Karibu Fadhaget Sanitarium Clinic

Tunapenda kukukaribisha katika Kitengo cha Sayansi ya Tiba Asilia.

Kitengo Cha Sayansi Ya Tiba Asilia

Kwa Muda mrefu tumekuwa tukisaidia wengi katika matibabu na kutengeneza dawa bora kabisa kiafya.

Je Unapenda Kufahamu Jinsi Ya Kupata Mapacha?

Tunafundisha jinsi ya kupata jinsia unayotaka, jinsi ya kupata mtoto kama umekosa mtoto kwa muda mrefu. Pia hata jinsi ya kupata watoto mapacha tunaweza kukusaidia.

Tunapatikana Katika Mikoa Zaidi ya 10 Tanzania

Tunazidi kuongeza matawi yetu nchini Tanzania na Nje ya Nchi. Kwa sasa tunapatikana katika mikoa zaidi ya 10 na tunazidi kuongeza matawi yetu. Karibu sana.

Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Sunday, May 25, 2014

THE FADHAGET SANITARIUM CLINIC INAKUPA SABABU ZA KUTOKA HARUFU MBAYA UKENI NA NAMNA YA KUJIKINGA


The Fadhaget Sanitarium Clinic inasema, wanawake na watu wengi huzani kuwa harufu mbaya itokayo ukeni ni matokeo ya uchavu na kutojisafisha vizuri… Matokeo yake huongeza jitihada katika kujisafisha bila mafanikio ya kuondokana na tatizo hili… Kihalisi, badala kusuluhisha, unapojisafisha zaidi ni unaongeza tatizo badala ya kutatua… Japokuwa ni kweli mara nyingine inaweza ikawa ni sababu ya uchafu… Ila mimi naamini walio wengi huwa wanazingatia usafi… Ndo maana nimeona leo tupeane mawazo juu ya tatizo hili, na kujua namna ya kujikinga

VISABABISHI
i. Bacteria
Tatizo hili husababishwa na Bakteria kwa asilimia kubwa. Kwa asili, ukeni huishi jamii ya bacteria waitwao Lactobacillus ambao jukumu lao kubwa ni kufanya mazingila ya uke kuwa katika hali nzuri. Kutokana na njia mbaya za kusafisha uke, hasa kujisafisha kupindukia, ama kwa kutumia sabuni zenye dawa, husababisha bacteria hawa kufa kwa wingi na mahala pake kuchukuliwa na aina zingine za bacteria ambao huzaana kwa wingi na kusababisha tatizo hili.
Pia kwa wale wanaojamiiana kinyume na maumbile, kuna hatari ya kuhamishia bacteria wanaoishi kwenye njia ya haja kubwa na kuwaamishia ukeni ambapo watazaliana na kukuletea madhala haya.

ii. Kuvu(fungus)
Hii mara nyingi huambatana na uchafu mzito utokao ukeni mfano wa maziwa mgando(mtindi)

iii. Magonjwa ya zinaa(STIs)
Kwa asilimia kubwa husababisha na Chlamyidia na kisonono(gonorrhoea). Yote mawili hutibika kirahisi, ila husababisha madhala makubwa zaidi yasipotibiwa kwa wakati. Tukio baya ni kuwa mwanamke anaweza akawa na magonjwa haya na asione dalili yoyote. Ila mara nyingine mwanamke anaweza kujisikia maumivu anapokojoa, na mara nyingine mkojo unakuwa kama una ukungu, vikiambatana na harufu mbaya.

iv. Maambukizi ya via vya uzazi vilivyo ndani ya nyonga[Pelvic Inflammatory Diseases(PID)]
Hii husababishwa na bacteria waambukizwao kwa njia ya ngono wanapofanikiwa kufika kwenye tumbo la uzazi na hata pia mirija ya mimba na hata kokwa(ovaries), hasa chlamydia. Mara nyingi mwanamke anaweza asijisikie chochote hadi pale atakapojisikia maumivu yasiyokwisha ya tumbo(chini ya kitovu), au itakapoingiliana na utungaji wa mimba. Na kama atajisikia, mara nyingi huwa ni maumivu ya nyonga, harufu mbaya, uchafu mzito ukeni, homa, maumivu wakai wa kukojoa na hata maumivu wakati wa kujamiiana.
Tatizo hili lisipotibiwa mapema laweza kusababisha utasa, ama mimba kutunga nje ya mji wa mimba.

v. Kansa ya uke na kansa ya shingo ya kizazi
Asilimia chache sana ya wanawake inaweza ikawa ni kutokana na kansa ya shingo ya kizazi ama ya uke. Hapa ndipo inapoonyesha kuwa tatizo hili siyo la kufumbia macho, na umuhimu wa kuwahi kwa wataalam wa tiba kwa uchunguzi wa mapema na kabla tatizo halijawa kubwa.

vi. Uchafu
Usipokuwa msafi kwa kiwango kikubwa utakuwa unakaribisha wadudu kuzaliana na kukuletea madhala. Pia unatakiwa kuwa makini wakati wa hedhi, na pia uchaguzi wa pedi, kwani kuna pedi ambazo zina kemikali za kukata harufu zinaweza kukudhulu.

JINSI YA KUJIKINGA
• Usiwe unaosha ukeni kupita kiasi kwani husababisha kuondoa bacteria wa asili wa ukeni(Lactobacilli) na kukaribisha bacteria wenye madhala.
• Pia epuka sabuni zenye dawa(antibacterial soap) usafishapo ukeni, kwani hii pia huua bacteria wa asili wa ukeni.
• Hii haimaanishi usiwe unasafisha ukeni. Usafi ni muhimu, kwani uchafu pia hukaribisha vimelea vya magonjwa.
• Kama tatizo limeshajitokeza, wahi haraka kwa wataalam wa tiba wakufanyie uchunguzi na kujua ni kipi kati ya vilivyotajwa hapo juu kilichosababisha. Daktari atakuchunguza na kujua kama ni bacteria, fungus ama ni dalili za awali za kansa na kuchukua hatua mapema kuepusha madhala zaidi.
• Kumbuka kujisafisha kupindukia si suluhisho kama tatizo limeshajitokea, kwani kunaweza kuzidisha tatizo badala ya kusuluhisha.

Saturday, May 24, 2014

THE FADHAGET INAKUPA JINSI YA KUPATA USINGIZI KWA AFYA YAKO


MAMBO mengi yanayohusu usingizi yamejulikana katika miaka 50 iliyopita. Mambo ambayo yamegunduliwa yamepinga dhana zenye kasoro ambazo zimekuwepo kwa muda mrefu. Dhana moja inasema kwamba wakati ambapo mtu amelala huwa hatendi kwani viungo vingi vya mwili hupumzika.
                              
                                                           Dr Fadhili Emily

Watafiti wa tiba wamechunguza mawimbi ya umeme yanayopita kwenye ubongo na kugundua kwamba kuna hatua mbalimbali za usingizi. Utendaji mwingi huendelea haraka-haraka katika ubongo wa mwanadamu katika vipindi fulani vya usingizi. Ili mtu apate usingizi wa kutosha, hatua hizo hujirudia mara nne au zaidi kila usiku, na kila hatua huchukua muda fulani.

Utata wa Usingizi
Usingizi wa kawaida umegawanywa katika vikundi viwili: kipindi cha kusogeza macho haraka (wakati wa ndoto) na kipindi cha kutosogeza macho haraka (wakati ambapo mtu haoti ndoto). Unaweza kutambua mtu akiwa katika kipindi cha kusogeza macho haraka kwa kuona mboni za macho zikisonga haraka macho yakiwa yamefungwa.
http://www.ynaija.com/wp-content/uploads/2012/10/AfricanAmericanWomanSleeping.jpg
Kipindi cha kutosogeza macho haraka kinaweza kugawanywa katika hatua nne. Baada tu ya kujiwekelea kitandani, unaingia katika hatua ya kwanza pole kwa pole, yaani, unasinzia. Katika hatua hiyo misuli hulegea na mawimbi ya umeme huongezeka ubongoni na hutukia bila mfuatano maalumu. Hatua hiyo inapotukia mara ya kwanza huchukua kati ya sekunde 30 na dakika 7. Katika hatua ya pili, mawimbi ya ubongo huwa makubwa, na hatua hiyo huchukua asilimia 20 ya muda wa kulala. Huenda ukawa na mawazo au picha zisizo kamili akilini, lakini hutambui kinachoendelea wala kuona hata ukifungua macho.

Hatua ya tatu ni ya usingizi mzito na ya nne ni ya usingizi mzito zaidi. Katika hatua hizo ubongo hutokeza mawimbi makubwa yanayosonga polepole. Wakati huo si rahisi kuamka, kwa sababu sehemu kubwa ya damu huelekezwa kwenye misuli. Wakati huo (ambao ni asilimia 50 hivi ya usingizi) ndipo mwili hujirekebisha na watoto wadogo hukua. Ni muhimu kujua kwamba mtu yeyote, iwe ni kijana au mtu mzima asiyepata sehemu hizo za usingizi anaweza kujihisi mchovu, atakosa uchangamfu, na hata kushuka moyo siku inayofuata.

Baada ya kila hatua kuna kipindi cha kusogeza macho haraka. Katika kipindi hicho cha kuota ndoto (kinachoanza baada ya kila dakika 90 hivi), damu zaidi huelekezwa kwenye ubongo na mawimbi ya ubongo hutenda kazi kwa njia ileile kama wakati ambapo mtu hajalala. Hata hivyo, huwezi kusogeza viungo vyako. Huenda hilo humzuia mtu anayeota ndoto asitende kupatana na ndoto zake, hivyo anaepuka kujiumiza au kuwaumiza wengine.

Vipindi vya kusogeza macho haraka, au vipindi vya ndoto, huchukua muda mrefu zaidi kila vinapotukia na yaelekea vinafaidi sana ubongo. Kama kompyuta, ubongo huchanganua habari zilizohifadhiwa, hufuta zile zisizo muhimu na kuhifadhi zile muhimu kwenye kumbukumbu la kudumu. Mtu asipopata vipindi vingi vya ndoto anaweza kupata matatizo ya kihisia. Kwa mfano, watu ambao hukosa usingizi hawapati vipindi vya kutosha vya ndoto na hilo huchangia mfadhaiko.

Hivyo, ni nini hutukia tunapokosa kulala usingizi wa kutosha kwa ukawaida (kimakusudi au tunaposhindwa kulala), yaani, kuwa na deni la usingizi? Tukikosa kulala vya kutosha mfululizo, hatutapata kipindi cha mwisho cha kusogeza macho haraka ambacho ndicho kirefu zaidi na muhimu kwa ubongo. Ikiwa hatulali vya kutosha kwa sababu ya kukatisha-katisha usingizi, hatuwezi kufikia kipindi cha usingizi mzito ambacho husaidia kurekebisha miili yetu. Wale wenye deni kubwa la usingizi hushindwa kukaza fikira kwa muda mrefu, husahau-sahau na kukosa maneno ya kutumia, hupunguza uwezo wao wa kufikiri vizuri na wa kubuni mambo.

Kwa nini mtu huhisi usingizi? Inaonekana mambo kadhaa yanahusika katika taratibu za kawaida za kulala na kuamka. Inaonekana kemikali za ubongo zinahusika. Pia, kuna kiini cha chembe za neva za ubongo ambacho hudhibiti vipindi vya usingizi. Kiini hicho kiko karibu na mahali ambapo neva za kuona hukutana. Mwangaza huathiri usingizi. Mwangaza mwingi hukuamsha, na giza hukusaidia kulala.

Joto la mwili linahusika pia. Ukiwa na joto jingi zaidi, hasa karibu na wakati wa adhuhuri na alasiri, wewe huwa macho zaidi. Kadiri joto la mwili linavyopungua, ndivyo unavyosinzia. Watafiti wanakubali kwamba kila mtu ana utaratibu wake wa kulala na kuamka.

