati nafuu. Hupoteza hamu ya tendo la ndoa, maumivu wakati wa tendo la ndoa na mwishowe hutokwa na damu ukeni baada ya tendo la ndoa.

Saratani inaposambaa na kushambulia shingo ya uzazi huathiri ukeni na kuumiza njia ya mkojo na kibofu.
Uke huvimba na kuonekana kuziba na mlango wa kizazi au ngozi ya ndani ya ukeni ikiguswa tu kidogo basi hutokwa na damu kwani huwa laini sana. Hii ni hatua mbaya na ya mwisho katika saratani inaposambaa.

Uchunguzi
Uchunguzi wa saratani ya shingo ya uzazi hufanyika katika vituo mbalimbali katika kampeni maalum dhidi ya saratani ya shingo ya uzazi.

Uchunguzi pia hufanyika katika hospitali za mikoa na wilaya katika kliniki za magonjwa ya kinamama ambapo vipimo mbalimbali hufanyika mojawapo ikiwa ni kuangalia mlango na shingo ya uzazi.

Kipimo cha Ultrasound pia kitafanyika kuangalia athari katika kizazi. Majimaji ya ukeni yatapimwa kuangalia maambukizi na uchunguzi wa awali wa saratani utafanyika.
Endapo mlango wa uzazi utakuwa umeathirika sana, basi kinyama kitatolewa na kupimwa katika maabara kubwa kuthibitisha tatizo.

Ushauri
Ni vema mwanamke yeyote anayejihisi maumivu chini ya tumbo na kutokwa na uchafu ukeni na muwasho uwepo au usiwepo awahi hospitali kwa uchunguzi. Waone madaktari wa kinamama kwa uchunguzi sahihi katika hospitali za mikoa.

Tuesday, June 10, 2014

FAHAMU AINA ZA KIHARUSI (STROKE)



Kiharusi au kwa Kiingereza Stroke ni kitendo cha baadhi ya viungo vya mwili kuwa na ganzi au kutojiweza kufanya kazi zake za kawaida.Kuna aina mbili za kiharusi, lakini kabla ya kuchambua hayo tuangalie, ni nini kinasababisha mtu kukumbwa na ugonjwa huu?


Mtu anaweza kupata dalili za ugonjwa huu wa kiharusi na baada ya dakika chake zikaisha.
Kiharusi kinampata binadamu baada ya eneo la ubongo kukosa damu kwa saa 24 ama zaidi au kunapotokea kizuizi cha damu au mishipa ya damu kushindwa kusafirisha damu au mshipa huo unapopasuka.

Kiharusi kimegawanyika katika aina kuu mbili kulingana na jinsi kinavyotokea, kwanza ni:

1. Kiharusi cha kukosa hewa kwenye ubongo kitaalamu huitwa Ischemic stroke. (Ischemic ni neno la Kigiriki lenye maana ya kuzuia damu).
Aina hii ya kiharusi hutokea iwapo usambazaji wa damu katika sehemu ya ubongo hupungua na kusababisha tishu za ubongo za eneo lililoathirika kushindwa kufanya kazi zake vizuri.

Hiki hutokea baada ya mshipa wa ateri kuziba kutokana na kuganda kwa damu, hali ambayo inasababisha damu isisafiri vyema na kuelekea kwenye ubongo.

Hali hiyo pia hufanya damu iliyoganda kuziba mishipa midogo ndani ya ubongo kitaalamu huitwa Cerebral thrombosis au kipande cha damu kumeguka na kwenda kuziba mshipa wa damu kwenye ubongo kitaalamu huitwa Cerebral embolism.

Lakini tatizo hili linaweza kutokea pale damu inapoganda sehemu nyingine ya mwili na kusafiri hadi kwenye mishipa ya ateri, hivyo kusababisha damu kwenda kwenye ubongo kukwama.
Hata hivyo, tatizo hili linaweza kusababisha kitu kinachoitwa Lacunar stroke, yaani vimirija vidogovidogo sana vya damu vilivyopo ndani ya ubongo, vinaziba.

