Karibu Fadhaget Sanitarium Clinic

Tunapenda kukukaribisha katika Kitengo cha Sayansi ya Tiba Asilia.

Kitengo Cha Sayansi Ya Tiba Asilia

Kwa Muda mrefu tumekuwa tukisaidia wengi katika matibabu na kutengeneza dawa bora kabisa kiafya.

Je Unapenda Kufahamu Jinsi Ya Kupata Mapacha?

Tunafundisha jinsi ya kupata jinsia unayotaka, jinsi ya kupata mtoto kama umekosa mtoto kwa muda mrefu. Pia hata jinsi ya kupata watoto mapacha tunaweza kukusaidia.

Tunapatikana Katika Mikoa Zaidi ya 10 Tanzania

Tunazidi kuongeza matawi yetu nchini Tanzania na Nje ya Nchi. Kwa sasa tunapatikana katika mikoa zaidi ya 10 na tunazidi kuongeza matawi yetu. Karibu sana.

Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Wednesday, May 23, 2012

MUDA WA KUTESEKA NA MAGONJWA UMEKWISHA KUTANA NA DOKTA FADHILI EMILLY UPONE KWA NJIA YA DAWA ZA MIME NA MATUNDA

Sunday, May 20, 2012


FADHAGET SANITARIUM CLINIC CD KUPATIKA SASA-Dr. Fadhili Emily
Dokta Fadhili amesema sasa unaweza kupata mafundisho kuhusiana na huduma za tiba zinazotolewa na Sanitarium Clinic iliyoko Mbezi Beach Tangi Bovu, Tandika Majaribio-Dar es Salaam Tanzania

Amewaomba watu wote kununua CD hii ili uweze kujifunza ni jinsi gani unaweza ukatibiwa magonjwa sugu kwa njia ya mimea na matunda.

Kama ungependa kujua zaidi jinsi ya kupata hizi CD, tafadhali wasiliana nasi kwa mawasiliano yaliyopo katika CD hapo chini:-







CD case imetengenezwa na Rulea Sanga +255 715 85 15 23 | rumatz2011@yahoo.com | www.rumaafrica.blogspot.com

Wednesday, May 9, 2012

FADHAGET SANITARIUM CLINIC
Dokta Fadhili Emily wa Fadhage Santarium Clinic


Ilianza mnamo mwaka 27/7/2011, ilikuwa na umahiri mkubwa sana na wengine walichukulia matibabu ya jadi. Lakini kupitia Fadhili Emily alihakikisha zana za ligha mbaya iliyokuwa ikipotosha huduma hii ya tiba halisi ya matunda na mimea inatambulika kama huduma sahihi yenye vipimo vya kisasa vyenye kutambulika kisayansi na kuvunja kauli mbaya za watu kusema ni huduma ya kijadi yani za kiganga

Katika kuthibitisha hilo alielimisha jamii tiba halisi za mimea na matunda kwamba ni tiba ambazo za zimetafitiwa na kuthoibitishwa na Elimu ya Chuo Kikuu Tanzania.


Baada ya kutambua chungwa lina Vitamin C, Alovera ina Alkolik asidi, muarobaini una sainatic asid, ndimu ina sitiriki asidi, na madaktari wamethibitisha kimataifa virutubisho vinavyotokana na mimea na matunda ikiwa vitachanganywa vyema vinaweza kutibu maradhi hasa yaliyo sugu.
Alovera

Ndimu

Ushahidi tunaweza kupata kutoka kwa madaktari mbalimbali walio vyuo vikuu vya tiba za mimea na matunda ulimwenguni, kama vile, Romalinda University of Medical Plant kilichoko California Marekani,  East Africa Medical Missionary cha nchini Kenya, Zuru National Remedies Citiovvasty, iliyoko south Afrika, na pande mabalimbali za ylimwengu.


Kwa kushirikiana na Fadhaget Santarium Clinic tiba hii inaonekana sio tiba ya jadi bali ni tiba inayotambulika kisayansi ulimwenguni



"GET TOGETHER PARTY" YAFANA NDANI YA THE ATRIUMS HOTEL USIKU WA JANA
Dokta wenu nilibahatika kufika mahali pale kushirikiana na wenzangu katoika kuhakikisha shughuli ya mtangazaji wetu Erick Brighton inakamilika

Nilifurahi sana kukutana na watu amba sijawahi kukutana nao, na niliweza kubadilishana mawazo na kutiana moyo katika kazi ya BWANA.