Unahitaji Kulala kwa Muda Gani?
Wanasayansi wanasema kwamba kwa wastani wanadamu wanahitaji kulala kwa saa nane hivi kila usiku. Lakini uchunguzi unaonyesha kwamba watu wana viwango mbalimbali vya usingizi.

Unaweza kutambua ikiwa unalala vya kutosha au una deni la usingizi ukijichunguza kinaganaga. Wataalamu wanasema mambo yafuatayo yanaonyesha kwamba mtu analala vya kutosha:

▪ Mtu anapata usingizi bila kutumia dawa za kulala au analala bila wasiwasi au mahangaiko.

▪ Mtu hatambui anapoamka usiku, lakini anapoamka anapata usingizi haraka.

▪ Mtu huamka saa zilezile kila asubuhi bila ugumu na bila kuamshwa na kengele ya saa.

▪ Mtu anapoamka, hasikii usingizi na anakuwa macho siku nzima.

Madokezo Muhimu
Vipi wale wanaokosa usingizi mara kwa mara? Wataalamu fulani wanatoa madokezo yafuatayo:

1. Usinywe kileo, kahawa au chai kabla tu ya kulala. Watu wengi wanaamini kimakosa kwamba kunywa vileo fulani kunaweza kuwasaidia kulala. Hata hivyo, uchunguzi wa kitiba unaonyesha kwamba vileo vinaweza kukufanya upoteze usingizi.

2. Acha kuvuta sigara. Kitabu kimoja kinasema: “Wavutaji wa sigara hawalali kwa urahisi kwa sababu sigara huongeza shinikizo la damu, mpigo wa moyo, na kusisimua ubongo. Wavutaji wa sigara huamka usiku mara nyingi, labda kwa sababu wakati huo hawavuti sigara.”

3. Epuka kufanya mambo yanayochosha akili na mwili kabla tu ya kulala. Mazoezi ya mwili humsaidia mtu kupata usingizi wa kutosha lakini si yanapofanywa kabla tu ya kulala. Kusuluhisha matatizo makubwa au kufanya kazi inayochosha akili kabla tu ya kulala kunaweza kukufanya ushindwe kutulia ambako hukusaidia upate usingizi.

4. Hakikisha kwamba hakuna kelele na mwangaza katika chumba chako cha kulala, na ikiwezekana kiwe baridi kidogo. Fikiria uchunguzi mmoja maarufu uliohusisha watu wanaoishi karibu na uwanja wa ndege ambao walidai kwamba hawasikii tena kelele za ndege. Walipochunguzwa, ilibainika kwamba bongo zao zilirekodi kelele za kila ndege iliyotua na kuondoka! Wachunguzi walikata kauli kwamba watu hao walipoteza saa moja ya usingizi kwa wastani kila usiku kuliko watu wanaoishi katika maeneo yenye utulivu. Vitu vya kuziba masikio na njia nyingine za kupunguza kelele vingewasaidia sana kupata usingizi mwanana. Wengine wameona kwamba mvumo mwanana kama vile wa feni unawasaidia kupunguza kelele zinazotoka nje.

5. Uwe mwangalifu kuhusu kutumia dawa za usingizi. Uthibitisho mwingi unaonyesha kwamba dawa nyingi za usingizi humfanya mtu awe mzoefu, huacha kufanya kazi baada ya muda, na zina madhara. Ikiwa ni lazima zitumiwe, basi inafaa kuzitumia kwa muda mfupi.

Kwa kuwa mfadhaiko unaweza kumfanya mtu akose usingizi, imeonekana kwamba jambo moja muhimu ni kustarehe na kutulia muda mfupi tu kabla ya kulala. Inafaa kusahau mahangaiko na kufanya jambo lenye kufurahisha, kama vile kusoma. Inafaidi sana kufuata shauri hili la Biblia: “Msihangaike juu ya kitu chochote, bali katika kila jambo kwa sala na dua pamoja na kutoa shukrani maombi yenu na yajulishwe Mungu; na amani ya Mungu . . . itailinda mioyo yenu na nguvu zenu za akili.”—Wafilipi 4:6, 7.

Maoni ya Kawaida Yenye Makosa

1. Kunywa vinywaji vyenye kafeini ndiyo njia bora ya kuwa macho unapoendesha gari kwa muda mrefu.
Uchunguzi unaonyesha kwamba mara nyingi madereva hujidanganya kwamba wako macho. Ikiwa huwezi kuepuka kuendesha gari kwa muda mrefu usiku, afadhali uegeshe gari mahali salama na kulala kidogo (kwa dakika 15 mpaka 30), kisha utembee au kukimbia-kimbia ukinyoosha mikono na miguu.

2. Ikiwa ninashindwa kulala, suluhisho ni kulala kidogo mchana.
Huenda hilo ni kweli, lakini wataalamu wengi wanaamini kwamba inafaa zaidi kulala kwa muda mrefu kila siku. Kulala kidogo mchana (kwa dakika 15 mpaka 30) kunaweza kukusaidia uwe macho alasiri bila kuharibu usingizi wako. Lakini kulala kidogo saa nne kabla ya wakati wa kulala kunaweza kuharibu usingizi wako.

3. Ndoto tunazokumbuka zinatuharibia usingizi.
Ndoto (ambazo sisi huota katika kipindi cha kusogeza macho haraka) huonyesha tulilala vizuri na kwa kawaida zinatokea mara nne au zaidi tunapolala usiku. Uchunguzi unaonyesha kwamba ndoto ambazo tunakumbuka ni zile ambazo tulikuwa tunaota wakati tulipoamshwa au ziliisha dakika chache kabla ya kuamka. Kwa upande mwingine, ndoto mbaya zinaweza kutufadhaisha na kutufanya tushindwe kulala tena.

Wednesday, May 21, 2014

THE FADHAGET SANITARIUM INAKULETEA SABABU ZA KUCHELEWA KUPATA HEDHI


Kwa kawaida mwanamke huacha kupata hedhi kitaalam huitwa Menopause anapofikisha umri wa miaka 42 -55 na kuendelea.
Leo tutazieleza sababu nje ya utaratibu huo wa kimaumbile unaoweza kumfanya mwanamke asipate hedhi na moja kubwa ni tabia ya maisha yake ya kila siku, yaani vyakula anavyokula (life style).


SIGARA
Tatizo moja kubwa ambalo huwakumba wanawake wanaovuta sigara ni kukosa hedhi au kuharakisha kutopata hedhi miaka miwili kabla ya wakati au umri wa miili yao kufanya hivyo.

UNENE
Wanawake wengine hukumbwa na tatizo hilo kutokana na kuongezeka uzito. Imethibitika kuwa uzito ukiwa mkubwa kwa wanawake unasababisha kuingia katika hatua za kuacha kupata hedhi kwa kuchelewa kwa mwaka mmoja zaidi ikilinganishwa na wanawake ambao hawana uzito mkubwa.Kitaalam hali hiyo inatokana na uingilianaji wa mafuta (kwa watu wanene au walio na uzito uliopitiliza) na homoni za kujamiiana yaani Sex homones.

ULEVI
Wanawake walevi wa pombe yaani wanaokunywa pombe kila siku nao wapo kwenye hatari ya kukumbwa na tatizo hili.
Lakini walio katika hatari zaidi ni wale wenye umri kati ya miaka 25 na 49, hawa wanaweza kufunga hedhi kama wataendelea na tabia hiyo ya unywaji wa pombe kila siku.

KUTOKULA NYAMA
Wengine ni wanawake ambao wanafanya mazoezi mazito mara kwa mara na wenye umri kati ya miaka 39 na 49 au wasiokula nyama au vyakula vinavyotokana na nyama (vegetarian) nao wamo katika hatari ya kukosa kuona siku zao za hedhi.
Wengi wa wanawake wanaopatwa na tatizo hili hukumbwa pia na tatizo la kuchelewa kuacha kupata hedhi kama inavyotakiwa wakiwa katika umri unaotakiwa na hali hiyo huwahatarisha kwani wanaweza kukumbwa na hatari ya kupata saratani ya matiti.
Menopause kama tulivyoeleza hapo juu, ni hatua ya kuacha kupata hedhi ambayo hutokea wakati mwanamke akiwa na umri wa miaka 42-55 na huambatana na usitishwaji wa kutolewa kwa mayai ya uzazi, kupungua kwa kiwango cha homoni za kujamiiana, hivyo kusababisha kupungua kwa hamu ya kujamiiana kwa mwanamke.
Hali hiyo husababisha tupu za mwanamke kuwa kavu, nywele kuwa nyembamba, matatizo wakati wa kulala, matiti kusinyaa na kupata hedhi bila mpangilio kabla ya kuacha kupata hedhi kabisa.

USHAURI
Mwanamke yeyote ambaye ataona dalili au kutopata hedhi yake muda muafaka ni vyema akaenda kumuona daktari ili afanyiwe uchunguzi na kama ataonekana ana tatizo la kiafya litapatiwa ufumbuzi. Wale wenye matatizo ya tumbo wamuone mtaalam.

Monday, May 19, 2014

MATATIZO YA KUPATA CHOO AU KUCHELEWA KUPATA CHOO (CONSTIPATION)


Ni nini tatizo la kupata haja kubwa?
Ni  haja kubwa inayopatikana isiyozidi mara tatu katika wiki na ama haja kubwa inayoleta shida kutoka kwake na utokaji wake ni mithili ya mavi ya mbuzi (uyabisi) hata kama inapatikana kila siku. Hali hii inaposhamiri muathirika hupata choo si zaidi ya mara tatu katika kipindi cha  mwezi mmoja.

Dr. Fadhili Emily akiwa katika makao makuu ya The Fadhaget Sanitarium Clinic
Ni moja miongoni mwa matatizo katika mfumo wa kusaga chakula yanayowakumba watu wengi si hapa kwetu Tanzania tu bali dunia nzima kwa jumla. Shida ya kupata choo ni hali inayowakabili watu mbalimbali.

Takriban ni wastan wa asilimia kumi na mbili ya watu duniani wanasadikiwa kuwa na tatizo la kuchelewa kupata haja kubwa. Katika hali ya kawaida mwanadamu hupata haja kubwa karibu kila siku au kila baada ya siku moja.
Kwa mtoto mchanga baada kuzaliwa huenda haja mara nne hadi tano kwa siku. Wale wanaonyonya maziwa ya mama (maziwa ya kifua) hupata haja mara nyingi zaidi ukilinganisha na wenzao wanaonyonya maziwa ya kopo yaani fomula (formula). Kwani baadhi yao hupata haja kila baada ya kunyonya wakati wenzao wa maziwa ya kopo hupata haja mara moja tu kwa kila baada siku mbili hadi tatu. Mtoto anaenyonya maziwa ya mama si aghlabu kupata shida ya haja kubwa. Anapotimiza umri wa miaka miwili mtoto hupata choo takriban mara moja hadi mbili kwa siku. Wakati mtoto wa umri wa miaka minne anapata haja kubwa mara moja kwa siku.


Jee hali ikoje hapa kwetu Zanzibar?
Katika kliniki zetu za upasuaji karibu asilimia kubwa ya wagonjwa wanaokuja kwa tatizo la kuumwa na tumbo wengi wao hubainika kuwa na hali isiyoridhisha katika masuala ya kupata haja kubwa. Aidha wagonjwa hao wamekuwa wakilalamika kuchelewa kupata au hupata haja kubwa kwa shida kabisa. Kwa watoto wachanga hali hii pia ipo, na kwa watu wazima kina mama husumbuliwa zaidi ukilinganisha na kina baba. Wazee nao hasa kwasababu ya umri ambapo maradhi mengi hujitokeza na pia kutoweza kujituma kama ilivyo kwa vijana, husumbuliwa na tatizo hili kwa kiasi kikubwa. Watu wengi wamekuwa wakijitibu wenyewe pasipo kujua nini hasa kinawasibu. Hali hiyo hupelekea kwa baadhi yao kupata madhara zaidi wasiyoyatarajia. Mathalan hupata vidonda vya tumbo, maumivu ya tumbo yasiokwisha, kuharisha mara kwa mara, na baadhi yao chango huziba hali inayowapelekea kufanyiwa opresheni ya dharura.
Kuchelewa kupata haja kubwa huwa ni sababu kuu ya kupata maumivu wakati wa kwenda haja. Hali inapokuwa mbaya mtu hukosa kabisa kupata choo na kujamba pia, na uchango wake mkubwa hujaa kinyesi. Kushindwa kupata haja kubwa ni dalili inayotokana na sababu nyingi. Sababu zenyewe zimejigawa namna mbili. Mosi, kuziba choo, na pili ni uchango kuwa na mwendo wa taratibu mno.