Hapo sasa binadamu huwa anakumbwa na kiharusi kinachojulikana kitaalamu Lacunar stroke japokuwa mara nyingi hii haiwaletei sana shida wagonjwa.

KIHARUSI CHA HAEMORRHAGE
Baada ya kufafanua kiharusi kinachoitwa ischaemia ambacho ndani yake tukaelezea pia kile kinachoitwa Lacunar stroke, sasa tuelezee aina ya kiharusi kiitwacho Haemorrhage.
Aina hii ya kiharusi, mrija wa damu karibu ama kwenye ubongo hupata mpasuko, hivyo kusababisha damu kuvuja na kitendo hicho ndicho kitaalamu huitwa Haemorrhage.

Kinachotokea ni kwamba damu inayovuja hukandamiza ubongo na kuuharibu, ubongo ni moja ya kiungo laini sana mwilini.

Katika hali ya kitaalamu inayoitwa Intra cerebral haemorrhage, uvujaji wa damu hufanyika ndani ya ubongo wenyewe. Mara nyingi aina hii ya kiharusi hutanguliwa na dalili za kichwa kuuma, au kuwepo kwa historia ya ajali ya kichwa.

Lakini kuna hali pia inayoitwa Subarachnoid haemorrhage ambapo mpasuko wa mshipa wa damu hufanyika karibu na eneo linalozunguka ubongo linaloitwa Subarachnoid.

Wakati fulani, mishipa ya damu huzungukwa na aina fulani za mafuta yasiyofaa mwilini, hali inayoitwa kitaalamu kama Atherosclerotic plaque. Hali hii husababisha kuganda kwa damu katika mishipa (thrombosis) hiyo.

WANAWAKE WANAVYO-SHAMBULIWA NA U.T.I


U.T.I kirefu chake ni Urinary Tract Infection ni maambukizi ya bakteria mbalimbali wanaoshambulia mfumo wa mkojo, yaani kwenye figo (kidney), kibofu cha mkojo na mifereji inayotoa mkojo (urethra)

Mifereji inayotoa mkojo kwenye figo (ureter) na mfereji unaotoa mkojo nje, mara nyingi bakteria hushambulia sehemu za chini za mfumo wa mkojo yaani urinary bladder na kitaalamu kuitwa bladder infection.

Bakteria hao baada ya kumuingia binadamu hupona mara moja pindi mgonjwa anapoanza dozi lakini kama wadudu hawa hawatatibiwa vizuri wanaweza kupanda na kushambulia figo na mshipa unaounga sehemu hiyo uitwao renal pelvis na kuleta madhara makubwa, hivyo kusababisha ugonjwa wa figo.

Kuna wadudu wanaotoka kwenye utumbo mkubwa wa binadamu ambao kila binadamu anaishi nao, hawa husaidia kulinda mwili na kitaalamu hujulikana kama normal flora na huwa ni askari wa mwili.

Vijidudu hivyo hushuka hadi kwenye mlango wa haja kubwa na kuenea mpaka sehemu za siri. Kama wataingia kwenye mfumo wa mkojo hushambulia sehemu hizo kwani wadudu hao wanakuwa hawajazoea mazingira ya sehemu za mkojo.

WANAWAKE WANAVYOSHAMBULIWA NA UTI
Mara nyingi wanawake ndiyo wanaoshambuliwa kirahisi na bakteria wa UTI kutokana na maumbile yao ya sehemu za siri.

Sababu kubwa ya kushambuliwa kirahisi ni kwa kuwa wanakuwa na mfereji mfupi wa kutoa nje mkojo (shot urethra).

Sababu nyingine inayosababisha UTI ni kutokumywa maji kwa wingi, hivyo kushindwa kwenda haja ndogo mara kwa mara.

Kama mtu ana ugonjwa wa mawe kwenye figo (kidney stone) pia kwa wanaume wenye ugonjwa wa kuvimba tezi la manii (enlarged prostate), wana uwezekano wa kukumbwa na maradhi haya.

Itaendelea wiki ijayo.