Uimbaji na vichekesho vilinifanya nifurahi sana, na nikajifunza kuwa palipo wengi hukosi jambo la kukuburudisha na kukukasilisha, ila kwangu usiku huyo ulikkuwa wa furaha ndani ya kiroho changu

Mungu na akubariki

Blogger Rulea Sanga na mwanakamati ya party hiyo alikuwa na haya ya kusema kuhusu party

"Usiku ulikuwa ni usiku wa furaha na kumtukuza Mungu, Erick Brighton ndiye mlengwa mkubwa katika party ya jana ambaye aliwakusanya watu kwaajili ya kuwakutanisha maproducer, waimbaji, watangazaji wa radio na TV, mabloggers na wachekeshaji, na kubwa zaidi ilikuwa ni siku ya kumchangia Erick katika harusi yake itayofanyika karibuni.

Burudani mabalimbali kutoka kwa waimbaji zilitawala zikiambatanishwa na vichekesho kutoka kwa wachekeshaji kama Masanja Mkandamizaji na Nyerere.

Kamati inawashukuru watu wote waliohudhuria mahali pale na Mungu awabariki, na msingi zaidi ni kuwasisitiza kwa wale walioahidi michango yao waiwakilishe kwa wahusika kabla ya jambo lenyewe la harusi"

 Mchekeshaji, Msanja Mkandamizaji (kushoto kwa hao waliosimama) akikandamiza na mdau wa blogu hii.
 Fadhili wa Fadhaget Santarium Clinic (kushoto) akiwa katika pozi na Mkandamizaji Masanja
 Mzee wa Blogu, Rulea Sanga (kulia) nikijipendekeza kwa mtalaamu wa magonjwa sugu Fadhili wa Fadhaget Santarium Clinic

Kike inapukutika
Mtangazaji wa Praise Power Erick Brighton katikati akijiandaa kuwalisha kike wapenzi wake


Monday, May 7, 2012

TUJIKUMBUSHE YAYOLIVUMA MITANDAONI KIPINDI CHA NYUMA
TAASISI YA THE FADHAGET DEVELOPMENT HOPE YATOA VIFAA VYA MICHEZO KWA ACOT SPORTS CLUB YA MTONI

Tunapenda kumshukuru Dr. FADHILI EMILY ambaye ni mkurugezi wa taasisi ya THE FADHAGET DEVELOPMENT HOPE wanahousika na kusaidia jamii, kutunza mazingira, kupiga vita madawa ya kulevya, migogoro ya mke na mume, umasikini na njaa. Tayari wamekwisha fungua kituo cha afya Tandika wana mitambo maalumu ya vipimo vya magonjwa ya aina zote na wana tengeneza dawa kwa kutumia matunda na mimea asilia. Kwa kuweza kutusaidia jezi seti moja na mipira miwili .
Ndugu wahariri,wanahabari na watanzania kwa ujumla ni furaha kwetu kuwaona mmefika hapa , siku hii ya leo,kwa kweli mnaitaji pongezi za pekee siku hii ya leo.
HISTORIA YA TAASISI
ACOT ni taasisi isiyo ya kiserikali ilianza rasmi 30/10/2010. Ni taasisi ambayo inatambuliwa na Serikali kwa kuwa tumepata usajili rasmi toka Serikalini. makazi yake ni mtoni kwa Aziz Ally, wilaya ya Temeke mkoa wa Dar es salaam. Sababu zilizotufanya tuanzishe ni nyingi lakini moja ya sababu hizo ni Kukuza na Kuendeleza vipaji vya vijana, Kielimu,Kiutamaduni na Kimichezo.
Baada ya kuona vijana wengi hasa wa wilaya yetu ya Temeke wanaishi katika mazingira magumu na pia wana vipaji tofauti ila wamekosa mtu wa kuwasimamia na kuwaendeleza pamoja na kuwapatia mahitaji muhimu kama vile chakula,maradhi na vifaa.

sisi tukiwa kama watanzania tumeona tujitokeze mbele yenu ili mtusaidie pale ambapo tumefikia ili tuweze kuwaendeleza baadhi ya vijana kimaisha maana vijana ni nguvu kazi ya Taifa. Tunajua kuwa kwamba tunadeni kubwa kwetu na Taifa letu la Tanzania hivyo kuendelea kuwaacha vijana hawa ni kupoteza muelekeo wetu.