SABABU
Zipo sababu kadhaa zinazopelekea kutokea kwa tatizo la kukosa kupata haja kubwa kikawaida, miongoni mwa hizo ni kama hizi zifuatazo:
  • Inaweza ikawa yenyewe tu bila kusababishwa na hali yoyote ile kama vile madhara ya dawa
fulani, au hali ya kiafya, na huwa haiambatani na maumivu ya tumbo. Kwa lugha nyengine ni kwamba sababu hasa huwa haijulikani. Hii ndio sababu maarufu kuliko nyengine zote.
  • Inaweza kusababishwa na mpangilio mbaya wa chakula, kutokula vyakula vyenye fiber (nyuzinyuzi), kunywa maji kidogo kuliko inavyotakiwa.
  • Matumizi ya dawa mbalimbali na baadhi ya athari zake kama vile baadhi ya dawa za kutibu presha (shinikizo la damu), dawa za kupunguza maumivu, dawa za kutibu degedege, dawa za kutibu mamivu ya tumbo ikiwa pamoja na dawa za kutibu mfadhaiko, dawa za kutibu alaji (makole).
  • Mgonjwa wa maradhi ya kisukari, maradhi ya misuli.
  • Maradhi ya uvimbe katika uti wa mgongo, kansa ya utumbo mkubwa, kidonda/kuchanika njia ya haja kubwa mlangoni yaani fisha (anal fissure).
  • Kwa makusudi tu mtu hujizuwia asiende haja kwa sababu labda hakuna choo cha kuridhisha, anaogopa maumivu hasa wale wenye fisha (anal fissure), ama kwa uvivu tu.
  • Watoto nao hupata tatizo la kuzaliwa nalo. Kukosekana mishipa ya fahamu katika sehemu ya utumbo mkubwa huwa ndio sababu inayopelekea utumbo huo kutosukuma kinyesi hivyo kusababisha kuchelewa kupata haja kubwa ambapo mara nyengine hupindukia kipindi cha wiki moja hadi mbili au hata zaidi. Kwa maana hiyo tumbo huvimba na mtoto hudhoofu kiafya. Hili ni tatizo la kipekee.
VIPI TUNACHUNGUZA
Maelezo ama dalili mgonjwa anazozielezea jinsi anavyosumbuka kupata haja kubwa, pekee hutoa taswira kamili ya tatizo linalomkabili. Miongoni mwa dalili hizo ni zile pamoja na kuwa na choo kigumu, hutoka kwa shida, hufanana na mavi ya mbuzi ama sungura yaani uyabisi. Dalili nyengine ni mbweo, kuvimba tumbo, maumivu ya tumbo, kuumwa na kichwa, uchovu, kutojiskia vizuri na pia kuwa na hisia za kutomaliza haja yote. Na anapoulizwa mgonjwa juu ya mpangilio wake wa mlo mara nyingi hubainika kutokutumia vyakula vyenye nyuzinyuzi (hivi ni vyakula vya sehemu ya mimea ambayo haisagwi na mwili wetu na hivyo kusukuma utumbo, huku ikifyonza maji wakati ikitoka na kufanikisha kupata haja kubwa). Wengi wao hawali nafaka, mboga za majani, na matunda kama mlo wa kawaida. Kutokunywa maji ya kutosha, kutofanya mazoezi kikawaida au wakati mwengine husababishwa na matumizi ya baadhi ya dawa ambazo kwa kuzitumia kwa kipindi cha muda mrefu hatimae huleta athari ya kuzuwia au kuchelewa kupata choo.
Tunachunguza kwa kuliangalia na kugusa tumbo, ikibidi huangalia njia ya haja kubwa, wakati mwengine hata kwa kutumia darubini maalum tunaweza kubaini tatizo hilo. Xray ya tumbo ingawa si lazima, nayo pia huweza kutumika kubainisha uwepo wa tatizo.

KINGA
JE, VIPI TUNAWEZA KUJIKINGA?
Ni rahisi zaidi kukinga usipate hali hii kuliko kutibu. Mara au pindi ukipata nafuu jambo la msingi ni kujitahidi kuendeleza mazoezi kwa maana ya matembezi, kuogelea, au kushiriki michezo ya aina yoyote ile ilimradi tu utoke jasho. Kunywa maji kiasi cha kutosha ambacho kwa wastani mtu mzima anatakiwa kwa siku anywe lita mbili hadi mbili na nusu kulingana na hali ya hewa. Kula mboga za majani kama vile mchicha, kisambu, mtoriro, kabichi, karoti na nyenginezo; nafaka kwa mfano karanga, mahindi, ngano, fiwi, mbaazi, kunde, maharage, njugu mawe na kadhalika; pendelea kula matunda hususan ndizi mbivu, embe, chenza na machungwa (kula hadi maganda ya ndani), papai, balungi, pea(parachichi), fenesi, epul (usilimenye), shelisheli na mengine mengi tu ambayo kwa kweli katika mazingira yetu Mola ametujaalia tunayo mengi sihaba. Yote haya hutengeneza mazingira mazuri ya kupata haja kubwa kikawaida na bila shida yoyote.
Na kwa watoto ni kuwapangia muda wa kwenda kujisaidia mapema asubuhi na kipindi cha takriban dakika thelathini baada kupata mlo.

NINI HASA KAZI YA VYAKULA VYENYE NYUZINYUZI?
Vyakula vya namna hii kwa kawaida havisagwi na mwili kwahiyo hupita katika utumbo na kutoka mwilini.Iwapo tutakula nafaka na matunda na mboga za majani tutakuwa na nafasi kubwa kujikinga kupata maradhi kama vile, maradhi ya moyo, unene wa maradhi (obesity), kuepuka kupata bawasili, na hata kusaidia mwili kudhibiti kiwango cha sukari katika damu kwa kuchelewesha uyeyukaji wake mwilini. Inadhibiti na kupunguza kiwango cha mafuta  mwilini kwa kuambatana nayo. Na kubwa zaidi huwa ni kinga tosha dhidi ya kansa ya utumbo mkubwa kwani hubeba sumu za kwenye utumbo na kutoka nazo. Kwa lugha isiyo ya kitaalamu labda tunaweza kusema na kumithilisha vyakula vya nyuzinyuzi vinafanyakazi kama brashi. Vinasafisha njia yote ya mfumo wa usagaji chakula.
TIBA
  • Ni pamoja na kunywa maji ya kutosha.
  • Kula vyakula vyenye nyuzinyuzi (fiber), hivi vingi vinapatikana katika mboga za majani, nafaka na matunda.
  • Matumizi ya haluli kama ni tiba inabidi kutumiwa kwa hadhari sana, kwa vile kuzoeleka kwake kunaweza kupelekea uchango ushindwe kufanyakazi wenyewe.
  • Nayo upigaji wa bomba hutumiwa zaidi kama kisisimuzi. Hatahivyo bomba huleta manufaa ama matokeo chanya zaidi pale tu kinyesi kinapokuwa kimejikusanya karibu na mlango wa haja kubwa.
ATHARI ZA MATATIZO YA HAJA KUBWA
Kukosa kupata haja kubwa au ama kupata haja kubwa kwa shida ikiwemo kupata choo kigumu kunaweza kusababisha miongoni mwa maradhi mengine ni pamoja na kupata bawasili, kidonda ama mpasuko katika mlango wa haja kubwa (fisha), kutoka futuru (mwijiko), mrundikano wa kinyesi katika uchango. Hali hii ikiachwa kuendelea tumbo litajaa na kuvimba, litakuwa gumu  na lenye maumivu. Mgonjwa anaweza akawa na dalili za kuziba utumbo yaani kutapika na kadhalika.

HADHARI
Siku zote yapaswa  tuwe makini na tuchukuwe hadhari pale inapotokezea kutopata haja kubwa kwa ghafla na ikadumu kwa siku kadhaa. Hali hii hutokea aghlabu sana kwa wazee na ni moja ya dalili ya kuwepo kwa uvimbe katika uchango mkubwa ambao mara nyingi huwa ni kansa ya utumbo. Bilashaka huambatana na dalili nyengine kama vile kutokwa damu njia ya haja kubwa wakati wa kujisaidia, kuharisha baadhi ya wakati na kupungua uzito wa mwili au kukonda na kadhalika.

USHAURI
Hapanashaka ili kupunguza tatizo hili ambalo linawakabili watu wengi katika jamii yetu, elimu ya chakula bora na mlo ulopangika ndio jibu sahihi ama muarubaini wa kutilia mkazo. Tuanzie skuli na majumbani mwetu kuwaelimisha hasa wanetu. Ni kweli kabisa tumejaaliwa rasilimali nyingi sana  kwa maana ya matunda ya msimu yanayofika kuzagaa kama uchafu na kuharibika, nafaka hadi kuoza ovyo, mboga za majani za kila aina, lakini la ajabu ni kuona watu wetu wengi hawajui thamani ya neema hiyo na kutokuitumia kwake ndio chanzo kikubwa cha maradhi mengi yanayotukabili. Hivyo basi tuwazoweshe watoto wetu kupenda kula matunda, nafaka na mboga za majani tangu wako wadogo, kwani si tu hupelekea kupata haja kubwa kikawaida bali pia vyakula hivi vimejaa vitamini mbalimbali muhimu kwa siha ya mwanadamu.
Muone daktari wako atakuskiliza, atakuchunguza na hatimae atakupa maelezo yenye tija kwako. Tukumbuke samaki mkunje angali mbichi, udongo upate ulimaji.

Thursday, May 15, 2014

MTANZANIA ONDOA HOFU, DENGUE INATIBIKA THE FADHAGET SANITARIUM CLINIC


KINGUNGE AWATAKA WATANZANIA KUONDOKANA NA IMANI POTOFU JUU YA TIBA ASILIA



Mlezi wa Chama Cha Utabibu wa Dawa Asilia Tanzania (ATME), Kingunge Ngombale (kushoto), akifungua mafunzo kwa wahariri na waandishi wa vyombo vya habari kuhusu tiba asilia katika ukumbi wa mikutano NIMR jijini Dar es Salaam. (kulia), Mwenyekiti wa Chama cha Utabibu wa Dawa Asili Tanzania (ATME), Bw.Simba Abdulrahman

Kingunge amewataka Watanzania kuondokana na imani potofu dhidi ya tiba asili na badala yake watumie ili kupona maradhi mbalimbali yanayowakabili

Lucey Samwel, kutoka kitengo cha Tiba asilia Wizara ya Afya akiwakilisha mada ya sera ya Afya, Sheria ya Tiba Asili na Tiba Mbadala, pamoja na taarifa mbalimbali zinazohusu Tiba Asilia na udhaifu katika usimamizi wa sheria ya TATM ya mwaka 2002.

Mkurugenzi wa Paseko T.H.P, Othman Shem akielezea kuhusiana na Tiba Asili Tanzania na changamoto zake.

Mwanasheria kutoka AUDA, Onesimo Munuo (kushoto), akielezea mapungufu ya utekelezaji ya Tiba asili na mbadala.


Wahariri na waandishi wa vyombo vya habari mbalimbali walihudhuria katika mafunzo hayo.