Monday, June 2, 2014

THE FADHAGET SANITARIUM CLINIC INAPENDA KUKUPA BAADHI YA SABABU ZA MWANAMKE KUSHINDWA KUPATA UJAUZITO


Moja ya matatizo yaliyoko katika jamii zetu na yamesababisha wanandoa wengi au wanawake wengi kukosa furaha, ni kukosa uwezo wa kupata ujauzito kwa mwanamke.

Sote tunafahamu kuwa, swala la mwanamke kupata ujauzito linahusisha pande zote mbili, yaani upande wa mwanamke na pia upande wa mwanamme, wote wawili wanapokuwa katika afya nzuri ndipo ujauzito unaweza kupatikana kwa mwanamke.

Miongoni mwa sababu zinazoweza kumfanya mwanamke ashindwe kupata ujauzito ni kama zifuatazo:


Matatizo katika homoni, hii ni kutokana na kwamba, mzunguko (Menstrual cycle) katika mwili wa mwanamke hutawaliwa na hizi kemikali asilia ndani ya mwili ambapo mabadiliko madogo yakitokea katika uzalishaji wa hizi homoni au homoni kuzalishwa katika wakati ambao siyo muafaka huweza kupelekea mwanamke akashindwa kupata ujauzito, pia tatizo la kuwa na uzito wa mwili mdogo sana au mkubwa sana pia huathiri hali nzima ya homoni na kupelekea kushindwa kupata ujauzito.

Umri, kwa wanawake uwezo wa kupata ujauzito unapungua kwa kadri umri unavyoongezeka, hii inatokana na kupungua kwa uzalishaji wa homoni husika wakati umri unavyoongezeka. Kuanzia miaka 35 na kuendelea huwa kunakuwa na tatizo la kushindwa kupata ujauzito kwa wanawake wengi.

Kuziba kwa mirija (fallopian tubes), hii husababisha mbegu za kiume (sperms) zishindwe kulifikia yai na kulirutubisha ili ujauzito utokee. Kuziba kwa mirija huweza kusababishwa na magonjwa yanayoambukizwa kwa njia ya kujamiiana, matatizo katika kizazi au upasuaji. Mara nyingi wanawake ambao mirija yao imeziba, hawahisi dalili zozote.
http://www.visualphotos.com/photo/2x4755886/pregnant_african_american_woman_eating_cake_BLD046307.jpg
Ute ute katika kizazi (mucus problems), ute unaopatikana katika kizazi cha mwanamke huwa na sifa ya kuruhusu mbegu za kiume ziweze kusafiri kwa urahisi na kulifikia yai ili kulirutubisha. Kwa baadhi ya wanawake ute huu unakuwa na uzito na kemikali ambazo ni vigumu kwa mbegu za kiume kuweza kupita, na wakati mwingine mwili wa mwanamke huzalisha sumu ambazo huziua mbegu za kiume, haya yote husababisha kukutana kwa yai na mbegu za kiume kusitokee na hivyo ujauzito kutopatikana.

Uvimbe katika kizazi (fibroids), hii huchangia asilimia tatu (3%) katika mwanamke kutopata ujauzito. Uvimbe huu ambao hutokea katika kuta za mji wa mimba, kwa namna moja au nyingine huweza kuzuia yai lililorutubishwa lisikae sehemu yake na hivyo kuathiri kizazi.

Matibabu ya kansa, kwa kutegemeana na aina ya matibabu, aina ya dawa au njia ya mionzi, hizi huweza kumuathiri mwanamke na kumsababishia kushindwa kupata ujauzito.

Ukomavu katika kizazi, kwa baadhi ya wanawake wanayo matatizo ambayo kizazi chao huwa hakijakomaa vizuri au katika kuzaliwa kwao walizaliwa na tatizo hili ambalo, kizazi hakiko sawa (abnormally developed uterus).

Asilimia kubwa ya matatizo ya mwanamke kushindwa kupata ujauzito yanayo tiba, kama unalo tatizo katika kupata ujauzito usikate tamaa, onana na wataalamu wa afya ili uweze kujua chanzo cha tatizo lako na kupatiwa msaada unaostahili.