CHANGA MOTO TUNAZO PATA
Kunachanga moto nyingi tunazo pata katika maisha haya ya kuwalea vijana lakini moja ya changamoto hizo ni ukosefu wa vifaa vya michezo na utamaduni kama vile Viatu,Mipira, Jezi,Bipsi,Koni,Nyavu, Shine Guard,Ngoma.
Pia Ukosefu wa Ada kwa ajili ya kuwaendeleza wachezaji wetu na wanajamii wetu kielimu zaidi.
Upungufu wa dawa za kuchukua,Clip bandage,diclopa,diclofenac,glucose,deepheat spray,na Chakula kama vile mchele,sukari,sembe.
Fedha za kuendeshea programu mbalimbali kwa maendeleo ya jamii yetu husika.
MAFANIKIO
Mafanikio tuliyoyapata tangu kujumuika kwetu ni pamoja na kusikilizana sisi kwa sisi kuwaelimisha vijana wenzetu kuhusu Ukimwi,Matumizi ya Kondom,Ujasiriamali kuachana na madawa ya kulevya kwa wale wanaotumia,Kuanzisha vikundi kulingana na fani zao ili kukuza vipaji vyao.
Kupitia vijana wetu tumeweza kuanzisha timu ya mpira wa miguu na imeweza kushiriki mashindano ya EAST AFRICA CUP 2011.Timu zilizoshiriki U16 ni kumi na nne Kutoka Kenya,Uganda,Zimbabwe,Zanzibar na Tanzania na tukafanikiwa kuwa washindi wa pili U16 na kuiletea sifa mtaa wetu,wilaya yetu hata mkoa wetu.
Kupitia mashindano hayo tumeweza kupata marafiki wengi wa kigeni kutoka nchi sita wanawataka wachezaji wetu wakacheze kwao.
Kupitia vijana wetu tumeweza kuanzisha kikundi cha ngoma za asili,na kuwafundisha ngoma mbalimbali za makabila tofauti kama vile Masewe,Mangaka,mganda wa kikutu,lingokwa,lumbunjumu na likaturinge,kupitia sanaa yao hiyo wameweza kupata marafiki wakigeni kutoka nchini Kenya na kikundi cha sanaa cha haba na haba kilichopo nchini Kenya .
Tunawasomesha vijana wetu katika shule za Msingi (vijana 6) ,Sekondali (vijana 20), vyuo vya ufundi stadi (vijana 5) na hata vyuo vikuu (vijana 3) na shule ya walemavu (2) wasichana na wavulana.
Pia tumeweza kuwapeleka vijana sita katika mafunzo ya UJASIRIAMALI katika chuo kikuu cha DSM Mlimani kitengo cha ujasiriamali (UDEC) yaliyofanyika 25/07/2011 mpaka 29 /07/2011 na kupata vyeti.
HITIMISHO
Pamoja na maelekezo yote haya ni vyema mkajua kuwa sisi mpaka sasa tupo katika wakati mgumu endapo kunatokea mashindano au mwaliko wowote ule,tatizo ni vitendea kazi hatuna na akuna sehemu, tunayojua kuwa tutaenda kusaidiwa.
Tunaomba sana tusaidiwe vitendea kazi kama vile,Kompyuta,Projector,Digital camera,Viatu vya Mpira(Njumu),Mipira, Jezi,Bipsi,Koni,Shine Guard itakuwa vizuri sana, kwani tunataka tuwe mfano wa kuigwa katika wilaya yetu ya Temeke na kata yetu ya mtoni na mtaa wetu wa sabasaba na hata taifa kwa ujumla.
Asanteni sana kwa kuweza kunisikiliza kama kuna mapungufu mtatusamehe lakini ni imani yetu tuta kuwa tumeeleweka mungu wabariki wote waliofika hapa siku hii ya leo.
Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki ACOT
Wenu Katika Ujenzi wa Taifa
Emmanuel Mwampishi.
Mkurugenzi