Mlezi wa Chama Cha Utabibu wa Dawa Asilia Tanzania (ATME), Kingunge Ngombale. Akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe mara baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo

Tuesday, May 13, 2014

TIBA YA UGONJWA UNAOSABABISHWA NA MBU DENGUE YAPATIKANA THE FADHAGET SANITARIUM CLINIC KWA DOCTOR FADHILI EMILY

The Fadhaget Sanitarium Clinic chini ya Dr. Fadhili Emily ni kitengo cha Sayansi na Tiba Asilia, tunakiri wazi ugonjwa wa  dengue ni fani yetu , mimi ugonjwa huu nimeufanyia utafiti mwaka 2010 nchini Afrika Kusini kupitia kitengo cha University of Medicine Plant  kilichopo Pritoria na ni wazi  kwamba ugonjwa huu ulikuwepo na tulikuwa tukiutibu kuanzia hapo.
http://zanzibariyetu.files.wordpress.com/2013/06/latest-dengue-fever-in-lahore-punjab-dengue-report-updates2.jpg?w=584&h=371
Ni wengi walikuwa wakisumbuliwa na ugonjwa huo na wakipima mahospitalini wanakutwa hawana malaria ila wanapofika The Fadhaget Sanitarium Clinic nawapa dawa zilizo na uwezo wa kirutubisho cha Ferus Hydroxide (Fe+) na Alcaroid Acid Synatic ni ndani ya masaa matano utaanza kuona uzima.

Piga simu kwa ushauri kama umeziona dalili kama hizo hapo juu kwa namba +255 757 505158 au +255 712 705158

Dr. Fadhili Emily
Tembelea
www.fadhaget.blogspot.com

JINSI YA KUFIKA
Kama unatokea Mwenge, panda magari ya Tegeta, shuka kituo cha Afrikana, uliza The Fadhaget Sanitarium Clinic kwa Dr. Fadhili Emily. Tupo hapa Dar es Salaam na mikoa 10 hapa nchini Tanzania

Monday, May 12, 2014

FIGO: MATATIZO YA FIGO NI TISHIO KWA WATANZANIA



Gharama kubwa za matibabu zawakatisha matumaini.

Hapa duniani kuna maradhi aina nyingi yanayotisha, yakisumbua binadamu, kuwatia ulemavu hata kuwa chanzo cha uchumi kutetereka, wakati mwingine kusababisha kifo. Miongoni mwa maradhi hayo ni kuharibika kwa figo.

Ugonjwa huo unaelezewa kwamba siyo tu unaleta maumivu kwa mgonjwa, bali pia hautibiki kirahisi pamoja na gharama za matibabu husika kuwa kubwa na wengi kushindwa kuzimudu.

Wataalamu wa afya wanasema kuwa, zipo sababu kadhaa zinazosababisha maradhi katika figo kwa binadamu ikiwamo matumizi mabaya ya dawa hasa za maumivu, dawa za kienyeji, baadhi ya dawa za Kichina, uvutaji wa sigara na unywaji wa pombe kupita kiasi.

Tiba ya usafishaji wa figo kwa kitaalamu (Dialysis), uhusika na utoaji wa maji yaliyojaa mwilini, uchafu, pia sumu zitokanazo na vyakula au dawa. Tiba ya 'Dialysis' ni ya gharama kubwa kwa kuwa kila mgonjwa anapohitaji kuipata, hutakiwa kutoa kiasi Sh300, 000, huku akitakiwa kuipata tiba hiyo angalau mara tatu kwa wiki ambapo hugharimu Sh900,000.

Dialysis ni mchakato wa kutoa maji yasiyohitaji kutoka kwenye damu ya mtu. Mchakato huo hufanyika baada ya figo kushindwa kufanya kazi na taka hizo kuingia kwenye mfumo wa damu. Kwa kawaida figo hufanya kazi ya kuchuja uchafu katika mwili, lakini baadhi ya watu huathirika na figo zao kushindwa kufanya kazi ya kuchuja uchafu huo kutokana na sababu mbalimbali zilizoainisha awali.

Usafishaji wa figo hufanywa kwa wagonjwa ambao figo zao zimeathirika kwa kiasi kikubwa na maradhi au hata kwa dharura.

Mgonjwa hutundikiwa mipira maalumu, huku kwenye mashine kukiwa na figo ya bandia ambayo kazi yake ni kupitisha damu, kuisafisha na kuirudishwa mwilini.

Kunakuwa na mipira kadhaa ikiwamo ya kupitishia damu kupeleka kwenye figo bandia, inayofanya kazi kama ya mwilini na mirija mingine ambayo ni mikubwa kiasi inatumika kutoa maji yasiyohitajika mwilini na sumu, huku mingine ikitumika kurudisha damu safi mwilini.

"Mgonjwa hulala akifanyiwa tiba hii kwa saa nne, bila kuchomwa sindano ya usingizi, kwa kuwa haina maumivu makali. Vilevile mgonjwa hutobolewa eneo maalumu mwilini kwa ajili ya kupitishia mipira. Kuna wanaotobolewa shingoni au mkononi kulingana na anavyotaka mgonjwa,"

Pamoja na tiba hiyo kuwa ghali, bado haina uhakika wa kupunguza tatizo kwa asilimia 100, bali kwa asilimia 40 hadi 50 pekee.
Mtaalamu huyo wa afya anaitaja tiba nyingine kuwa ni ya kupandikiza figo, (kidney transplant) ambayo kwa sasa haifanyiki nchini. Hata hivyo ili kufanyiwa upandikizaji huo nje ya nchi, mgonjwa anahitaji zaidi ya Sh20 milioni.

"Tiba hii hufanywa hasa kwa mgonjwa ambaye figo yake imekufa na haiwezi kufanywa tena nchini," anasema Dk Kisanga.

Madhara ya tiba hizo

Tiba ya figo ina madhara kiafya hasa kwa walio kwenye hatua ya tano ya tiba hiyo. Madhara hayo ni pamoja na maradhi ya moyo, miguu kukaza na maumivu ya kifua.

Kazi kuu za figo mwilini

Figo ni miongoni mwa viungo muhimu katika mfumo wa utendaji kazi wa mwili wa binadamu.

Kawaida, mwili wa binadamu una figo mbili zenye maumbo yanayofanana, yakiwa yamejificha nje ya utando unaozunguka tumbo, chini kidogo ya mbavu.

Kazi kuu za figo ni kuchuja vitu mbalimbali pamoja na sumu katika damu, kusaidia kuhifadhi,kudhibiti kiwango cha maji na madini (electrolytes) mwilini.

Figo huchuja vitu hivyo pamoja na maji yaliyo mwilini na kutengeneza mkojo, huchuja pia maji yasiyohitajika mwilini huku yakinyonya madini na kemikali muhimu kuzirudisha katika mzunguko wa damu na kutoa nje uchafu usiohitajika, pamoja na kusaidia kutengeneza kiasili cha erythropoletin ambacho ni muhimu katika utengenezaji wa chembechembe nyekundu za damu, hupokea asilimia 25 ya damu na kila figo ina chembechembe hai ndogo milioni moja, pia kusaidia kudhibiti na kurekebisha shinikizo la damu mwilini (blood pressure).

Aina za ugonjwa wa figo

Aina za ugonjwa huu kuwa ni mbili; ya kwanza ni ile ya figo kushindwa kufanya kazi kwa ghafla na muda mfupi; pili ni ile ya figo kushindwa kufanya kazi polepole na kwa muda mrefu.
Figo kushindwa kufanya kazi polepole na kwa muda mrefu.

Kwa aina hii ya ugonjwa, figo huharibiwa taratibu na kuendelea kupunguza uwezo wake wa kufanya kazi kadiri siku zinavyokwenda.

Dalili za aina hii ya ugonjwa huchelewa kujitokeza na wakati mwingine mwenye tatizo hajisikii dalili yeyote, hadi pale inapotokea akaugua ugonjwa mwingine na daktari kuhisi tatizo, ndipo hugundulika kuwa na ugonjwa huo baada ya vipimo.

Sababu za figo kushindwa kufanya kazi ghafla
Sababu kubwa ni kupungua kwa mzunguko wa damu kwenye figo, kemikali za mwilini au kushambuliwa na sumu.

"Kushuka kiwango cha mzunguko wa damu humpata mtu ambaye anatapika sana na hanywi maji ya kutosha, anayeharisha sana na hanywi maji ya kutosha na wale ambao hupoteza damu nyingi kama vile kwenye ajali,"

Sababu nyingine kuwa ni pamoja na ugonjwa wa moyo, moyo kushindwa kusukuma damu kwa ghafla, au waliougua maradhi ya moyo kwa muda mrefu.

"Tatizo la figo kushindwa kufanya kazi kwa ghafla pia humpata mtu ambaye ana bakteria kwenye mzunguko wa damu, ambao wanaweza kusababisha homa 'Septicemia' na kuugua malaria," anasema Dk Kisanga.

Sababu zinazofanya figo ishindwe kufanya kazi taratibu na kwa muda mrefu na hatimaye kushindwa kabisa kuwa ni presha kuwa juu, kisukari, magonjwa yanayosababishwa na bakteria, HIV, saratani na sumu mbalimbali zinazoingia mwilini.

Dalili za figo kushindwa kufanya kazi vizuri

Dalili ya kwanza ni kupungua kwa kiasi cha mkojo, kushindwa kupumua, kusikia kichefuchefu, kutapika na kuvimba miguu.

Nyingine ni maji kujaa mwilini, madini ya mwili kuwa juu hasa ya 'potashiamu', asidi nyingi, matatizo katika moyo, ubongo, kukosa hamu ya kula na kudhoofika mwili.

Dalili nyingine kwa wagonjwa ambao hawagunduliki mapema ni kuvimba macho wakati wa asubuhi na uvimbe kupungua baadaye.

Nyingine ni kuvimba miguu asubuhi, kupungukiwa damu mwilini kama dalili za kwanza (kwani figo ikishindwa kufanya kazi ya kusaidia kutengeneza damu).

Saturday, May 10, 2014

ZIFAHAMU NJIA KUMI ZA KUKUSAIDIA KUPUNGUZA UNENE KWA KUPITIA BLOGU YA THE FADHAGET SANITARIUM CLINI

The Fadhaget Sanitarium Clinic chini ya Dr. Fadhili Emily leo imeona ni vizuri kuongea na watu wanene wanaohitaji kuwa wembamba. Unaweza kuzaliwa na unene na wengine wanapata unene ukubwa kutokana na sababu mbalimbali. Sasa ninaomba twende sawa kuangalia ni jinsi gani ya kupungu za unene na vitu gani vya kuzingatia
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg3kYhjbbIXqfbLhL-h6EFdGYRdY4hdsqUhyphenhyphenSrMmTQxuXSQrrvG88AYJntbrsGhQXRfSjtQYoBRZi9iVa6bY5yQT5gA8sAMV_cO-7IERvO6G0yGHXdRB_Ezubw0Y0TP4IxCviMnDigsUSE/s1600/UNENE.jpg

1-ULAJI

Ipo mifumo miwili ya kula. Chakula unachokula na namna unavyokila.

Unavyokula.

-Kuna kula vyakula vidogo vidogo vyenye madini, vitamini, mafuta nk mara nyingi kwa siku; au kula milo michache (mmoja au miwili) mikubwa ili kujaza tumbo. Ulaji mdogo mdogo husaidia afya na kuingia mwilini vyema kuliko ulaji mkubwa wa mara chache. Tumbo lina musuli zinazofanya kazi kama mashine au mnyama. Gari likijaa sana hupata taabu kwenda. Punda hivyo hivyo. Ulaji mdogo mdogo unaosambazwa mara kadhaa kwa siku ni bora maana mwili unachambua kila kitu kwa wepesi na haraka. Unapokula milo michache mikubwa unapalilia zaidi mafuta mwili.

(PENDEKEZO la kwanza. Asubuhi, kunywa maji kwanza, matunda, kisha ndiyo chai na vitu vingine kama mkate au maandazi…)

-Wapo wanaodai kwamba wanakula matunda na mboga.

Tatizo ni kwamba mipangilio yao huwa ya makosa. Mathalan wengi hula matunda baada ya chakula. Vimeng’enya chakula (enzymes) tumboni hufanya kazi namna tofauti. Mathalan vile vinavyonyambua matunda ni tofauti na vinavyomeng’enya vitu vigumu zaidi kama nyama au wanga. Matunda hunyambuliwa haraka zaidi kuliko vyakula vingine. Hivyo ni bora kula matunda dakika10-20 kabla ya chakula. Ukila baadaye matunda hugeuzwa aina fulani ya pombe (fermented food) inayoelea tu juu ya chakula na kubakia kitu kingine badala ya kuingizwa haraka ndani ya damu kupitia utumbo mdogo, uwengu, moyo, ini, nk.

Tatizo jingine ni kupika sana mboga hadi zikapoteza nguvu.

-Mseto wa vyakula pia ni muhimu. Kwa mfano vyakula vyenye uchachu (“acid”) na vile vinavyomumunyuka haraka (“alkaline”) havitakiwi viliwe pamoja. Mfano ni matunda. Matunda chachu kama machungwa, mananasi na maembe yatakiwa yawe pamoja; na yale laini zaidi: ndizi mbivu, matikiti maji, mapapai, matufaha, nk yaende kivyake, maana yana mfumo tofauti, wa kumeng’enywa.

Mpishi Patrick Maka ( katikati, akiwa na wenzake kazini Dar) ni kati ya wapishi wa Kitanzania wanaopigania sana ulaji wa chakula bora

Hali hiyo pia iko katika nyama. Nyama nyeupe (ndege na samaki) tofauti na nyama nyekundu (ng’ombe, kondoo, nk) ziliwe tofauti.

Chakula unachokula

Waafrika hatuna tabia ya kula mboga mboga mbichi. Tunafuata ladha na mazoea kuliko thamani.

Bara letu lina mboga na vyakula bora kuliko bara lolote duniani lakini sisi tunakufa mapema na kwa utapia mlo kuliko wale wanaotoka nchi kame. Ulaya nzima imejazana mboga mboga zinazoagizwa toka Afrika. Kenya na Tanzania zinauza mboga za maharagwe mabichi (green beans), matunda toka Afrika Kusini na Ivory Coast; nk. Waafrika tunapenda kujaza matumbo. Unene umekithiri hata wale walio matajiri waliosoma bado wanakufa kwa kisukari shauri ya kutokula mboga mbichi.

Ulaji wa mboga mbichi ni upi?

Ni mathalani ulaji wa salad. Tanzania tunaita kachumbari. Lakini si lazima iwe kachumbari ya nyanya, vitunguu na chumvi tu. Waweza kuchanganya matango, nyanya kwa maparachichi; au vitunguu saumu, giligilani na karote. Huu mseto wa mboga mbichi ni mzuri ukienda na chakula chenye nyama za minofu na wanga (ugali, wali, ndizi za kupika nk). Ulaji wa wanga asubuhi, mchana na jioni kila siku huchangia sana katika unene.

(PENDEKEZO LA 2. Ugali kwa samaki; mboga ya majani ya matango kwa nyanya. Usiweke chumvi kwenye hiyo mboga mbichi ya majani.)

Majani na mimea yamezingirwa na barafu Ulaya- vyakula vingi vya watu hawa huagiziwa na kutegemewa Afrika. Lakini wanakula vizuri kutuzidi. Kwanini? Picha na F. Macha

2-UNYWAJI MAJI

Waafrika hatunywi maji, hasa wanawake. Wanaokunywa maji zaidi ni wacheza michezo. Wengi wetu hunywa zaidi soda (vinywaji baridi kama Cocacola, Pepsi, Mirinda ,Tangawizi na gesi za kisasa kama Red Bull) zilizojaa gesi inayoleta vidonda tumboni; na chai. Kuliko maji. Na maji haya hutakiwa dakika 10-20 kabla ya chakula au nusu saa kuendelea baada ya chakula. Ukila chakula huku unasakatia maji huimanisha mtu una kiu. Ulaji chakula na unywaji maji ni vitu viwili tofauti. Ila utawaona watu wanakula huku wakibugia maji. Unapokula chakula huku unabugia maji unapunguza nguvu za chakula, unajaza tumbo maji na kuchelewesha mmeng’enyo wa chakula (digestion).

Chakula kisipomeng’enywa vizuri kinaketi tu tumboni. Matokeo wengi wetu tuna matumbo makubwa. Kama hufanyi mazoezi lile tumbo linakwenda pembeni (chini ya mbavu) hasa kwa watu wa makamo linaleta maradhi kama kisukari, kiungulia, kuvimbiwa, uyabisi wa tumbo, nk. Kizungu huitwa “love handles.”…

Farasi ni mnyama asiyeliwa ovyo Uingereza; hufugwa tu kwa kazi na michezo. Ipo hoteli moja Scotland imeanza kupika nyama yake kwa chips. Imeandamwa sana na "wapinzani wa kula nyama" wa Kitasha... (Picha na F. Macha)

3-SUALA LA UMENG’ENYAJI

Chakula huanza kumeng’enywa au kusagwa (kwa lugha iliyozoeleka) mdomoni. Mate yako mdomoni ni chanzo cha uchambuaji chakula. Unapobugia chakula bila kutafuna sawasawa unasababisha mambo mawili. Moja chakula kutochambuliwa vizuri, pili chakula kwenda kukaa tu tumboni, au kama kikipita hakisaidii lolote mwilini. Utafunaji wa taratibu husaidia umeng’enyaji. Chakula kinapofika tumboni hukaa pale dakika ishirini. Hapo huchanganywa na asidi (ya manjano iitwayo Hydrochloric) inayokibadilisha tayari kupelekwa utumbo mkubwa, kupitia kongosho. Kule uchafu utapelekwa chini na rutuba kusafirishwa na utumbo mdogo kuelekea katika uwengu, moyo. Moyo utadunda chakula kilichoshageuzwa damu kuelekea mwilini kufanya kazi na akiba hubakishwa katika ini.

Sasa kama usipotafuna vizuri, ukila huku unakunywa sana maji au vinywaji vingine chakula hakimeng’enywi vizuri. Ndiyo maana unawaona watu wengine wanakula sana lakini hawana afya. Wanaugua ovyo ovyo, wanatoka jasho ovyo, wanajamba ovyo, wana matumbo makubwa, wanavimbiwa, wanakaa siku nyingi bila kwenda choo (inatakiwa mtu kwenda haja kubwa mara moja au mbili kwa siku) nk.


4-ULAJI WA VYAKULA VYA MAFUTA

Mafuta ni suala muhimu sana mwilini. Ila ulaji wake shurti uwe wa mpangilio. Yaani unaowiana. Lazima mtu uwe na wastani mzuri wa vyakula vya nguvu, yaani “wanga” (ugali, ndizi, wali, viazi mbalimbali, mikate, mahindi, nk), ujenzi yaani “protini” (mboga na nyama), “madini” (mbegu mbegu mbichi si za kukaanga sana na chumvi) na “vitamini” (matunda, maziwa, mayai, nk).

Waafrika tunapenda nyama. Nyama ni muhimu sana maana ina madini aina ya chuma (nyama nyekundu) protini,nguvu na mafuta. Ila mafuta yaliyoko katika nyama mara nyingi si mazuri shauri hayatoki, huganda. Chukua nyama ya kuku na samaki ambayo huwa na ngozi. Wengi wetu hupenda sana kula ile ngozi ya wanyama hawa kwa kuwa tamu. Lakini haya ni mafuta mabaya.

Mafuta ya samaki lakini ni mazuri. Samaki anayo mafuta ya Omega-3 ambayo husaidia mwili na kinga maradhi mwilini.

Tunapokula nyama choma au ya kukaanga, lazima tule pia mboga za majani (mbichi) na si vizuri kula nyama kila siku. Kama huwezi kukaa bila nyama kila siku, fanya mazoezi ya mwili.

PENDEKEZO LA 3- Kula mbegu mbegu za korosho, karanga au mlozi (ziwe mbichi badala ya kukaanga na chumvi) kati kati ya siku. Haya ni mafuta yenye rutuba mwilini kuliko nyama za mafuta.

Chips za Magimbi zilizopikwa na kuonyeshwa ndani ya tovuti ya Miriam Rose , dada wa Kibongo anayetukuza mapishi ya Kitanzania duniani. Habari zaidi tembelea : http://www.tasteoftanzania.com

5-MAZOEZI YA MWILI NA VIUNGO

Mazoezi ni mfalme wa kupunguza unene.

Ukiwauliza wengi watakuambia wanafanya kazi ngumu za sulubu (wanachuruzikwa jasho) kwa hiyo hayo ni mazoezi. Ila kazi na mazoezi ni vitu viwili tofauti. Ingekuwa kufanya kazi ni mazoezi basi kusingekuwa na wastani mfupi wa maisha kwa maskini hasa sisi Waafrika.

Wengine watadai kwamba walipokuwa wadogo shuleni walifanya mazoezi sasa wamekuwa watu wazima (miaka 40 kuendelea) kwamba eti mazoezi ni suala la ujana; kumbe kadri unavyokuwa ki umri ndivyo kadri unavyotakiwa kufanya mazoezi na kujitazama zaidi kiafya.

Watazame Wachina na Wajapani wanavyoishi maisha marefu.

Mazoezi ni shughuli inayokufanya kwanza uheme (mapafu na moyo kwenda kasi), viungo na mifupa kujinyoosha (stretching), kutoka jasho na usafishaji wa damu. Mazoezi yanayosaidia haya ni pamoja na kutembea kasi, kukimbia, kuogelea, michezo mbalimbali ya riadha (kama mpira wa miguu, nyavu, kikapu, mikono, nk); michezo ya kupigana na kujilinda yaani masho ati(karate, kung fu, judo, capoeira, krav maga, jiu jitsu, systema, kickboxing, thai boxing, kempo, kalari payatu, aikido, nk) …

Ni muhimu mwanadamu ufanye mazoezi makali ya viungo mara mbili tatu kwa juma. Si vizuri kufanya kila siku kwani musuli na mishipa inahitaji kupumzika na kukua.

Kama unapenda kuinua vyuma lazima uwe na mwalimu wa kukuelekeza; na si vizuri kufanya kila siku. Wastani wa mara mbili tatu kwa juma inatosha kabisa.

Mdau wa Kitoto naikabili bahari shakiri na baridi sana ya English Channel. Kuogelea ni moja ya tizi bab kubwa lisilohitaji kingine bali mwili wako...maji bure asilia ya Muumba al Dunia. (Picha na A. Macha)

6-UPO UFANYAJI MAZOEZI WA AINA MBILI

Mazoezi ya nguvu ya kuhema niliyotaja hapo juu (cardio-vascular) na yale laini ya kujinyoosha yaani ambayo hutumia zaidi nguvu za ndani na pumzi. Haya ya pili ni kama Yoga (India) , Tai Chi Chuan (China) na aina mpya mazoezi iliyoanza Majuu miaka ya karibuni yaani Pilates (hutamkwa hivyo hivyo ilivyoandikwa Pilates). Haya laini yanawafaa zaidi watu wazima na nchini China na Japan mathalan utawakuta wazee wa miaka 80 hadi 90 bado wanayafanya. Husaidia moyo, damu na akili.

Michezo na mazoezi ya mwili ni njia kuu ya kupunguza unene, kurefusha maisha, kuchangamsha ubongo, kupunguza ulevi, uvutaji sigara, dawa za kulevya, tabia mbaya za uvivu, ugomvi, nk. Mataifa yenye watu wanaofanya mazoezi kama Japan, Brazili, India, China nk huwa na wachapa kazi wengi na wananchi wanaoipenda jamii yao.

Chakula cha wanga kwa wingi kilichozoeleka sana Afrika ni kitamu; ila kinakosa mboga mbichi za majani, yaani Saladi- (Picha na F Macha)

7-KULA SANA CHUMVI SI VIZURI

Ulaji chumvi mwingi hutokana na suala la ladha. Kisayansi vyakula vyote vina chumvi asilia sema tu tumezoea kuongezea madini hii iitwayo Sodium. Sodium inachangia sana kufupisha maisha. Huifanya mishipa ya damu ichoke; ni kama bomba lolote la maji ukilitazama baadaye hugeuka rangi kutokana na yale maji kupita pale kila siku.

Kwa wale tunaoishi nchi za joto na kutoka sana jasho kula chumvi ni muhimu. Ila tatizo letu ni kwamba hatunywi maji ya kutosha. Mtu ukiwa na kiu unakunywa soda au kinywaji cha sukari; inakuwa kama unaendelea kuutesa mwili. Kwa vipi? Mishipa inayopitisha damu mwilini badala ya kusaidiwa kwa maji inawekewa kazi zaidi ya kusafisha sukari na chumvi. Ndiyo maana vifo vingi vinatokea mapema; wastani wetu wa maisha haupiti miaka 50.

Utafiti uliofanywa chuo kikuu cha California, Marekani mwanzoni mwa 2010, umethitibisha kwamba vifo vingi duniani husababishwa na maradhi ya moyo na saratani ambavyo hutokana na uvutaji sigara, unene, ulevi na ulaji sana wa chumvi na sukari. Tukipunguza ulaji wa chumvi tunasaidia pia kupunguza maradhi ya moyo, utafiti unasema.

Mabasi ya ghorofa daraja mashuhuri la Tower Hill, London. Asilia kubwa ya wakazi hapa wanahusudu sana mazoezi shauri mji umebanana sana na hewa si safi. Taswira ilipigwa na mpiga picha Mike Nicholas, baharia wa Kibongo mkazi, Denmark, alipotembelea jiji hili la nne duniani kwa gharama, karibuni .

8-TAFITI ZA VYUO KADHAA ULIMWNGUNI KUHUSIANA NA AFYA

-Jarida la Kimarekani la sayansi lilieleza mwaka jana kwamba utapunguza ugonjwa wa moyo (ambao husababishwa na unene , wasiwasi na purukshani) kwa asilia mia 42 kama utakula matunda na mboga za majani peke yake kila siku, juu ya msosi wa kawaida.

(PENDEKEZO LA KULA- Na 4- Kula mlo wako. Baada ya saa mbili au tatu, sakatia tunda au matunda; baada ya mlo mwingine, kula sahani ya mseto wa mboga mbichi kama karote na matango. Utaona tofauti ya afya, ngozi, wajihi, kinyesi, usingizi, nk. Kidesturi tumezoea kunywa chai au soda za sukari sukari na gesi kati kati nya milo badala ya matunda na mboga mbichi za majani).

-Utafiti uliofanywa na wanasayansi chuo kikuu cha South Carolina mwanzo wa mwaka 2010 kuhusu faida za kuogelea.

Zoezi la kuogelea lina faida zaidi ya kukimbia au kutembea kwa vile huchanganya mazoezi makali na pumzi, kusaidia mapafu na moyo. Utafiti ulithibitisha kuogelea hupunguza hatari za kifo kwa asili mia hamsini.

-Utafiti wa jarida la chuo cha uganga Ulaya umeeleza (desemba 2009) kwamba kulala nusu saa kila mchana (“nap”) husaidia kupunguza ugonjwa wa moyo kwa asilimia 37.

-Uchunguzi wa chuo cha michezo cha Hispania mwanzoni mwa 2010 umethibitisha kwamba ukikimbia mara tatu kwa juma (jogging) unaongeza nyege mwilini kwa asili mia 75. Hasa kwa watu wa makamo mnaoanza kupoteza nguvu za urijali.

-Uchunguzi chuo kikuu cha Leeds, Uingereza mwanzoni mwa 2010 umeonyesha unapotembea kwa miguu, ukikwepa barabara kubwa zisisokuwa na mioshi ya magari (pollution) unapunguza matatizo ya maradhi ya hewa chafu kama pumu, mapafu na appendix.

-Uchunguzi wa chuo kikuu cha Texas mwaka 2010 umegundua kwamba kula tunda la divai nyekundu mara kwa mara husaidia kupunguza kupata ugonjwa wa kisukari.

-Hapo hapo tunaelezwa kwamba watu weusi na bara la Asia wanakumbwa zaidi na ugonjwa wa kisukari kutokana na vinywaji vya sukari sukari na gesi (fizzy drinks). Ukinywa kiasi cha miligramu 300 za vinywaji hivi (Cocacola, Red Bull, Fanta, nk) kwa siku unajitahadharisha kupata kisukari.

Njiwa London, mtaa wa Westbourne Park. Huruhusiwi kisheria kumpiga manati, kumuua au kumfanya ndege huyu kitoweio nchi hii.

9-KUFUNGA

Neno kufunga linatambuliwa rasmi kuhusiana na Waislamu (mwezi Ramadhani) au Wakristo (Lenti nk). Ufungaji huo una masharti mengine ya kidini tofauti na haya ya kiafya.

Mathalani wafungaji hawa hula chakula kingi usiku; ukihesabu wanafunga wastani wa saa 12 tu. Kawaida ukitaka virusi na takataka nyingine mwilini zitoweke, au viungo vipumzike wahitaji saa 20 kuendelea.

Ufungaji ninaouongelea ni ufungaji wa kutokula kabisa kwa saa 24, 36 hadi 48 kuendelea…

Ufungaji ni nini?

Kama mashine yeyote mwili wa mwanadamu unahitaji kupumzika na kujisafisha. Hata tukiwa tumelala bado viungo mbalimbali mwilini vinafanya kazi. Kwa hiyo faida ya kwanza kabisa ya kufunga ni kuupumzisha mwili kama mfanyakazi yeyote anapokwenda likizo.

Faida ya pili ya kufunga ni kusafisha mwili kutokana na uchafu ambao haukutoka (kinyesi hakitoi mabaki yote toka utumbo mkubwa), dawa na takataka za mazingira tunayoyavutia hewa, virusi au kuyanywa katika maji na vyakula mbalimbali na pia uchafu wa hisia, yaani hasira, huzuni, nk.

Kuna ufungaji wa aina mbalimbali.

1-Kufunga kwa kunywa maji tu, saa 24 kuendelea…

2-Kufunga kwa kutokunywa maji au kula chochote, saa 24 kuendelea…

3-Kufunga kwa kula tu matunda au mboga zilizopondwa kama karote, matango nk, saa 24 kuendelea…

Ufungaji huu unatakiwa ufanywe kwa mpangilio. Kitu muhimu si tu kufunga bali NAMNA unavyofungua. Ukianza kula tena, unaanza taratibu. Kawaida ni vizuri kuanza na maji, kikombe au bilauri ya kwanza taratibu. Subiri tena nusu saa, bilauri nyingine, halafu hadi ya tatu, halafu ndiyo matunda yasiyo ya chachu, na kadhalika. Kuanza kufungua kwa kunywa chai ya maziwa, uji au vyakula vingine vya wanga hakusadii sana mfungo huu.

Maana lengo lake ni kusafisha mwili.

PENDEKEZO LA 5- Kwa wenye imani za kidini. Unaweza pia kufunga hivi ukawa pia unasali au kuvaa mavazi yanayokufanya mtu wa amani. Ukifanya hivi unajitakasa kimwili na kiroho. Si lazima ungojee ile miezi ya kufunga na wengine.

10-USINGAJI

Usingaji au masaji ni njia nzuri sana ya kupunguza unene. Ikiwa unaangalia namna unavyokula, unafanya mazoezi na kusingwa mara moja au mbili kwa mwezi unaupalilia mwili vizuri. Nini faida ya usingaji? Kusinga husaidia ngozi, mishipa ya damu na sura nzima ya mwili na taswira yako mwanadamu. Wengi wetu tunaposikia neno kusinga tunafikiria usingaji wa mapenzi. Hivi ni vitu viwili tofauti kwani usingaji wa mapenzi unaimanisha mahusiano ya kihisia.

Kifupi mwanadamu unatakiwa uwe unautunza na kuungalia mwili wako kama nyumba au hekalu lako. Wengi wetu tunaoga, tunajipaka marashi, tunasuka, tunanyoa nywele au ndevu; lakini miili yetu kiundani inaoza taratibu…

Thursday, May 8, 2014

USIWAZE JUU YA VIDONDA VYA TUMBO, JIBU LAKO LIKO THE FADHAGET SUNITARIUM CLINIC



The Fadhaget Sanitarium Clini inasema pole sana kwa kusumbuka na tatizo hilo ulinalo. Umefika wakati na saa wa kupokea matunda yako. Dawa zetu zimehakikishwa na zimedhibishwa kwa magonjwa sugu kupokea uponyaji wao.

Katika toleo la 12 la mfululizo wa makala haya, Dk. Khamis Zephania alieleza dalili za tumbo kujaa gesi na tatizo la kufunga choo. Sasa endelea kumfuatilia katika sehemu hii ya 13.


Kiungulia: Pia huitwa acid reflux, au GERD. Wakati asidi inapokuwa chini, usagaji wa chakula huwa chini pia na mgumu. Matokeo yake ni kwamba chakula hukaa ndani ya tumbo kwa muda mrefu na kutoa gesi ambayo huchoma ndani ya tumbo na koo.

Kupungua damu (anemia): Huu ni upungufu wa madini ya chuma. Tatizo hili mara nyingi huhusiana na maambukizo ya H. pylori. Wakati H. pylori anaposababisha asidi ndogo ya tumbo huwa vigumu kumeng’enya protini (ambayo ina madini ya chuma). Hali hii husababisha kupungua damu. Pia kuchuruzika damu kwa muda mrefu huweza kusababisha kupungua damu.

Pumzi mbaya: Viumbe hivi vinavyofahamika kama H. pylori vinavyokaa ndani ya asidi ya tumbo hutengeneza ammonia, ambayo matokeo yake huleta pumzi mbaya.

Maumivu ya kifua: Wakati H. pylori anaposababisha uvimbe ndani ya tumbo, taarifa za maumivu kutoka tumboni huweza kuakisiwa kifuani, begani na maeneo ya tumbo.

Kuharisha: Kuharisha huweza kutokea mara chache, au pia huweza kutokea kila siku kutegemeana na usugu wa H. pylori.

Kichefuchefu na kutapika: H. pylori husababisha kichefuchefu, lakini sababu yake haiko wazi sana. Isipokuwa inadhaniwa kwamba mwili wenyewe unajaribu kumuondoa H. pylori. Dalili hizi zinaweza kufikiriwa kimakosa na hali za kutapika kwa akina mama wajawazito.

Uvimbetumbo (gastritis): Uvimbetumbo ni uvimbe wa kunyanzi za tumbo. H. pylori hutumia umbile lake la kizibuo (corkscrew) kuchimba ndani na kujeruhi kunyanzi za tumbo, ambapo matokeo yake ni uvimbe unaowaka.

Dalili nyingine za vidonda vya tumbo ambazo hazina sura maalum ni hofu, wasiwasi, mfadhaiko, uchovu au kuwa na nguvu kidogo, maumivu ya kichwa au kipanda uso, matatizo ya ngozi, kusongeka kabla ya hedhi (pre-menstrual stress), matatizo katika uwazi wa puani na matatizo ya usingizi.

Kupungua nguvu za kiume: Vidonda vya tumbo huweza kupunguza nguvu za kiume. Kwa sababu hudhuru sehemu za jirani zinazohusika na utendaji wa nguvu za kiume kama vile ini, n.k.

MAGONJWA MAPYA NA DALILI ZA HATARI

Karibu asilimia 0.46 ya watu duniani hufa kutokana na madhara yaletwayo na vidonda vya tumbo.
Watu wanafahamu kuwa vidonda vya tumbo vinaleta maumivu katika tumbo, lakini wengi hawafahamu kama vidonda vya tumbo ni tishio la maisha. Vidonda vya tumbo vinaweza kuzalisha magonjwa mapya na kufanya matibabu kuwa magumu.

Vidonda vingi vya tumbo vinaweza kutibiwa kabla havijazaa magonjwa mapya. Hata hivyo, katika baadhi ya watu, vidonda vya tumbo vinaweza kuzalisha matatizo makubwa kama vile kupenya katika viungo vingine (penetration), kutoboa (perforation), utokaji wa damu (hemorrhage), kuziba (obstructon) na saratani (cancer).

Magonjwa mapya kama vile kutoka damu (bleeding) au kupasuka, huambatana na dalili za shinikizo la damu la kushuka (low blood pressure), kama vile kizunguzungu na udhaifu.

Dalili za hatari hizi ni: Shida ya kumeza chakula au kucheua (regurgitation), kudumu kujisikia kichefuchefu na kutapika, kutapika damu au matapishi yenye sura ya unga wa kahawa, choo cheusi kinachofanana kama lami (chenye damu iliyomeng’enywa iliyotolewa kutoka katika kidonda), kupungua uzito ghafla, kupungua damu (kukwajuka na kudhoofika), maumivu makali ya ghafla tumboni ambayo humuondolea mtu nguvu na kupungua nguvu za kiume.

Hapa tutajadili magonjwa mapya ambayo huweza kuzalishwa na vidonda vya tumbo, magonjwa ambayo huweza kuleta dalili tulizozieleza.

Kupenya katika viungo (penetration): Kidonda kinaweza kupenya na kuingia kwenye kuta za misuli ya tumbo au duodeni (sehemu ya awali ya utumbo mdogo) na kuendelea hadi kwenye kiungo cha jirani.

Upenyaji huu husababisha maumivu makali ya kuchoma na ya kudumu, ambayo yanaweza kuhisiwa nje ya eneo linalohusika – kwa mfano, mgongo unaweza kuuma pindi kidonda cha duodeni kinapopenya kwenye kongosho.

yanaweza kuongezeka pale mtu anapobadilisha namna ya ukaaji. Kama dawa hazitaweza kutibu upasuaji unaweza kuhitajika.

Itaendelea:

Tuesday, May 6, 2014

YASEMEKANA RAY C AMEUGUWA UGONJWA WA DENGE ALAZWA MWANANYAMALA

Ray C akiwa amelazwa katika moja ya wodi za hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam jana Jumatatu. Picha na Rafael Lubava

Kwa mujibu wa vyanzo vyetu, mwanamuziki huyo ambaye amekuwa katika tiba ya kuachana na matumizi ya dawa za kulevya hospitalini hapo, alifikishwa hapo jana Jumatatu asubuhi na baadhi ya madaktari walibainisha kuwa Ray C anasumbuliwa na ugonjwa wa dengue ambao umelipuka katika maeneo mengi jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

MWANAMUZIKI mwenye sauti ya mvuto, Ray C, amelazwa katika hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam akikabiliwa na homa kali.

Kwa mujibu wa vyanzo vyetu, mwanamuziki huyo ambaye amekuwa katika tiba ya kuachana na matumizi ya dawa za kulevya hospitalini hapo, alifikishwa hapo jana Jumatatu asubuhi na baadhi ya madaktari walibainisha kuwa Ray C anasumbuliwa na ugonjwa wa dengue ambao umelipuka katika maeneo mengi jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

“Tumemfanyia vipimo, ana homa kali sana lakini hana malaria. Baada ya kuchunguza dalili, tumechukua vipimo na kubaini kwamba amepata maambukizi ya dengue, hivyo tunaendelea kumpa matibabu kwa sasa,” alieleza daktari ambaye hakutaka kutajwa jina lake.

Mwanaspoti iliyofika wodini alimolazwa mwanamuziki huyo, lilijaribu kuzungumza naye, lakini manesi wazuia wa kusema hapaswi kuamshwa kwa kuwa alikuwa amepewa dawa za kutuliza maumivu na kushusha homa.

Ray C amekuwa katika tiba ya kuacha dawa za kulevya na amekuwa akisaidiwa kurejea katika sanaa ya muziki ambayo alikuwa akiifanya vizuri kabla ya kuingia kwenye wimbi hilo.

Ugonjwa huo dengue uliotajwa kumsumbua kwa sasa umewakumba wananchi wengi wa Dar es Salaam na unaenezwa na mbu weusi waitwao Aedes Egypitia.

Mbu hao ambao huonekana zaidi mchana, huzaliana katika maji safi yaliyotuama.

Usiku wa kuamkia juzi Jumapili, Ray C alikuwapo kwenye ukumbi Mlimani City kwenye hafla ya Tuzo za Muziki za Kilimanjaro ambapo hakuonekana kuwa na dalili zozote za kuumwa.

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UGONJWA WA HOMA YA DENGUE (DENGUE FEVER)




Utangulizi

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inapenda kutoa taarifa kwa umma kuhusu kuendelea kuwepo kwa ugonjwa wa homa ya dengue hapa nchini. Ugonjwa huu ulithibitishwa kuwepo hapa nchini hususan hapa jijini Dar es Salaam mnamo mwishoni mwa mwezi wa Januari 2014. Hadi sasa idadi ya wagonjwa ambao wamethibishwa kuwa na ugonjwa huu kwa kipindi hiki ni 70 ikiwa ni wagonjwa 58 Kinondoni, 7 Temeke na 5 Ilala. Kwa kipindi cha wiki mbili zilizopita idadi hii ya wagonjwa imeongezeka mara mbili kuliko siku za nyuma. Vilevile kumekuwepo kifo cha mtu mmoja katika hosipitali ya Mwananyamala.

Aidha, ugonjwa huu si mpya hapa nchini kwani uligundulika kwa mara ya kwanza mnamo Juni 2010 mkoani Dar es Salaam ambapo idadi ya watu waliothibika kuwa na ugonjwa ilikuwa 40, pia kati ya mwezi Mei hadi Julai 2013, wagonjwa 172 walithibitishwa kuwa na ugonjwa huu.
Homa ya Dengue

Homa ya dengue ni ugonjwa unaosababishwa na kirusi ambacho kinaenezwa na mbu wa aina ya Aedes ambao ni weusi na madoadoa meupe yenye kungaa.

Dalili za ugonjwa huu ni homa ya ghafla, kuumwa kichwa hususani sehemu za macho, maumivu ya viungo na uchovu. Dalili hizi huanza kujitokeza kuanzia kati siku ya 3 na 14 tangu mtu alipoambukizwa kirusi cha homa ya denge. Kwa wakati mwingine dalili za ugonjwa huu zinaweza kufanana sana na dalili za malaria, hivyo basi wananchi wanaaswa kuwa wakati wakipata homa kuhakikisha wanapima ili kugundua kama wana vimelea vya malaria ua dengue ili hatua stahiki zichukuliwe.
Vilevile mara chache mgonjwa anaweza kutokwa na damu sehemu za fizi, mdomoni, puani, kwenye macho na pia njia ya haja kubwa na ndogo. Dalili hizi za kutokwa damu pia zimeanza kuonekana hapa Dar es Salaam kwa wagonjwa watatu ambapo mmojawapo alipoteza maisha.

Virusi vya homa ya dengue vinaenezwa kwa binadamu baada ya kuumwa na mbu aina ya “Aedes”. Mbu hawa hupendelea kuzaliana kwenye maji yaliyotuama karibu na makazi ya watu au hata ndani ya nyumba. Viluwiluwi vya mbu hawa huweza kuishi katika mazingara ya ndani ya nyumba mpaka wakawa mbu kamili na kuanza kusambaza ugonjwa huu kwa binadamu. Mbu hawa huwa na tabia ya kuuma zaidi wakati wa mchana.

Ugonjwa huu hauenezwi kutoka binadamu mmoja kwenda kwa mwingine bila ya kuwepo na kuumwa na mbu mwenye vimelea. Hadi sasa hakuna chanjo ya homa ya denge. Mgonjwa mwenye homa ya dengue anatibiwa kutokana na dalili zitakazoambatana na ugonjwa huu kama vile homa, kupungukiwa maji au damu. Mgonjwa mwenye dalili za homa ya denge anashauriwa kuwahi mapema kwenye kituo cha kutolea huduma za afya ili kupata huduma stahiki kwani endapo mgonjwa atachelewa kupatiwa matibabu anaweza kupoteza maisha.

Jinsi ya kujikinga na ugonjwa wa homa ya dengue
  • Kuangamiza mazalio ya mbu
  • Fukia madimbwi ya maji yaliyotuama au nyunyuzia dawa ya kuua viluwiluwi vya mbu kwenye madimbwi hayo
  • Ondoa vitu vyote vinavyoweza kuweka mazalio ya mbu kama vile, vifuu vya nazi, makopo, magurudumu ya magari yaliyotupwa hovyo, nk.
  • Fyeka vichaka vilivyo karibu na makazi ya watu
  • Hakikisha maua yandayopandwa kwenye makopo au ndoo hayaruhusu maji kutuama
  • Funika mashimo ya maji taka kwa mfuniko imara
  • Safisha gata za paa la nyumba ili kutoruhusu maji kutuama
Kujikinga na kuumwa na mbu
  • Tumia dawa za kufukuza mbu “mosquito repellants”
  • Vaa nguo ndefu kujikinga na kuumwa na mbu
  • Tumia vyandarua vyenye viuatilifu (hata kwa wale wanaolala majira ya mchana)
  • Weka nyavu kwenye madirisha na milango ya nyumba za kuishi
Hivyo ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha kuwa mazalio ya mbu yanaangamizwa na pia kujizuia kuumwa na mbu.

Hatua zilizochukuliwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii


• Kutoa taarifa ya tahadhari ya ugonjwa kwa Waganga Wakuu wote wa Mikoa na Wilaya kwa Tanzania Bara kupitia Makatibu Tawala na Wakurugenzi.

• Ufuatiliaji wa homa hii ulianza kufanyika katika Manispaa ya Kinondoni iliyoonekana kuwa na wagonjwa wengi zaidi ikafuatiwa na Ilala na Temeke. Pia uchunguzi utaendelea katika Mikoa na Wilaya nyingine tukianzia na zile wilaya zitakazoonekana kuwa na ongezeko la wagonjwa wenye homa.

• Kutuma vipeperushi vya ugonjwa huu katika maeneo ya mipakani ili iwapo msafiri anayeondoka au kurudi nchini akiwa na dalili tajwa atoe taarifa kwa watumishi wa afya wa mpakani ili hatua stahili ziweze kuchukuliwa.

• Kutoa mafunzo kwa watumishi wa afya kwenye vituo vya kutolea huduma na mipakani kuhusu namna ya kutambua, matibabu na kujikinga dhidi ya maambukizo ya ugonjwa huu pamoja na uchukuaji wa sampuli iwapo mgonjwa atapatikana.

• Kuimarisha ufuatiliaji wa magonjwa nchi nzima kwa kutumia mfumo uliopo wa ukusanyaji wa taarifa, ambapo tunaendelea kupata taarifa za kila siku juu ya mwenendo wa ugonjwa huu

• Kutoa elimu kwa waandishi wa habari ili waweze kuisambaza kwa jamii

• Kuimarisha mfumo wa ufuatiliaji wa ugonjwa wa dengue uliopo kwenye vituo maalumu ‘Sentinel Surveillance Sites’

• Kuimarisha Utambuzi wa ugonjwa katika maabara ili kuweza kuthibitisha ugonjwa huu

• Kufanya tathmini ya mazalio ya mbu ili kubaini ukubwa wa tatizo, jamii ya mbu wanaoambukiza ugonjwa, mazingira yao na jinsi ya kuwathibiti

Hitimisho
Wananchi wanashauriwa kutokuwa na hofu kuhusu ugonjwa huu bali wanashauriwa kwenda katika vituo vya tiba mara mnapoona dalili.

Jamii inashauriwa kuhakikisha kuwa mazalio yote ya mbu yanaangamizwa na pia kuzuia kuumbwa na mbu

Vilevile, wizara inasisitiza kuwa hakuna vikwazo vyovyote vilivyowekwa kwa ajili ya wasafiri wanaoingia na wanaotoka nchini. Wizara itaendelea kushirikiana na sekta mbalimbali kufuatilia na kudhibiti ugonjwa huu.

Mhe. Dkt. Seif Suleiman Rashid (Mb)
Waziri – Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii
25 Machi 2014

Friday, May 2, 2014

UGONJWA WA KASWENDE UNAVYOSUMBUA WATU WENGI DUNIANI..NINI CHA KUFANYA KUONDOKANA NA UGONJWA HUU?

Kaswende ni ugonjwa wa zinaa unaosababishwa na bakteria ya spirochete Treponema pallidum baadhi ya spishi pallidum. Njia ya kawaida zaidi ya kuambukizwa ni kupitia kufanya ngono; hata hivyo, kaswende pia inaweza kuambukizwa kutoka kwa mama hadi kwa fetasi wakati wa ujauzito au wakati wa kuzaliwa kwa mtoto, na kusababisha kuzaliwa na kaswende. Magonjwa mengine ya binadamu yanayohusiana niTreponema pallidumbakteria inajumusiha buba (baadhi ya spishi pertenue), pinta (baadhi ya spishi carateum) na bejel (baadhi ya spishi endemicum).

Dalili na ishara za kaswende hutofautiana kulingana na hatua iliyoko kati ya hatua nne. Hatua ni ya kwanza, ya pili, fiche, na ya mwisho. Hatua ya kwanza kawaida inajitokeza kimoja na shanka utokeaji wa kidonda kwa ngozi isiyowasha, ngumu, isiyokuwa na uchungu). Hatua ya pili ya kaswende hujitokeza na upele ambayo mara kwa mara inahusisha viganja vya mikono na nyayo za miguu. Hatua fiche ya kaswende hujitokeza na dalili kiasi au hata bila. Hatua ya mwisho ya kaswende hujitokeza na guma, dalili zinazohusiana na mfumo wa neva, au zinazohusiana na moyo.

Hata hivyo, kaswende imeitwa "mwiigaji mkuu" sababu mara nyingi hujitokeza kwa njia isiyo ya kawaida.
(Bonyeza hapa kuangalia picha sehemu ya uume iliyoathirika. Uwe na umri wa miaka zaidi 18)

Kwa kawaida kaswende hutambulika kwa uchunguzi wa damu;hata hivyo, bakteria inaweza kuonekana kwa kutumia hadubini. Kaswende inaweza kutibiwa kwa njia inayofaa kwa kutumia antibiotiki, haswa ndani ya misuli penisilini G. Hii inapendekezwa kwa watu walio na aleji ya penisilini, seftriaksoni. Inaaminika kwamba kufikia mwaka wa 1999 watu milioni 12 walikuwa wameambukizwa kaswende ulimwenguni na zaidi ya asilimia 90 ya hali hizi kutoka kwa nchi zinazoendelea. Hali za kaswende zilipungua kwa kasi baada ya penisilini kupatikana kwa urahisi katika miaka ya 1940, lakini viwango vya maambukizi vimeongezeka tangu mwaka 2000 katika nchi nyingi. Mara nyingi kaswende hupatikana pamoja na virusi vinavyosababisha UKIMWI (VVU). Hii imehusishwa na sehemu ya matendo ya ngono yasiyokuwa salama kati ya wanaume wanaofanya ngono na wanaume wengine;Ongezeka la uasherati; ukahaba; na kupungua kwa matumizi ya kondomu


Dalili na ishara
Kaswende inaweza kuwa katika hatua moja kati ya hatua nne tofauti: ya kwanza, ya pili, fiche, na ya mwisho,[4] na pia inaweza kujitokeza wakati wa kuzaliwa.[5] ilirejelewa kama "mwiigaji mkuu" na Sir William Osler kutokana na njia mbalimbali inavyojitokeza[4][6]
Hatua ya kwanza

Hatua ya kwanza shanka ya kaswende kwa mkono

Hatua ya kwanza ya kaswende kawaida hupatikana kwa kuwasiliana kwa njia ya moja kwa moja kwa ngono na vidonda vilivyoambukizwa vya mtu mwingine.[7]Takriban siku 3 hadi 90 baada ya kuathiriwa hapo awali ( wastani ya siku 21 ) kidonda kwa ngozi, iitwayo shanka, hutokea mahali palipogusana.[4] Huu ni mfano hasa (Asilimia 40 ya wakati) kidonda kimoja, kigumu, kisichokuwa na uchungu, kisichowasha na sehemu yake ya chini iliyokuwa safi na mipaka mikali kati ya sentimita 0.3 na 3.0 kwa ukubwa .[4] Hata hivyo, kidonda, kinaweza kuonekana kuwa tofauti sana. [8] Katika viwango, hugeuka kutokamacule hadi kipelena kisha kwa uyeyukaji au donda.[8] Mara chache, kutakuwa na vidonda kadhaa. (~40%),[4] Hii pia ni ya kawaida mtu anapoambukizwa Virusi Vya Ukimwi

Shanka yanaweza kuwa na uchungu au nyororo (30%), na zinaweza kutokea nje viungo vya uzazi (2–7%). Mahali pa kawaida zaidi pa chanikeri kwa wanawake ni kwa seviksi(44%). Mahali pa kawaida zaidi kwa wanaume wanaovutiwa na jinsia tofauti ni Kwa uume (99%). Wakati mwingine shanka hutokea kwa tupu ya nyama au rektamu kwawanaume wanaojishirikisha ngono na wanaume wengine (34%).[8]Tenzi kuvimba mara kwa mara (80%)hutokea pahali palipo ambukizwa,[4] hutokea siku 7 hadi 10 baada ya kutokea kwa shanka[8]kidonda kinaweza kuendelea kutokea wiki watatu hadi sita bila matibabu[4]
Hatua ya pili


 Mfano hasa unaojitokeza kwa hatua ya pili ya kaswende na upele kwa viganja vya mikono


Nyekundu vipele na vipele kuzidi mwilini kutokana na hatua ya pili ya kaswende

Hatua ya pili ya kaswende hutokea takriban wiki nne hadi kumi baada ya hatua ya kwanza ya maambukizi.[4] hatua ya pili ya ugonjwa unaweza kujitokeza kwa njia nyingi tofauti, lakini kwa kawaida dalili sana sana huhusisha ngozi, membreni ute, na tezi ya limfu.[9] kunaweza kuwa na upele mwekundu-waridi-isiyokuwa na mwasho kwa kiwiliwili pamoja na limbu (miguu na mikono), ikiwa ni pamoja na viganja na nyayo.[4][10] Vipele vinaweza kuwa makulopapula au yenye pustuli. inaweza kutengeneza chunjua kama vidonda iliyopana, nyeupe na sawa sawa inayojulikana kama kondiloma latum kwa membreni yenye utes. Vidonda hivi vyote vinamaambukizi na yanahifadhi bakteria. Dalili zingine inaweza ni pamoja na homa, uchungu wa koo, hitilafu ya mwili,kupunguza uzito, kutokwa na nywele, na maumivu ya kichwa.[4] matokeo yasiyo kuwa ya kawaida ni pamoja na hepatitisi, figo ugonjwa, athritisi,periostitisi, neuritsi ya kuona, uveitisi, na keratitisi ya interstitial.[4][11]

Kwa kawaida dalili kali uyeyuka baadaye kati ya wiki tatu hadi sita;[11] hata hivyo, katika hali iliyokaribia 25%, dalili ya hatua ya pili yanaweza kurudi. Watu wengi walio katika hatua ya pili ya kaswende (40–85% ya wanawake, 20–65% ya wanaume) hawatoi ripoti kuwa na shanka ya kiwango kilicho juu cha hatua ya kwanza ya kaswende.[9]
Hatua fiche

Hatua fiche ya kaswende imefafanuliwa kama kuwa na serologic utambuzi wa maambukizi bila dalili ya magonjwa.[7] Imeelezwa zaidi kama ya hapo awali (chini ya mwaka wa 1 mwaka mmoja baada ya hatua ya pili ya kaswende) katika Marekani[11] Uingerezani, masaa hizi huitwa miaka miwili ya hatua fiche ya kaswende ya mapema na iliyochelewa.[8] Dalili ya hatua fiche ya kaswende ya mapema huweza kurudi tena. Hatua fiche ya kaswende iliyochelewa huwa haina dalili za magonjwa (hayana dalili), na hatua fiche ya kaswende iliyochelewa haiambukizwi kwa urahisi kama hatua fiche ya kaswende ya mapema.[11]
Hatua ya mwisho

Hatua ya mwisho ya kaswende inaweza kutokea takriban miaka mitatu hadi 15 baada ya maambukizi ya kwanza, na inaweza kugawanywa kwa aina tatu tofauti: kaswende iliyosababishwa na guma (15%), iliyochelewa kaswende katika mfumo wa neva (6.5%), na kaswende inayoathiri moyo na mishipa ya damu (10%).[4][11] Bila matibabu, theluthi moja ya watu ambao wameambukizwa kaswende hupata hatua ya mwisho ya kaswende.[11] Watu walio na awamu ya mwisho ya kaswende hawawezi kuambukiza wengine.[4]

Kaswende inayosababishwa na gum, pia inayoitwa hafifu kaswende, kwa kawaida hutokea moja kwa miaka 46 baada ya maambukizi ya awali, kwa wastani wa miaka.15 Hatua hii ni sifa ya muundo sugu wa guma, ambayo ni uvimbe nyororo zinazofanana na vidonge vya inflamesheni vinavyoweza kuwa zinabadilika kulingana na ukubwa. Kawaida huathiri ngozi, mifupa, na ini, lakini inaweza kutokea mahali popote.[4]

Kaswende katika mfumo wa neva inamaanisha maambukizi inayohusisha mfumo mkuu wa neva. Unaweza kutokea mapema, ikiwa aidha isiyo kuwa na dalili ya ugonjwa au ya kusababisha kaswende meninjitisi; au inaweza kuchelewa, kama kaswende ya veni za tando za ubongo, paresi ya jumla, au tabesi dorsalisi, ambayo inahusu usawa wa mwili na uchungu mkali kwa limbu za chini. Kaswende ya neva iliyochelewa huja kabisa baada ya miaka minne hadi 25 baada ya maambukizi ya hapo awali. Kaswende ya veni za utando za ubongo hufanana hasa ikiwa haiwezi kuzuiliwa kifafa, na paresi ya jumla hufanana hasa na dimenshia na tabtesi dorsalisi.[4] Pia, kunaweza kuwa na Mboni za Agryll Robertson ambazo ni mboni ndogo kwa macho zinazofinyika mtu anapotazama vitu vilivyokaribu, lakini hayafinyiki zikiwa wazi kwa mwanga mkali.

Kaswende ya moyo na mishipa kwa kawaida hutokea miaka 10 hadi30 baada ya maambukizi ya awali. Tatizo la kawaida kabisa ni ule wa kaswende ya kuvimba kwa aota, ambayo inaweza kusababisha aneurisimi kuundwa.[4]
Ya kuzaliwa nayo Kaswende ya kuzaliwa nayo inaweza kutokea wakati wa mimba au wa kuzaa. Theluthi-mbili ya watoto wazawa wanazaliwa bila dalili. Dalili ambazo huendelea zaidi ya miaka michache ya kwanza ya maisha ni pamoja na: kunenepa nenepa kwa ini au wengu (70%), upele (70%), joto jingi mwilini (40%), kaswende ya neva (20%), na ugonjwa wa mapafu kuvimba (20%). Ikiwa haita tibiwa, kaswende ya kuzaliwa ya baadae inaweza kutokea kwa 40 %, ikiwa ni pamoja na: pua lenye umbo la tandikoulemavu, Higoumenakis sign, saber shin, au Clutton's joints, miongoni mwa zingine

SIFAHAMU OFISI ZA THE FADHAGET SANITARIUM CLINIC ZILIZOPO KATIKA MIKOA KUMI TANZANIA